4/10/2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Pili


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Pili


Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu ni Bwana wa kanuni zinazoudhibiti ulimwengu, Anadhibiti kanuni zinazoongoza kuishi kwa vitu vyote, na pia Anadhibiti ulimwengu na vitu vyote kiasi kwamba vinaweza kuishi pamoja; Anaifanya ili kwamba visikwishe au kutoweka ili kwamba binadamu aendelee kuishi, binadamu anaweza kuishi katika mazingira hayo kupitia uongozi wa Mungu.

4/07/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Pili


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Pili 


Mwenyezi Mungu anasema, “Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno ambalo amesema na kila kitendo amefanya kinahusiana na ukweli. Ukweli huu na maneno haya sio tu ndoto isiyo na msingi, lakini bali yake yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake.

4/06/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu (II)” Sehemu ya Kwanza


Mwenyezi Mungu anasema, “Ni kwa sababu watu wanaishi miongoni mwa tabia potovu na wanaishi katika dunia ya uovu na uchafu. Kila kitu wanachoona, kila kitu wanachogusa, kila kitu wanachopitia ni uovu wa Shetani na upotovu wa Shetani na pia kufanya mipango, kupigana wenyewe kwa wenyewe, na vita vinavyotokea miongoni mwa watu walio chini ya ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, hata wakati Mungu anafanya kazi Yake kwa watu, na hata wakati Anazungumza nao na kufichua tabia na kiini Chake hawawezi kuona ama kujua utakatifu na kiini cha Mungu ni nini.

4/03/2019

Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza


Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Uzito wa Matokeo katika Mioyo ya Watu
Imani za Watu Haziwezi Kubadilishwa na Ukweli
Kunayo Maoni Mengi Yanayohusu Kiwango Ambacho Mungu Hutumia Kuasisi Matokeo ya Binadamu

4/01/2019

Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance


Wimbo wa Kuabudu | “Wale Wanaompenda Mungu kwa Dhati Wote ni Watu Waaminifu” | Kids Dance


Safi na mwaminifu, kama mtoto bila hatia,
mchangamfu na mwenye nguvu za ujana,
wao ni kama malaika wanaokuja ulimwenguni.
Bila udanganyifu, na mioyo iliyo wazi tu, wao ni waadilifu.
Wanatoa mioyo yao kwa Mungu na kupata imani Yake.
Wao ni watu waaminifu ambao Mungu anapenda.
Kuacha maneno ya Mungu yatuongoze kila siku,
tumebarikiwa na Roho Mtakatifu anatuongoza.

3/31/2019

Neno la Mungu | Sura ya 34

Mwenyezi Mungu ni mwenye nguvu zote , mwenye kutimiliza yote na Mungu wa kweli kabisa! Habebi tu nyota saba, ana Roho saba, ana macho saba, anafungua mihuri saba na kufungua hati ya kukunja yenye maandishi, lakini zaidi ya hayo Yeye anaendesha mapigo saba na vikasa saba na kufungua radi saba; zamani za kale Yeye alipiga vinumbi saba! Vitu vyote vilivyoumbwa na kufanywa kuwa kamili na Yeye vinapaswa kumsifu, kumpa adhama na kutukuza kiti Chake cha enzi. Ee, Mwenyezi Mungu! Wewe ni kila kitu, Wewe umetimiza kila kitu, na kila kitu kinakamilika na Wewe, vyote vinang’aa, vyote vimekombolewa, vyote viko huru, vyote viko imara na vyenye nguvu! Hakuna chochote kilichofichwa wala kufungwa, na Wewe mafumbo yote yanafumbuliwa.

3/30/2019

Neno la Mungu | Sura ya 33

Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo safi na waaminifu duniani hawapendwi na watu? Mimi ni kinyume kabisa cha jinsi ilivyo. Inakubalika kwa watu waaminifu kuja Kwangu; Nafurahia mtu wa aina hii, pia Ninamhitaji mtu wa aina hii. Hii ni haki Yangu hasa. Watu wengine ni wajinga; hawawezi kuhisi kazi ya Roho Mtakatifu na hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu. Hawawezi kuona familia yao na hali zinazowazingira kwa uwazi, wanafanya vitu bila kufikiri na kupoteza fursa nyingi za neema. Mara kwa mara wanajuta matendo yao na wanapokabiliwa na jambo, tena hawawezi kuliona kwa uwazi.