Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Pili
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Tembea katika Njia ya Mungu: Mche Mungu na Kuepuka Maovu
Mungu Hutumia Majaribio Tofauti ili Kupima Kama Watu Humcha Mungu na Kujiepusha na Maovu
Kutomcha Mungu na Kutojiepusha na Maovu ni Kumpinga Mungu
Soma Zaidi:
Mwenyezi Mungu anasema,“Katika kila enzi, Mungu huwapa binadamu baadhi ya maneno Anapofanya kazi ulimwenguni, huku akimwambia mwanadamu kuhusu baadhi ya ukweli. Ukweli huu unahudumu kama njia ambayo binadamu anafaa kuitii, njia ya kutembelewa na binadamu, njia ambayo humwezesha binadamu kumcha Mungu na kujiepusha na uovu, na njia ambayo watu wanafaa kuweka katika vitendo na kuitii katika maisha yao na kwenye mkondo wa safari zao za maisha. Ni kwa sababu hizi ambapo Mungu anampa binadamu maneno haya. Binadamu anafaa kuyatii maneno haya yanayotoka kwa Mungu, na kuyatii ni kupokea uzima. Kama mtu hataweza kuyatii, na hayatii kwenye matendo, na haishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu katika maisha yake, basi mtu huyo hautilii ukweli katika matendo. Na kama hawatilii ukweli katika matendo, basi hawamchi Mungu na hawaepuki uovu, wala hawawezi kumtosheleza Mungu. Kama mtu hawezi kumtosheleza Mungu, basi hawezi kupokea sifa ya Mungu; mtu wa aina hii hana matokeo. Hivyo basi ni vipi katika mkondo wa kazi ya Mungu ndipo Anapoasisi matokeo ya mtu? Ni mbinu gani anayoitumia Mungu kuasisi matokeo ya binadamu? Pengine nyinyi hamlielewi suala hili sasa hivi, lakini Nitakapowaambia mchakato jambo hili litakuwa wazi kabisa. Hii ni kwa sababu watu wengi tayari wamelipitia suala hili wenyewe.
Katika mkondo wa kazi ya Mungu, kuanzia mwanzo hadi sasa, Mungu Amepanga majaribio kwa kila mtu—au mnaweza kusema, kila mtu anayemfuata Yeye—na majaribio haya yanakuja kwa ukubwa tofauti. Wapo wale ambao wamepitia jaribio la kukataliwa na familia zao; wapo wale ambao wamepitia jaribio la mazingira mabovu; wapo wale ambao wamepitia majaribio ya kukamatwa na kuteswa; wapo wale ambao wamepitia majaribio ya kukumbwa na chaguo; na wapo wale ambao wamekumbwa na majaribio ya pesa na hadhi. Nikizungumza kwa ujumla, kila moja wenu amekabiliwa na aina zote za majaribio. Kwa nini Mungu anafanya kazi hivyo? Kwa nini Mungu Anamtenda hivi kila mtu? Ni matokeo aina gani Anayotaka kuyaona? Hii ndiyo hoja muhimu kuhusu kile Ninachotaka kuwaambia: Mungu anataka kuona kama mtu huyu ni yule anayemcha Mungu na kujiepusha na uovu. Maana ya haya ni kwamba wakati Mungu anakupa jaribio, na kukufanya kukabiliwa na baadhi ya hali, Anataka kukupima na kujua kama wewe ndiye yule mtu anayemcha Mungu, mtu huyo anayejiepusha na uovu au la. Kama mtu amekumbwa na wajibu wa kutunza sadaka, na anakutana na sadaka ya Mungu, basi unadhani kwamba hiki ni kitu ambacho Mungu amepanga? Bila shaka! Kila kitu unachokumbana nacho ni kitu ambacho Mungu amepanga. Unapokumbwa na suala hili, Mungu atakuangalia kwa siri, namna ulivyochagua, namna unavyotenda, na kile unachofikiria. Matokeo yake ya mwisho ndiyo ambayo Mungu anayajali zaidi, sababu ni matokeo ambayo yatamruhusu Yeye kupima kama umetimiza kiwango cha Mungu katika jaribio hilo au la. Hata hivyo, wakati watu wanapokumbwa na baadhi ya masuala haya, mara nyingi hawafikirii kuhusu ni kwa nini wanakumbwa na mambo hayo, au kile kiwango ambacho kinahitajika na Mungu. Hawafikirii kuhusu kile Mungu anachotaka kutoka kwao, kile Anachotaka kupata kutoka kwao. Wakati wanapokumbwa na suala hili, mtu wa aina hii anafikiria tu: “Hili ni jambo ambalo nimekumbwa nalo; lazima niwe makinifu, wala si mzembe! Haijalishi ni nini, hii ni sadaka ya Mungu na siwezi kuigusa.” Mtu huyo anasadiki kwamba anaweza kutimiza jukumu lake kupitia kufikiria huko sahili. Je, Mungu ataweza kutosheka na matokeo ya jaribio hili? Au Hatatosheka? Mnaweza kuzungumzia suala hili. (Kama mtu anamcha Mungu katika moyo wake, kisha anapokumbwa na wajibu unaomruhusu kukutana na sadaka ya Mungu, anaweza kufikiria namna ilivyo rahisi kukosea tabia ya Mungu, ili wawe na hakika ya kuendelea kwa tahadhari.) Mwitikio wako u katika njia sahihi, lakini bado haujafika. Kutembea katika njia ya Mungu hakuhusu kuangalia sheria juujuu. Badala yake, kunamaanisha kwamba unapokabiliwa na suala, kwanza kabisa, unaliangalia kama ni hali ambayo imepangwa na Mungu, wajibu uliopewa wewe na Yeye, au kitu ambacho Amekuaminia wewe, na kwamba unapokabiliana na suala hili, unapaswa kuliona kama jaribio kutoka kwa Mungu. Wakati unapokabiliwa na suala hili, lazima uwe na kiwango, lazima ufikirie kwamba suala hilo limetoka kwa Mungu. Lazima ufikirie ni vipi ambavyo utashughulikia suala hili kiasi cha kwamba unaweza kutimiza wajibu wako, na kuwa mwaminifu kwa Mungu; namna ya kulifanya bila ya kumghadhabisha Mungu; au kukosea tabia Yake. Tumetoka tu kuzungumzia kutunza sadaka. Swala hili linahusu sadaka, na linahusisha pia wajibu wako, jukumu lako. Unahitajika kuwajibikia jukumu hili. Ilhali unapokabiliwa na suala hili, kunalo jaribio lolote? Lipo! Jaribio hilo linatoka wapi? Jaribio hilo linatoka kwa Shetani, na linatoka pia kwa tabia potovu na ya uovu ya binadamu. Kwa sababu kunalo jaribio, hili linahusisha kuwa shahidi; kuwa shahidi ni jukumu na wajibu wako pia. Baadhi ya watu husema: “Hili ni suala dogo; kwa kweli linahitajika kulifanya suala hili dogo kuwa kubwa hivyo?” Ndiyo pana haja! Kwa sababu ili kutembea katika njia ya Mungu, hatuwezi kuwachilia chochote kinachotuhusu sisi wenyewe, au kinachofanyika karibu nasi, hata yale mambo madogo madogo. Haijalishi kama tunafikiria tunafaa kumakinika au la, mradi tu suala lolote linatukabili hatufai kuliacha. Lote linafaa kuonekana kama jaribio la Mungu kwetu. Mwelekeo aina hii uko vipi? Kama unao mwelekeo aina hii, basi unathibitisha hoja moja: Moyo wako unamcha Mungu, na moyo wako uko radhi kujiepusha na maovu. Kama unalo tamanio hili la kumtosheleza Mungu, basi kile unachotia katika matendo hakiko mbali na kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.
Kunao mara nyingi wale wanaosadiki kwamba masuala ambayo hayatiliwi maanani na watu, masuala ambayo kwa kawaida hayatajwi—haya ni mambo madogo tu, na hayana chochote kuhusiana na kutia ukweli katika matendo. Wakati watu hawa wanakabiliwa na suala kama hilo, hawalifikirii sana na wanaliachilia tu. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba, suala hili ni funzo ambalo unafaa kulidadisi, funzo kuhusu namna ya kumcha Mungu, namna ya kujiepusha na maovu. Zaidi, kile unachofaa kujali hata zaidi ni kujua kile Mungu anachofanya wakati suala hili linapoibuka kukabiliana na wewe. Mungu yuko kando yako, anaangalia kila mojawapo ya maneno na vitendo vyako, anaangalia hatua zako, mabadiliko ya akili zako—hii ni kazi ya Mungu. Baadhi ya watu husema: “Basi kwa nini siihisi?” Huihisi kwa sababu namna ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu haijawa ndiyo njia muhimu zaidi kwako kushughulikiwa. Hivyo basi, huwezi kuhisi kazi ngumu ya Mungu katika binadamu, inayojionyesha kulingana na fikira tofauti na vitendo tofauti vya watu. Wewe u makini! Suala kubwa ni lipi? Swala dogo ni lipi? Masuala yote yanayohusu kutembea katika njia ya Mungu hayagawanywi kwa masuala makubwa au madogo. Mnaweza kulikubali hilo? (Tunaweza kulikubali.) Kuhusiana na masuala ya kila siku, kunayo yale ambayo watu wanayaona kuwa makubwa sana na muhimu, na mengine yanaonekana kuwa mambo madogo madogo tu. Mara nyingi watu huyaona masuala haya makubwa kuwa ndiyo muhimu zaidi, na wanayachukulia kwamba yametumwa na Mungu. Hata hivyo, kwenye mkondo wa masuala haya makubwa kujitokeza, kutokana na kimo finyu cha binadamu, na kutokana na kiwango cha binadamu kisichotosha, mara nyingi binadamu haendani sawa na nia za Mungu, hawezi kupata ufunuo wowote, na hawezi kufaidi maarifa yoyote halisi yenye thamani. Kuhusu masuala madogo, haya yanapuuzwa tu na binadamu, kuachwa kuponyoka kidogokidogo. Hivyo basi, wamepoteza fursa nyingi sana za kuchunguzwa mbele ya Mungu, kujaribiwa na Yeye. Je unafaa kuwapuuza watu, masuala na hali hizi siku zote ambazo Mungu anakupangilia wewe, hii itamaanisha nini? Inamaanisha kwamba kila siku, hata kila wakati, siku zote unakana ukamilifu wa Mungu kwako, na uongozi wa Mungu. Kila Mungu anapopanga hali hizi kwako wewe, Yeye anakuangalia kwa siri, Anauangalia moyo wako, Anaziangalia fikira na hali zako, Anaangalia namna unavyofikiria wewe, Anaangalia namna unavyochukua hatua. Kama wewe ni mtu asiyejali—mtu ambaye hajawahi kujali kuhusu njia ya Mungu, neno la Mungu, au ukweli—basi hutajali, hutatilia maanani kile ambacho Mungu anataka kukamilisha, na yale ambayo Mungu anakuhitaji wewe kufanya wakati Anapopanga hali hizi kwako wewe. Hutajua pia namna ambavyo masuala haya ya kila siku yanavyohusiana na ukweli au nia za Mungu. Baada ya kukabiliana na hali nyingi kama hizi na majaribio mengi kama haya, huku naye Mungu haoni mafanikio yoyote kutokana na wewe, ataweza kuendelea vipi? Baada ya kukabiliwa na majaribio mara kwa mara, humkuzi Mungu katika moyo wako, na hushughulikii zile hali ambazo Mungu anakupangia wewe kama zilivyo—kama majaribio ya Mungu au mitihani ya Mungu. Badala yake unakataa fursa ambazo Mungu amekupa wewe moja baada ya nyingine, na unaziacha kutokomea mara kwa mara. Je huu si kutotii kwa kiwango cha juu na binadamu? (Naam, ni kutotii.) Je, Mungu atahuzunika kwa sababu ya haya? (Naam Atahuzunika.) Mungu hatahuzunika! Mkinisikia Nikiongea hivi mnashtuka kwa mara nyingine tena. Kwani umesahau, ilisemekana hapo awali kwamba Mungu huhuzunika siku zote? Mungu hatahuzunika? Ni lini basi Mungu atahuzunika? Usijali, Mungu hatahuzunika na hali hii. Basi mwelekeo wa Mungu kwa aina hii ya tabia iliyoelezwa kwa muhtasari hapo juu ni upi? Wakati watu wanapokataa majaribio, mitihani, ambayo Mungu anawapa, wakati wanapoikwepa, kunao mwelekeo mmoja tu ambao Mungu anao kwa watu kama hawa. Mwelekeo huu ni upi? Mungu husukumia mbali aina hii ya watu kutoka kina cha moyo Wake. Kunazo safu mbili za maana ya kauli “sukumia mbali”. Ninawezaje kuzielezea? Ndani kabisa ya moyo, kauli hii inao mkazo wa kuchukiza, wa chuki Na je, safu ya pili ya maana? Sasa hiyo ndiyo sehemu inayoashiria kukata tamaa dhidi ya kitu. Nyote mnajua “kukata tamaa” kunamaanisha nini, ni kweli? Kwa ufupi, kusukumia mbali kunamaanisha uamuzi na mwelekeo wa mwisho wa Mungu kwa watu wanaokuwa na mwenendo huu. Ni chuki ya kupindukia dhidi yao, maudhi, na hivyo basi uamuzi wa kuwaacha. Huu ndio uamuzi wa mwisho wa Mungu kwa mtu ambaye hajawahi kutembea katika njia ya Mungu, ambaye hajawahi kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, nyote mnaweza kuona sasa umuhimu wa msemo huu Niliouzungumzia?
