Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 9
Katika mawazo ya watu, Mungu ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu haneni lugha ya mwanadamu, wala mwanadamu hawezi kunena lugha ya Mungu, na kwa Mungu, madai ya mwanadamu Kwake ni rahisi, ilhali matakwa ya Mungu kwa mwanadamu hayafikiki na hayafikiriki kwa mwanadamu. Ukweli, hata hivyo, ni kinyume kabisa: Mungu anataka tu "asilimia 0.1" ya mwanadamu. Hili si la kushangaza tu kwa kila mtu, lakini pia huwafanya wahisi kukanganyikiwa sana, kama kwamba wote wamechanganyikiwa.