Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kusubiri. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kusubiri. Onyesha machapisho yote

10/02/2017

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashriki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kutanafusi kwa Mwenye Uweza


Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huifahamu kamwe kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako na kila kitu ambacho mwenye Uweza alikupa.