Sasa mnaelewa mbinu ambayo Mungu hutumia kuasisi matokeo kwa binadamu? (Kupanga hali tofauti kila siku.) Kupangilia hali tofauti—hivi ndivyo watu wanavyoweza kuhisi na kugusa. Basi nia ya Mungu kwa haya yote ni nini? Nia ni kwamba Mungu anataka kumpa kila mmoja wetu majaribio katika njia tofauti, katika nyakati tofauti, na katika sehemu tofauti. Ni dhana zipi za binadamu zinazopimwa katika jaribio? Haijalishi kama wewe ni mtu wa aina ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katika kila suala unalokabiliwa nalo, unalosikia kuhusu, unaloliona, na unalolipitia wewe binafsi au la. Kila mmoja atakabiliwa na aina ya jaribio, kwa sababu Mungu ni mwenye haki kwa watu wote. Baadhi ya watu husema: “Nimesadiki Mungu kwa miaka mingi; inakuaje kwamba sijawahi kabiliwa na jaribio?” Unahisi hujakabiliwa na jaribio kwa sababu kila wakati Mungu amepanga hali kwako wewe, hujazichukulia hali hizo kwa umakinifu, na hujataka kutembea kwa njia ya Mungu. Hivyo basi huna kamwe hisia zozote za majaribio ya Mungu. Baadhi ya watu husema: “Nimekabiliwa na majaribio machache, lakini sijui njia bora ya kufanya mazoezi. Hata ingawa nilitenda, bado sijajua kama nilisimama imara wakati huo wa majaribio.” Watu walio na aina hii ya hali bila shaka hawamo katika kundi la walio wachache. Hivyo basi ni nini kiwango ambacho Mungu hupimia watu? Ni vile tu Nilivyosema muda mfupi uliopita: Kila kitu unachofanya, kila kitu unachofikiria, na kila kitu unachoelezea—ni kumcha Mungu na kujiepusha na uovu? Hivi ndivyo inavyobainika kama wewe ni mtu unayemcha Mungu na kujiepusha na maovu au la. Hii ni dhana rahisi? Ni rahisi mno kusema, lakini ni rahisi pia kutia katika matendo? (Si rahisi mno.) Kwa nini si rahisi mno? (Kwa sababu watu hawamjui Mungu, hawajui namna ambavyo Mungu humfanya binadamu kuwa mtimilifu, na hivyo basi wanapokabiliwa na masuala hawajui namna ya kutafuta ukweli ili kutatua tatizo lao; watu lazima wapitie majaribio mbalimbali, usafishaji, kuadibu, na hukuma kabla ya kuwa na uhalisia wa kumcha Mungu.) Mnasema hivyo, lakini kulingana na vile mnavyojua, kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kunaonekana rahisi kufanywa kwa sasa. Kwa nini Nasema hivi? Kwa sababu mmesikiliza ibada nyingi, na umepokea kiwango kingi cha kunyunyiziwa kwa uhalisia wa ukweli. Hii imewaruhusu kuelewa namna ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa mujibu wa nadharia na kufikiria. Kuhusiana na matendo yenu ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, haya yote yamekuwa yenye manufaa na kuwafanya kuhisi kwamba kitu kama hicho kinaweza kutimizika. Basi ni kwa nini katika uhalisia wa mambo watu hawajawahi kukitimiza? Hii ni kwa sababu kiini halisi cha asili ya binadamu hakimchi Mungu na kinapenda maovu. Hiyo ndiyo sababu halisi.”
Sikiliza zaidi: Neno la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni