Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III
Mamlaka ya Mungu (II)
Leo tutaendelea na ushirika wetu kuhusu mada ya “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee.” Tayari tumekuwa na ushirika mara mbili katika mada hii, wa kwanza kuhusiana na mamlaka ya Mungu na wa pili kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu. Baada ya kusikiliza ushirika huu mara mbili, je, mmepata ufahamu mpya wa utambulisho wa Mungu, hadhi, na hali halisi? Je, maono haya yamewasaidia kufikia maarifa mazito zaidi na uhakika wa ukweli kuuhusu uwepo wa Mungu? Leo Ninapanga kufafanua mada hii ya “Mamlaka ya Mungu.”
Kuelewa Mamlaka ya Mungu Kutoka kwa Mitazamo Mikubwa na Midogo
Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka. Hivyo ni kusema kwamba, ni Muumba tu—Mungu Yule wa Kipekee—ambaye anaonyeshwa kwa njia hii na ndiye aliye na hali halisi hii. Kwa nini tuzungumzie mamlaka ya Mungu? Mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanatofautiana vipi na mamlaka yaliyomo kwenye akili ya binadamu? Ni nini maalum sana kuyahusu? Na kunao umuhimu gani haswa kuyazungumzia hapa? Kila mmoja wenu lazima aweze kutilia maanani kwa umakinifu suala hili. Kwa watu wengi zaidi, “Mamlaka ya Mungu” ni fikira isiyoeleweka, ile ambayo ni ngumu sana kupata kuielewa, na mazungumzo yoyote kuihusu huenda yasizae matunda mazuri. Kwa hivyo lazima kutakuwepo na pengo kati ya maarifa ya mamlaka ya Mungu ambayo binadamu anaweza kumiliki, na hali halisi ya mamlaka ya Mungu. Ili kuliziba pengo hili, mtu lazima kwa utaratibu aweze kuelewa mamlaka ya Mungu kwa njia ya watu halisi-maishani, matukio, vitu au mambo muhimu yanayopatikana katika uwezo wa binadamu, na ambayo binadamu wanaweza kuyaelewa. Ingawaje kauli hii “Mamlaka ya Mungu” inaweza kuonekana kama isiyoeleweka, mamlaka ya Mungu kwa kweli si ya dhahania kamwe. Yeye yupo na binadamu kila dakika ya maisha yake, akimwongoza kila siku. Kwa hivyo, katika maisha ya kila siku ya kila mtu ataweza haswa kuona na kupitia dhana halisi ya mamlaka ya Mungu. Uhalisi huu ni ithibati tosha kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo, na unakuruhusu kabisa kutambua na kuelewa hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya.
Mungu aliumba kila kitu, na baada ya kukiumba, Anao utawala juu ya kila kitu. Kuongezea kuwa na utawala juu ya kila kitu, pia anadhibiti kila kitu. Wazo hili linamaanisha nini “Mungu anadhibiti kila kitu”? Hali hii inaweza kuelezewa vipi? Hali hii inatumika vipi katika maisha halisi? Mnawezaje kuyajua mamlaka ya Mungu kwa kuelewa hoja hii kwamba “Mungu Anadhibiti kila kitu”? Kutoka kwenye kauli ile ile “Mungu anadhibiti kila kitu” tunafaa kuona kwamba kile ambacho Mungu anadhibiti si sehemu ya sayari, sehemu ya uumbaji, wala sehemu ya mwanadamu, lakini kila kitu: kuanzia kwa viumbe vile vikubwa hadi vile vidogovidogo, kuanzia kwa vile vinavyoonekana hadi visivyoonekana, kuanzia kwa nyota ulimwenguni hadi kwenye vitu vilivyo na uhai ulimwenguni, pamoja na viumbe vidogovidogo visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida au viumbe vilivyo katika maumbo mengine. Huu ndio ufafanuzi hakika wa “kila kitu” ambacho Mungu “anadhibiti,” na ndio upana ambao Mungu anaonyesha ukuu Wake, urefu wa utawala na kanuni Yake.
Kabla ya binadamu hawa kujitokeza, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa uwepo wavyo wote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata ruwaza maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data yenye uhakika; njia ambazo zinasafiria, kasi na ruwaza ya mizingo yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa hakika na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kupotoka hata chembe. Hakuna nguvu inaweza kubadilisha au kutatiza mizingo yazo au ruwaza zao ambazo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum zinazotawala mzunguko wazo na data yenye uhakika inayozifafanua iliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu ruwaza fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje binadamu hawakubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na ruwaza zinazoonyesha mzunguko wavyo, vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Hoja hii inampa binadamu mshawasha wa kukubaliana na kutambua kwamba kunaye Mwenyezi aliye miongoni mwa ruwaza hizi za mzunguko, anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei-kimaumbile lakini zinaamrishwa na Bwana na Mungu. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.
Kwenye kiwango cha mambo madogomadogo, milima, mito, maziwa, bahari, na maeneo ya ardhi yote ambayo binadamu anatazama nchini, misimu yote ambayo yeye anapitia, mambo yote yanayopatikana kwenye ulimwengu, kukiwemo mimea, wanyama, vijiumbe na binadamu, vyote viko chini ya ukuu wa Mungu na vinadhibitiwa na Mungu Mwenyewe. Katika ukuu na udhibiti wa Mungu, vitu vyote vinakuwepo au vinatoweka kulingana na fikira Zake, maisha ya vitu hivi yanatawaliwa na sheria fulani, na vinakua na kuzaana kulingana nazo. Hakuna binadamu au kiumbe chochote kilicho juu ya sheria hizi. Kwa nini hali iko hivi? Jibu la pekee tu ni, kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Au, nikijibu kwa njia nyingine, kwa sababu ya fikira za Mungu na matamshi ya Mungu; kwa sababu Mungu Mwenyewe hufanya haya yote. Hivi ni kusema, ni mamlaka ya Mungu na ni akili ya Mungu ambayo iliunda sheria hizi; zitasonga na kubadilika kulingana na fikira Zake, na kusonga huku na mabadiliko haya yote yanafanyika au kutoweka kwa minajili ya mpango Wake. Hebu tuchukulie magonjwa ya mlipuko, kwa mfano. Yanazuka tu bila onyo, hakuna anayejua asili yake, au sababu maalum zinazoelezea ni kwa nini huwa yanafanyika, na kila wakati magonjwa ya mlipuko yanapofika mahali fulani, wale walio na bahati mbaya hawawezi kukwepa maafa. Sayansi ya binadamu inafafanua na kutuelewesha kwamba magonjwa ya mlipuko yanasababishwa na kuenea kwa vijiumbe maradhi vibaya au haribifu, na kasi yao, eneo lao, na mbinu ya kuenea kwake haiwezi kutabiriwa au kudhibitiwa na sayansi ya binadamu. Ingawaje binadamu huvipinga vijiumbe maradhi hivi kwa kila namna inayowezekana, huwa hauwezi kudhibiti ni watu gani au wanyama gani ambao wanaathiriwa kwa vyovyote vile wakati kunapokuwa na mkurupuko wa magonjwa mlipuko. Kitu cha pekee ambacho binadamu wanaweza kufanya ni kujaribu kuyazuia, kuyapinga, na kuyafanyia utafiti. Lakini hakuna anayejua chanzo asilia kinachoelezea mwanzo au mwisho wa magonjwa mlipuko yoyote ya kibinafsi, na hakuna anayeweza kuyadhibiti. Wakiwa wamekabiliwa na ongezeko na kuenea kwa magonjwa mlipuko, suala la kwanza ambalo binadamu hufanya ni kuunda chanjo, lakini mara nyingi magojwa mlipuko hayo hutoweka kabisa kabla ya hata chanjo kuwa tayari. Kwa nini magonjwa mlipuko hutoweka kabisa? Wengine husema kwamba viini vimeweza kudhibitiwa, wengine husema kwamba vimetoweka kabisa kwa sababu ya mabadiliko katika misimu…. Kuhusiana na ikiwa makisio haya ya kuchanganyikiwa ni kweli au la, sayansi haiwezi kutupa ufafanuzi wowote, na wala haitoi jibu lolote lenye uhakika. Kile ambacho binadamu wanakabiliwa nacho si makisio haya tu lakini pia ukosefu wa mwanadamu katika kuelewa na woga wa magonjwa mlipuko haya. Hakuna anayejua, baada ya kila kitu kuchambuliwa, ni kwa nini magonjwa mlipuko haya huanza au ni kwa nini huisha. Kwa sababu binadamu wanayo imani tu katika sayansi, unategemea pakubwa kwa sayansi hiyo, lakini hautambui mamlaka ya Muumba au kuukubali ukuu Wake, hautawahi kuwa na jibu.
Katika ukuu wa Mungu, mambo yote yapo na huangamia kwa sababu ya mamlaka Yake, kwa sababu ya usimamizi Wake. Baadhi ya mambo huja na kwenda polepole, na binadamu hawezi kutambua ni wapi yalitokea au kung’amua sheria ambazo mambo haya hufuata, sisemi hata kuelewa sababu za mambo haya kuja na kwenda. Ingawaje binadamu anaweza kushuhudia, kusikia, au kupitia yote yanayokuja na kuisha miongoni mwa mambo yote; ingawaje mambo haya yanao mwelekeo kwa binadamu, na ingawaje binadamu hung'amua kupitia kwa yaliyofichika akilini mwake, hali isiyokuwa ya kawaida, hali ya mara kwa mara au hata hali ya ajabu ya mambo mbalimbali, bado hajui chochote kuhusu mapenzi ya Muumba na akili Yake ambavyo vinaelezea mambo hayo. Kunazo hadithi nyingi zinazotokana na haya mambo yote, ukweli mwingi uliofichwa. Kwa sababu binadamu amepotoka na kwenda mbali na Muumba, kwa sababu hakubali hoja hii kwamba Mamlaka ya Muumba ndiyo hutawala mambo yote, hatawahi kujua kila kitu kinachofanyika katika ukuu Wake. Kwa sehemu nyingi zaidi, udhibiti na ukuu wa Mungu huzidi mipaka ya fikra ya binadamu, maarifa ya binadamu, kuelewa kwa binadamu, kuhusu kile ambacho sayansi ya binadamu inaweza kutimiza; uwezo wa binadamu walioundwa hauwezi kushindana nao. Baadhi ya watu husema “Kwa sababu hujashuhudia ukuu wa Mungu wewe mwenyewe, unawezaje kusadiki kwamba kila kitu kinatokana na mamlaka Yake?” Kuona si kuamini kila mara; kuona si kutambua na kuelewa kila mara. Kwa hivyo “sadiki” hutokea wapi? Ninaweza kusema kwa uhakika, “Sadiki inatokana na kiwango na kina cha kuelewa kwa watu kwa, na hali wanayopitia wao, uhalisi na chanzo kikuu cha mambo.” Kama unasadiki kwamba Mungu yupo, lakini huwezi kutambua, na wala huwezi kuelewa, hoja ya udhibiti wa Mungu na ukuu wa Mungu katika mambo yote, basi katika moyo wako hutawahi kukubali kwamba Mungu anayo mamlaka kama haya na kwamba mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Hutawahi kukubali kwa kweli Muumba kuwa Bwana wako, Mungu wako.
Hatima ya Binadamu na Hatima ya Ulimwengu Haviwezi Kutenganishwa na Ukuu wa Muumba
Nyinyi nyote ni watu wazima. Baadhi yenu ni wa umri wa kati; baadhi mmefikisha umri wa uzee. Kutoka kwa yule asiyesadiki hadi kwa yule anayesadiki, na kuanzia mwanzo wa kusadiki kwa Mungu hadi kukubali neno la Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu, je, ni maarifa kiwango kipi mliyopata kuuhusu ukuu wa Mungu? Ni maono yapi mliyopata kwenye hatima yenu ya kuwa binadamu? Je, mtu anaweza kutimiza kila kitu anachotamani katika maisha? Je, ni mambo mangapi kwenye miongo michache iliyopita katika kuwepo kwenu mliyoweza kutimiza kama mlivyopenda? Ni mambo mangapi hayafanyiki kama yalivyotarajiwa? Ni mambo mangapi hutupata kwa mshangao mzuri? Ni mambo mangapi ambayo ungali unasubiri kutimia—unasubiri bila kufahamu muda sahihi, unasubiria mapenzi ya Mbinguni? Mambo mangapi yanakufanya uhisi kana kwamba huna wa kukusaidia na umezuiliwa? Watu wote wanayo matumaini kuhusu hatima yao, na hutarajia kwamba kila kitu katika maisha yao kitaenda sawa na wanavyopenda, kwamba hawatakosa chakula wala mavazi, kwamba utajiri wao utaongezeka pakubwa. Hakuna anayetaka maisha ya kimaskini na ya taabu, yaliyojaa ugumu, na kuandamwa na majanga. Lakini watu hawawezi kuona mbele au kudhibiti mambo haya. Pengine kwa baadhi ya watu, yaliyopita ni mchanganyiko tu wa yale mambo waliyoyapitia; hawajifunzi katu ni nini mapenzi ya Mbinguni, wala hawajali mapenzi hayo ni yapi. Wanaishi kwa kudhihirisha maisha yao bila kufikiria, kama wanyama, wakiishi siku baada ya siku, bila kujali kuhusu hatima ya binadamu ni nini, kuhusu ni kwa nini binadamu wako hai au vile wanavyostahili kuishi. Watu hawa hufikia umri wa uzee bila ya kufaidi ufahamu wowote wa hatima ya binadamu, na mpaka wakati ule wanapokufa hawana habari yoyote kuhusu maana ya maisha. Watu kama hao wamekufa; ni viumbe bila roho; wao ni wanyama. Ingawaje katika kuishi miongoni mwa mambo haya yote, watu hupata furaha kutoka kwa njia nyingi ambazo ulimwengu hutosheleza mahitaji yao ya anasa, ingawaje wanauona ulimwengu huu wa anasa ukiwa unapiga hatua bila kusita, hali yao binafsi waliyoipitia—kile ambacho mioyo yao na roho zao zinahisi na kupitia—hakina uhusiano wowote na mambo ya anasa, na hakuna kitu chochote cha anasa ambacho kinaweza kuchukua nafasi yake. Ni utambuzi ndani ya moyo wa mtu, kitu ambacho hakiwezi kuonekana kwa jicho vivyo hivyo tu. Utambuzi huu umo katika ufahamu wa mtu wa, na hisia za mtu za, maisha ya binadamu na hatima ya binadamu. Na mara nyingi humwongoza mtu katika kuelewa kwamba Bwana yule asiyeonekana anapanga vitu vyote, Anaunda kila kitu kwa ajili ya binadamu. Katikati ya haya yote, mtu hawezi kuepuka ila kukubali mipangilio na mipango ya hatima ya mambo; wakati uo huo, mtu hawezi kuepuka ila kukubali njia iliyo mbele ambayo Muumba amempangia, ukuu wa Muumba dhidi ya hatima ya mtu. Hii ndiyo hoja isiyopingika. Haijalishi ni maono na mtazamo gani ambao mtu anao kuhusu hatima yake, hakuna anayeweza kubadilisha hoja hii.
Pale utakapoenda kila siku, kile utakachofanya, yule au kile utakachokumbana nacho, kile utakachosema, kile kitakachokufanyikia—je, kati ya vyote hivi kipo kinachoweza kutabirika? Watu hawawezi kutabiri matukio haya yote, sikutajii kudhibiti namna ambavyo yanavyoendelea. Katika maisha, matukio haya yasiyotabirika hufanyika kila wakati, na ni tukio la kila siku. Mabadiliko haya ya kila siku na njia ambazo yanajitokeza, au ruwaza ambazo yanajitokeza, ni vikumbusho vya kila wakati kwa binadamu kwamba hakuna kinachofanyika bila mpango, kwamba matukio ya mambo haya, na kutoepukika kwa mambo haya, haviwezi kubadilishwa na mapenzi ya binadamu. Kila tukio linaonyesha onyo kutoka kwa Muumba kwa mwanadamu, na pia linatuma ujumbe kwamba, binadamu hawawezi kudhibiti hatima zao wenyewe; na wakati uo huo kila tukio ni upingaji wa malengo yasiyo na mwelekeo, yasiyo na maana ya ubinadamu na tamanio la kuchukua hatima yake na kutaka kuidhibiti mwenyewe. Ni sawa na makofi yenye nguvu juu ya masikio ya binadamu moja baada ya jingine, yanayolazimisha binadamu kufikiria upya ni nani, hatimaye, atatawala na kudhibiti hatima yao. Na kama vile malengo na matamanio yao yanavyokiukwa mara kwa mara na kusambaratika, binadamu kwa kawaida huishia kukubali kwa nadharia yao bila kufahamu kile ambacho hatima yao imesheheni, kukubali kwa uhalisi, kwa mapenzi ya Mbinguni na ukuu wa Muumba. Kutokana na mabadiliko haya ya kila siku katika hatima za maisha yote ya binadamu, hakuna kitu ambacho hakifichui mipango ya Muumba na ukuu Wake; hakuna kile ambacho hakiutumi ujumbe huu kwamba “yale mamlaka ya Muumba hayawezi kupitwa,” ambacho hakionyeshi ukweli wa milele kwamba “mamlaka ya Muumba ni ya juu zaidi.”
Hatima za binadamu na zile za ulimwengu zimeingiliana kwa ndani na ukuu wa Muumba, zimefungamanishwa na haziwezi kutenganishwa na mipango ya Muumba; na hatimaye, haziwezi kutenganishwa na mamlaka ya Muumba. Kupitia kwenye sheria za mambo yote binadamu huja kuelewa mipango ya Muumba na ukuu Wake; kupitia kwenye sheria za namna ya kuishi ambazo anaona katika utawala wa Muumba; kutoka kwenye hatima za mambo yote anapata hitimisho kuhusu njia ambazo Muumba huonyesha ukuu Wake na kuvidhibiti; na kwenye mzunguko wa maisha ya binadamu na mambo yote ambayo binadamu kwa kweli hupitia ile mipango na mipangilio ya Muumba kwa mambo yote na kwa viumbe vyote vilivyo hai na anashuhudia kwa kweli namna ambavyo mipango na mipangilio hiyo inavyozidi sheria zote za nchi, kanuni, na taasisi, mamlaka na nguvu zote nyingine. Kwa mujibu wa haya, binadamu wanashawishiwa kutambua kwamba, ukuu wa Muumba hauwezi kukiukwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, kwamba hakuna nguvu zinazoweza kuharibu au kubadilisha matukio na mambo yaliyoamuliwa kabla na Muumba. Ni kupitia kwenye sheria na kanuni hizi takatifu ambapo binadamu na viumbe vyote wanaweza kuishi na kuzalisha, kizazi baada ya kizazi. Je, huu si mfano halisi wa mamlaka ya Muumba? Ingawaje binadamu huona, kwenye sheria zile za malengo, ukuu wa Muumba na utaratibu Wake wa matukio yote na mambo yote, ni watu wangapi wanaweza kung’amua kanuni ya ukuu wa Muumba juu ya ulimwengu? Ni watu wangapi wanaweza kujua, kutambua, kukubali kwa kweli na kujinyenyekeza kwa ukuu na mpangilio wa Muumba dhidi ya hatima zao wenyewe? Nani, ambaye baada ya kusadiki hoja ya ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote, ataweza kusadiki kwa kweli na kutambua kwamba Muumba pia anaamrisha hatima hii ya maisha ya binadamu? Ni nani anayeweza kuelewa kwa kweli hoja hii kwamba hatima ya binadamu imo kwenye kiganja cha mkono wa Muumba? Aina ya mtazamo ambao binadamu wanafaa kuchukua katika ukuu wa Muumba, wanapokabiliwa na hoja kwamba Anatawala na kudhibiti hatima ya binadamu, ni uamuzi ambao kila binadamu ambaye kwa sasa anakabiliwa na hoja hii lazima ajiamulie mwenyewe.
Awamu Sita katika Maisha ya Binadamu
Katika mkondo wa maisha ya mtu, kila mtu hufikia kwenye misururu ya awamu muhimu. Hizi ni hatua za kimsingi zaidi, na muhimu zaidi, zinazoamua hatima ya maisha ya mtu. Kile kinachofuata ni ufafanuzi mfupi kuhusu mafanikio haya ambayo kila mtu lazima apitie kwenye mkondo wa maisha yake.
Kuzaliwa: Awamu ya Kwanza
Mahali ambapo mtu amezaliwa, amezaliwa katika familia ya aina gani, jinsia ya mtu, umbo la mtu, na wakati wa kuzaliwa: haya ndiyo maelezo ya awamu ya kwanza ya maisha ya binadamu.
Hakuna yeyote aliye na chaguo kuhusu sehemu hizi za awamu hii; zote ziliamuliwa kabla, mapema kabisa na Muumba. Haziathiriwi na mazingira ya nje kwa vyovyote vile, na hakuna masuala yanayosababishwa na binadamu yanaweza kubadilisha hoja hizi ambazo Muumba aliamua kabla. Kwa mtu kuweza kuzaliwa inamaanisha kwamba Muumba tayari ametimiza hatua ya kwanza ya hatima ambayo Amempangilia mtu huyo. Kwa sababu Aliamua kabla maelezo haya yote tena mapema mno, hakuna aliye na nguvu za kubadilisha maelezo yoyote yale. Licha ya hatima ya baadaye ya mtu, hali za kuzaliwa kwa mtu ziliamuliwa kabla, na zinabakia kama zilivyo; haziathiriwi kwa njia yoyote ile na hatima ya mtu katika maisha, wala haziathiri kwa vyovyote vile ukuu wa Muumba juu yazo.
1. Maisha Mapya Yanazaliwa Kulingana na Mipango ya Muumba
Ni maelezo yapi ya awamu ya kwanza—mahali mtu anapozaliwa, familia ya mtu, jinsia ya mtu, umbo la mwili wa mtu, muda wa kuzaliwa kwa mtu—ambayo mtu anaweza kuchagua? Bila shaka, kuzaliwa kwa mtu ni tukio asiloweza kuchagua: Mtu anazaliwa bila hiari yake, katika mahali fulani, muda fulani, kwenye familia fulani, akiwa na umbo fulani la kimwili; mtu anakuwa mmojawapo wa familia fulani bila hiari, anarithi kizazi fulani cha familia. Mtu hana chaguo kwenye awamu hii ya kwanza ya maisha, lakini anazaliwa kwenye mazingira yanayochaguliwa kulingana na mipango ya Muumba, kwenye familia mahususi, na jinsia na umbo mahususi, kwenye wakati mahususi ambao unaunganishwa kwa undani na mkondo wa maisha ya mtu huyu. Mtu anaweza kufanya nini katika awamu hii muhimu? Yote yakisemwa, kwa kweli mtu hana chaguo kuhusu maelezo yoyote yale yanayohusu kuzaliwa kwake. Kama isingekuwa kuamua kabla kwa Muumba na mwongozo Wake, mtu aliyezaliwa upya kwenye ulimwengu huu asingejua ni wapi atakapoenda au ni wapi atakapoishi, asingekuwa na mahusiano yoyote, asingekuwa na popote na asingekuwa na maskani yoyote halisi. Lakini kwa sababu ya mipangilio makinifu ya Muumba, anaanza safari ya maisha yake akiwa na mahali pa kuishi, wazazi, na mahali anapoita nyumbani na watu wa ukoo. Kotekote kwenye mchakato huu, mwanzo wa maisha haya mapya unaamuliwa na mipango ya Muumba, na kila kitu ambacho mtu huyu atakuja kumiliki ataweza kukabidhiwa na Muumba. Kutoka kwenye kiumbe kinachoelea-kisichokuwa na jina lolote hadi kinapoanza kuwa na nyama–na–damu polepole, kinachoweza kuonekana, na hatimaye kuwa binadamu anayeweza kushikika, mojawapo ya viumbe vya Mungu, anayefikiria, anayepumua, anayehisi joto na baridi, anayeshiriki katika shughuli za kawaida za kiumbe kilichoumbwa kwenye ulimwengu yakinifu na ambaye atapitia mambo haya yote ambayo kiumbe kilichoumbwa lazima kipitie maishani. Kule Kuamuliwa kabla kwa kuzaliwa kwa mtu na Muumba kunamaanisha kwamba ataweza kumpa mtu huyu mambo yote yanayohitajika kwa kuishi kwake; na kwamba mtu anazaliwa vilevile inamaanisha kwamba yeye atapokea mambo yote yanayohitajika kutoka kwa Muumba, kwamba kuanzia wakati ule kwenda mbele yeye ataishi katika umbo jingine, linalotolewa na Muumba na linalotii ukuu wa Muumba.
2. Kwa Nini Binadamu Tofauti Wanazaliwa Katika Hali Tofauti
Mara nyingi watu wanapenda kufikiria kwamba, kama wangezaliwa tena, wangezaliwa kwenye familia maarufu; kama wangekuwa wanawake, wangefanana na Binti wa Kifalme Anayependeza na wangependwa na kila mtu, na wangezaliwa wanaume, wangekuwa Kaka Mwenye Mvuto na Haiba, wasikose mahitaji yoyote, huku ulimwengu mzima ukiwaitikia mara moja kila unapoitwa na wao. Mara nyingi kuna wale walio na picha nyingi kuhusu kuzaliwa kwao na huwa hawajatosheka kabisa na huko kuzaliwa kwao, wanachukia familia zao, umbo lao, jinsia yao, na hata wakati wa kuzaliwa kwao. Ilhali watu hawajawahi kuelewa ni kwa nini wamezaliwa katika familia fulani au kwa nini wanafanana jinsi fulani. Hawajui kwamba, licha ya ni wapi wamezaliwa au ni vipi wanavyoonekana, wanafaa kuendeleza wajibu mbalimbali na kutimiza kazi maalum tofautitofauti katika usimamizi wa Muumba—kusudi hili halitawahi kubadilika. Ingawa katika macho ya Muumba, mahali anapozaliwa mtu, jinsia ya mtu, umbo la mwili wa mtu hivi vyote ni vitu vya muda. Ni misururu ya mambo madogomadogo katika kila awamu ya usimamizi Wake wa mwanadamu kwa ujumla. Na hatima halisi ya mtu na mwisho wake vyote haviamuliwi kutokana na wapi ambapo yeye amezaliwa katika awamu yoyote ile, lakini vinaamuliwa na kazi maalum ambayo yeye atatekeleza katika kila maisha, kwa hukumu ya Muumba kwao wakati ambapo usimamizi Wake wa mpango vitakamilika.
Inasemekana kwamba kunayo sababu katika kila athari, na kwamba hakuna athari ambayo haina sababu. Na kwa hivyo kuzaliwa kwa mtu kumefungamanishwa haswa na maisha yake ya sasa na yale ya awali. Kama kifo cha mtu kinasitisha awamu yake ya sasa ya maisha, basi kuzaliwa kwa mtu ndio mwanzo wa mzunguko mpya; kama mzunguko wa kale unawakilisha maisha ya awali ya mtu, basi mzunguko huo mpya kwa kawaida ndio maisha yao ya sasa. Kwa sababu kuzaliwa kwa mtu kunaunganishwa na maisha ya kale ya mtu huyu pamoja na maisha ya sasa ya mtu huyu, mahali anapoishi, familia yake, jinsia, umbo na mambo mengine kama hayo, ambayo yanahusiana na kuzaliwa kwa mtu, vyote vinahusiana na mambo yote. Hii inamaanisha kwamba, mambo yanayoathiri kuzaliwa kwa mtu hayaathiriwi tu na maisha ya awali ya mtu, lakini yanaamuliwa na hatima ya mtu katika maisha ya sasa. Hii inaelezea mseto wa hali tofauti ambazo watu wanazaliwa: Baadhi wanazaliwa katika familia fukara, wengine katika familia tajiri. Baadhi wanazaliwa katika kundi la watu wa kawaida, wengine wanazaliwa katika ukoo wa kipekee. Baadhi wanazaliwa kusini, wengine wanazaliwa kaskazini. Baadhi wanazaliwa jangwani na wengine wanazaliwa katika ardhi zenye rotuba. Kuzaliwa kwa baadhi ya watu kunaandamana na vifijo, vicheko, na sherehe, wengine wanaleta machozi, janga, na matatizo. Baadhi wanazaliwa ili wathaminiwe, wengine wawekwe pembeni kama magugu. Baadhi wanazaliwa wakiwa na heshima na staha na wengine wanazaliwa wakiwa na mikosi na mikasa. Baadhi wanapendeza kuwatazama, na wengine wanatisha kuwatazama. Baadhi wanazaliwa usiku wa manane, wengine wanazaliwa chini ya jua kali la utosi. … Kuzaliwa kwa watu wa kila aina kunaamuliwa na hatima ambazo Muumba ameweka kwa ajili yao; kuzaliwa kwao kunaamua hatima zao pamoja na wajibu ambao wataendeleza na kazi maalum watakazotimiza. Yote haya yanategemea ukuu wa Muumba, ulioamuliwa kabla na Yeye; hakuna anayeweza kukimbia kundi hili lao lililoamuliwa kabla, hakuna anayeweza kubadilisha hali za[a]kuzaliwa kwao, na hakuna anayeweza kuchagua hatima yake binafsi.
Kukua: Awamu ya Pili
Kutegemea na aina gani ya familia ambayo wamezaliwa ndani, watu hukua katika mazingira tofauti ya nyumbani na wakajifunza mafunzo tofauti kutoka kwa wazazi wao. Hii huamua masharti ambayo mtu anafikisha umri wa kubaleghe na kukua[b] inawakilisha awamu ya pili muhimu ya maisha ya mtu. Inajulikana kwamba, watu hawana chaguo katika awamu hii, vilevile. Hii pia imepangwa, ilipangwa kabla.
1. Hali Ambazo Mtu Hukulia Ndani Zimepangwa na Muumba
Mtu hawezi kuchagua watu au mambo ambayo yataweza kumhimiza na kumwathiri anapokua. Mtu hawezi kuchagua ni maarifa au mbinu gani atapata, ni mazoea gani ataishia kuwa nayo. Mtu hana kauli kuhusiana na wazazi na watu wake wa ukoo, aina ya mazingira ambayo atakulia ndani; mahusiano yake na watu, matukio, na mambo yaliyo katika mazingira yake na namna yanavyoathiri maendeleo yake, vyote ni zaidi ya udhibiti wake. Ni nani anayeamua mambo haya, basi? Ni nani anayeyapangilia? Kwa sababu watu hawana chaguo katika suala hili, kwa vile hawawezi kuamua mambo haya wao wenyewe, na kwa sababu bila shaka hayajipangi yenyewe kwa kawaida, ni wazi kabisa kwamba kuundwa kwa haya yote kunategemea mikono ya Muumba. Kama vile tu Muumba anavyopanga hali fulani za kuzaliwa kwa kila mtu, Yeye hupangilia pia hali mahususi ambazo mtu hukulia, bila shaka. Kama kuzaliwa kwa mtu kutaleta mabadiliko kwa watu, kwa matukio, na mambo yanayomzunguka yeye, basi kukua na maendeleo ya mtu huyo vyote vitaweza kuwaathiri vilevile. Kwa mfano, baadhi ya watu wanazaliwa katika familia fukara, lakini wanalelewa wakiwa wemezungukwa na utajiri; wengine wanazaliwa katika familia tajiri lakini husababisha utajiri wa familia zao kupungua, kiasi cha kwamba wanalelewa katika mazingira ya kimaskini. Hakuna kuzaliwa kwa yeyote kunatawaliwa na kanuni isiyobadilika, na hakuna anayelelewa katika hali zisizozuilika, na zisizobadilika. Haya si mambo ambayo binadamu anaweza kufikiria au kudhibiti; mambo haya yote ni mazao ya hatima ya mtu, na yanaamuliwa na hatima ya mtu. Bila shaka, kimsingi ni kwamba yote haya yaliamuliwa kabla katika hatima ya mtu na Muumba, yanaamuliwa na ukuu wa Muumba juu ya, na mipango Yake ya, hatima ya mtu huyu.
2. Hali Mbalimbali Ambazo Watu Hukulia Ndani Husababisha Wajibu Tofauti
Hali za kuzaliwa kwa mtu huanzisha katika kiwango cha kimsingi mazingira na hali ambazo hukulia ndani, na hali ambazo mtu hukulia ndani vilevile ni zao la hali za kuzaliwa kwake. Kwenye wakati huu mtu anaanza kujifunza lugha, na akili za mtu zinaanza kukumbana na kuchanganua mambo mengi mapya, na katika mchakato huu mtu anakua bila kusita. Mambo ambayo mtu anasikia kwa masikio yake, anaona kwa macho yake, na anang’amua kwa akili zake huboresha na kuhuisha kwa utaratibu ulimwengu wa ndani wa mtu. Watu, matukio, na mambo ambayo mtu anakumbana nayo, maarifa ya kawaida, maarifa, na mbinu anazojifunza, na njia za kufikiria ambazo mtu anaathiriwa nazo, anaambiwa au kufunzwa, vyote vitamwongoza na kuathiri hatima ya maisha yake. Lugha anayojifunza mtu anapokua na njia yake ya kufikiria haviwezi kutenganishwa kutoka kwenye mazingira ambayo yeye analelewa katika ujana wake, na hayo mazingira yana wazazi, ndugu zake, na watu wengine, matukio, na mambo yanayomzunguka. Kwa hivyo mkondo wa maendeleo ya mtu unaamuliwa na mazingira ambayo yeye anakulia ndani, na pia unategemea watu, matukio, na mambo ambayo mtu anakumbana nayo kwenye kipindi hiki cha muda. Kwa sababu masharti ambayo mtu hukulia ndani yaliamuliwa kabla na tena mapema mno, mazingira anayoishi kwenye mchakato huu pia, kwa kawaida, yaliamuliwa kabla. Hayaamuliwi na chaguo na mapendeleo ya mtu, lakini yanaamuliwa kulingana na mipango ya Muumba, yanaamuliwa na mipangilio makinifu ya Muumba, na ukuu wa Muumba juu ya hatima ya mtu huyo katika maisha. Kwa hivyo watu ambao mtu yeyote hukumbana nao katika mkondo wa kukua, na mambo ambayo mtu hukutana nayo, vyote vimeunganishwa bila kuzuilika kwa mipango na mipangilio ya Muumba. Watu hawawezi kutabiri aina hizi za mahusiano mapevu, wala hawawezi kuyadhibiti au kuweza kuyaelewa. Mambo mengi tofauti na watu wengi tofauti wanao mwelekeo wa mazingira ambayo mtu hukulia, na hakuna binadamu anaweza kupangilia na kupanga mtandao mpana kama huo wa maunganisho. Hakuna mtu au kitu isipokuwa Muumba anaweza kudhibiti kujitokeza, kuwepo, na kutoweka kwa watu mbalimbali, matukio na mambo, na ni mtandao mpana ajabu wa maunganisho unaounda maendeleo ya mtu kama ilivyoamuliwa kabla na Muumba, na kuunda mazingira tofauti ambayo watu wanakulia ndani, na kuunda wajibu mbalimbali unaohitajika kwa minajili ya kazi ya Muumba ya usimamizi, kuweka misingi thabiti, yenye nguvu ili watu waweze kukamilisha kwa ufanisi kazi yao maalum.
Uhuru: Awamu ya Tatu
Baada ya mtu kupita utoto na wakati wake wa kubaleghe na kwa utaratibu bila kuzuilika kufikia ukomavu, hatua inayofuata ni kwake yeye kuuaga kabisa ule ujana wake, kuwaaga wazazi wake, na kukabiliana na barabara iliyo mbele yake akiwa mtu mzima huru. Wakati huo[c] lazima wakabiliane na watu, matukio na mambo yote ambayo mtu mzima lazima apitie, na kukabiliana na viungo mbalimbali katika msururu wa hatima yake. Hii ndiyo awamu ya tatu ambayo lazima mtu apitie.
1. Baada ya Kuwa Huru, Mtu Huanza Kupitia Ukuu wa Muumba
Kama kuzaliwa kwa mtu na kulelewa kwake ni “kipindi cha matayarisho” katika safari ya mtu maishani, kuweka lile jiwe la msingi katika hatima ya mtu, basi uhuru wa mtu ndio mazungumzo nafsi ya kufungua hatima ya maisha ya mtu. Kama kuzaliwa na kukua kwa mtu ni utajiri ambao wameweza kulimbikiza kwa minajili ya hatima yao maishani, basi uhuru wa mtu huyo unaanza wakati ule wanaanza kutumia au kuongeza utajiri huo. Wakati mtu anawaacha wazazi na kuwa huru, masharti ya kijamii ambayo anakabiliana nayo, na aina ya kazi na ajira inayopatikana kwa mtu, vyote vinaamriwa na hatima na havina uhusiano wowote na wazazi wa mtu. Baadhi ya watu huchagua kozi nzuri katika chuo na huishia kupata kazi ya kutosheleza baada ya kuhitimu, na hivyo basi kupiga hatua ya kwanza ya mafanikio katika safari yao ya maisha. Baadhi ya watu hujifunza na kumiliki mbinu nyingi tofauti na ilhali hawapati kazi katu ambayo inawafaa au hawapati cheo chao, bila kutaja kwamba hawana ajira yoyote; wakati wa safari ya maisha yao wanajipata wakiwa wamekwazwa katika kila kona, wameandamwa na matatizo, matumaini yao madogo na maisha yao hayana uhakika. Baadhi ya watu wanatia bidii katika masomo yao, ilhali wanakosa kwa karibu sana fursa zao zote za kupokea elimu ya juu zaidi, na wanaonekana kuwa na hatima ya kutotimiza fanisi, matamanio yao ya kwanza kabisa katika safari yao ya maisha yanatowekea tu hewani. Bila kujua[d] kama barabara iliyo mbele ni laini au yenye miamba, wanahisi kwa mara ya kwanza namna ambavyo hatima ya binadamu imejaa vitu vya kubadilikabadilika, na wanachukulia maisha kwa tumaini na hofu. Baadhi ya watu, licha ya kutokuwa na elimu nzuri sana, huandika vitabu na kutimiza kiwango cha umaarufu; baadhi, ingawaje hawajui kusoma na kuandika sana, huunda pesa katika biashara na hivyo basi wanaweza kujikidhi…. Kazi anayochagua mtu, namna mtu anavyozumbua riziki: je, watu wanao udhibiti wowote kuhusu, kama wanaweza kufanya uchaguzi mzuri au uchaguzi mbaya? Je, yanapatana na matamanio na uamuzi wao? Watu wengi zaidi hutamani wangeweza kufanya kazi kidogo na kupata mapato mengi zaidi, wasitie bidii sana katika jua na mvua, wavalie vyema, wametemete na kung’aa wakiwa kila pahali, kuwapita sana wengine kwa uwezo, na kuleta heshima kwa mababu wao. Matamanio ya watu ni timilifu kweli, lakini watu wanapochukua hatua zao za kwanza katika safari ya maisha yao, wanaanza kwa utaratibu kutambua namna ambavyo hatima ya binadamu ilivyo na hali ya kutokuwa timilifu, na kwa mara ya kwanza wanang’amua kwa kweli hoja hii kwamba, ingawaje mtu anaweza kufanya mipango thabiti kwa minajili ya mustakabali wake, ingawaje mtu anaweza kuhodhi mawazoni ndoto shupavu, hakuna yule aliye na uwezo au nguvu za kutambua ndoto zake mwenyewe, hakuna yule aliye katika hali ya kudhibiti mustakabali wake. Siku zote kutakuwepo na kitalifa fulani kati ya ndoto za mtu na uhalisia ambao lazima mtu akabiliane nao; mambo siku zote hayawi vile ambavyo mtu angetaka yawe, na watu wanapokumbwa na uhalisi kama huu hawawezi kutimiza hali ya kutosheka au kuridhika. Baadhi ya watu wataenda hadi kiwango chochote cha kufikirika, wataweza kutia bidii za kipekee na kujitolea pakubwa kwa minajili ya riziki na mustakabali wao, katika kujaribu kubadilisha hatima yao wenyewe. Lakini hatimaye, hata kama wataweza kutambua ndoto na matamanio yao kupitia kwa njia ya bidii yao wenyewe, hawawezi kubadilisha hatima zao, na haijalishi watajaribu vipi kwa njia ya ukaidi hawatawahi kuzidi kile ambacho hatima yao imewapangia. Licha ya tofauti katika uwezo, kiwango cha akili, na hiari ya kutenda, watu wote ni sawa mbele ya hatima, jambo ambalo halileti utofauti kati ya wakubwa na wadogo, wale wa kiwango kile cha juu na cha chini, wanaotukuzwa na wakatili. Ile kazi ambayo mtu anafuatilia, kile anachofanya mtu ili kuzumbua riziki, na kiwango kipi cha utajiri ambacho mtu amelimbikiza katika maisha yake vyote haviamuliwi na wazazi wa mtu, vipaji vya mtu, jitihada za mtu au malengo ya mtu, vyote vinaamuliwa kabla na Muumba.
2. Kuwaacha Wazazi wa Mtu na Kuanza kwa Bidii Kuendeleza Wajibu Wako Kwenye Ukumbi wa Sanaa wa Maisha
Wakati mtu anapofikia ukomavu, mtu anaweza kuacha wazazi wake na kulikanyaga guu lake nje kivyake, na ni katika wakati huu ambapo mtu huanza kwa kweli kuonyesha wajibu wake binafsi, kwamba kazi maalum ya mtu maishani husita kutoeleweka na polepole kuanza kuwa wazi. Kimsingi mtu huyo bado huonyesha uhusiano wa karibu na wazazi wake, lakini kwa sababu kazi yake maalum na wajibu anaoendeleza katika maisha huwa hauna uhusiano wowote na mama na baba wa mtu huyo, kwa hakika uhusiano huu wa karibu huvunjika polepole kwa kadiri ambavyo mtu anazidi kuendelea kuwa huru. Kutoka katika mtazamo wa kibiolojia, watu bado hawana budi kutegemea wazazi katika njia za kufichika akilini, lakini kama tutaongea kwa malengo, mara baada ya kukua huwa na maisha tofauti kabisa na yale ya wazazi wao, na wataweza kutekeleza wajibu watakaoamua kufanya kwa uhuru wao. Mbali na kuzaliwa na kulea watoto, jukumu la kila mzazi katika maisha ya mtoto ni kuweza kuwapatia tu mazingira rasmi ya kukulia ndani, bila malipo yoyote isipokuwa kule kuamuliwa kabla kwa Muumba ambako kunachukua mwelekeo katika hatima ya mtu huyu husika. Hakuna anayeweza kudhibiti ni mustakabali gani ambao mtu atakuwa nao; huwa umeamuliwa kabla na mapema sana, na hata wazazi wa mtu hawawezi kubadilisha hatima yake. Kulingana na mambo ya hatima, kila mtu yuko huru na kila mtu anayo hatima yake. Kwa hivyo hakuna wazazi wa mtu yeyote wanaweza kuiondoa hatima ya mtu katika maisha au kusisitizia ushawishi wowote ule mdogo katika wajibu ambao mtu huendeleza maishani. Inaweza kusemekana kwamba, familia ambayo mtu ameamuliwa kuzaliwa ndani, na mazingira ambayo mtu atakulia ndani, ni yale masharti ya awali ya kutimiza kazi maalum ya mtu maishani. Yote haya hayaamui kwa vyovyote vile hatima ya mtu katika maisha au aina ya hatima ambayo mtu huyo atatimiza katika kazi yake maalum. Na kwa hivyo hakuna wazazi wa mtu yeyote yule wanaweza kusaidia katika kutimiza kazi hii maalum katika maisha, hakuna watu wowote wa ukoo wanaweza kusaidia mtu kuchukua wajibu huu katika maisha. Vile ambavyo mtu hutimiza kazi yake maalum na katika aina gani ya mazingira ya kuishi ambayo mtu hutekeleza wajibu wake, vyote vinaamuliwa na hatima ya mtu maishani. Kwa maneno mengine, hakuna masharti yoyote mengine yenye malengo yanaweza kuathiri kazi maalum ya mtu, ambayo imeamuliwa kabla na Muumba. Watu wote hukomaa katika mazingira yao binafsi ya kukulia, na kisha kwa taratibu, hatua kwa hatua, huanza safari katika barabara zao binafsi za maisha, hutimiza hatima walizopangiwa na Muumba, kwa kawaida, bila hiari wao huingia katika bahari kuu ya binadamu na kuchukua nafasi zao binafsi katika maisha, pale ambapo wao huanza kutimiza majukumu yao kama viumbe vilivyoumbwa kwa minajili ya kuamuliwa kabla kwa Muumba, kwa minajili ya ukuu Wake.
Ndoa: Awamu ya Nne
Wakati mtu anavyokua mzee na kukomaa, mtu huanza kukua na kuwa mbali na wazazi wake na mazingira ambayo amezaliwa na kulelewa, na badala yake mtu huanza kutafuta mwelekeo wa maisha yake na kufuatilia shabaha binafsi kwa njia ya maisha iliyo tofauti na ile ya wazazi. Kwenye kipindi hiki cha muda mtu hahitaji tena wazazi wake, bali mwandani ambaye anaweza kuishi maisha yake na mtu huyo: mwenza, mtu ambaye hatima yake imejipinda kwake ndani kwa ndani. Kwa njia hii, tukio kuu ambalo mtu hukabiliana nalo kufuatia uhuru wake ni ndoa, awamu ya nne ambayo lazima mtu apitie.
1. Mtu Hana Chaguo Kuhusu Ndoa
Ndoa ni tukio muhimu katika maisha ya mtu yeyote; ni wakati ule ambao mtu huanza kwa kweli kuendeleza aina mbalimbali za majukumu, huanza kwa utaratibu kutimiza aina mbalimbali za kazi maalum. Watu huwa na picha nyingi kuhusu ndoa kabla ya kuipitia wao wenyewe, na picha hizi zote ni nzuri. Wanawake hufikiria kwamba waume wao watakuwa Kaka Mwenye Mvuto na Haiba, nao wanaume hufikiria kwamba wataweza kuoa Binti wa Kifalme Anayependeza. Kubuni huku kwa mawazo kunaonyesha kwamba kila mtu anayo mahitaji fulani ya ndoa, orodha fulani ya kile anachohitaji na viwango anavyopenda. Ingawaje katika enzi hii ya maovu watu wanaambiwa kila mara kuhusu ujumbe uliopotoka juu ya ndoa, hali ambayo husababisha hata mahitaji mengi zaidi, pamoja na kupatia watu aina zote za mizigo na mitazamo isiyo ya kawaida, mtu yeyote aliyepitia ndoa anajua kwamba haijalishi ni kiasi kipi ambacho mtu ataielewa, haijalishi pia mtu anao mtazamo gani katika ndoa hiyo, ndoa si suala la chaguo la mtu binafsi.
Mtu hukumbana na watu wengi katika maisha yake, lakini hakuna anayejua ni nani atakayekuwa mwandani wake katika ndoa. Ingawaje kila mtu anazo fikira zake binafsi na mtazamo wake wa kibinafsi kuhusu suala la ndoa, hakuna anayeweza kuona mbele na kujua ni nani atakayekuwa mwandani wake wa kweli hatimaye, na fikira za mtu huwa zinachangia kidogo sana. Baada ya kukutana na mtu unayempenda, unaweza kumfuatilia mtu huyo; kama mtu huyo amevutiwa na wewe au la, kama mtu huyo anaweza kuwa mwandani wako au la, si wewe kuamua. Kiini cha mahaba yenu si haswa mtu ambaye mtaweza kuishi naye katika maisha yako; na huku haya yakiendelea mtu ambaye hukuwahi kutarajia anaingia katika maisha yako na kuwa mwandani wako, anakuwa msingi muhimu sana katika hatima yako, nusu yako ile nyingine, ambaye hatima yako imefungamanishwa naye ajabu. Na kwa hiyo, ingawaje kunazo ndoa milioni kwa milioni ulimwenguni, kila ndoa ni tofauti: Ni ndoa ngapi ambazo hazitoshelezi, ni ngapi zinayo furaha; ni ngapi zinazopatikana Mashariki na Magharibi, ni ngapi Kaskazini na Kusini; ni ngapi ambazo wanandoa wanafaa na wamelingana, na ni ngapi zenye kiwango sawa; ni ngapi zenye furaha na utulivu, ni ngapi zenye maumivu na huzuni; ni ngapi zinaonewa wivu na wengine, na ni ngapi hazieleweki na hazipendelewi kabisa; ni ngapi zimejaa furaha, na ni ngapi zimejaa machozi na zinakatisha tamaa.…. Kwenye ndoa hizi zote, binadamu wanafichua utiifu na kujitolea kwa maisha katika ndoa hizo, au pendo, au mtagusano, na hali ya kutotenganishwa, au kukata tamaa na kutoeleweka, au usaliti, au hata chuki. Haijalishi kama ndoa inaleta furaha au maumivu, kazi maalum ya kila mmoja katika ndoa iliamuliwa kabla na Muumba na haitabadilika; kila mmoja lazima aitimize. Na hatima ya kibinafsi inayokuwa katika kila ndoa haibadiliki; iliamuliwa kitambo naye Muumba.
2. Ndoa Inazaliwa Kutokana na Hatima ya Wandani Wawili
Ndoa ni awamu muhimu katika maisha ya mtu. Ni zao la hatima ya mtu, kiungo muhimu katika hatima ya mtu; haiundwi kwa misingi ya uamuzi wa mtu yeyote binafsi au mapendeleo yake, na haiathiriwi na mambo yoyote ya nje, lakini inaamuliwa kabisa na hatima za wandani wawili, kupitia kwa maandalizi na kuamuliwa kabla kwa Muumba kuhusiana na hatima za wanandoa hao. Ukiangalia juujuu, kusudi la ndoa ni kuendeleza kizazi cha binadamu, lakini kwa kweli ndoa si chochote ila ni kawaida ya dini ambayo mtu anapitia katika mchakato wa kutimiza kazi yake maalum. Wajibu mbalimbali ambao watu huendeleza katika ndoa si ule tu wa kuleta kizazi kinachofuata; kunao wajibu mbalimbali ambao mtu huwa nao na kazi maalum ambazo mtu lazima atimize kwenye mkondo wa kuendeleza ndoa. Kwa sababu kuzaliwa kwa mtu huathiri mabadiliko ya watu, matukio, na mambo yanayomzunguka, ndoa ya mtu itaweza pia kuathiri bila shaka watu hao, na zaidi itawabadilisha kwa njia tofauti.
Wakati mtu anapokuwa huru, mtu huanza safari yake binafsi ya maisha, inayoongoza mtu hatua kwa hatua kuelekea kwa watu, na kwa matukio, na kwa vitu vinavyohusiana na ndoa ya mtu; na wakati uo huo, yule mtu mwengine atakayeunda ile ndoa anakaribia, hatua kwa hatua, kuelekea watu ao hao, matukio na hata mambo. Kwenye ukuu wa Muumba, watu wawili wasiohusiana walio na hatima inayohusiana wanaingia kwa utaratibu kwenye ndoa na kuwa, kimiujiza, familia, “nzige wawili wanaoshikilia kamba moja.” Kwa hivyo mtu anapoingia kwenye ndoa, safari ya mtu katika maisha itaathiri na kumgusa yule mwenzake, na vilevile safari ya mwandani katika maisha itashawishi na kugusa hatima ya yule mwenzake katika maisha. Kwa maneno mengine, hatima za mwanadamu zimeingiliana na hakuna yule anayeweza kutimiza kazi yake maalum maishani au kutekeleza wajibu wake kabisa akiwa huru mbali na wengine. Kuzaliwa kwa mtu kunao mwelekeo kwa msururu mkubwa wa mahusiano; kukua pia kunahusisha msururu mkubwa wa mahusiano; na vilevile, ndoa inakuwepo bila shaka na kuendelezwa katika mtandao mpana na mgumu wa miunganisho ya binadamu, ikihusisha kila mwanachama na kuathiri hatima ya kila mmoja ambaye ni sehemu yake. Ndoa si mazao ya familia za wanachama wale wawili, hali ambazo wao walilelewa, maumbo yao, umri wao, ubora wao, vipaji vyao, au mambo mengine yoyote; badala yake, inatokana na kazi maalum ya pamoja na hatima inayohusiana. Hii ndiyo asili ya ndoa, zao la hatima ya binadamu lililopangwa na lililopangiliwa na Muumba.
Uzao: Awamu ya Tano
Baada ya kuoa, mtu anaanza kulea kizazi kijacho. Mtu hana uwezo wa kujua atakuwa na watoto wangapi na watoto hawa watakuwa aina gani; hili pia linaamuliwa na hatima ya mtu, iliyoamuliwa kabla na Muumba. Hii ndiyo awamu ya tano ambayo lazima mtu apitie.
Kama mtu amezaliwa ili kutimiza jukumu la mtoto wa mwengine, basi mtu analea kizazi kijacho ili kutimiza jukumu la mzazi wa mwengine. Mabadiliko haya ya majukumu yanamfanya mtu kupitia awamu tofauti za maisha kutoka mitazamo tofauti. Yanampa pia mtu mseto tofauti wa mambo mbalimbali ya maisha kupitia, ambapo mtu anajua ukuu ule wa Muumba, pamoja na hoja kwamba hakuna mtu anayeweza kuzidi au kubadilisha kile ambacho Muumba aliamua kabla.
1. Mtu Hana Udhibiti wa Hatima ya Uzao Wake
Kuzaliwa, kukua, na kuoa ni awamu ambazo zinaleta aina tofauti na viwango tofauti vya masikitiko. Baadhi ya watu hawatosheki na familia zao au maumbo yao ya kimwili; baadhi hawapendi wazazi wao; baadhi wanachukia au wanalalamikia mazingira ambayo walikulia ndani. Na kwa baadhi ya watu wengi, miongoni mwa masikitiko haya yote, ndoa ndiyo ambayo haitoshelezi zaidi. Licha ya vile ambavyo unayo masikitiko kwa kuzaliwa kwako, au kukua kwako, au ndoa yako, kila mmoja ambaye amepitia awamu hizi amejua kwamba hawezi kuchagua ni wapi au ni lini alizaliwa, ni vipi anavyofanana, wazazi wake ni nani, na mume au mke wake ni nani, lakini wanaweza kukubali tu mapenzi ya Mbinguni. Lakini wakati wa watu kulea kizazi kijacho unapowadia, wataweza kuweka matamanio yao yote ambayo hayajatimizwa katika nusu ya kwanza ya maisha yao kwenye vizazi vyao, wakitumai kwamba, uzao wao utajaliza sehemu ile ambayo wao wamepitia masikitiko, kwenye nusu ile ya kwanza ya maisha yao. Kwa hivyo watu hujihusisha katika aina zote za fantasia kuhusu watoto wao: kwamba binti zao watakua na kuwa warembo ajabu, watoto wao wa kiume watakuwa wanaume wa kipekee; kwamba binti zao watakuwa na maadili na wenye vipaji nao watoto wao wa kiume watakuwa wanafunzi werevu, na wanariadha sifika; na kwamba binti zao watakuwa watulivu na waadilifu, wenye akili razini, kwamba watoto wao wa kiume watakuwa wenye akili, wenye uwezo na wanaojali. Wanatumai kwamba wawe watoto wa kike au wa kiume wataheshimu wazee wao, watajali wazazi wao, watapendwa na kusifiwa na kila mmoja… Kufikia hapa matumaini ya maisha yanajitokeza upya, na matamanio mapya yanapata nguvu katika mioyo ya watu. Watu wanajua kwamba hawana nguvu na tumaini katika maisha haya, kwamba hawatakuwa na fursa nyingine, tumaini jingine, la kujitokeza mbele ya watu, na kwamba hawana chaguo lolote ila kukubali hatima zao. Na kwa hivyo wanatazamia matumaini yao yote, matamanio na maadili yao ambayo hayajatimizwa, hadi kwenye kizazi kijacho, wakitumai uzao wao unaweza kuwasaidia kutimiza ndoto zao na kutambua matamanio yao; na kwamba binti zao na watoto wao wa kiume wataleta utukufu katika jina la familia, kuwa muhimu, kuwa matajiri au maarufu; kwa ufupi, wanataka kuuona utajiri wa watoto wao ukizidi na kuzidi. Mipango na fantasia za watu ni timilifu; kwani hawajui kwamba idadi ya watoto walio nayo, umbo, uwezo na kadhalika wa watoto wao, si juu yao kuamua, kwamba hatima za watoto wao hazimo kamwe katika viganja vya mikono yao? Binadamu si waendeshaji wa hatima yao binafsi, ilhali wanatumai kubadilisha hatima ya kizazi kichanga zaidi; hawana nguvu za kutoroka hatima zao wenyewe, ilhali, wanajaribu kudhibiti zile za watoto wao wa kiume na kike. Je, hawazidishi ukadiriaji wao? Je, huu si ujinga na hali ya kutojua kwa upande wa binadamu? Watu huenda kwa mapana yoyote kwa minajili ya uzao wao, lakini hatimaye, idadi ya watoto aliyonayo mtu, na vile ambavyo watoto wake walivyo, si jibu la mipango na matamanio yao. Baadhi ya watu hawana hela lakini wanazaa watoto wengi; baadhi ya watu ni tajiri ilhali hawana mtoto. Baadhi wanataka binti lakini wananyimwa tamanio hilo; baadhi wanataka mtoto wa kiume lakini wanashindwa kuzaa mtoto wa kiume. Kwa baadhi, watoto ni baraka; kwa wengine, mtoto ni laana. Baadhi ya wanandoa ni werevu, ilhali wanawazaa watoto wanaoelewa polepole; baadhi ya wazazi ni wenye bidii na waaminifu, ilhali watoto wanaowalea ni wavivu. Baadhi ya wazazi ni wapole na wanyofu lakini wana watoto wanaogeuka na kuwa wajanja na wenye inda. Baadhi ya wazazi wana akili na mwili timamu lakini wanajifungua watoto walemavu. Baadhi ya wazazi ni wa kawaida na hawajafanikiwa ilhali watoto wao wanafanikiwa pakubwa. Baadhi ya wazazi ni wa hadhi ya chini ilhali watoto wanaowalea ni wenye taadhima. …
2. Baada ya Kulea Kizazi Kijacho, Watu Hufaidi Ufahamu Mpya wa Hatima Yao
Watu wengi wanaooa hufanya hivyo karibu kwenye umri wa miaka thelathini, na kwa wakati huu wa maisha, mtu hana ufahamu wowote wa hatima ya binadamu. Lakini wakati watu wanapoanza kulea watoto, kwa kadri uzao wao unapokua, wanatazama kizazi kipya kikirudia maisha na hali zote walizopitia katika kizazi cha awali, na wanaona maisha yao ya kale yakijionyesha kwao na wanatambua kwamba barabara inayotumiwa na kizazi kile kichanga zaidi, kama tu yao, haiwezi kupangwa wala kuchaguliwa. Wakiwa wamekabiliwa na hoja hii, hawana chaguo lolote bali kukubali kwamba hatima ya kila mtu iliamuliwa kabla; na bila ya hata kutambua wanaanza kwa utaratibu kuweka pembeni matamanio yao binafsi, na hisia kali katika mioyo yao inapungua na kuwatoka…. Kwenye kipindi hiki cha muda, mtu ameweza kupita sehemu nyingi zaidi na muhimu katika mafanikio ya maisha yake na ametimiza ufahamu mpya wa maisha, na kuchukua mtazamo mpya. Je, mtu wa umri huu anaweza kutarajia kwa siku za usoni kiasi kipi cha mambo na matarajio yake ni yapi? Ni mwanamke yupi mwenye umri wa miaka hamsini na mmoja angali anaota kuhusu Kaka Mwenye Mvuto na Haiba? Ni mwanamume yupi wa miaka hamsini na mmoja angali anatafuta Binti wa Kifalme Anayependeza? Ni mwanamke yupi wa umri wa kati atakuwa anatumai kugeuka kutoka kwa mtoto wa bata mwenye sura mbaya hadi batamaji? Je, wanaume wazee zaidi wangali wana msukumo sawa wa ajira na wanaume wachanga? Kwa ujumla, haijalishi kama mtu ni mwanamume au mwanamke, yeyote anayeishi na kuufikia umri huu anao uwezekano wa kuwa na mtazamo wa kueleweka na kutumika kiasi fulani katika ndoa, familia, na watoto. Mtu kama huyo, kimsingi hana machaguo yoyote yaliyobakia, hana msukumo wowote wa kukabiliana na hatima yake. Kwa mujibu wa kile ambacho binadamu amepitia, punde tu mtu anapofikia umri huu mtu huanza kwa kawaida kuwa na mtazamo kwamba “lazima mtu akubali hatima yake; watoto wake wanao utajiri wao binafsi; hatima ya binadamu inaamriwa Mbinguni.” Watu wengi ambao hawaelewi ukweli, baada ya kupitia mabadiliko, mahangaiko, na ugumu wote wa ulimwengu huu, watatoa muhtasari wa utambuzi wao wa maisha ya binadamu kwa maneno matatu: “Hiyo ndiyo hatima!” Ingawaje kauli hii inatoa muhtasari wa hitimisho ya watu wa ulimwengu na utambuzi kuhusu hatima ya binadamu, ingawaje inaelezea kutoweza kusaidika kwa binadamu na inaweza kusemekana kwamba inapenyeza na ni sahihi, ni kilio cha mbali kutoka kwa ufahamu wa ukuu wa Muumba, na si kibadala cha maarifa ya mamlaka ya Muumba.
3. Kusadiki Katika Hatima si Kibadala cha Maarifa ya Ukuu wa Muumba
Baada ya kuwa mfuasi wa Mungu kwa miaka mingi, je, kunayo tofauti kubwa katika maarifa yenu ya hatima na yale ya watu wa ulimwengu? Je, mmeelewa kwa kweli kule kuamuliwa kabla kwa Muumba, na unaweza kujua kwa kweli ukuu wa Muumba? Baadhi ya watu wanao ufahamu mkuu, wa kina wa kauli hii “hiyo ndiyo hatima,” ilhali hawasadiki hata kidogo katika ukuu wa Mungu, hawasadiki kwamba hatima ya binadamu hupangiliwa na kupangwa na Mungu, na hawako radhi kunyenyekea mbele ya ukuu wa Mungu. Watu kama hao ni kana kwamba wanaelea baharini, wanatoswatoswa na mawimbi, huku wakielea na kufuata mkondo wa maji, wasiwe na chaguo ila kusubiri kimyakimya na kuachia maisha yao hatima. Ilhali hawatambui hatima ya binadamu inategemea ukuu wa Mungu; hawawezi kujua ukuu wa Mungu wao binafsi, na hivyo basi kutimiza utambulisho wa mamlaka ya Mungu, kunyenyekea katika mipango na mipangilio ya Mungu, kuacha kukinzana na hatima na kuishi katika utunzwaji, ulinzi na mwongozo wa Mungu. Kwa maneno mengine, kukubali hatima si jambo sawa na kunyenyekea kwa ukuu wa Muumba; kusadiki hatima hakumaanishi kwamba mtu akubali, atambue, na ajue ukuu wa Muumba; kusadiki katika hatima ni ule utambulisho wa hoja hii na suala hili la nje, ambalo ni tofauti na kujua namna Muumba Anavyotawala hatima ya binadamu, kuanzia katika kutambua kwamba Muumba ndiye chanzo cha kutawala juu ya hatima za mambo yote na hata zaidi kunyenyekea kwa mipangona mipangilio ya Muumba kwa ajili ya hatima ya binadamu. Kama mtu anasadiki tu katika hatima—hata anahisi kwa kina kuihusu—lakini papo hapo hawezi kujua, kutambua, kunyenyekea, na kukubali ukuu wa Muumba kuhusu ile hatima ya binadamu basi maisha yake yatakuwa kwa kweli msiba mkuu, maisha yaliyopita kwa masikitiko, utupu; yeye atakuwa hawezi kutii utawala wa Muumba, kuwa binadamu aliyeumbwa katika hali ya kweli zaidi ya kauli hiyo, na kufurahia idhini ya Muumba. Mtu anayejua na kupitia kwa kweli ukuu wa Muumba anafaa kuwa katika hali amilifu, isiyo baridi au ya kutoweza kusaidika. Huku wakati uo huo akikubali kwamba mambo yote yanategemea hatima ya maisha, yeye anafaa kumiliki ufafanuzi sahihi wa maisha na hatima: kwamba kila maisha yanategemea ukuu wa Muumba. Wakati mtu anapoangalia nyuma kwenye barabara aliyotembelea, wakati mtu anapokusanya tena kila awamu ya safari ya maisha yake, mtu anaona kila hatua, haijalishi kama barabara ya mtu inakuwa mbaya au nzuri, Mungu alikuwa akiongoza njia ya mtu, akipanga kila kitu. Ilikuwa ni mipangilio ya umakinifu ya Mungu, upangiliaji Wake makinifu ulioongoza mtu, bila kujua, hadi kufikia leo. Ili kuweza kukubali ukuu wa Muumba, ili kupokea wokovu Wake—utajiri mwingi ulioje! Kama mtazamo wa mtu katika hatima ni wa baridi, inathibitisha kwamba yeye anakinzana na kila kitu ambacho Mungu amempangilia, kwamba yeye hana mtazamo wa kunyenyekea. Kama mtazamo wa mtu katika ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni amilifu, basi mtu anapotazama nyuma katika safari yake, wakati mtu anapong'amua kwa kweli ukuu wa Mungu, mtu huyo ataweza kutamani kwa dhati kunyenyekea kila kitu ambacho Mungu amepangilia, atakuwa na jitihada zaidi na ujasiri wa kumwacha Mungu kuunda hatima yake, ili kuacha kuasi dhidi ya Mungu. Kwani mtu anaona kwamba akikosa kuelewa hatima, wakati mtu haelewi ukuu wa Mungu, wakati mtu anapotutusa mbele kwa hiari yake, akichechemea na kupenyeza kwenye ukungu, safari inakuwa ngumu sana, ya kuvunja moyo. Kwa hivyo wakati watu wanapotambua ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu, wale walio werevu wanachagua kuijua na kuikubali, kuaga kwaheri siku zenye maumivu ambapo walijaribu kuwa na maisha mazuri kwa nguvu za mikono yao miwili, badala ya kuendelea kung’ang’ana dhidi ya hatima na kuzitafuta zile shabaha maarufu za maisha kwa njia yao wenyewe. Wakati mtu hana Mungu, wakati mtu hawezi kumwona Mungu, wakati hawezi kutambua waziwazi ukuu wa Mungu, kila siku inakosa maana, inakosa thamani, na kuwa yenye taabu. Popote pale mtu yupo, kazi yoyote ile anayofanya, mbinu za mtu za kuzumbua riziki na kutafuta shabaha zake huweza kumletea kitu kimoja ambacho ni kuvunjika moyo kusikoisha na mateso yasiyopona, kiasi cha kwamba mtu hawezi kuvumilia kuangalia nyuma. Ni pale tu mtu anapokubali ukuu wa Muumba, ananyenyekea katika mipangona mipangilio Yake, na kutafuta maisha ya kweli ya binadamu, ndipo mtu atakapokuwa huru kwa utaratibu dhidi ya kuvunjika moyo na kuteseka, kutupilia mbali utupu wote wa maisha.
4. Wale tu Wanaonyenyekea Ukuu wa Muumba Ndio Wanaweza Kupata Uhuru wa Kweli
Kwa sababu watu hawatambui mipango ya Mungu, na ukuu wa Mungu, siku zote wanakabiliana na hatima hiyo kwa kuasi, kwa mtazamo wa kuasi, na siku zote wanataka kutupilia mbali mamlaka na ukuu wa Mungu, na mambo yale ambayo hatima imewahifadhia, wakitumai kwamba watabadilisha hali zao za sasa na kubadilisha hatima yao. Lakini hawawezi kufaulu; wanazuiliwa kwa kila sehemu ya mabadiliko katika maisha. Mvutano huu, unaoendelea ndani ya nafsi ya mtu, ni wa maumivu; maumivu haya hayasahauliki; na wakati wote huu mtu anapoteza maisha yake mwenyewe. Sababu ya maumivu haya ni nini? Je, ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu au kwa sababu ya mtu kuzaliwa bila bahati? Bila shaka kati ya sababu hizi hakuna iliyo kweli. Kimsingi, ni kwa sababu ya njia ambazo watu huchukua, njia ambazo watu huchagua kuishi katika maisha yao. Baadhi ya watu huenda wasitambue mambo haya. Lakini unapojua kwa kweli, unapotambua kwa kweli kwamba Mungu anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, unapoelewa kwa kweli kwamba kila kitu ambacho Mungu amekupangilia na kukuamulia ni chenye manufaa makubwa, na ni ulinzi mkubwa, basi unahisi maumivu yako yakipungua kwa utaratibu, na uzima wako wote unaanza kutulia, kuwa huru na kukombolewa. Tukiamua kutokana na hali za wingi wa watu, ingawaje kwa kiwango cha kibinafsi hawataki kuendelea kuishi kama walivyokuwa wakiishi awali, ingawaje wanataka tulizo katika maumivu yao, kimsingi hawawezi kung’amua kwa kweli thamani na maana halisi ya ukuu wa Muumba ya hatima ya binadamu; hawawezi kutambua kwa kweli na kunyenyekea kwa ukuu wa Muumba, isitoshe kujua namna ya kutafuta na kukubali mipango na mipangilio ya Muumba. Kwa hivyo kama watu hawawezi kutambua hoja kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote ya binadamu, kama hawawezi kunyenyekea kwa kweli chini ya utawala wa Muumba, basi itakuwa vigumu sana kwao kutoendeshwa na kutiwa pingu za miguu na, fikira hii kwamba “hatima ya mtu imo kwenye mikono ya mtu,” itakuwa vigumu kwao kutupilia mbali maumivu ya kung’ang’ana kwao kwingi dhidi ya hatima na mamlaka ya Muumba, ni wazi kwamba hali hii pia itakuwa ngumu kwao katika kuweza kukombolewa kwa kweli na kuwa huru, kuwa watu wanaoabudu Mungu. Kunayo njia rahisi zaidi ile ya kujifanya kuwa huru kutoka katika hali hii: kuaga kwaheri njia yako ya awali ya kuishi, kuaga kwaheri shabaha zako za maisha za awali, kuhitimisha na kuchambua hali ya maisha ya awali, filosofia, mambo uliyofuatilia, matamanio, na maadili, na kisha kuyalinganisha yote haya na mapenzi ya Mungu na mahitaji ya binadamu, na kuona kama yoyote kati ya haya yanakubaliana na mapenzi na mahitaji ya Mungu, kujua kama yoyote kati ya haya yanakuletea maadili sahihi ya maisha, yanakuongoza katika ufahamu mwingi zaidi wa ukweli, na kuruhusu mtu kuishi kwa ubinadamu na mfano wa binadamu. Unapochunguza mara kwa mara na kuchambua kwa makini shabaha mbalimbali za maisha ambazo watu hufuatilia na njia zao tofauti za kuishi, utapata kwamba hata hakuna moja kati ya hizo zote ambayo inaingiliana na nia ya Muumba wakati Alipoumba binadamu. Zote hizi zinawavuta watu mbali na ukuu na utunzwaji wa Muumba; zote ni mitego ambayo binadamu hujipata amenaswa nayo, na ambayo inawaelekeza jehanamu. Baada ya kutambua haya, kazi yako ni kuweka pembeni mtazamo wako wa maisha ya awali, kuwa mbali na mitego mbalimbali, kumwachia Mungu kuchukua usukani wa maisha yako na kukufanyia mipangilio, jaribu tu kunyenyekea katika mipango na mwongozo wa Mungu, kutokuwa na chaguo, na kuwa mtu anayemwabudu Mungu. Haya yote yanaonekana kuwa rahisi, lakini ni jambo gumu kufanya. Baadhi ya watu wanaweza kuvumilia maumivu yake, wengine hawawezi. Baadhi wako radhi kutii, wengine hawako radhi. Wale wasiokuwa radhi wanakosa tamanio na uamuzi wa kufanya hivyo; wanayo habari kamili kuhusu ukuu wa Mungu, wanajua vyema kabisa kwamba ni Mungu anayepangilia na kupanga hatima ya binadamu, na ilhali wangali wanang'ang'ana tu, bado hawajaridhiana na nafsi zao kuhusiana na kuziacha hatima zao kwenye kiganja cha mkono wa Mungu na kunyenyekea katika ukuu wa Mungu, na zaidi, wanachukia mipango na mipangilio ya Mungu. Kwa hivyo, siku zote kutakuwa na baadhi ya watu wanaotaka kujionea wenyewe kile wanachoweza kufanya; wanataka kubadilisha hatima zao wenyewe kwa mikono yao miwili, au kutimiza furaha kwa kutumia nguvu zao wenyewe, kuona kama wanaweza kukiuka mipaka ya mamlaka ya Mungu na kuinuka juu ya ukuu wa Mungu. Huzuni ya binadamu, si kwamba binadamu anatafuta maisha mazuri, si kwamba anatafuta umaarufu na utajiri au anang'ang'ana dhidi ya hatima yake mwenyewe kupitia kwenye ukungu, lakini kwamba baada ya yeye kuona uwepo wa Muumba, baada ya yeye kujifunza hoja kwamba Muumba anao ukuu juu ya hatima ya binadamu, bado hawezi kurekebisha njia zake, hawezi kuvuta miguu yake kutoka kwenye mtego, lakini anaufanya moyo wake kuwa mgumu na anasisitizia makosa yake. Afadhali aendelee kutapatapa kwenye matope, akiapa kwa ukaidi dhidi ya ukuu wa Muumba, akiupinga mpaka mwisho wake mchungu, bila ya hata chembechembe kidogo ya majuto, na mpaka pale anapolazwa akiwa amevunjika na anavuja damu ndipo anapoamua hatimaye kusalimu amri na kugeuka na kubadilisha mwenendo. Kwa kweli huu ni huzuni kwa binadamu. Kwa hivyo Ninasema, wale wanaochagua kunyenyekea ni werevu na wale waliochagua kutoroka ni vichwa vigumu.
Kifo: Awamu ya Sita
Baada ya mahangaiko mengi na masikitiko mengi, na kuvunjwa moyo kwingi, baada ya furaha nyingi na huzuni nyingi na baada ya misukosuko ya maisha, baada ya miaka mingi sana isiyosahaulika, baada ya kutazama misimu ikipita na kujirudia, mtu hupita kwenye kiungo muhimu sana cha maisha bila ya arifa, na kwa ghafla tu mtu anajipata kwenye miaka yake ya kufifia. Alama za muda zimejichora kotekote kwenye mwili wa mtu: Mtu hawezi tena kusimama wima, kichwa cha nywele nyeusi kinageuka na kuwa cha nywele nyeupe, macho maangavu na mazuri yanabadilika na kuanza kufifiliza na kuwa na wingu mbele yao, nayo ngozi laini, yenye unyumbufu inageuka na kuwa na makunyanzi na madoadoa. Kusikia kwa mtu kunaanza kufifia, meno yake kulegea na kuanza kujiangukia, mwitikio wa mtu unaanza kuchelewachelewa, kutembea kunakuwa ni kwa kujikokota.... Wakati huu mtu ameaga kwaheri kabisa miaka yake ya nguvu ya ujana wake na kuingia katika maisha yake ya kwaheri: umri wa uzee. Kisha, mtu atakabiliana na kifo, awamu ya mwisho ya maisha ya binadamu.
1. Muumba Pekee Ndiye Anayeshikilia Nguvu za Maisha na Kifo juu ya Binadamu
Kama kuzaliwa kwa mtu kulipangiwa na maisha ya awali ya mtu, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa hatima hiyo. Kama kuzaliwa kwa mtu ndiyo mwanzo wa kazi maalum ya mtu ya maisha, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa kazi hiyo maalum. Kwa sababu Muumba amepangilia mseto maalum wa hali mbalimbali za kuzaliwa kwa mtu, ni wazi na dhahiri shahiri kwamba amepangilia pia mseto wa hali zisizobadilika kwa minajili ya kifo cha mtu. Kwa maneno mengine, hakuna anayezaliwa kwa bahati na hakuna kifo cha mtu ambacho hakitarajiwi, na si kuzaliwa, si kufa vyote vina uhusiano na maisha ya mtu ya awali na ya sasa. Hali za kuzaliwa na kifo cha mtu, vyote viliamuliwa kabla na Muumba; hii ni kudura ya mtu, hatima ya mtu. Kama vile tu mengi yanaweza kuzungumzwa kuhusu kuzaliwa kwa mtu, hata kifo cha kila mtu kitafanyika katika mseto tofauti katika hali maalum, hivyo basi urefu wa maisha tofauti miongoni mwa watu na njia tofauti pamoja na nyakati tofauti zinaandama vifo vyao. Baadhi ya watu wana nguvu na afya na ilhali wanakufa mapema; wengine ni wanyonge na wanauguaugua ilhali wanaishi hadi umri wa uzee, na wanaaga dunia kwa amani. Baadhi wanafarakana na dunia kutokana na sababu zisizokuwa za kawaida, wengine kutokana na sababu za kawaida. Baadhi wanakata roho wakiwa mbali na nyumbani, wengine wanayafumba macho yao wakiwa na wapendwa wao kando yao. Baadhi ya watu hufia hewani, wengine wakafia chini ya nchi. Wengine huzama chini ya maji, wengine nao kwenye majanga. Baadhi hufa asubuhi, wengine hufa usiku. ...Kila mtu hutaka kuzaliwa kwa heshima, maisha mazuri, na kifo kitukufu, hakuna mtu anayeweza kuendeleza hatima yake mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kukwepa ukuu wa Muumba. Hii ni hatima ya binadamu. Binadamu anaweza kufanya aina zote za mipango ya siku zote za usoni, lakini hakuna mtu anayeweza kupanga njia na muda wa kuzaliwa kwake na kuondoka kwake ulimwenguni. Ingawaje watu hufanya kila wawezalo kuepuka na kuzuia kuja kwa kifo chao, ilhali, bila wao kujua, kifo huwa kinakaribia polepole. Hakuna anayejua ni lini atakapofarakana na dunia au ni vipi atakavyofanya hivyo, isitoshe hata pale hayo yote yatakapofanyikia. Bila shaka, si binadamu wanaoshikilia nguvu za maisha na kifo, wala si kiumbe fulani kwenye ulimwengu wa kimaumbile, lakini ni Muumba, ambaye mamlaka yake ni ya kipekee. Maisha na kifo cha binadamu si zao la sheria fulani ya ulimwengu wa kimaumbile, lakini athari ya ukuu wa mamlaka ya Muumba.
2. Yule Asiyejua Ukuu wa Muumba Atahangaika kwa Woga wa Kifo
Wakati mtu anapoingia kwenye umri wa uzee, changamoto anazokabiliana nazo si kutosheleza mahitaji ya familia au kuanzisha maono makubwa katika maisha yake, lakini namna ya kuyaaga maisha yake, namna ya kukutana na mwisho wa maisha yake, namna ya kuweka kikomo kwenye mwisho wa uwepo wake binafsi. Ingawaje juujuu inaonekana kwamba watu hutilia makini kidogo kwa kifo, hakuna anayeweza kuepuka kuchunguza suala hili, kwani hakuna anayejua ikiwa ulimwengu mwingine uko kule upande mwingine wa kifo, ulimwengu ambao binadamu hawawezi kung’amua au kuhisi, ulimwengu wasiojua chochote kuuhusu. Hali hii huwafanya watu kuwa na wasiwasi kukabiliana na kifo moja kwa moja, wasiwasi wa kukabiliana nacho kama inavyostahili, na badala yake wanafanya kadri ya uwezo wao kuepuka mada hii. Na kwa hivyo mada hii humfanya kila mmoja kutishika kuhusu kifo, huongezea uzito kwenye fumbo hili kuhusiana na hoja hii isiyokwepeka ya maisha, huweka kivuli kisichoisha juu ya moyo wa kila mmoja.
Wakati mtu anapohisi mwili wake unaanza kudhoofika, wakati mtu anapohisi kwamba kifo chake chakaribia, mtu huhisi tishio, woga usioelezeka. Woga wa kifo humfanya mtu kuhisi kuwa mpweke zaidi na asiyejiweza, na kwa wakati huu mtu hujiuliza: Nilitoka wapi? Ninaenda wapi? Je, hivi ndivyo nitakavyokufa, huku maisha yangu yakinipita kwa haraka hivi? Je, huu ndio wakati unaoadhimisha mwisho wa maisha yangu? Ni nini, hatimaye, maana ya maisha? Maisha yana thamani gani, kwa kweli? Je, yanahusu umaarufu na utajiri? Je, yanahusu kulea familia? ... Haijalishi kama mtu amewahi kufikiria maswali haya mahususi, haijalishi ni vipi mtu ana woga wa kifo, katika kina cha moyo wa kila mmoja siku zote kuna tamanio la kutaka kuchunguza zaidi mafumbo, hisia zisizoeleweka kuhusu maisha, pamoja na haya yote, ni uhusiano wa karibu na ulimwengu wenyewe, na kutotaka kuuacha. Pengine hakuna anayeweza kufafanua zaidi ni nini ambacho binadamu huogopa, ni nini ambacho binadamu hutaka kuchunguza zaidi, na nini kile ambacho ana uhusiano wa karibu nacho na kinachomfanya kutotaka kuondoka au kukiacha nyuma …
Kwa sababu wanaogopa kifo, watu huwa na wasiwasi mno; kwa vile wanaogopa kifo, vipo vitu vingi ambavyo hawawezi kuachilia. Wakati wako karibu kufa, baadhi ya watu huhangaika kuhusu hiki au kile; wanakuwa na wasiwasi kuhusu watoto wao, wapendwa wao, utajiri wao, ni kana kwamba kwa kuwa na wasiwasi hivyo wanaweza kuondoa mateso na hofu ambayo kifo huleta, ni kana kwamba kwa kuendeleza aina fulani ya urafiki wa karibu na wale wanaoishi wanaweza kukwepa ile hali ya kutoweza kujisaidia na upweke unaoandamana na kifo. Katika kina cha moyo wa binadamu kunao woga usiokamilika, woga wa kuachwa na wapendwa, woga wa kutowahi kutuliza macho yako kwenye mbingu za samawati, woga wa kutowahi tena kuangalia ulimwengu huu yakinifu. Nafsi pweke, iliyozoeana na wapendwa wake, husita kuachilia mshiko wa maisha na kuondoka, ikiwa pekee, kuelekea kwenye ulimwengu usiojulikana, usiozoeleka.
3. Maisha ya Kuishi Ukitafuta Umaarufu na Utajiri Yatamwacha Mtu Akiwa na Hasara Akikabiliana na Kifo
Kwa sababu ya ukuu na kuamuliwa kabla kwa Muumba, nafsi pweke iliyoanza bila chochote kwa jina lake huweza kupata wazazi na familia, fursa ya kuwa mwanachama wa kizazi cha binadamu, fursa ya kupitia maisha ya binadamu na kuona ulimwengu; na pia inafaidi fursa ya kupitia ukuu wa Muumba, kujua uzuri wa uumbaji wa Muumba, na zaidi kuliko vyote, kujua na kutii mamlaka ya Muumba. Lakini watu wengi zaidi huwa hawatumii vizuri fursa hii nadra na ya kipekee. Mtu hutumia nguvu zake zote maishani akipigana dhidi ya hatima yake, akatumia muda wake wote akihangaika na akijaribu kulisha familia yake na akisafiri huku na kule kati ya kutafuta utajiri na hadhi katika jamii. Mambo ambayo watu huthamini ni familia, pesa, na umaarufu; wanaona mambo haya kuwa mambo yenye thamani zaidi katika maisha. Kila mtu hulalamikia hatima yake, ilhali bado wanazisukuma hatima hizi nyuma ya akili zao na wanabaki na maswali ambayo ni lazima zaidi kuchunguza na kuelewa: kwa nini binadamu yuko hai, namna ambavyo binadamu anafaa kuishi, ni nini maana na thamani ya maisha. Katika maisha yao yote, hata hivyo iwe miaka mingapi, wanakimbilia tu kuhusu kutafuta umaarufu na utajiri, mpaka ujana wao ukawaacha, mpaka wakawa na nywele za kijivu na makunyanzi kwenye uso wao; mpaka wakagundua utajiri na umaarufu ni vitu visivyoweza kusitisha mtu kuelekea katika udhaifu unaotokana na uzee, kwamba pesa haiwezi kujaza utupu wa moyo: mpaka wanapoelewa kwamba hakuna mtu ambaye anaachwa nje kutoka kwenye sheria ya kuzaliwa, kuwa mzee, magonjwa, na kifo, kwamba hakuna mtu anayeweza kutoroka hatima ile inayomsubiri. Mpaka tu pale ambapo anapolazimishwa kukabiliana na awamu ya mwisho maishani ndipo anapong’amua kwa kweli kwamba hata kama mtu anamiliki mamilioni ya mali, hata kama mtu anayo heshima na cheo kikubwa, hakuna anayeweza kutoroka kifo, kwamba kila mtu atarudi kwenye sehemu yake asilia: nafsi pweke, bila chochote kwa jina lake. Wakati mtu anapokuwa na wazazi, mtu husadiki kwamba wazazi wa mtu ni kila kitu; wakati mtu anapokuwa na mali, mtu hufikiri kwamba pesa ndio kitu cha muhimu, kwamba ni rasilimali za mtu maishani; wakati watu wanapokuwa na hadhi katika jamii, wanaishikilia na hata wanaweza kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya hadhi hiyo. Ni pale tu ambapo watu wanakaribia kuondoka ulimwenguni ndipo wanapotambua kwamba mambo yale waliyoishi katika maisha yao wakifuatilia si chochote bali mawingu yanayopita, hakuna chochote kati ya vitu hivi ambacho wanaweza kushikilia, hakuna hata chochote wanachoweza kwenda nacho, hakuna hata chochote kinachoweza kuwaondolea kifo, hakuna kile kinachoweza kuwapa ushirika au tulizo wakati nafsi yao inapokuwa pweke ikielekea kufa; na hata, hakuna kati ya hivyo vyote vinavyoweza kumpa mtu wokovu, na kuwaruhusu kushinda kifo. Umaarufu na utajiri ambao mtu hupata kwenye ulimwengu yakinifu humpa mtu kutosheka kwa muda, anasa ya kupita, hisia ya uwongo ya utulivu, na kumfanya mtu kupoteza njia. Na kwa hivyo watu, wanapong’ang’ana kila pahali kwenye bahari pana ya binadamu, wakitafuta amani, tulizo na utulivu wa moyo, wanafunikwa zaidi na zaidi na mawimbi. Wakati ambapo watu hawajapata maswali ambayo ni muhimu zaidi kuelewa—ni wapi wametoka, ni kwa nini wako hai, ni wapi wanakoenda na kadhalika—wanashawishiwa na umaarufu na utajiri, wanapotoshwa, wanadhibitiwa na vitu hivyo, na wanaishia kupotea bila kujua njia. Muda huyoyoma; miaka hupita kama kupepeswa kwa jicho; kabla ya mtu kutambua, mtu huaga kwaheri miaka yake bora zaidi ya maisha yake. Wakati mtu anakaribia kuondoka ulimwenguni, mtu anafika katika utambuzi wa taratibu kwamba kila kitu ulimwenguni kinamwacha polepole, kwamba mtu hawezi kushikilia tena vitu alivyomiliki; kisha mtu anahisi kwa kweli kwamba hamiliki chochote kamwe, kama mtoto mchanga anayelia ambaye ndio mwanzo amezaliwa na kubisha mlango ulimwenguni. Wakati huu, mtu anashawishiwa kutafakari kile ambacho amefanya maishani, thamani ya kuwa hai, ni nini maana yake, kwa nini mtu alikuja ulimwenguni; na wakati huu, mtu anaendelea kutaka kujua kama kweli kunayo maisha baada ya kifo, kama Mbinguni kweli ipo, kama kweli kunayo adhabu... Kwa kadri mtu anavyokaribia kifo, ndipo anavyotaka zaidi kuelewa maisha yanahusu nini haswa; kwa kadri mtu anavyokaribia kifo, ndipo moyo wake unapoonekana kuwa mtupu; kwa kadri mtu anavyokaribia kifo, ndipo anapohisi kuwa hawezi kusaidika; na kwa hivyo woga wa mtu kuhusu kifo unazidi kuwa mwingi siku baada ya siku. Kunazo sababu mbili zinazoelezea kwa nini watu huwa hivi wanapokaribia kifo: Kwanza, wako karibu kupoteza umaarufu na utajiri ambao maisha yao yalitegemea, wako karibu kuacha nyuma kila kitu kinachoonekana ulimwenguni; na pili, wako karibu kukabiliana, wakiwa peke yao, na ulimwengu usiojulikana, wenye mafumbo, himaya isiyojulikana ambapo wana woga wa kukanyaga guu lao kule, kule wasikokuwa na wapendwa na mbinu zozote za kupata msaada. Kwa hizo sababu mbili, kila mmoja anayekabiliana na kifo huhisi vibaya, hupitia hali ya wasiwasi na hujipata katika hali ya kutoweza kusaidika ambayo hawajawahi kupitia awali. Kwa hakika punde watu wanapofikia wakati huu ndipo wanapotambua kwamba kitu cha kwanza ambacho mtu lazima aelewe, anapokanyaga guu lake hapa duniani, ni wapi binadamu hutoka, kwa nini watu wako hai, nani anayeamuru hatima ya binadamu, ni nani anayekidhi mahitaji ya binadamu, na Aliye na ukuu juu ya uwepo wa binadamu. Hizi ndizo rasilimali za kweli za maisha, msingi muhimu kwa kuwepo kwa binadamu, kutojifunza namna ya kutosheleza familia ya mtu au namna ya kutimiza umaarufu na utajiri, kutojifunza namna ya kujitokeza katika umati au namna ya kuishi maisha mazuri zaidi, bila kutaja namna ya kutia fora na kushindana kwa ufanisi dhidi ya wengine. Ingawaje mbinu mbalimbali za kuishi ambazo watu huishi wakijaribu kumiliki zinaweza kumpa wingi wa tulizo la mali, hazijawahi kumpa mtu amani ya kweli moyoni na tulizo, lakini badala yake hufanya watu kila wakati kupoteza mwelekeo wao, kuwa na wakati mgumu kujidhibiti, kukosa kila fursa ya kujifunza maana ya maisha; na kuunda mawimbi fiche ya matatizo kuhusu namna ya kukabiliana kikamilifu na kifo. Kwa njia hii, maisha ya watu yanaharibika. Muumba hushugulikia kila mmoja bila mapendeleo, huku akipatia kila mmoja wetu fursa ya kutosha maisha yote ili kuweza kupitia na kujua ukuu Wake, ilhali ni mpaka tu kifo kinapokaribia, wakati kivuli cha kifo kinaponing’inia karibu na mtu, ndipo mtu huyu huanza kuona nuru—na kisha muda huwa umeyoyoma mno.
Watu huishi maisha yao wakitafuta pesa na umaarufu; wanashikilia nyuzi hizi, wakifikiri kwamba ndizo mbinu zao pekee za msaada, ni kana kwamba wakiwa nazo wangendeelea kuishi, wangejitoa kwenye hesabu ya wale watakaokufa. Lakini pale tu wanapokuwa karibu kufa ndipo wanapotambua namna ambavyo vitu hivi vilivyo mbali na wao, namna walivyo wanyonge mbele ya kifo, namna wanavyosambaratika kwa urahisi, namna walivyo wapweke na wasivyoweza kusaidika, na hawana popote pa kugeukia. Wanatambua kwamba maisha hayawezi kununuliwa kwa pesa au umaarufu, kwamba haijalishi mtu ni tajiri vipi, haijalishi cheo chake kilivyo cha hadhi, watu wote ni maskini kwa njia sawa na wanaofanya mambo bila mpango mbele ya kifo. Wanatambua kwamba pesa haiwezi kununua maisha, kwamba umaarufu hauwezi kufuta kifo, kwamba si pesa wala umaarufu vinaweza kurefusha maisha ya mtu kwa hata dakika moja, hata sekunde moja. Watu wanapohisi hivi zaidi, ndipo wanapotamani zaidi kuishi; watu wanapohisi hivi zaidi, ndipo wanapohofia kukaribia kwa kifo. Ni katika wakati huu tu ndipo wanapotambua kwa kweli kwamba maisha yao si yao, si yao kudhibiti, na kwamba mtu hana usemi kuhusu iwapo ataishi au atakufa, kwamba haya mambo yote yanapatikana nje ya udhibiti wa mtu.
4. Njoo Chini ya Utawala wa Muumba na Ukabiliane na Kifo kwa Utulivu
Wakati ule ambao mtu anazaliwa, nafsi ya mtu iliyo pweke inaanza kupitia maisha hapa duniani, inapitia mamlaka ya Muumba ambayo Muumba ameipangilia. Ni wazi kwamba, kwa mtu husika, ile nafsi, hii ni fursa nzuri kabisa ya kupata maarifa kuhusu ukuu wa Muumba, kujua mamlaka Yake na kuyapitia binafsi. Watu wanaishi maisha yao kulingana na sheria za hatima zilizowekwa wazi kwao na Muumba, na kwa mtu yeyote mwenye akili razini aliye na dhamiri, kuelewa ukuu wa Muumba na kutambua mamlaka yake kwenye mkondo wa miongo yao mbalimbali hapa nchini si jambo gumu kufanya. Kwa hivyo inafaa kuwa rahisi sana kwa kila mtu kutambua, kupitia kwa yale ambayo yeye mwenyewe amepitia maishani kwa kipindi cha miongo mbalimbali, kwamba hatima zote za binadamu zimeamuliwa kabla, na kung’amua au kujumlisha ni nini maana ya kuishi. Wakati uo huo ambao mtu anakumbatia mafunzo haya ya maisha, mtu ataelewa kwa utaratibu ni wapi maisha yanatokea, kunga’mua hasa ni nini ambacho moyo unahitaji kwa kweli, nini kitaongoza mtu kwenye njia ya kweli ya maisha, kazi maalum na shabaha ya maisha ya binadamu inafaa kuwa nini; na mtu ataanza kutambua kwa utaratibu kwamba kama mtu hataabudu Muumba, kama mtu hataingia kwenye utawala Wake, basi mtu anakabiliana na kifo—wakati nafsi iko karibu kukabiliana na Muumba kwa mara nyingine—moyo wa mtu utajazwa hofu na ugumu usio na mipaka. Kama mtu amekuwepo ulimwenguni kwa miongo kadhaa ilhali hajajua ni wapi maisha ya binadamu hutoka, angali hajatambua ni kwenye viganja vya mikono ya nani hatima ya binadamu huwa, basi si ajabu hataweza kukabiliana na kifo kwa utulivu. Mtu aliyepata maarifa ya ukuu wa Muumba baada ya kupitia miongo kadhaa ya maisha, ni mtu aliye na shukrani sahihi ya maana na thamani ya maisha; mtu aliye na kina cha maarifa kuhusu kusudi la maisha, aliye na hali halisi aliyopitia na anaelewa ukuu wa Muumba; na hata zaidi, mtu anayeweza kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Muumba. Mtu kama huyo anaelewa maana ya uumbaji wa Mungu wa mwanadamu, anaelewa kwamba binadamu anafaa kumwabudu Muumba, kwamba kila kitu anachomiliki binadamu kinatoka kwa Muumba na kitarudi kwake siku fulani isiyo mbali sana kwenye siku za usoni; mtu kama huyo anaelewa kwamba Muumba hupangilia kuzaliwa kwa binadamu na ana ukuu juu ya kifo cha binadamu, na kwamba maisha na kifo vyote vimeamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba. Kwa hiyo, wakati mtu anapong’amua mambo haya, mtu ataanza kuweza kukabiliana na kifo kwa utulivu na kwa kawaida, kuweka pembeni mali yake yote ya dunia kwa utulivu, kukubali na kunyenyekea kwa furaha kwa yote yatakayofuata, na kukaribisha awamu ya mwisho ya maisha iliyopangiliwa na Muumba badala ya kutishika vivyo hivyo tu na kung’ang’ana dhidi ya kifo. Ikiwa mtu anayaona maisha kama fursa ya kupitia ukuu wa Muumba na kujua mamlaka yake, ikiwa mtu anayaona maisha yake kama fursa nadra ya kutekeleza wajibu wake akiwa binadamu aliyeumbwa na kutimiza kazi yake maalum, basi mtu atakuwa ana mtazamo sahihi wa maisha, ataishi maisha yaliyobarikiwa na yanayoongozwa na Muumba, atatembea kwenye nuru ya Muumba, atajua ukuu wa Muumba, atakuwa katika utawala Wake, atakuwa shahidi wa matendo Yake ya kimiujiza na mamlaka Yake. Ni wazi kwamba, mtu kama huyo atahitajika kupendwa na kukubaliwa na Muumba, na mtu kama huyo ndiye anaweza kushikilia mtazamo mtulivu mbele ya kifo, na anayeweza kukaribisha awamu hii ya mwisho kwa furaha. Bila shaka Ayubu alikuwa na mtazamo kama huu kwa kifo; alikuwa katika nafasi ya kukubali kwa furaha awamu ya mwisho ya maisha, na baada ya kuhitimisha safari yake ya maisha vizuri, baada ya kukamilisha kazi yake maalum alirudi upande wa Muumba.
