Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Roho Mtakatifu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Roho Mtakatifu. Onyesha machapisho yote

11/17/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Ni njia gani ambayo Mungu hutumia kumkamilisha mwanadamu? Ni vipengele vipi vinavyojumuishwa? Je, uko tayari kukamilishwa na Mungu? Je, uko tayari kukubali hukuma na kuadibu kwa Mungu? Unajua nini kuhusu maswali haya? Kama huwezi kuzungumzia maarifa kama haya, basi hii inaonyesha kwamba bado huijui kazi ya Mungu na hujapatiwa nuru katu na Roho Mtakatifu. Binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa. Wanaweza tu kupokea kiasi kidogo cha neema ili kufurahia kwa muda mfupi na haiwezi kuendelezwa kwa kipindi kirefu. Kama mtu hufurahia tu neema ya Mungu, hawezi kukamilishwa na Mungu.