2/13/2019

Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)" Sehemu ya Pili


Matamshi ya Mungu | "Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I Mamlaka ya Mungu (I)" Sehemu ya Pili


 Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.

Maudhui ya video hii:
Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena
Kwenye Siku ya Tano, Maisha ya Maumbo Tofauti na Pana Yaonyesha Mamlaka ya Muumba kwa Njia Tofauti
Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine
Katika Mamlaka ya Muumba, Viumbe Vyote ni Timilifu
Hakuna Kiumbe Chochote Kati ya Vile Vilivyoumbwa na Vile Ambavyo Havikuumbwa Kinaweza Kubadilisha Utambulisho wa Muumba

Soma zaidi:

Mwenyezi Mungu anasema,“Katika ulimwengu huu mpya, ambao mwanadamu bado alikuwa hajaonekana, Muumba alikuwa ametayarisha jioni na asubuhi, ile anga, ardhi na bahari, nyasi, miti isiyozaa na aina mbalimbali za miti, na nuru, misimu, siku, na miaka kwa minajili ya maisha mapya ambayo Angeumba hivi karibuni. Mamlaka na nguvu za Muumba vyote vilionyeshwa katika kila kiumbe kipya Alichokiumba, na maneno na kufanikiwa Kwake vyote vilifanyika sawia, bila ya hitilafu yoyote ndogo na bila ya kuchelewa kokote kudogo. Kujitokeza na kuzaliwa kwa viumbe hivi vyote vipya kulikuwa ithibati ya mamlaka na nguvu za Muumba: Yeye ni mzuri sawa tu na neno Lake, na neno Lake litakamilika, na kile kinachokamilika kinadumu milele. Hoja hii haijawahi kubadilika: ndivyo ilivyokuwa kale, ndivyo ilivyo leo, na ndivyo itakavyokuwa daima dawamu. Unapoyaangalia kwa mara nyingine maneno hayo ya maandiko, unahisi kwamba yangali mapya kwako? Je, umeyaona maudhui mapya, na kufanya ugunduzi mpya? Hii ni kwa sababu vitendo vya Muumba vimechangamsha moyo wako na kuongoza mwelekeo wa maarifa yako ya mamlaka na nguvu Zake, na yakakufungulia mlango wa ufahamu wa Muumba, na vitendo na mamlaka Yake vimeweza kupatia maneno haya uhai. Na kwa hivyo katika maneno haya binadamu ameona maonyesho halisi, na wazi ya mamlaka ya Muumba, na kuweza kushuhudia kwa kweli mamlaka makuu ya Muumba, na kutazama mamlaka yake yasiyokuwa ya kawaida na nguvu za Muumba.

Mamlaka na nguvu za Muumba hutoa muujiza baada ya muujiza na huvutia umakinifu wa binadamu, naye binadamu hawezi kukwepa haya ila kuyaangazia tu macho matendo haya ya kipekee yaliyozaliwa kutokana na utekelezwaji wa mamlaka husika. Nguvu zake za kipekee zafurahisha baada ya kufurahisha, na binadamu anabaki akishangaa na akijawa na furaha, naye anatweta kwa kuvutiwa, anastaajabishwa, na kushangilia; nini kingine tena, binadamu amefurahishwa kwa kumtazama alivyo, na kilichozaliwa ndani yake ni heshima, kustahi, na mtagusano wa karibu. Mamlaka na vitendo vya Muumba vinayo athari kwa roho ya binadamu na hutakasa roho ya binadamu na zaidi, kutosheleza roho ya binadamu. Kila mojawapo ya fikira Zake, kila mojawapo ya matamshi Yake, na kila ufunuo wa mamlaka Yake ni kiungo muhimu miongoni mwa viumbe vyote, na ni utekelezaji mkuu wenye thamani zaidi wa kuunda ufahamu na maarifa ya kina ya mwanadamu. Tunapohesabu kila kiumbe kilichozaliwa kutokana na matamshi ya Muumba, roho zetu zinavutiwa kwa maajabu ya nguvu za Mungu, na tunajipata tukifuata nyayo za Muumba hadi kwenye siku inayofuata: siku ya tano ya uumbaji wa Mungu wa viumbe vyote.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni