Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu
Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu
Kama Sikushiriki kuhusu mambo haya, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeweza kutazama tabia ya kweli ya Mungu katika hadithi za Biblia. Hii ni ukweli. Hiyo ni kwa sababu, ingawaje hadithi hizi za kibiblia zilirekodi baadhi ya mambo ambayo Mungu alifanya, Mungu aliongea mambo machache na hakuitambulisha tabia Yake kwa njia ya moja kwa moja au kuwasilisha mbele waziwazi mapenzi Yake kwa binadamu.