5. Bidii na Faida za Ayubu katika Maisha Zamruhusu Kukabiliana na Kifo kwa Utulivu
Katika Maandiko imeandikwa kuhusu Ayubu: “Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana na mwenye kujawa na siku.” (Ayubu 42:17). Hii inamaanisha kwamba wakati Ayubu alipoaga dunia, hakuwa na majuto na hakuhisi maumivu, lakini aliondoka kimaumbile ulimwenguni. Kama vile kila mmoja anavyojua, Ayubu alikuwa mwanamume aliyemcha Mungu na aliyeambaa maovu alipokuwa hai; Mungu alimpongeza kwa matendo yake ya haki, watu waliyakumbuka, na maisha yake, zaidi ya yeyote yule mwengine, yalikuwa na thamani na umuhimu. Ayubu alifurahia baraka za Mungu na aliitwa mtakatifu na Yeye hapa duniani, na aliweza pia kujaribiwa na Mungu na kujaribiwa na Shetani; alisimama kuwa shahidi wa Mungu na alistahili kuwa mtu mtakatifu. Kwenye miongo mbalimbali baada ya kujaribiwa na Mungu, aliishi maisha ambayo yalikuwa yenye thamani zaidi, yenye maana zaidi, yaliyokita mizizi, na yenye amani zaidi kuliko hata awali. Kutokana na matendo yake ya haki, Mungu alimjaribu; kwa sababu ya matendo yake ya haki, Mungu alionekana kwake na kuongea naye moja kwa moja. Kwa hiyo, kwenye miaka yake baada ya kujaribiwa, Ayubu alielewa na kushukuru thamani ya maisha kwa njia thabiti zaidi, aliweza kutimiza ufahamu wa kina zaidi wa ukuu wa Muumba, na akapata maarifa yenye hakika na usahihi zaidi kuhusu namna ambavyo Muumba anavyotoa na kuzichukua baraka zake. Biblia inarekodi kwamba Yehovah Mungu alimpa hata baraka nyingi zaidi Ayubu kuliko hapo awali, Akimweka Ayubu katika nafasi bora zaidi ya kujua ukuu wa Muumba na kujua kukabiliana na kifo akiwa mtulivu. Kwa hiyo, Ayubu alipozeeka na kukabiliana na kifo, bila shaka asingekuwa na wasiwasi na mali yake. Hakuwa na wasiwasi wowote, hakuwa na chochote cha kujutia, na bila shaka hakuogopa kifo; kwani aliishi maisha yake akitembea ile njia ya kumcha Mungu, kuepuka maovu, na hakuwa na sababu yoyote ya kuwa na wasiwasi kuhusu mwisho wake mwenyewe. Ni watu wangapi leo wanaweza kuchukua hatua kwa njia zote hizo ambazo Ayubu alitumia alipokabiliwa na kifo chake mwenyewe? Kwa nini hakuna mtu anayeweza kuendeleza mwelekeo wa mtazamo rahisi kama huu? Kunayo sababu moja tu: Ayubu aliishi maisha kwenye harakati ya kutafuta kimsingi kusadiki, utambuzi, na unyenyekevu kwa ukuu wa Mungu, na ilikuwa katika kusadiki huku, utambuzi huu na unyenyekevu huu ambapo aliweza kupitia zile awamu muhimu za maisha, aliishi kwa kudhihirisha miaka yake ya mwisho na akajuliana hali na awamu yake ya mwisho ya maisha. Licha ya kile ambacho Ayubu alipitia, bidii zake na shabaha zake katika maisha zilikuwa za furaha na wala si zenye maumivu. Alikuwa na furaha si tu kwa sababu ya baraka au shukrani aliyopewa yeye na Muumba, lakini muhimu zaidi kwa sababu ya shughuli zake na shabaha za maisha, kwa sababu ya maarifa yaliyoongezeka kwa utaratibu na ufahamu wa kweli wa ukuu wa Muumba ambao alitimiza kupitia kwa kumcha Mungu na kwa kuepuka maovu, na zaidi, kwa sababu ya matendo Yake ya maajabu ambayo Ayubu alipitia kibinafsi wakati huu akiwa chini ya ukuu wa Muumba, na hali aliyopitia yenye uchangamfu na isiyosahaulika na kumbukumbu za kuwepo kwake, kuzoeana na wenzake, na kuzoeana kati yake yeye na Mungu; kwa sababu ya tulizo na furaha zilizotokana na kujua mapenzi ya Muumba; kwa sababu ya kustahi kulikotokea baada ya kuona kwamba Yeye ni mkubwa, ni wa ajabu, Anayependeka, na ni mwaminifu. Sababu ya Ayubu kuweza kukabiliana na kifo bila ya kuteseka ni kwamba alijua kwamba, kwa kufa, angerudi kwenye upande wa Muumba. Na zilikuwa shughuli zake katika maisha zilizomruhusu kukabiliana na kifo akiwa ametulia, kukabiliana na matarajio ya Muumba kuchukua tena maisha yake, kwa moyo mzuri, na zaidi ya yote, kusimama wima, kutotikisika na kuwa huru kutokana na mashaka mbele ya Muumba. Je, watu wanaweza siku hizi kutimiza aina ya furaha ambayo Ayubu alikuwa nayo? Je, nyinyi wenyewe mko katika hali ya kufanya hivyo? Kwa sababu watu siku hizi wako hivyo, kwa nini hawawezi kuishi kwa furaha, kama alivyofanya Ayubu? Kwa nini hawawezi kutoroka mateso yanayotokana na woga wa kifo? Wakati wanapokabiliwa na kifo, baadhi ya watu hujiendea haja ndogo; wengine hutetemeka, wakazirai, na wakalalamika dhidi ya Mbinguni na binadamu vilevile, wengine hata wakalia kwa huzuni na kutokwa machozi. Kwa vyovyote vile, hii ndiyo miitikio ya ghafla inayofanyika wakati kifo kinapokaribia. Watu huwa na tabia hii ya kuaibisha haswa kwa sababu, ndani ya mioyo yao, wanaogopa kifo, kwa sababu hawana maarifa yaliyo wazi na uwezo wa kushukuru ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hata kujinyenyekeza mbele ya vitu hivi; kwa sababu watu hawataki chochote ila kupangilia na kutawala kila kitu wenyewe, kudhibiti hatima zao binafsi, maisha yao binafsi na hata kifo. Si ajabu, hivyo basi, kwamba watu hawajawahi kuweza kuacha woga wa kifo.
6. Ni kwa Kukubali tu Ukuu wa Muumba Ndipo Mtu Anaweza Kurejea Upande Wake
Wakati mtu hana maarifa yaliyo wazi na hajapitia ukuu wa Mungu na mipangilio Yake, maarifa ya mtu kuhusu hatima na yale ya kifo yatakuwa yale yasiyoeleweka. Watu hawawezi kuona waziwazi kwamba haya yote yamo kwenye kiganja cha mkono wa Mungu, hawatambui kwamba Mungu ameushika usukani na Anashikilia ukuu juu yao, hawatambui kwamba binadamu hawezi kutupa nje au kutoroka ukuu kama huo; na kwa hivyo wakati wanapokabiliwa na kifo hakuna mwisho wowote katika maneno yao ya mwisho, wasiwasi wao, na hata majuto. Wanalemewa sana na mambo mengi, wanajivuta ajabu, kunakuwa na mkanganyo mkubwa, na haya yote yanawafanya kuogopa kifo. Kwani mtu yeyote aliyezaliwa ulimwenguni humu, kuzaliwa kwake kunahitajika, na kuaga kwake hakuwezi kuepukika, na hakuna mtu anayeweza kuupiga chenga mkondo huu. Kama mtu atataka kuondoka ulimwenguni humu bila maumivu, kama mtu atataka kukabiliana na awamu ya mwisho ya maisha bila kusitasita au wasiwasi, njia pekee ni kutokuwa na majuto. Na njia pekee ya kuondoka bila majuto ni kujua ukuu wa Muumba, kujua mamlaka yake, na kunyenyekea mbele zake. Ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuwa mbali na mahangaiko ya binadamu, maovu, utumwa wa Shetani; ni kwa njia hii ndipo mtu anaweza kuishi maisha kama ya Ayubu, akiongozwa na akibarikiwa na Muumba, maisha yaliyo huru na yaliyokombolewa, maisha yenye thamani na maana, maisha yenye uaminifu na moyo wazi; ni kupitia kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kunyenyekea, kama Ayubu, kujaribiwa na kunyang’anywa na Muumba, kunyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Muumba; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kumwabudu Muumba maisha yake yote na kuweza kupata pongezi Lake, kama Ayubu alivyopata, na kusikia sauti Yake, kumwona akionekana; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi na kufa kwa furaha, kama Ayubu, bila ya maumivu, bila wasiwasi, bila majuto; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi kwa nuru, kama Ayubu, kupita kila mojawapo ya awamu ya maisha kwa nuru, na kukamilisha vizuri safari yake kwa nuru, kutimiza kwa ufanisi kazi yake maalum—kupitia, kujifunza, na kujua ukuu wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa—na kuiaga dunia kwa nuru, na milele hadi milele kusimama upande wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa, kilichopongezwa na Yeye.
Usikose Fursa ya Kujua Ukuu wa Muumba
Awamu sita zilizofafanuliwa hapo juu ni awamu muhimu zilizowekwa wazi na Muumba ambazo kila mtu wa kawaida lazima apitie katika maisha yake. Kila mojawapo ya awamu hizi ni za kweli; hakuna mojawapo kati yazo ambayo inaweza kuepukwa, na zote zinasheheni uhusiano na kuamuliwa kabla kwa Muumba na ukuu Wake. Hivyo basi kwa binadamu, kila mojawapo ya awamu hizi ni sehemu muhimu ya kujikagua, na namna ya kupitia kila mojawapo vizuri ni suala muhimu sana ambalo nyinyi nyote mnakabiliwa nalo.
Mkusanyiko wa miongo ambayo inaunda maisha ya binadamu si mirefu sana wala mifupi sana. Miaka ishirini na-kitu iliyopo katikati ya kuzaliwa na kukomaa hupita kwa muda mfupi tu wa kupepesa jicho, na ingawaje wakati huu katika maisha mtu anachukuliwa kuwa mtu mzima, watu katika kundi hili la umri wanajua machache sana kuhusu maisha ya binadamu na hatima ya binadamu. Wanapozidi kupata uzoefu zaidi, ndipo wanapopiga hatua kwa utaratibu hadi kwenye umri wa miaka ya kati. Watu katika miaka yao ya thelathini na arubaini huanza kuupata uzoefu unaoanza kuota wa maisha na hatima yake, lakini fikira zao kuhusu mambo haya zingali na ukungu mwingi sana akilini mwao. Si mpaka umri wa arubaini ndipo baadhi ya watu huanza kumwelewa binadamu na ulimwengu, vilivyoumbwa na Mungu, na kung’amua kwamba maisha ya binadamu yanahusu tu, kile ambacho hatima ya binadamu inahusu. Baadhi ya watu, ingawaje wamekuwa wafuasi wa muda mrefu wa Mungu na sasa wanao umri wa kati, bado hawamiliki maarifa na ufafanuzi sahihi wa ukuu wa Mungu, sikwambii hata unyenyekevu wa kweli. Baadhi ya watu hawajali chochote isipokuwa namna ya kupokea baraka, na ingawaje wameishi kwa miaka mingi, hawajui au hawaelewi hata kidogo hoja ya ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu, na kwa hivyo bado hawajaingia hata kwenye kipindi cha matendo halisi cha kunyenyekea katika mipango na mipangilio ya Mungu. Watu kama hao ni wajinga kabisa; watu kama hao wanaishi maisha yao bure bilashi.
Kama maisha ya binadamu yangegawanywa kulingana na kiwango cha mtu cha kile alichopitia maishani na maarifa yake kuhusu hatima ya binadamu, basi yangegawanywa kwa sura tatu. Sura ya kwanza ni ujana, miaka ile ya kati ya kuzaliwa na umri wa kati, au kuanzia kuzaliwa hadi kugonga miaka thelathini. Sura ya pili ni ya ukomavu, kuanzia umri wa miaka ya kati hadi umri wa uzee, au kuanzia thelathini hadi sitini. Na sura ya tatu ni kile kipindi cha uzee wa mtu, kuanzia umri wa uzee, kuanzia miaka sitini hivi, mpaka pale mtu anapoondoka ulimwenguni. Kwa maneno mengine, kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka ya kati, maarifa ya watu wengi kuhusu hatima na maisha ni finyu na ni yale ya kuiga tu kama kasuku, fikira za wengine yanayokosa hali halisi iliyo ya kweli na ya matendo. Kwenye kipindi hiki, mtazamo wa mtu kuhusu maisha, na namna ambavyo mtu anapojipanga katika ulimwengu vyote ni vya juujuu na vinyonge sana. Hiki ndicho kipindi cha mtu cha utoto. Baada tu ya mtu kuonja furaha na huzuni zote za maisha ndipo anapofaidi na kupata ufahamu halisi wa hatima, ndipo mtu—kwa kufichika akilini, na ndani kabisa ya moyo wake—huanza kwa utaratibu kushukuru kutoweza kurudishwa nyuma kwa hatima, na kuanza kutambua polepole kwamba ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu kwa kweli upo. Kwa kweli hiki ndicho kipindi cha kuanza kukomaa kwa mtu. Baada ya mtu kusita kupambana dhidi ya hatima, na pale ambapo mtu hayuko radhi tena kuvutwa kwenye mabishano, lakini anajua msimamo wake, anajinyenyekeza kwa mapenzi ya Mbinguni, na kujumlisha mafanikio na makosa ya maisha ya mtu huyo, na anasubiria hukumu ya Muumba kwa maisha ya mtu—hiki ni kipindi cha ukomavu. Tukitilia maanani aina hizi tofauti za kile mtu amepitia na kufaidi ambako watu hupata kwenye vipindi hivi vitatu, katika hali za kawaida fursa ya mtu ya kujua ukuu wa Muumba si kubwa sana. Kama mtu ataishi kufikisha umri wa miaka sitini, mtu anayo miaka thelathini tu au karibu na hapo kuujua ukuu wa Mungu; kama mtu atataka kipindi kirefu zaidi cha muda, hilo linawezekana tu kama maisha ya mtu yatakuwa marefu zaidi, tuseme kama mtu ataweza kuishi karne moja. Kwa hivyo Ninasema, kulingana na kanuni za sheria za kawaida za uwepo wa binadamu, ingawaje ni mchakato mrefu sana kuanzia wakati ule mtu anakumbana na mada ya kujua ukuu wa Muumba hadi pale ambapo mtu anaweza kutambua hoja ya ukuu wa Muumba, na kutoka hapo mpaka pale ambapo mtu anaweza kujinyenyekeza kwa utawala huo, kama kwa hakika mtu atahesabu miaka hiyo, miaka hiyo haizidi thelathini au arubaini hivi ambapo mtu anayo fursa ya kufaidi haya yote. Na mara nyingi, watu hujisahau kutokana na matamanio yao na malengo yao ya kupokea baraka; hawawezi kutambua ni wapi ambapo kiini halisi cha maisha ya binadamu kipo, hawang’amui umuhimu wa kujua ukuu wa Muumba, na kwa hivyo hawafurahii fursa hii yenye thamani ya kuingia kwenye ulimwengu wa binadamu kuhusiana na maisha ya binadamu na kile alichopitia, kupitia ukuu wa Muumba, na hawatambui namna lilivyo jambo la thamani kwa kiumbe chochote kilichoumbwa kupokea mwongozo wa kibinafsi kutoka kwa Muumba. Kwa hivyo Ninasema, watu wale wanaotaka kazi ya Mungu kuisha haraka, wanaopenda Mungu angepangilia mwisho wa binadamu haraka iwezekanavyo, ili waweze mara moja kutazama hali Yake halisi na muda si muda kubarikiwa, wanayo hatia ya aina mbaya zaidi ya kutotii na ujinga wa kupindukia. Na kwa wale wanaotamani, kwenye muda wao finyu, kung’amua fursa hii ya kipekee ili kuujua ukuu wa Muumba, hao ni watu werevu, wenye akili zao. Matamanio haya mawili tofauti yanafichua mitazamo miwili tofauti na shughuli za kufuatilia: Wale wanaotafuta baraka ni wachoyo na waovu; hawatilii maanani mapenzi yoyote ya Mungu, wala hawatafuti kujua ukuu wa Mungu, wasiwahi kutamani kujinyenyekeza katika utawala huo, wanataka kuishi tu wanavyopenda. Wao ni watovu wa wema; wao ndio wanaofaa kuangamizwa. Wale wanaotafuta kumjua Mungu wanaweza kuweka pembeni matamanio yao, wako radhi kujinyenyekeza kwa ukuu wa Mungu na mipangilio ya Mungu; wanajaribu kuwa aina ya watu ambao wananyenyekea katika mamlaka ya Mungu na kutimiza tamanio la Mungu. Watu kama hao huishi kwa nuru, huishi katikati ya baraka za Mungu; kwa hakika wataweza kupongezwa na Mungu. Haijalishi ni nini, chaguo la binadamu halina manufaa, binadamu hawana kauli yoyote kuhusiana na muda gani ambao kazi ya Mungu itachukua. Ni bora zaidi kwa watu kujiweka katika huruma ya Mungu, kunyenyekea katika ukuu Wake. Usipojiweka katika huruma Yake, ni nini utakachofanya? Je, Mungu atakuwa na hasara yoyote? Usipojiweka katika huruma Yake, ukijaribu kuushika usukani, unafanya chaguo la kijinga, na wewe tu ndiwe utakayepata hasara hatimaye. Endapo tu watu watashirikiana na Mungu haraka iwezekanavyo, endapo tu watafanya hima kukubali mipango Yake, kujua mamlaka Yake, na kutambua yote ambayo Amewafanyia, ndipo watakuwa na tumaini, ndipo maisha yao yatapata maana na kuepuka kuwa hapo tu, ndipo watakapopata wokovu.
