7/03/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu


Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu

Kama Sikushiriki kuhusu mambo haya, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeweza kutazama tabia ya kweli ya Mungu katika hadithi za Biblia. Hii ni ukweli. Hiyo ni kwa sababu, ingawaje hadithi hizi za kibiblia zilirekodi baadhi ya mambo ambayo Mungu alifanya, Mungu aliongea mambo machache na hakuitambulisha tabia Yake kwa njia ya moja kwa moja au kuwasilisha mbele waziwazi mapenzi Yake kwa binadamu. Vizazi vya baadaye vimechukulia rekodi hizi kama tu hadithi, na hivyo yaonekana kwa watu kwamba Mungu anajificha kutoka kwa binadamu na kwamba si mwili wa Mungu ambao umefichwa kutoka kwa binadamu, lakini tabia na mapenzi Yake. Baada ya ushirika wangu leo, bado unahisi kwamba Mungu amefichwa kabisa kutoka kwa binadamu? Bado unasadiki kwamba tabia ya Mungu imefichwa kutoka kwa binadamu?
Tangu wakati wa uumbaji, tabia ya Mungu imeenda sako kwa bako na kazi Yake. Haijawahi kufichwa kutoka kwa binadamu, lakini imewekwa kadamnasi na kwa dhahiri kabisa kwa binadamu. Ilhali, kwa kadri muda unavyopita, moyo wa binadamu umekua hata mbali zaidi na Mungu, na kwa kuwa upotovu wa mwanadamu umekuwa wa kina zaidi, binadamu na Mungu wamekuwa mbali na mbali zaidi kati yao. Kwa utaratibu lakini kwa uhakika, binadamu ametoweka kutoka kwa macho ya Mungu. Binadamu ameshindwa kuweza “kuona” Mungu, jambo ambalo limemwacha yeye bila “habari” zozote kuhusu Mungu; hivyo, hajui kama Mungu yupo, na hata anaenda mbali mno kiasi cha kukataa kabisa kuwepo kwa Mungu. Kwa hivyo, kutofahamu kwa binadamu kuhusu tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho si kwa sababu Mungu amefichwa kutoka kwa binadamu, lakini kwa sababu moyo wake umemgeukia Mungu. Ingawaje binadamu anamsadiki Mungu, moyo wa binadamu haupo na Mungu, na hajui chochote kuhusu namna ya kumpenda Mungu, wala hataki kumpenda Mungu, kwani moyo wake haujawahi kusonga karibu na Mungu na siku zote anamuepuka Mungu. Kutokana na haya, moyo wa binadamu umekuwa mbali sana na Mungu. Kwa hivyo moyo wake uko wapi? Kwa hakika, moyo wa binadamu haujaenda popote: Badala ya kuupatia moyo huo Mungu, au kuufichua kwa Mungu ili Aweze kuuona, amejiekea yeye mwenyewe. Hiyo ni licha ya ukweli kwamba baadhi mara nyingi wanamwomba Mungu na kusema, “Ee Bwana, utazame moyo wangu—unajua yote ninayofikiria,” na baadhi hata huapa kumruhusu Mungu kuwafikiria, kwamba waweze kuadhibiwa kama watavunja kiapo chao. Ingawaje binadamu anamruhusu Mungu kuangalia ndani ya moyo wake, hii haimanishi kwamba anaweza kutii mipango na mipangilio ya Mungu, wala kwamba ameacha hatima na matarajio yake na mambo yake yote katika udhibiti wa Mungu. Hivyo, licha ya viapo unavyotoa kwa Mungu au mwelekeo kwake Yeye, kwa macho ya Mungu moyo wako ungali umefungwa kwake Yeye, kwani unamruhusu Mungu tu kuangalia kwenye moyo wako lakini humruhusu Yeye kuudhibiti. Kwa maneno mengine, hujampa Mungu moyo wako kamwe, na unazungumza tu maneno yanayosikika kuwa matamu ili Mungu asikie; nia zako mbalimbali za kijanja, huku, unajificha kutoka kwa Mungu, unajificha usionekane na Mungu, pamoja na maajabu, njama, na mipango yako, na unashikilia matarajio na hatima yako mikononi mwako, ukiwa na hofu kubwa kwamba huenda yakachukuliwa na Mungu. Hivyo, Mungu hatazamii uaminifu wa binadamu kwake Yeye. Ingawaje Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, na Anaweza kuona kile ambacho binadamu anafikiria na anataka kufanya moyoni mwake, na Anaweza kuona ni mambo yapi yamewekwa ndani ya moyo wake, moyo wa binadamu haumilikiwi na Mungu, hajautoa ili udhibitiwe na Mungu. Hivi ni kusema, Mungu anayo haki ya kuangalia, lakini Hana haki ya kuudhibiti moyo huo. Kwenye nadharia za kibinafsi za binadamu, binadamu hataki wala hanuii kujiacha kwenye huruma za Mwenyezi Mungu. Binadamu hajajifungia tu kutoka kwa Mungu, bali kunao hata watu wanaofikiria njia za kusetiri mioyo yao, kwa kutumia mazungumzo matamu na sifa za kinafiki ili kuunda hali ya uongo na kupata uaminifu wa Mungu, na kuficha uso wao wa kweli dhidi ya kuonekana na Mungu. Nia yao ya kutomruhusu Mungu kuona ni kutoruhusu Mungu kuelewa namna walivyo kwa kweli. Hawataki kuitoa mioyo yao kwa Mungu lakini wanajihifadhia wao wenyewe. Maandishi madogo ya haya ni kwamba kile ambacho binadamu anafanya na kile ambacho anataka kimepangiliwa chote, kikapigiwa hesabu, na kuamuliwa na binadamu mwenyewe; haihitaji kushiriki au kuingilia kati kwa Mungu, na isitoshe hahitaji mipango na mipangilio ya Mungu. Hivyo, iwapo ni kuhusiana na amri za Mungu, agizo Lake, au mahitaji ambayo Mungu anamwekea binadamu, uamuzi wa binadamu unatokana na nia na maslahi yake mwenyewe, katika mazingira na hali yake mwenyewe ya wakati huo. Siku zote binadamu anatumia maarifa na maono ambayo amezoeana nayo, na akili zake binafsi ili kuamua na kuchagua njia anayofaa kutembelea na haruhusu uingiliaji kati au udhibiti wa Mungu. Huu ndio moyo wa binadamu ambao Mungu anaona.
Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona, anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye. Tangu Alipoanza kusimamia, Mungu amekuwa akisubiria binadamu kumpa moyo wake, kumwacha Mungu kuutakasa na kuufaa ipaswavyo, kumfanya yeye kumtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu, kumfanya yeye kumstahi Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu amewahi kutazamia mbele na kusubiria matokeo haya. Kunao watu kama hawa miongoni mwa rekodi za Biblia? Yaani, kunao wowote kwenye Biblia wanaoweza kutoa mioyo yao kwa Mungu? Kunaye yeyote anayetangulia kabla ya enzi hii? Leo, hebu tuendelee kusoma simulizi za Biblia na kuangalia kama kile kilichofanywa na mhusika huyu—Ayubu—kina muunganisho wowote na mada ya “kumpa Mungu moyo wako” ambalo tunazungumzia kuhusu leo. Hebu tuone kama Ayubu alimtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu.
Maoni yako ni yapi kuhusu Ayubu? Wakitolea mifano ya maandiko asilia, baadhi ya watu husema kwamba Ayubu “alimcha Mungu na kujiepusha na maovu.” “Alimcha Mungu na kujiepusha na maovu: Huo ndio ukadiriaji mojawapo asilia wa Ayubu uliorekodiwa kwenye Biblia. Kama uliyatumia maneno yako binafsi, unawezaje kumzungumzia Ayubu? Baadhi ya watu wanasema kwamba Ayubu alikuwa binadamu mzuri mwenye busara, baadhi wanasema kwamba alikuwa na imani ya kweli kwa Mungu; baadhi wanasema kwamba Ayubu alikuwa binadamu mwenye haki na utu. Mmeiona imani ya Ayubu, hivi ni kusema, katika mioyo yenu mnaambatisha umuhimu mkubwa kwa na mnaionea wivu imani ya Ayubu. Leo, basi, hebu tuzungumzie kile kilichomilikiwa na Ayubu ambacho Mungu anafurahishwa sana naye. Kisha, hebu tusome maandiko yaliyo hapa chini.
C. Ayubu
1. Ukadiriaji wa Ayubu na Mungu na kwenye Biblia
(Ayubu 1:1) Palikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, jina lake aliitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu .
(Ayubu 1:5) Na ilikuwa hivyo, hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote.
(Ayubu 1:8) Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?
Ni nini hoja kuu unayoiona kwenye vifungu hivi? Vifungu hivi vitatu vifupi vya maandiko vyote vinahusu Ayubu. Ingawaje ni vifupi, vinaelezea waziwazi alikuwa mtu wa aina gani. Kupitia kwa ufafanuzi wake kuhusu tabia ya kila siku ya Ayubu na mwenendo wake, vinaelezea kila mmoja kwamba, badala ya kukosa msingi, ukadiriaji wa Mungu ya Ayubu ulikuwa na msingi wake na ulikuwa umekita mizizi. Vinatuambia kwamba iwapo ni utathmini wa binadamu kuhusu Ayubu (Ayubu 1:1), au utathmini wa Mungu kuhusu yeye (Ayubu 1:8), tathmini zote zinatokana na matendo ya Ayubu mbele ya Mungu na binadamu (Ayubu 1:5)
Kwanza, hebu tukisome kifungu nambari moja: “Palikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, jina lake aliitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.” Ukadiriaji wa kwanza wa Ayubu kwenye Biblia, sentensi hii ndiyo utathmini wa mwandishi kuhusu Ayubu Kiasili, unawakilisha pia ukadiriaji wa binadamu kuhusu Ayubu, ambayo ni “mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu” Kisha, hebu tuusome utathmini wa Mungu kuhusu Ayubu: “kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu” (Ayubu 1:8). Kati ya tathmini hizi mbili, moja ilitoka kwa binadamu, na nyingine ikatoka kwa Mungu; ni ukadiriaji aina mbili ulio na maudhui moja. Inaweza kuonekana, basi, kwamba tabia na mwenendo wa Ayubu ulijulikana kwa binadamu, na pia ulisifiwa na Mungu. Kwa maneno mengine, mwenendo wa Ayubu mbele ya binadamu na mwenendo wake mbele ya Mungu ulikuwa sawa; aliweka tabia yake na motisha yake mbele ya Mungu siku zote, ili hivi viwili viweze kuangaliwa na Mungu, na yeye alikuwa mmoja aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hivyo, katika macho ya Mungu, kati ya watu duniani, ni Ayubu tu ambaye alikuwa mtimilifu na mnyofu, ndiye aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu
...

Juni 13, 2014

Tanbihi:
a. Maandishi asilia yanasoma “vitendo.”
b. Maandishi asilia yameacha “kichwa cha.”
c. Maandishi asilia yameacha “kupotezwa kwa.”
d. Maandishi asilia yameacha “ yaliyokuwa yameenda.”
e. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni