Maneno ya Mungu | Sura ya 59
Tafuta mapenzi Yangu zaidi katika mazingira unayoyakabili na kwa hakika utapata kibali Changu. Ilmradi uwe tayari kwenda katika utafutaji na kuhifadhi moyo ambao unanicha, Mimi Nitakupea yote unayokosa. Kanisa sasa linaingia utendaji rasmi na mambo yote yanaingia kwenye alama sahihi. Mambo hayako yalivyokuwa wakati mlipokuwa na limbuko la mambo yajayo. Lazima msiwe wa kuchanganyikiwa au kuwa bila utambuzi.