Hakuna Anayeweza Kubadilisha Hoja Kwamba Mungu Anashikilia Ukuu juu ya Hatima ya Binadamu
Baada ya kusikiliza kila kitu Nilichomaliza kusema, je, fikira yenu ya hatima imebadilika? Mnaelewa vipi hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Ili kuiweka kwa urahisi, katika mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi mbovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye mzingo wa hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali isiyoshindika ya mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanavyodhibiti na kutawala ulimwengu. Ni hii hali ya kutoshindika, mfumo huu wa kudhibiti na kutawala, ambao unawajibikia sheria zinazoamuru maisha ya mambo yote, zinazoruhusu binadamu kuweza kuhama hadi kwenye mwili tofauti baada ya kifo tena na tena bila uingiliaji kati, zinazofanya ulimwengu kugeuka mara kwa mara na kusonga mbele, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka. Mmeshuhudia hoja hizi zote na unazielewa, haijalishi kama ni za juujuu ama ni za kina; kina cha ufahamu wako kinategemea kile unachopitia na maarifa ya ukweli, na maarifa yako kuhusu Mungu. Kujua kwako vyema uhalisia wa ukweli, ni kiwango kipi ambacho umepitia matamshi ya Mungu, ni vipi unajua vyema hali halisi ya Mungu na tabia yake—hii inawakilisha kina cha ufahamu wako wa ukuu na mipangilio ya Mungu. Je, uwepo wa ukuu wa Mungu na mipangilio unategemea kama binadamu wanainyenyekea? Je, hoja kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya inaamuliwa na kama binadamu watayanyenyekea? Mamlaka ya Mungu yapo licha ya hali mbalimbali; katika hali zote, Mungu anaamuru na kupangilia hatima ya kila binadamu na mambo yote kulingana na fikira Zake, mapenzi Yake. Hali hii haitabadilika kwa sababu binadamu hubadilika, na iko huru wala haitegemei mapenzi ya binadamu, haiwezi kubadilishwa na mabadiliko yoyote ya muda, anga, na jiografia, kwani mamlaka ya Mungu ndiyo hali yake halisi kabisa. Kama binadamu anaweza kujua na kuukubali ukuu wa Mungu, na kama binadamu anaweza kuunyenyekea, haiwezi kwa vyovyote vile kubadilisha hoja kwamba ukuu wa Mungu upo juu ya hatima ya binadamu. Hivi ni kusema kwamba, haijalishi ni mtazamo gani ambao binadamu atachukua kwa ukuu wa Mungu, hauwezi tu kubadilisha hoja kwamba Mungu anashikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote. Hata kama hutanyenyekea katika ukuu wa Mungu, angali Anaamuru hatima yako; hata kama huwezi kujua ukuu Wake, mamlaka Yake yangali yapo. Mamlaka ya Mungu na hoja ya ukuu wa Mungu dhidi ya hatima ya binadamu viko huru dhidi ya mapenzi ya binadamu, havibadiliki kulingana na mapendeleo na machaguo yako ya binadamu. Mamlaka ya Mungu yapo kila mahali, kila saa, kila muda. Kama mbingu na nchi zingepita, mamlaka Yake yasingewahi kupita, kwani Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anamiliki mamlaka ya kipekee, na mamlaka Yake hayazuiliwi au kuwekewa mipaka na watu, matukio, au vitu, na anga au na jiografia. Siku zote Mungu hushikilia mamlaka Yake, huonyesha uwezo Wake, huendeleza usimamizi Wake wa kazi kama kawaida; kila wakati Anatawala viumbe wote, hutosheleza viumbe wote, huunda na kupangilia viumbe wote, kama Alivyofanya siku zote. Hakuna anayeweza kubadilisha hili. Hii ni hoja; huu umekuwa ukweli usiobadilika tangu zama za kale!
Mtazamo na Matendo Bora ya Mtu Anayependa Kujinyenyekeza katika Mamlaka ya Mungu
Mwanadamu anatakiwa kuwa na mtazamo gani sasa katika kujua na kujali mamlaka ya Mungu, hoja ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu? Hili ni tatizo la kweli linalokabili kila mmoja. Wakati wa kukabiliana na matatizo ya kweli ya maisha, unafaa kujua na kuelewa vipi mamlaka ya Mungu na ukuu Wake? Wakati hujui namna ya kuelewa, kushughulikia, na kupitia matatizo haya, ni mtazamo gani unaofaa kutumia ili kuonyesha nia yako, tamanio lako, na uhalisia wako wa kujinyenyekeza katika ukuu na mipangilio ya Mungu? Kwanza lazima ujifunze kusubiri; kisha lazima ujifunze kutafuta; kisha lazima ujifunze kujinyenyekeza. “Kusubiri” kunamaanisha kusubiria muda wa Mungu, kusubiria watu, matukio, na mambo ambayo Amekupangilia wewe, kusubiria mapenzi Yake ili yaweze kwa utaratibu kujifichua kwako. “Kutafuta” kunamaanisha kuangalia na kuelewa nia za Mungu katika fikira Zake kwako wewe kupitia watu, matukio, na mambo ambayo Amekuwekea wazi, kuelewa ukweli kupitia mambo hayo, kuelewa kile ambacho binadamu lazima watimize na njia ambazo lazima waendeleze, kuelewa kile ambacho lazima kitimizwe na njia ambazo lazima wahifadhi, waelewe ni matokeo gani ambayo Mungu analenga kutimiza kwa binadamu na ni utimilifu gani Analenga kutimiza ndani yao. “Kujinyenyekeza,” bila shaka, kunaashiria kukubali watu, matukio, na mambo ambayo Mungu amepanga, kukubali ukuu Wake na, kwa yote, kupata kujua namna ambavyo Muumba anaamuru hatima ya binadamu, namna Anavyomjaliza binadamu na maisha Yake, na namna Anavyofanya kazi ya ukweli katika binadamu. Mambo yote katika mipangilio na ukuu wa Mungu hutii sheria za kimaumbile, na kama utaamua kumwachia Mungu kupangilia na kuamuru kila kitu kwa niaba yako, unafaa kujifunza kusubiri, unafaa kujifunza kutafuta, unafaa kujifunza kujinyenyekeza. Huu ndio mtazamo ambao kila mtu anayetaka kujinyenyekeza katika mamlaka ya Mungu lazima awe nao, ubora wa kimsingi ambao kila mmoja anayetaka kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu lazima aumiliki. Ili kushikilia mtazamo kama huu, kumiliki ubora kama huu, lazima mfanye kazi kwa bidii zaidi; na ndipo mnapoweza kuingia kwenye uhalisi wa kweli.
Kumkubali Mungu kama Bwana Wenu wa Kipekee Ndiyo Hatua ya Kwanza katika Kutimiza Wokovu
Ukweli kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni ukweli ambao kila mmoja lazima atilie maanani kwa umakinifu, lazima apitie na aelewe katika moyo wake; kwani ukweli huu unao mwelekeo katika maisha ya kila mmoja, kwenye maisha ya kale, ya sasa, na ya siku za usoni ya kila mmoja, kwenye awamu muhimu ambazo kila mtu lazima apitie maishani, katika maarifa ya binadamu kuhusu ukuu wa Mungu na mtazamo ambao anafaa kuwa nao katika mamlaka ya Mungu, na kawaida, kwa kila hatima ya mwisho ya kila mmoja. Kwa hivyo inachukua nguvu za maisha yako yote kujua na kuyaelewa. Unapochukua mamlaka ya Mungu kwa umakinifu, unapoukubali ukuu wa Mungu, kwa utaratibu utaanza kutambua na kuelewa kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo. Lakini kama hutawahi kutambua mamlaka ya Mungu, hutawahi kukubali ukuu Wake, basi haijalishi ni miaka mingapi utakayoishi, hutafaidi hata chembe maarifa ya ukuu wa Mungu. Kama hutajua na kuelewa kwa kweli mamlaka ya Mungu, basi utakapofika mwisho wa barabara, hata kama utakuwa umesadiki katika Mungu kwa miongo mingi, hutakuwa na chochote cha kuonyesha katika maisha yako, maarifa yako ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu yatakuwa kwa hakika sufuri bin sufuri. Huoni kuwa jambo hili ni la huzuni mno? Kwa hivyo haijalishi umetembea kwa umbali gani maishani, haijalishi unao umri wa miaka mingapi sasa, haijalishi safari inayosalia itakuwa ya umbali gani, kwanza lazima utambue mamlaka ya Mungu na kuyamakinikia, ukubali hoja kwamba Mungu ni Bwana wako wa kipekee. Kutimiza maarifa yaliyo wazi, sahihi na kuelewa ukweli huu kuhusiana na ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni funzo la lazima kwa kila mmoja, ndio msingi wa kuyajua maisha ya binadamu na kutimiza ukweli, ndiyo maisha ya kila siku na mafunzo ya kimsingi ya kumjua Mungu ambayo kila mmoja anakabiliana nayo, na ambayo hakuna yeyote anayeweza kuyakwepa. Kama baadhi yenu mngependa kuchukua njia za mkato ili kufikia shabaha hii, basi Ninawaambia, hilo haliwezekani! Kama baadhi yenu mwataka kukwepa ukuu wa Mungu, basi hilo nalo ndilo haliwezekani zaidi! Mungu ndiye Bwana wa pekee wa binadamu, Mungu ndiye Bwana wa pekee wa hatima ya binadamu, na kwa hivyo haiwezekani kwa binadamu kuamuru hatima yake mwenyewe, haiwezekani kwake kuishinda. Haijalishi uwezo wa mtu ni mkubwa kiasi kipi, mtu hawezi kuathiri, sikwambii kuunda, kupangilia, kudhibiti, au kubadilisha hatima za wengine. Yule Mungu Mwenyewe wa kipekee ndiye Anayeweza kuamuru tu mambo yote kwa binadamu, kwani Yeye tu ndiye anayemiliki mamlaka ya kipekee yanayoshikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu; na kwa hivyo Muumba pekee ndiye Bwana wa kipekee wa binadamu. Mamlaka ya Mungu yanashikilia ukuu sio tu juu ya binadamu walioumbwa, lakini juu ya hata viumbe ambavyo havikuumbwa visivyoweza kuonekana na binadamu, juu ya nyota, juu ya ulimwengu mzima. Hii ni hoja isiyopingika, hoja ambayo kweli ipo, ambayo hakuna binadamu au kiumbe chochote kinaweza kubadilisha. Kama baadhi yenu mngali hamjatosheka na mambo kama yalivyo, mnaamini kwamba mna ujuzi fulani maalum au uwezo, na bado mnafikiria mnaweza kubahatika na kubadilisha hali zenu za sasa au vinginevyo kuzitoroka; kama utajaribu kubadilisha hatima yako kupitia kwa jitihada za binadamu, na hivyo basi kujitokeza kati ya wengine na kupata umaarufu na utajiri; basi Ninakwambia, unayafanya mambo kuwa magumu kwako, unajitakia taabu tu, unajichimbia kaburi lako mwenyewe! Siku moja, hivi karibuni au baadaye, utagundua kwamba ulifanya chaguo baya, kwamba jitihada zako ziliambulia patupu. Malengo yako, tamanio lako la kupambana dhidi ya hatima, na mwenendo wako binafsi wa kupita kiasi, utakuongoza kwenye barabara isiyoweza kukurudisha kule ulikotoka, na kwa hili utaweza kujutia baadaye. Ingawaje sasa huoni ubaya wa athari hiyo, unapopitia na kushukuru zaidi na zaidi ukweli kwamba Mungu ndiye Bwana wa hatima ya maisha, utaanza kwa utaratibu kutambua kile Ninachozungumzia leo na athari zake za kweli. Haijalishi kama kwa kweli unao moyo na, haijalishi kama wewe ni mtu anayependa ukweli, inategemea tu ni mtazamo aina gani ambao utachukua kuhusiana na ukuu wa Mungu na ule ukweli. Na, hili linaamua kama kweli unaweza kujua na kuelewa mamlaka ya Mungu. Kama hujawahi katika maisha yako kuhisi ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hujawahi kutambua na kukubali mamlaka ya Mungu, basi utakosa thamani kabisa, bila shaka utakuwa athari ya chukizo na zao la kukataliwa na Mungu, hayo yote ni kutokana na njia uliyochukua na chaguo ulilofanya. Lakini wale ambao, katika kazi ya Mungu, wanaweza kukubali jaribio Lake, kukubali ukuu Wake, kujinyenyekeza katika mamlaka Yake, na kufaidi kwa utaratibu hali halisi waliyopitia na matamshi Yake, watakuwa wametimiza maarifa halisi ya mamlaka ya Mungu, ufahamu halisi wa ukuu Wake, na watakuwa kwa kweli watakuwa wanatii Muumba. Watu kama hao tu ndio watakaokuwa wameokolewa kwa kweli. Kwa sababu wameujua ukuu wa Mungu, kwa sababu wameukubali, shukrani yao ya na kujinyenyekeza kwao katika hoja ya Mungu juu ya hatima ya binadamu ni ya halisi na sahihi. Wanapokabiliana na kifo wataweza, kama Ayubu, kuwa na akili isiyotishika na kifo, kujinyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Mungu katika mambo yote, bila chaguo lolote la kibinafsi, bila tamanio lolote la kibinafsi. Mtu kama huyo tu ndiye atakayeweza kurudi katika upande wa Muumba kama kiumbe cha kweli cha binadamu kilichoumbwa.
Tanbihi:
a. Maandishi asilia yameacha kauli "zile hali za."
b. Maandishi asilia yanasoma "hii."
c. Maandishi asilia yameacha "Katika wakati huu."
d. Maandishi asilia yameacha "Bila kujua."
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni