12/07/2018

Neno la Mwenyezi Mungu|Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Roho Mtakatifu

Neno la Mwenyezi Mungu|Kuhusu Kila Mmoja Kutekeleza Wajibu Wake


 Katika mkondo wa sasa, kila mtu anayempenda Mungu kwa kweli ana fursa ya kukamilishwa na Yeye. Bila kujali kama yeye ni kijana au mzee, mradi tu anatazamia kwa hamu kumtii Mungu na kumheshimu Yeye, wataweza kukamilishwa na Yeye. Mungu huwakamilisha watu kulingana na kazi zao tofauti. Mradi tu umefanya yote kwa nguvu yako na kuitii kazi ya Mungu utakuwa na uwezo wa kukamilishwa na Yeye.

12/06/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mustakabali

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali?


Je, unaweza kuonyesha tabia ya Mungu ya nyakati kwa lugha inayofaa iliyo na umuhimu wa nyakati? Kupitia uzoefu wako wa kazi ya Mungu, unaweza kueleza kwa undani tabia ya Mungu? Utaielezaje vizuri, kikamilifu? Ili kupitia haya, watu wengine wapate kufahamu uzoefu wako. Utawezaje kupitisha uliyoyaona na kupitia kwa maskini hawa wa kuhurumiwa, na waumini wa kidini wa kumcha Mungu waliojitolea na waliojawa na njaa na kiu cha haki na wanaongoja uwe mchungaji wao?

12/05/2018

New Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa" | Bwana Yesu Kristo Atarudi Vipi?


New Swahili Gospel Movie "Siri ya Utauwa" | Bwana Yesu Kristo Atarudi Vipi?

Utambulisho

Lin Bo'en alikuwa mzee wa kanisa katika kanisa la nyumbani Uchina. Wakati wa miaka yake yote kama muumini, alihisi kwamba ameheshimiwa kuteseka kwa ajili ya Bwana, na alithamini kumfahamu na kumpata Bwana Yesu Kristo zaidi ya kitu kingine chochote duniani. Siku moja ya jaala, alienda nje kuhubiri na akasikia habari fulani za kushtua: Bwana Yesu amerudi katika mwili, na Yeye ni Kristo wa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu! Lin Bo'en alikanganyikiwa. Wakati Bwana atarudi, Anatakiwa kushuka na mawingu, kwa hiyo angejipatiaje mwili na kufanya kazi Yake kwa siri? Ni siri gani zilifichwa katika kupata mwili kwa Mungu? Ikiwa Bwana amerudi kweli, kwa nini hatujanyakuliwa? … Mjadala mkali sana unajitokeza kati ya Lin Bo'en na wafanyakazi wenzake na wahubiri kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu … Je, hatimaye wataweza kuelewa kwamba Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu, kuonekana kwa Mungu katika mwili?

Masomo yanayohusiana: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kurudi kwa Yesu mara ya pili

12/04/2018

Worship and Praise Dance | "Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu" | The Kingdom of Christ Is Paradise for the Honest (Swahili Subtitles)

Worship and Praise Dance | "Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu" | The Kingdom of Christ Is Paradise for the Honest (Swahili Subtitles)


Safi na mwaminifu kama mtoto, asiye na hatia na mchangamfu, aliyejawa na nguvu za ujana,
wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni.
Hakuna uongo, udanganyifu au hadaa, na moyo ulio wazi na mwaminifu, wanaishi na heshima.
Wanaitoa mioyo yao kwa Mungu, Mungu anawaamini, na wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda.
Wale wanaopenda ukweli wote wana mioyo ya uaminifu.
Watu waaminifu hufurahia kutenda ukweli, na kwa kumtii Mungu mioyo yao ina amani.
Wanamcha Mungu, wanaepuka maovu na wanaishi kulingana na maneno ya Mungu.
Wanaishi katika maneno ya Mungu na wamewekwa huru na kuachiliwa.
Wanakubali uchunguzi wa Mungu na kuishi mbele Yake. Kumpenda Mungu ni kuwa na furaha na mwenye shangwe.

12/03/2018

Wimbo Mpya wa Dini "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu" | Have You Enjoyed the Joy of Gaining the Work of the Holy Spirit? (Official Video)


Wimbo Mpya wa Dini "Unapoufungua Moyo Wako kwa Mungu"

Wakati hamumwelewi Mungu na hamjui asili Yake,

mioyo yenu haiwezi kamwe kufunguka, kufungukia Mungu.

Mara utakapomwelewa Mungu wako, utaelewa kilicho moyoni Mwake,

na kufurahia kilicho ndani Yake kwa imani na usikivu wako wote.

Unapofurahia kile kilicho ndani ya moyo wa Mungu, kidogo kidogo, siku baada ya siku,

unapofurahia kile kilicho ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utakuwa wazi Kwake.

12/02/2018

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu


Kufahamu kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mtu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia.

12/01/2018

Swahili Christian Sketch "Onyo Kutoka kwa Historia" (Kichekesho)


Swahili Christian Sketch "Onyo Kutoka kwa Historia" (Kichekesho)


Miaka elfu mbili iliyopita, wakati Bwana Yesu alipotokea na kufanya kazi, Mafarisayo walikwamia sheria na kukashifu kazi Yake, wakisema kuwa kazi Yake ilienda zaidi ya Maandiko.Ili kulinda hali zao na maisha yao, walijitahidi kwa nguvu zao zote ili kuwazuia watu kutafuta kazi ya Bwana Yesu, na kujiunga na serikali ya Kirumi kumsulubisha msalabani. Katika siku za mwisho, wakati Bwana Yesu anapoonekana tena katika mwili ili kufanya kazi, viongozi wa ulimwengu wa kidini wanarudia tukio la janga la kihistoria la upinzani wa Mafarisayo kwa Bwana Yesu. Je, wanapingaaje kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Kupitia kwa mchungaji anayeigiza kama Mfarisayo katika tukio, mchezo huu unadhihirisha jinsi wachungaji na wazee wa kisasa wanavyoshikilia Biblia ili kumpinga Mungu, na inaonyesha wazi kwamba njia wanayoitembea ni sawa na ile ya Mafarisayo.

Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?