Mwenyezi Mungu anasema, "Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho."
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja” (Luka 12:40).
“Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa” (Mathayo 24:37).
“Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia” (Mathayo 24:27).
“Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24-25).
“Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha” (Mathayo 25:6).
“Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).
“Na nikapinduka ili kuiona sauti hiyo iliyonizungumzia. Na baada ya kupinduka, nikatazama vinara saba vya taa vilivyokuwa vya dhahabu; Na hapo katikati ya hivyo vinara saba vya taa nilimwona mtu aliyefanana na Mwana wa Adamu, aliyekuwa amevalia nguo iliyofika katika miguu yake, na kifuani alikuwa amefungwa kanda ya dhahabu. Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye” (Ufunuo 1:12-16).
Maneno Husika ya Mungu:
Yesu alisema kwamba Angewasili kama Alivyoondoka, lakini unajua maana halisi ya maneno Yake? Je, angeweza kwa kweli kukwambia? Unajua tu kwamba Atawasili kama Alivyoondoka juu ya wingu, lakini unajua hasa jinsi Mungu Mwenyewe hufanya kazi Yake? Ikiwa ungeweza kuona kweli, basi maneno ya Yesu yanapaswa kuelezwa vipi?
Alisema: Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika siku za mwisho, Yeye Mwenyewe hatajua, malaika hawatajua, wajumbe wa mbinguni hawatajua, na watu wote hawatajua. Baba tu ndiye atakayejua, yaani, Roho pekee ndiye atajua Hata Mwana wa Adamu Mwenyewe hajui, lakini wewe unaweza kuona na kujua? Ikiwa ungekuwa na uwezo wa kujua na kuona kwa macho yako mwenyewe, je, maneno hayo hayakusemwa bure? Na Yesu alisema nini wakati huo? “Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa. Basi kutakuwa na watu wawili shambani; mmoja wao atachukuliwa, na mwingine kuachwa. … Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu.” Wakati siku hiyo itakapofika, Mwana wa Adamu Mwenyewe hataijua. Mwana wa Adamu inahusu umbo la Mungu lililopata mwili wa Mungu, ambaye atakuwa mtu wa kawaida. Hata Mwana wa Adamu mwenyewe hajui, kwa hiyo wewe ungejuaje?
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili