Matamshi ya Mungu | “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” Sehemu ya Kwanza
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Uzito wa Matokeo katika Mioyo ya Watu
Imani za Watu Haziwezi Kubadilishwa na Ukweli
Mwenyezi Mungu anasema:
Imani za Watu Haziwezi Kubadilishwa na Ukweli
Kunao baadhi ya watu wanaoweza kuvumilia ugumu; wanaweza kulipia bei; tabia yao ya nje ni nzuri sana; wanaheshimika sana; na wanatamaniwa na wengine. Mnafikiria nini: Je, tabia kama hii ya nje inaweza kuchukuliwa kama ya kutia ukweli katika matendo? Mnaweza kusema kwamba mtu huyu anatosheleza nia za Mungu? Kwa nini mara kwa mara watu wanamwona mtu wa aina hii na kufikiria kwamba wao wanamtosheleza Mungu, wanafikiria kwamba wanatembelea njia ile ya kutia ukweli katika matendo, kwamba wanatembea katika njia ya Mungu? Kwa nini baadhi ya watu hufikiria kwa njia hii? Upo ufafanuzi mmoja tu kwa haya. Na ufafanuzi huu ni upi? Sababu ni kwamba kwa kiasi kikubwa cha watu, maswali kama kutia ukweli katika matendo ni nini, kutosheleza Mungu ni nini, ni nini kuwa na uhalisia wa ukweli—maswali haya hayako wazi sana. Hivyo basi kunao baadhi ya watu ambao mara nyingi wanadanganywa na wale ambao kwa nje wanaonekana wa kiroho, wanaonekana wa kilodi, wanaonekana kuwa na taswira za ukuu. Kuhusiana na watu hao wanaoweza kuzungumzia barua na falsafa, na ambao hotuba na vitendo vyao vinaonekana kuwa vyenye kustahili uvutiwaji, wale wanaowatamani hawajawahi kuangalia kiini halisi cha vitendo vyao, kanuni zinazoendesha vitendo vyao, shabaha zao ni nini. Na hawajawahi kuangalia kama watu hawa wanatii Mungu kwa kweli, na kama wao ni watu wanaomcha Mungu kwa kweli na kujiepusha na uovu au la. Hawajawahi kutambua kile kiini halisi cha ubinadamu cha watu hawa. Badala yake, kutoka kwenye hatua ya kwanza ya kujua na kuzoeana nao, hatua kwa hatua wanaanza kuwapenda watu hawa, kuwatukuza watu hawa, na hatimaye watu hawa wanakuwa sanamu zao. Aidha, katika akili za baadhi ya watu, sanamu hizi wanazoziabudu, wanaosadiki wanaweza kuacha familia na kazi zao, na kulipa ile bei kwa juujuu—sanamu hizi ndizo ambazo kwa kweli zinatosheleza Mungu, ndizo zile zinazoweza kupokea kwa kweli matokeo mazuri na hatima nzuri. Katika akili zao, sanamu hizi ndizo wale watu ambao Mungu husifu. Ni nini husababisha watu kuwa na aina hii ya kusadiki? Ni nini kiini halisi cha suala hili? Ni nini matokeo hali hii inaweza kuleta? Hebu na tuzungumzie kwanza suala la kiini chake halisi.
Soma Zaidi: APP ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni