7/30/2018

Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote





Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

Utambulisho

I
Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibuwa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safari ya maisha. Vyovyote vilivyo msingi wako ama safari iliyo mbele yako, hakuna anayeweza kuepuka utaratibu na mpango ambao Mbingu imeweka, na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake, kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote ndiye ana uwezo wa kazi kama hii.

II
Tangu siku ambayo mwanadamu alikuja kuwepo Mungu amekuwa imara katika kazi Yake, Akisimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na kusonga kwa vitu vyote. Kama vitu vyote, mwanadamu kwa kimya na bila kujua anapokea uboreshaji wa utamu, mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya utaratibu wa mkono wa Mungu.

III
Moyo na roho ya mwanadamu viko mkononi mwa Mungu, na maisha yote ya mwanadamu yanatazamwa machoni mwa Mungu. Bila kujali kama unaamini katika hili ua la, chochote na vitu vyote, viishivyo au vilivyokufa, vitageuka, vibadilike, vifanywe upya, na kupotea kulingana na fikira za Mungu. Hivi ndivyo Mungu hutawala juu ya vitu vyote.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Yaliyopendekezwa: Kuhusu Umeme wa Mashariki, Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni