11/10/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Mwenyezi Mungu,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho


Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho? Hakuna kati yenu aliye wazi sana juu ya hili. Maisha ya kawaida ya kiroho hayakomi tukwa ombi, wimbo, maisha ya kanisa, kula na kunywa maneno ya Mungu, na matendo mengine kama haya, bali yana maana ya kuishi maisha ya kiroho yaliyo mapya na ya kusisimua. Siyo kuhusu mbinu, lakini matokeo. Watu wengi sana wanafikiri kwamba ili kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho lazima mtu asali, aombe, ale na anywe maneno ya Mungu, au kujaribu kuelewa maneno ya Mungu.

11/09/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje


Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Uhusiano wa kawaida na Mungu unamaanisha kuweza kutoshuku au kukataa kazi yoyote ya Mungu na kutii, na zaidi ya hayo unamaanisha kuwa na nia sahihi mbele ya Mungu, sio kufikiria kujihusu, daima kuwa na maslahi ya familia ya Mungu kama jambo muhimu zaidi haijalishi kile unachofanya, kukubali kutazamiwa na Mungu, na kukubali mipangilio ya Mungu.

11/08/2018

"Kubisha Hodi Mlangoni" (2) - Ni Makosa Gani Ambayo Hufanyika kwa Urahisi Zaidi Katika Kumkaribisha Bwana

 

Utambulisho

    Watu wengi wa imani katika jamii za kidini wanaamini kile wachungaji na wazee wa kanisa wanachokisema, "Maneno na kazi zote za Mungu ziko katika Biblia. Haiwezekani kwa maneno yoyote ya Mungu kuonekana nje ya Biblia." Je, kuna msingi wa kibiblia wa dai hili, hata hivyo? Je, Bwana Yesu aliyasema maneno haya? Katika Ufunuo, imetabiriwa mara nyingi, "Yeye aliye na sikio, na asikie lile Roho anayaambia makanisa." Maneno ya Bwana yanalisema kwa dhahiri sana: Wakati Bwana atarudi katika siku za mwisho, Atanena tena. Katika suala la kuukaribisha ujio wa Bwana, tusipoondoka kwa Biblia na kutafuta anachokisema Roho kwa makanisa, tutaweza kumkaribisha Bwana?

Tazama Video: Umeme wa Mashariki Sinema za Injili, Filamu za Injili

11/07/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Mwenyezi Mungu anasema, "Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu ameamulia kabla watu wengi kumhudumia Yeye, wakiwemo watu kutoka kila nyanja ya maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake Mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni imetimia. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia Yeye. Kila mtu anayehudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na uweza wa Mungu, pamoja na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni. Mungu huja hapa ulimwenguni kimatendo ili kufanya kazi Yake na kuwasiliana na watu ili nao waweze kuona vizuri zaidi matendo Yake. Leo, ni bahati kubwa kwa kundi hili lenu kumhudumia Mungu wa vitendo.

11/06/2018

“Kubisha Hodi Mlangoni” (1) - Ni Desturi Gani Muhimu Zaidi ya Kuukaribisha Ujio wa Bwana


Utambulisho

  Bwana Yesu alisema, "Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata" (Yohana 10:27). Pia imetabiriwa mara nyingi katika Ufunuo, "Yeye aliye na sikio, na asikie lile Roho anayaambia makanisa." Sauti na maneno ya Roho ni sauti ya Bwana, na ni kondoo wa Mungu mbao watatambua sauti ya Mungu. Ni tendo gani, basi, lililo muhimu kwa Wakristo wanapoukaribisha ujio wa Bwana?

      Tazama Video: Umeme wa Mashariki Sinema za Injili, Filamu za Injili

11/05/2018

"Wakati wa Mabadiliko"(2) - Njia ya Pekee ya Kuinuliwa Kwenda Katika Ufalme wa Mbinguni



    Utambulisho

   Watu wengine huamini, kwa kuwa Mungu aliweza kuumba mbingu na dunia na vitu vyote kwa neno moja, kuweza kuwafufua wafu kwa neno moja, Mungu pia Ataweza kubadili taswira zetu mara moja, kutufanya watakatifu, kutuinua hewani kukutana na Bwana wakati Atakaporudi katika siku za mwisho. Je, kweli ni ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni? Je, kazi ya kurudi kwa Mungu katika siku za mwisho rahisi hivyo jinsi tunavyofikiri?

Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?


Swahili Christian Skit "Mipaka ya Meya wa Kijiji" | Why Is There No Religious Freedom in China?



    Utambulisho

    Mchezo mfupi Mipaka ya Meya wa Kijiji inaeleza hadithi ya kweli ya mume na mke Wakristo ambao wanalazimishwa kutoroka kwa sababu ya mateso ya serilaki ya CCP.
    
    Mkristo Liu Ming'en anahukumiwa na CCP miaka saba gerezani kwa kuamini katika Mungu. Hata baada ya kuachiliwa kutoka gerezani, anabakia kuwa wakulengwa na uchunguzi mkali wa CCP. Meya wa kijiji anatumia mfumo wa wajibu wa kaya-tano , kamera za usalama, ziara za nyumba, na njia nyingine kumzuia Liu Ming'en na mkewe kuamini katika Mungu, lakini hakuna inayoleta na matokeo yanayotakiwa.