Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho?
Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho? La, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo! Hii ni kwa sababu vikao hivi vya ushirika vilitupa tu ufahamu wa sehemu ya tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho—na wala si kila kitu, au uzima Wake wote. Vikao hivi vya ushirika vilikuwezesha wewe kuelewa sehemu ya kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na kupitia kwa hayo uliweza kuielewa tabia ya Mungu, na kile Anacho, na alicho, pamoja na mtazamo na kufikiria kuliko kila kitu ambacho Amefanya. Hata hivyo huu ni ufahamu tu wa moja kwa moja, wa matamshi, na katika moyo wako, unabakia kutojua ni kiwango kipi haswa ambacho ni kweli. Ni nini hasa huamua kama kunao uhalisia wowote katika ufahamu wako wa mambo kama haya? Yanaamuliwa na kiwango kipi cha maneno na tabia ya Mungu ambayo kwa kweli umepitia kwenye yale yote ya kweli ambayo wewe umepitia, na kiwango kipi ambacho umeweza kuona na kujua kwenye hali hizi halisi ambazo ulipitia. “Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vilituruhusu kuelewa mambo yanayofanywa na Mungu, fikira za Mungu, na, zaidi ya yote, mtazamo wa Mungu kwa mwanadamu na msingi wa hatua Zake, pamoja na kanuni za vitendo Vyake. Na kwa hivyo tumekuja kuelewa tabia ya Mungu, na kujua Mungu kwa uzima Wake.” Je, kunaye aliyesema maneno haya? Ni sahihi kusema hivi? Kwa kweli ni wazi kwamba si sahihi. Na kwa nini Nasema kwamba si sahihi? Tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho, vyote vinaonyeshwa katika mambo ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye ametamka. Binadamu anaweza kuelewa kile Anacho na alicho kupitia kwa kazi ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye ameongea, lakini hii ni kusema tu kwamba ile kazi na maneno humwezesha binadamu kuelewa sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya kile Anacho na alicho. Kama binadamu atataka kufaidi ufahamu mwingi zaidi na ulio wazi kuhusu Mungu, basi binadamu lazima apitie maneno na kazi nyingi zaidi za Mungu. Ingawaje binadamu hufaidi tu ufahamu kiasi wa Mungu wakati anapokuwa akipitia sehemu ya maneno au kazi ya Mungu, je, ufahamu huu wa kiasi unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu? Je, unawakilisha hali halisi ya Mungu? Bila shaka unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu, na hali halisi ya Mungu, hapo hapana shaka. Haijalishi ni lini au wapi, au ni kwa njia gani ambayo Mungu hufanya kazi Yake, au ni umbo gani ambalo humwonekania binadamu, au ni kwa njia gani Anaonyesha mapenzi Yake, kila kitu Anachofichua na kuonyesha huwakilisha Mungu Mwenyewe, hali halisi ya Mungu na kile Anacho na alicho. Mungu hutekeleza kazi Yake na kile Anacho na alicho, na katika utambulisho Wake wa kweli; Huu ni ukweli mtupu. Ilhali, leo, watu wanao ufahamu kiasi tu wa Mungu kupitia maneno Yake, na kupitia kile wanachosikia wanaposikiliza mahubiri, na kwa hivyo hadi kufikia kiwango fulani, ufahamu huu unaweza kusemwa tu kuwa maarifa ya kinadharia. Kwa mtazamo wa hali zenu halisi, mnaweza kuthibitisha tu ufahamu au maarifa ya Mungu ambayo mmesikia, kuona, au kujua na kuelewa katika moyo wako leo kama kila mmoja wenu atashuhudia haya kupitia kwa yale yote halisi aliyoyapitia, na anakuja kuyajua kidogokidogo. Kama Singeweza kushiriki maneno haya na wewe, je, ungeweza kutimiza maarifa ya kweli ya Mungu ukiwa pekee kupitia kwa yale yote uliyoyapitia? Kufanya hivyo, Naogopa, kunaweza kuwa vigumu sana. Hiyo ni kwa sababu lazima watu wawe kwanza na maneno ya Mungu ili kujua namna ya kuyapitia. Hata hivyo wingi wa maneno ya Mungu ambayo watu hushiriki, hicho ndicho kiwango wanachoweza kupitia. Maneno ya Mungu huongoza njia iliyo mbele, na humpa binadamu mwongozo katika yale yote anayoyapitia. Kwa ufupi, kwa wale walio na baadhi ya mambo ya kweli waliyoyapitia, vikao hivi mbalimbali vya mwisho vitawasaidia kutimiza ufahamu wa kina wa kweli, na hali yenye uhalisia zaidi kuhusu maarifa ya Mungu. Lakini kwa wale wasiokuwa na hali yoyote ya kweli ya waliyoipitia, au ambao wameanza tu hali yao wanayopitia, au wameanza tu kugusia uhalisia wa mambo, huu ni mtihani mkubwa.
Yale maudhui makuu ya vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika yalihusu "tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe." Ni nini ulichoona kwenye sehemu zile muhimu na kuu kati ya kila kitu Nilichoongea? Kupitia kwenye vikao hivi vya ushirika, unaweza kutambua kwamba Yule aliyefanya kazi, na Akaweza kufichua tabia hizi, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye na ukuu juu ya mambo yote? Kama jibu lako ni ndiyo, basi ni nini kinachokuongoza katika hitimisho kama hilo? Ni katika dhana zipi uliweza kufikia hitimisho hili? Je, kunaye yeyote anayeweza kuniambia Mimi? Ninajua kwamba vikao vya mwisho vya ushirika vilikuathiri kwa undani, na vilikupa mwanzo mpya katika moyo wako kwa minajili ya maarifa yako kwa Mungu, jambo ambalo ni kuu. Lakini ingawaje umeweza kuchukua hatua kubwa katika ufahamu wako wa Mungu ukilinganishwa na awali, ufafanuzi wako wa utambulisho wa Mungu bado unahitaji hatua zaidi ya majina ya Yehova Mungu wa Enzi ya Sheria, Bwana Yesu wa Enzi ya Neema, na Mwenyezi Mungu wa Enzi ya Ufalme. Hivi ni kusema kwamba, ingawaje vikao hivi vya ushirika kuhusu "tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe" viliweza kukupa ufahamu fulani wa maneno yaliyowahi kuzungumzwa na Mungu, na kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na uwepo na vinavyomilikiwa vilivyowahi kufichuliwa na Mungu, huwezi kutoa ufafanuzi wa ukweli na mpangilio sahihi wa neno “Mungu.” Na wala huna mpangilio wa kweli na sahihi na maarifa ya hali na utambulisho wa Mungu Mwenyewe, hii ni kusema, katika hadhi ya Mungu miongoni mwa mambo yote na kotekote kwenye ulimwengu mzima. Hii ni kwa sababu, kwenye vikao vya ushirika vya awali kuhusu Mungu Mwenyewe na tabia ya Mungu, maudhui yote yalitokana na maonyesho na ufunuo mbalimbali wa awali kuhusu Mungu uliorekodiwa kwenye Biblia. Ilhali ni vigumu kwa binadamu kugundua uwepo na miliki ambazo zinamilikiwa na kuonyeshwa na Mungu wakati wa, au nje ya, usimamizi na wokovu Wake kwa mwanadamu. Kwa hivyo, hata kama utaelewa nafsi na miliki za Mungu ambazo zilifichuliwa kwenye kazi Aliyowahi kufanya, ufafanuzi wako wa utambulisho na hadhi ya Mungu ungali mbali sana na ule wa Mungu wa kipekee, Yule anayeshikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na ni tofauti na ule wa Muumba. Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vilifanya kila mmoja kuhisi kwa njia moja: Binadamu angejuaje fikira za Mungu? Kama kweli mtu angejua, basi mtu huyo bila shaka angekuwa Mungu, kwa maana Mungu Mwenyewe ndiye anayejua fikira Zake, na Mungu Mwenyewe tu ndiye anayejua msingi na mtazamo wa kila kitu Anachofanya. Yaonekana ya kueleweka na ya mantiki kwako wewe kutambua utambulisho wa Mungu kwa njia kama hiyo, lakini ni nani anayeweza kujua kutoka kwenye tabia na kazi ya Mungu kwamba kwa kweli hii ni kazi ya Mungu Mwenyewe, na wala si kazi ya binadamu, kazi ambayo haiwezi kufanywa kwa niaba ya Mungu na binadamu? Nani anayeweza kuona kwamba kazi hii inapatikana katika uongozi wa ukuu wa Yule aliye na hali halisi na nguvu za Mungu? Hii ni kusema kwamba, kupitia sifa au hali halisi gani ndipo unapotambua kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe, aliye na utambulisho wa Mungu, na Ndiye aliye na ukuu juu ya viumbe vyote? Umewahi kufikiria hivi? Kama hujawahi, basi hii inathibitisha hoja moja: Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vimeweza kukupa tu ufahamu fulani wa kipande cha historia ambapo Mungu alifanya kazi Yake, na mtazamo, maonyesho, na ufunuo wa Mungu kwenye kipindi cha kufanyika kwa kazi hiyo. Ingawaje ufahamu kama huo unafanya kila mmoja wenu kutambua bila ya shaka yoyote kwamba Yule aliyetekeleza awamu hizi mbili za kazi ni Mungu Mwenyewe ambaye tunamsadiki na kumfuata, na Ndiye lazima siku zote tumfuate, tungali hatuna uwezo wa kutambua kwamba Yeye ni Mungu aliyekuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, na Atakayeendelea kuwepo milele hadi milele, na wala hatuwezi kutambua kwamba Yeye Ndiye anayetuongoza na Anayeshikilia utawala juu ya wanadamu wote. Kwa kweli hujawahi kufikiria kuhusu tatizo hili. Awe ni Yehova Mungu au Bwana Yesu, ni kupitia kwa dhana zipi za hali halisi na maonyesho husika ndipo unaweza kutambua kwamba Yeye si Mungu tu ambaye lazima umfuate, lakini pia Ndiye anayeamuru mwanadamu na Anayeshikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu, ambaye, vilevile, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee anayeshikilia ukuu dhidi ya mbingu na ardhi na viumbe vyote? Ni kupitia kwenye njia gani ndipo unapotambua kwamba Yule unayemsadiki na kumfuata ni Mungu Mwenyewe anayeshikilia ukuu juu ya viumbe vyote? Ni kupitia kwenye njia gani ndipo unapounganisha Mungu unayemsadiki na Mungu anayeshikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu? Ni nini kinachokuruhusu kutambua kwamba Mungu unayemsadiki ndiye yule Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye mbinguni na ulimwenguni, na miongoni mwa viumbe vyote? Hili ndilo tatizo ambalo Nitatatua kwenye sehemu ijayo.
Matatizo ambayo hujawahi kufikiria kuhusu au huwezi kufikiria kuhusu ndiyo yayo hayo ambayo yanaweza kuwa muhimu zaidi kwa kumjua Mungu, na ambayo kwayo unaweza kutafuta ukweli usioweza kufikirika kwa mwanadamu. Wakati matatizo haya yanapokukumba, na lazima wewe ndiwe unayefaa kuyakabili, na unahitajika kufanya uamuzi, kama hutaweza kuyatatua kikamilifu kwa sababu ya ujinga au kutojua kwako, au kwa sababu yale yote uliyopitia wewe ni ya juujuu sana na unakosa maarifa ya kweli ya Mungu, basi yatakuwa kizuizi kikubwa zaidi na changamoto kubwa zaidi kwenye njia yako ya kumsadiki Mungu. Na kwa hivyo Nahisi kwamba tunahitajika kabisa kushiriki pamoja nanyi mada hii. Je, unajua tatizo lako ni nini sasa? Je, unatambua matatizo Ninayoyazungumzia? Je, matatizo haya ndiyo utakayokabiliana nayo? Je, haya ndiyo matatizo usiyoyaelewa? Je, haya ndiyo matatizo ambayo hayajawahi kukutokea? Je, matatizo haya ni muhimu kwako? Je, ni matatizo kweli? Suala hili ni chanzo cha mkanganyo mkuu kwako, na hivyo inaonekana kwamba huna ufahamu wa kweli wa Mungu unayemsadiki, na kwamba humchukulii Yeye kwa umakinifu. Baadhi ya watu husema, “Ninajua Yeye ni Mungu, na kwa hivyo ninamfuata Yeye kwa sababu maneno Yake ni maonyesho ya Mungu. Hayo yanatosha. Thibitisho lipi zaidi linahitajika? Kwa kweli hatuhitaji kuibua shaka kuhusu Mungu? Kwa kweli hatupaswi kumjaribu Mungu? Kwa kweli hatuhitaji kuulizia hali halisi ya Mungu na utambulisho wa Mungu Mwenyewe?” Bila kujali kama unafikiria kwa njia hii, huwa Siyaulizi maswali fulani ili kukukanganya kuhusu Mungu, au kukufanya umjaribu Mungu, na isitoshe ili kukupa shaka kuhusu utambulisho na hali halisi ya Mungu. Badala yake, Ninafanya hivi ili kuhimiza ndani yenu ufahamu mkubwa zaidi wa hali halisi ya Mungu, na uhakika na imani kubwa zaidi kuhusu hadhi ya Mungu, ili Mungu awe Ndiye wa pekee katika mioyo ya wale wote wanaomfuata Mungu, na ili ile hadhi ya asili ya Mungu—kama Muumba, Kiongozi wa viumbe vyote, Mungu Mwenyewe wa kipekee—iweze kurejeshwa katika mioyo ya kila kiumbe. Hii pia ndiyo mada itakayohusu ushirika wetu.
Sasa hebu na tuanze kusoma maandiko yafuatayo kutoka kwenye Biblia.
1. Mungu Hutumia Maneno ili Kuumba Viumbe Vyote
Mwa 1:3-5 Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza.
Mwa 1:6-7 Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo.
Mwa 1:9-11 Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane; na kukawa vivyo hivyo. Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema. Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.
Mwa 1:14-15 Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile.
Mwa 1:20-21 Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri.
Mwa 1:24-25 Naye Mungu aksema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri.
Kwenye Siku ya Kwanza, Mchana na Usiku wa Mwanadamu Vinazaliwa na Kujitokeza Waziwazi kwa Msaada wa Mamlaka ya Mungu
Hebu na tuweze kuangalia fungu la kwanza: “Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza” (Mwa 1:3-5). Fungu hili linafafanua kitendo cha kwanza cha Mungu wakati wa mwanzo wa uumbaji, na siku ya kwanza ambayo Mungu alipitisha ambapo kulikuwa na jioni na asubuhi. Lakini ilikuwa siku ya kipekee: Mungu alianza kutayarisha nuru ya viumbe vyote, na, vilevile, Akagawa nuru kutoka kwa giza. Kwenye siku hii, Mungu alianza kunena, na matamshi na mamlaka Yake vyote vilikuwa pamoja. Mamlaka Yake yalianza kujitokeza miongoni mwa viumbe vyote, na nguvu Zake zikaenea miongoni mwa viumbe vyote kutokana na maneno Yake. Kuanzia siku hii kuendelea mbele, viumbe vyote viliumbwa na vikawa viko tayari kwa sababu ya maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu, na vikaanza kufanya kazi kwa msaada wa maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu. Wakati Mungu aliposema maneno haya “Na kuwe na mwanga,”kulikuwepo na nuru. Mungu hakuanza kushughulikia shughuli yoyote; nuru ilikuwa imeonekana kama matokeo ya maneno Yake. Hii ilikuwa nuru ambayo Mungu aliita mchana, na ambayo binadamu angali anaitegemea kwa minajili ya kuwepo kwake leo. Kwa amri ya Mungu, hali yake halisi na thamani havijawahi kubadilika na havijawahi kutoweka. Uwepo wake unaonyesha mamlaka na nguvu za Mungu, na unatangaza uwepo wa Mungu, na unathibitisha, tena na tena, utambulisho na hadhi ya Muumba. Haiwezi kushikika, au kuonekana, lakini ni nuru halisi inayoweza kuonekana na binadamu. Kuanzia wakati huo kusonga mbele, kwenye ulimwengu huu mtupu ambao “nchi ilikuwa ya ukiwa na tupu; na kulikuwa na giza sehemu ya juu ya vilindi,” kulikuwepo kiumbe kile cha kwanza cha kushikika. Kiumbe hiki kilitokana na maneno ya kinywa cha Mungu na kikaonekana kwenye tukio la kwanza la kuumbwa kwa viumbe vyote kwa sababu ya mamlaka na matamshi ya Mungu. Muda mfupi baadaye, Mungu aliamuru nuru na giza kutengana…. Kila kitu kilibadilika na kilikamilishwa kwa sababu ya maneno ya Mungu…. Mungu akaiita nuru hii “Mchana,” na giza hili Akaliita “Usiku.” Kuanzia wakati huo, jioni ya kwanza na asubuhi ya kwanza ziliweza kuumbwa katika ulimwengu ambao Mungu alinuia kuumba, na Mungu akasema hii ndiyo iliyokuwa siku ya kwanza. Siku hii ilikuwa siku ya kwanza ya vile vilivyoumbwa na Muumba wa viumbe vyote, na ilikuwa mwanzo wa kuumbwa kwa viumbe vyote, na ndio wakati wa kwanza ambao mamlaka na nguvu za Muumba vilikuwa vimeonyeshwa katika ulimwengu huu ambao Alikuwa ameumba.
Kupitia maneno haya, binadamu anaweza kutazama mamlaka ya Mungu, na mamlaka ya maneno ya Mungu, na nguvu za Mungu. Kwa sababu Mungu tu ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na kwa hivyo Mungu pekee ndiye aliye na mamlaka, na kwa sababu Mungu ndiye anayemiliki mamlaka kama hayo, kwa hivyo Mungu pekee ndiye aliye na nguvu kama hizo. Je, binadamu au kifaa chochote kingeweza kumiliki mamlaka na nguvu kama hizi? Je, kunalo jibu katika moyo wako? Mbali na Mungu, je, kuna kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki mamlaka kama hayo? Umewahi kuona mfano wa kiumbe kama hiki kwenye vitabu vingine vyovyote au machapisho? Kunayo rekodi yoyote kwamba mtu aliumba mbingu na ulimwengu na viumbe vyote? Jambo hili halionekani katika vitabu au rekodi nyingine zozote; haya ndiyo, bila shaka, maneno ya kipekee yenye mamlaka na nguvu kuhusu uumbaji wa kupendeza wa Mungu wa ulimwengu, yaliyorekodiwa kwenye Biblia, na maneno haya yanazungumzia mamlaka ya kipekee ya Mungu, na utambulisho wa kipekee wa Mungu. Je, mamlaka na nguvu kama hizi zinaweza kusemekana kuwa zinaashiria utambulisho wa kipekee wa Mungu? Yanaweza kusemwa yanamilikiwa na Mungu, na Mungu pekee? Bila shaka, Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki mamlaka na nguvu kama hizi! Mamlaka na nguvu hizi vyote haviwezi kumilikiwa au kubadilishwa na kiumbe chochote kingine kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa! Je, hii ni mojawapo ya sifa za Mungu Mwenyewe wa kipekee? Je, umewahi kuishuhudia? Maneno haya yanaruhusu watu kuelewa kwa haraka na waziwazi hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka ya kipekee, na nguvu za kipekee, na Anamiliki utambulisho na hadhi isiyo ya kawaida. Kutokana na ushirika wa hapa juu, je, unaweza kusema kwamba Mungu unayemsadiki ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee?
Kwenye Siku ya Pili, Mamlaka ya Mungu Yalipangilia Maji, na Kufanya Mbingu, na Anga za Mbinu za Kimsingi Zaidi za Kuishi kwa Binadamu Kuonekana
Hebu na tusome fungu la pili la Biblia: “Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo” (Mwa 1:6-7). Ni mabadiliko gani yaliyofanyika baada ya Mungu kusema “Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji”? Maandiko yanasema: “Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu.” Ni nini kilichokuwa matokeo baada ya Mungu kutamka hivi na kufanya hivyo? Jibu linapatikana kwenye sehemu ya mwisho ya fungu hili: “na kukawa vivyo hivyo.”
Sentensi hizi fupi mbili zinarekodi tukio la kupendeza, na zinafafanua mazingira mazuri—utekelezaji wa kipekee ambapo Mungu aliyatawala maji, na kuunda anga ambayo binadamu angeishi …
Katika picha hii, maji na anga vinaonekana mbele ya macho ya Mungu papo hapo, na vyote vinagawanywa kwa mamlaka ya matamshi ya Mungu, na kugawanywa kwa sehemu ya juu na ya chini kwa njia ambayo iliteuliwa na Mungu. Hivi ni kusema, anga iliyoumbwa na Mungu haikufunika tu maji yaliyo chini, lakini pia ilishikilia maji yaliyo juu…. Katika haya, binadamu hawezi kufanya chochote ila kukodoa macho, kushangaa, na kutweta kwa kuvutiwa na maajabu ya onyesho hilo ambalo Muumba aliyahamisha maji, na kuyaamuru maji, na kuumba anga, na yote haya Alifanya kupitia kwa nguvu za mamlaka Yake. Kupitia kwa matamshi ya Mungu, na nguvu za Mungu, na mamlaka ya Mungu, Mungu aliweza kutimiza tendo jingine kubwa. Je, hizi si nguvu za mamlaka ya Muumba? Hebu na tutumie maandiko haya katika kufafanua vitendo vya Mungu: Mungu aliyatamka matamshi Yake na kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu kulikuwa na anga katikati ya maji. Wakati uo huo, badiliko la ajabu lilitokea kwenye nafasi hii kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu, na halikuwa badiliko katika hali ya kawaida, lakini aina fulani ya kibadala ambapo kitu kisichokuwepo kiligeuka na kuwa kitu kilichopo. Yote haya yalizaliwa kwenye fikira za Muumba, na yakawa kitu kilichopo kutoka kwenye kitu kisichokuwepo kwa sababu ya matamshi yaliyotamkwa na Muumba, na, vilevile, kuanzia sasa kwenda mbele yangekuwepo na kuwa imara, kwa minajili ya Muumba, na yangesonga, kubadilika, na kupata nguvu kulingana na fikira za Muumba. Ufahamu huu unafafanua kitendo cha pili cha Muumba katika viumbe Vyake vya ulimwengu mzima. Yalikuwa maonyesho mengine ya mamlaka na nguvu za Muumba, na ulikuwa utekelezaji mwingine anzilishi uliofanywa na Muumba. Siku hii ndiyo iliyokuwa siku ya pili ambayo Muumba alikuwa amepitisha tangu kuwekwa msingi kwa ulimwengu, na ilikuwa siku nyingine nzuri Kwake: Alitembea miongoni mwa nuru, Aliileta anga, Aliyapangilia na kuyatawala maji, na vitendo Vyake, mamlaka Yake, na nguvu Zake vyote viliweza kuanza kazi kwenye siku hiyo mpya …
Je, kulikuwepo na anga katikati ya maji kabla ya Mungu kutamka matamshi Yake? Bila shaka la! Na je, baada ya Mungu kusema “Na kuwe na mbingu katikati ya maji”? Viumbe vilivyonuiwa na Mungu vilionekana; kulikuwa na anga katikati ya maji, na maji yaligawanywa kwa sababu Mungu alisema hivyo “na uigawanye maji kutoka kwa maji.” Kwa njia hii, kufuatia maneno ya Mungu, viumbe vipya viwili, viumbe viwili vilivyozaliwa na vilivyokuwa vipya vilionekana miongoni mwa viumbe vyote kutokana na mamlaka na nguvu za Mungu. Na unahisi vipi kuhusu kujitokeza kwa viumbe hivi viwili vipya? Je, unahisi ukubwa wa nguvu za Muumba? Unahisi ile nguvu ya kipekee na isiyo ya kawaida ya Muumba? Ukubwa wa msukumo na nguvu kama hizo unatokana na mamlaka ya Mungu na mamlaka haya ni kiwakilishi cha Mungu Mwenyewe, na sifa ya kipekee ya Mungu Mwenyewe.
Je, ufahamu huu umekupa mtazamo mwingine kamilifu wa upekee wa Mungu? Lakini haya ni machache tu kati ya mengi; mamlaka na nguvu za Muumba vinazidi haya yote. Upekee wake hauko hivyo tu kwa sababu Anamiliki hali halisi isiyo kama ya viumbe vingine, lakini pia kwa sababu ya mamlaka na nguvu Zake kuwa zisizo za kawaida, zisizo na mipaka, bora kabisa kuliko vyote, na inapita vitu vyote, na vilevile, kwa sababu mamlaka Yake na kile Anacho na alicho kinaweza kuumba maisha, na kufanya miujiza, na Anaweza kuumba kila mojawapo ya dakika na sekunde iliyo ya kustaajabisha na isiyo ya kawaida, na wakati uo huo, Anaweza kutawala maisha Anayoyaumba na kushikilia ukuu Wake juu ya miujiza na kila mojawapo ya dakika na sekunde Anazoumba.
Kwenye Siku ya Tatu, Matamshi ya Mungu Yazaa Ardhi na Bahari, na Mamlaka ya Mungu Yasababisha Ulimwengu Kujaa Maisha
Sasa, hebu na tusome sentensi ya kwanza ya Mwanzo 1:9-11: “Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ni mabadiliko gani yaliyotokea baada ya Mungu kusema tu, “Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane”? Na hii nafasi iliyokuwa katikati ya nuru na anga ilikuwa nini? Katika Maandiko, imeandikwa: “Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema.” Hivi ni kusema, kulikuwepo sasa na ardhi na bahari kwenye anga hii, nayo ardhi na bahari viliweza kutenganishwa. Kujitokeza kwa vitu hivi vipya kulifuata amri kutoka kwenye kinywa cha Mungu, “na kukawa vivyo hivyo.”Je, Maandiko yanafafanua Mungu akiwa ameshughulika kila pahali wakati Akifanya haya? Je, yanafafanua Mungu akiwa anajihusisha katika kazi ngumu? Kwa hivyo, haya yote yaliwezaje kufanywa na Mungu? Mungu aliwezaje kusababisha vitu hivi vipya kuumbwa? Tunaelewa wenyewe bila kuelezewa, kwamba Mungu alitumia matamshi kutimiza mambo haya yote, kuumba uzima wa haya yote.
Kwenye mafungu matatu yaliyo hapo juu, tumejifunza kunatokea matukio matatu makubwa. Matukio haya matatu makubwa yalionekana, na yakaumbwa kuwa hivyo, kupitia kwa matamshi ya Mungu, na ni kwa sababu ya matamshi Yake ndipo, moja baada ya lengine, yaliweza kujitokeza mbele ya macho ya Mungu. Kwa hivyo inaweza kuonekana kwamba “Mungu huongea, na ikatimizwa; huamuru, na ikawa imara” haya si maneno matupu. Hali hii halisi ya Mungu inathibitishwa wakati ule ambao fikira Zake zinaeleweka, na wakati ambapo Mungu hufungua kinywa Chake kuongea, hali Yake halisi inajionyesha kikamilifu.
Hebu na tuendelee hadi kwenye sentensi ya mwisho ya fungu hili: “Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.”Huku Mungu akiongea, mambo haya yote yaliumbika kufuatia fikira za Mungu, na kwa muda mfupi tu, mseto wa viumbe vidogo vinyonge vyenye maisha vilikuwa vinachomoza vichwa vyao kwa kusita huku vichwa vyao vikiwa juu kupitia kwenye ardhi, na hata kabla ya kukung’uta chembechembe za uchafu kutoka kwenye miili yao vilikuwa vikipungiana mikono kusalimiana kwa hamu, kuitikia na kuufurahia ulimwengu. Vilishukuru Muumba kwa maisha aliyovipatia, na kuutangazia ulimwengu kwamba vilikuwa sehemu ya viumbe vyote, na kwamba kila kimojawapo kingejitolea katika maisha yavyo ili viwe vinaonyesha mamlaka ya Muumba. Kama vile matamshi ya Mungu yalivyotamkwa, ardhi ikawa yenye rutuba na kijani, aina zote za miti ambayo ingeweza kufurahiwa na binadamu iliweza kuota na kuchipuka kutoka kwenye ardhi, na milima na nchi tambarare vyote vikawa na idadi kubwa ya miti na misitu…. Ulimwengu huu tasa, ambao hakukuwahi kuwepo na chembechembe zozote za maisha, ulifunikwa mara moja na wingi wa nyasi, mimea ya msimu na miti na ilikuwa ikifurika kwa kijani kibichi kingi…. Harufu nzuri ya nyasi na mnukio wa mchanga uliosambazwa kupitia hewani, na mseto wa mimea vyote vilianza kupumua kulingana na mzunguko wa hewa, na vikaanza pia mchakato wa kukua. Wakati uo huo, kutokana na maneno ya Mungu na kufuatia fikira za Mungu, mimea yote ilianza mizunguko isiyoisha ya maisha ambapo inakua, inanawiri, inazaa matunda na kuzaana na kuongezeka. Ilianza kutii kwa umakinifu mikondo yao husika ya maisha, na kuanza kutekeleza wajibu wao husika miongoni mwa viumbe vyote…. Yote ilizaliwa na kuishi, kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingepokea matoleo na ustawishi usiosita wa Muumba, na siku zote ingeendelea kuishi kwa shauku katika kila pembe ya ardhi ili kuonyesha mamlaka na nguvu za Muumba, na siku zote ingeonyesha nguvu za maisha walizopewa na Muumba …
Maisha ya Muumba ni yale yasiyo ya kawaida, fikira Zake ni zile zisizo za kawaida, na mamlaka Yake ni yale yasiyokuwa ya kawaida, na kwa hivyo, wakati matamshi Yake yalipotamkwa, yale matokeo ya mwisho yalikuwa “na ikawa hivyo.” Ni wazi kwamba, Mungu hahitaji kufanya kazi kwa mikono Yake wakati Anapofanya matendo; Anatumia tu fikira Zake kutoa amri, na matamshi Yake ili kuagizia, na kwa njia hii mambo yanatimizwa. Kwenye siku hii, Mungu aliyakusanya maji katika mahali pamoja, na Akaiacha ardhi kavu kujitokeza, baada ya hapo Mungu aliifanya nyasi kuota kutoka kwenye ardhi, na papo hapo palimea mimea ya msimu iliyozaa mbegu, na miti ya kuzaa matunda, na Mungu akaainisha kila mojawapo kulingana na aina, na kusababisha kila mmea kuwa na mbegu yake. Haya yote yaliwezekana kulingana na fikira za Mungu na amri za matamshi ya Mungu, na kila mmea ulijitokeza, mmoja baada ya mwingine, kwenye ulimwengu huu mpya.
Wakati Alikuwa aanze kazi Yake, Mungu tayari alikuwa na picha ya kile Alichonuia kutimiza katika akili Zake na wakati ambapo Mungu alianza kutimiza mambo haya, na ndio wakati ambao pia Mungu alikifungua kinywa Chake kuongea kuhusu maudhui ya picha hii, mabadiliko katika viumbe vyote yalianza kufanyika kutokana na mamlaka na nguvu za Mungu. Bila ya kujali namna Mungu alivyofanya, au Alivyoonyesha mamlaka Yake, kila kitu kilitimizwa hatua kwa hatua kulingana na mpango wa Mungu na kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na mabadiliko ya hatua kwa hatua yalifanyika kati ya mbingu na ardhi kutokana na matamshi na mamlaka ya Mungu. Mabadiliko na matukio haya yote yalionyesha mamlaka ya Muumba, na nguvu za maisha ya Muumba zisizo za kawaida na zenye ukubwa. Fikira Zake si mawazo mepesi, au picha tupu, lakini mamlaka yanayomiliki nishati kuu na ile isiyo ya kawaida, na ndio nguvu zinazosababisha viumbe vyote kubadilika, kufufuka, kupata nguvu upya, na kuangamia. Na kwa sababu ya haya, viumbe vyote hufanya kazi kwa sababu ya fikira Zake, na, wakati uo huo, yote haya yanatimizwa kwa sababu ya matamshi kutoka kinywa Chake….
Kabla ya viumbe vyote kujitokeza, kwenye akili za Mungu mpango wa Mungu ulikuwa umeundwa kitambo, na ulimwengu mpya ulikuwa umetimizwa kitambo. Ingawaje kwenye siku ya tatu mimea aina yote ilijitokeza ardhini, Mungu hakuwa na sababu yoyote ya kusitisha hatua za uumbaji Wake kwa ulimwengu huu, Alinuia kuendelea kunena matamshi Yake, kuendelea kutimiza uumbaji wa kila kiumbe kipya. Angenena, angetoa amri Zake, na angeonyesha mamlaka Yake na kuendeleza nguvu Zake, na Alitayarisha kila kitu Alichokuwa amepanga ili kutayarishia viumbe vyote na mwanadamu ambaye Alinuia kuumba….
Kwenye Siku ya Nne, Misimu, Siku, na Miaka ya Mwanadamu Iliumbika Huku Mungu Akionyesha Mamlaka Yake kwa Mara Nyingine Tena
Muumba alitumia matamshi Yake kutimiza mpango Wake, na kwa njia hii Alipitisha siku tatu zake za kwanza kwenye mpango Wake. Kwenye siku hizi tatu, Mungu hakuonekana kushughulika kila pahali, au kujichosha Yeye Mwenyewe; kinyume cha mambo ni kwamba, Alikuwa na siku tatu za kwanza nzuri katika mpango Wake na Alitimiza utekelezaji mkubwa wa mabadiliko makubwa ya ulimwengu. Ulimwengu mpya kabisa ulijitokeza mbele ya macho Yake, na, kipande kwa kipande, picha nzuri na ya kupendeza ambayo ilikuwa imefichwa ndani ya fikira Zake ilikuwa tayari imefichuliwa kwa matamshi ya Mungu. Kujitokeza kwa kila kiumbe kipya kulikuwa sawa na kuzaliwa kwa mtoto mchanga, na Muumba alifurahia sana picha hii ambayo iliwahi kuwa kwenye fikira Zake, lakini ambayo sasa ilikuwa imepewa uhai. Wakati huu, moyo Wake ulifaidi sehemu ndogo ya kutosheka, lakini mpango Wake ulikuwa ndio tu umeanza. Punde si punde, siku mpya ilikuwa imewadia—na ukurasa unaofuata ulikuwa upi kwenye mpango wa Muumba? Ni nini Alichosema? Na Aliwezaje kuonyesha mamlaka Yake? Na, wakati uo huo, ni mambo yapi mapya yaliyokuja kwenye ulimwengu huu mpya? Kufuatia mwongozo wa Muumba, kuangaza kwetu kwa macho kunatufikisha kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa viumbe vyote, siku ambayo ilikuwa ni mwanzo mpya. Bila shaka, kwa Muumba, bila tashwishi ilikuwa ni siku nyingine nzuri, na siku nyingine yenye umuhimu mkubwa kwa mwanadamu wa leo. Ilikuwa, bila shaka, siku yenye thamani isiyopimika. Ilikuwaje nzuri, ilikuwaje muhimu, na ilikuwaje yenye thamani isiyopimika? Hebu na tuweze kusikiliza matamshi yaliyotamkwa na Muumba….
“Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile”(Mwa 1:14-15). Haya yalikuwa maonyesho mengine ya mamlaka ya Mungu yaliyoonyeshwa kwa viumbe kufuatia uumbaji Wake wa ardhi kavu na mimea iliyokuwa ndani yake. Kwa Mungu, kitendo kama hicho kilikuwa rahisi kwa kiasi fulani, kwa sababu Mungu ana nguvu kama hizo; Mungu ni mzuri kama vile tu neno Lake lilivyo, na neno Lake litaweza kutimizwa. Mungu aliamuru nuru kujitokeza mbinguni, na nuru hizi hazikuangaza tu kwenye mbingu lakini pia kwenye ardhi, lakini pia zilihudumu kama ishara za mchana na usiku, kwa minajili ya misimu, siku, na miaka. Kwa njia hii, kama vile Mungu alivyoongea kwa matamshi Yake, kila kitendo ambacho Mungu alipenda kutimiza kilitimizwa kulingana na maana ya Mungu na kwa njia iliyoteuliwa na Mungu.
Nuru kwenye mbingu ni viumbe vilivyo kwenye mbingu vinavyoweza kuonyesha nuru; vinaweza kuangazia mbingu, na vinaweza kuangazia ardhi na bahari. Vinazunguka kulingana na mpigo na mara ngapi ambapo vimeamriwa na Mungu, na vinaangaza sehemu mbalimbali zenye vipindi tofauti vya muda kwenye ardhi, na kwa njia hii mizunguko ya kuzunguka kwa nuru hizi husababisha mchana na usiku kujitokeza upande wa mashariki na magharibi mwa ardhi, na wala si tu ishara za usiku na mchana, lakini kupitia kwa mizunguko hii tofauti inaweza kuadhimisha pia karamu na siku mbalimbali maalum za mwanadamu. Ndizo nyongeza na saidizi timilifu kwa misimu minne—mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe—iliyotolewa na Mungu, pamoja na vile ambavyo nuru hizi huhudumu kwa mpangilio maalum kama alama za mara kwa mara na sahihi kwa minajili ya vipimo mbalimbali, siku, na miaka ya mwanadamu. Ingawaje ilikuwa baada tu ya mwanzo wa kilimo ndipo mwanadamu alipoanza kuelewa na kukumbana na utofautishi wa vipimo vya muda, siku, na miaka iliyosababishwa na nuru hizi zilizoumbwa na Mungu, kwa hakika, vipindi vya muda, siku, na miaka ambavyo binadamu anaelewa leo vilianza kutolewa kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa viumbe vyote na Mungu, na vilevile ndivyo ilivyokuwa kwenye mizunguko inayobadilishana ya mchipuko, kiangazi, mapukutiko, na kipupwe ambavyo binadamu anapitia na vinaanza kitambo kwenye siku ya nne ya uumbaji wa Mungu wa vitu vyote. Nuru zile zilizoumbwa na Mungu zilimwezesha binadamu kuweza kutofautisha mara kwa mara, kwa hakika, na waziwazi usiku na mchana, na kuhesabu siku, na kuweza kufuatilia waziwazi vipindi vile vya muda na miaka. (Siku ya mwezi mzima ilikuwa kukamilika kwa mwezi mmoja, na kutokana na haya binadamu alijua kwamba kule kuangazia kwa nuru kulianzisha mzunguko mpya; siku ile ya nusu mwezi ilikuwa ni kukamilika kwa nusu moja ya mwezi, jambo ambalo lilimfahamisha binadamu kwamba kipindi kipya cha muda kilikuwa kimeanza, ambapo binadamu angeweza kujua ni mchana na usiku ngapi vilikuwa kwenye kipindi cha muda, na ni vipindi vingapi vya muda vilikuwa kwenye msimu, na ni misimu mingapi ilikuwa kwenye mwaka, na vyote hivi vilionyeshwa mara kwa mara.) Kwa hivyo, binadamu angeweza kufuatilia kwa urahisi vipindi vya muda, siku, na miaka iliyowekewa alama na mizunguko ya nuru hizo. Kuanzia sasa kusonga mbele, mwanadamu na viumbe vyote viliishi bila kufahamu miongoni mwa mabadiliko yenye mpangilio ya usiku na mchana na kubadilishwa kwa misimu iliyotokana na mizunguko ya nuru. Huu ndio ulikuwa muhimu wa uumbaji wa Muumba wa nuru kwenye siku ya nne. Vilevile, nia na umuhimu wa hatua hii ya Muumba vilikuwa bado haviwezi kutenganishwa na mamlaka na nguvu Zake. Na kwa hivyo, nuru zilizoumbwa na Mungu na thamani ambayo zingeleta hivi karibuni kwa binadamu ilikuwa ni mafanikio mengine katika uonyeshaji wa mamlaka ya Muumba.
Katika ulimwengu huu mpya, ambao mwanadamu bado alikuwa hajaonekana, Muumba alikuwa ametayarisha jioni na asubuhi, ile anga, ardhi na bahari, nyasi, miti isiyozaa na aina mbalimbali za miti, na nuru, misimu, siku, na miaka kwa minajili ya maisha mapya ambayo Angeumba hivi karibuni. Mamlaka na nguvu za Muumba vyote vilionyeshwa katika kila kiumbe kipya Alichokiumba, na maneno na kufanikiwa Kwake vyote vilifanyika sawia, bila ya hitilafu yoyote ndogo na bila ya kuchelewa kokote kudogo. Kujitokeza na kuzaliwa kwa viumbe hivi vyote vipya kulikuwa ithibati ya mamlaka na nguvu za Muumba: Yeye ni mzuri sawa tu na neno Lake, na neno Lake litakamilika, na kile kinachokamilika kinadumu milele. Hoja hii haijawahi kubadilika: ndivyo ilivyokuwa kale, ndivyo ilivyo leo, na ndivyo itakavyokuwa daima dawamu. Unapoyaangalia kwa mara nyingine maneno hayo ya maandiko, unahisi kwamba yangali mapya kwako? Je, umeyaona maudhui mapya, na kufanya ugunduzi mpya? Hii ni kwa sababu vitendo vya Muumba vimechangamsha moyo wako na kuongoza mwelekeo wa maarifa yako ya mamlaka na nguvu Zake, na yakakufungulia mlango wa ufahamu wa Muumba, na vitendo na mamlaka Yake vimeweza kupatia maneno haya uhai. Na kwa hivyo katika maneno haya binadamu ameona maonyesho halisi, na wazi ya mamlaka ya Muumba, na kuweza kushuhudia kwa kweli mamlaka makuu ya Muumba, na kutazama mamlaka yake yasiyokuwa ya kawaida na nguvu za Muumba.
Mamlaka na nguvu za Muumba hutoa muujiza baada ya muujiza na huvutia umakinifu wa binadamu, naye binadamu hawezi kukwepa haya ila kuyaangazia tu macho matendo haya ya kipekee yaliyozaliwa kutokana na utekelezwaji wa mamlaka husika. Nguvu zake za kipekee zafurahisha baada ya kufurahisha, na binadamu anabaki akishangaa na akijawa na furaha, naye anatweta kwa kuvutiwa, anastaajabishwa, na kushangilia; nini kingine tena, binadamu amefurahishwa kwa kumtazama alivyo, na kilichozaliwa ndani yake ni heshima, kustahi, na mtagusano wa karibu. Mamlaka na vitendo vya Muumba vinayo athari kwa roho ya binadamu na hutakasa roho ya binadamu na zaidi, kutosheleza roho ya binadamu. Kila mojawapo ya fikira Zake, kila mojawapo ya matamshi Yake, na kila ufunuo wa mamlaka Yake ni kiungo muhimu miongoni mwa viumbe vyote, na ni utekelezaji mkuu wenye thamani zaidi wa kuunda ufahamu na maarifa ya kina ya mwanadamu. Tunapohesabu kila kiumbe kilichozaliwa kutokana na matamshi ya Muumba, roho zetu zinavutiwa kwa maajabu ya nguvu za Mungu, na tunajipata tukifuata nyayo za Muumba hadi kwenye siku inayofuata: siku ya tano ya uumbaji wa Mungu wa viumbe vyote.
Hebu tuendelee kusoma Maandiko fungu hadi fungu, tunapoangalia vitendo vingi zaidi vya Muumba.
Kwenye Siku ya Tano, Maisha ya Maumbo Tofauti na Pana Yaonyesha Mamlaka ya Muumba kwa Njia Tofauti
Maandiko yanasema, “Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri”(Mwa 1:20-21). Maandiko yanatwambia waziwazi kwamba, kwenye siku hii, Mungu aliumba viumbe vya majini na ndege wa hewani, hivi ni kusema kwamba Aliwaumba samaki na ndege mbalimbali, na akawaainisha kila mmoja wao kulingana na aina. Kwa njia hii, ardhi, mbingu, na maji vyote vilitajirishwa na uumbaji wa Mungu …
Kama vile maneno ya Mungu yalivyotamkwa, maisha mapya mazuri, kila mojawapo ikiwa na umbo tofauti, kwa ghafla vilipata uhai miongoni mwa matamshi ya Muumba. Viliingia ulimwenguni vikijitikisatikisa kwa minajili ya kupata nafasi, kuruka, kurukaruka kwa furaha…. Samaki wa maumbo na ukubwa wote waliweza kuogelea majini, samakigamba wa kila aina waliweza kukua kwenye michanga, viumbe vyenye magamba, vyenye maganda na vile visivyokuwa na uti wa mgongo viliweza kukua kwa haraka kwa maumbo tofauti, haijalishi kama vilikuwa vikubwa au vidogo, virefu au vifupi. Na ndivyo pia ilivyokuwa kwa aina tofauti za mwani kuanza kukua kwa haraka, ikiyumbayumba kutokana na msongo wa maisha mbalimbali ya majini, yasiyosita, na yanayosihi yale maji tulivu, ni kana kwamba yanataka kuyaambia: Tikisa mguu! Walete marafiki wako! Kwani hutawahi kuwa pekee tena! Kuanzia muda ule ambao viumbe mbalimbali vilivyo na uhai viliumbwa na Mungu na kuonekana majini, kila maisha mapya yalileta nguvu kwenye maji yaliyokuwa tulivu kwa muda mrefu, na kuweza kuanzisha enzi mpya…. Kuanzia hapo kwenda mbele, viumbe hivi viliishi pamoja, kimoja kando ya kingine na vikaweza kutangamana pamoja, na wala havikujiona tofauti. Yale maji yalikuwepo kwa minajili ya viumbe vilivyokuwa ndani yake, yakipatia uhai kila maisha yaliyokuwa karibu na kumbatio lake, na kila maisha yalikuwepo kwa minajili ya maji kwa sababu ya uhai wake. Kila moja ilipatia uhai mwenzake, na wakati uo huo, kila kimoja, kwa njia hiyo, kilitolea ushuhuda wa miujiza na ukubwa wa uumbaji wa Muumba, na kwa nguvu zisizoshindwa za mamlaka ya Muumba …
Kwa vile bahari haikuwa tulivu tena, ndivyo pia maisha yalivyoanza kujaza mbingu. Mmoja baada ya mwengine, ndege, wakubwa na wadogo, walipaa kwenye mbingu kutoka ardhini. Tofauti na viumbe vya baharini, walikuwa na mbawa na manyoya ambayo yalifunika maumbo yao membamba na yenye neema. Walipigapiga mbawa zao, kwa maringo na majivuno wakionyesha koti lao la kupendeza la manyoya na kazi zao maalum pamoja na mbinu walizopewa na Muumba. Walipaa kwa uhuru, na kwa mbinu walizokuwa nazo wakapaa katikati ya mbingu na ardhi, kotekote kwenye mbuga na misitu…. Walikuwa ndio wapenzi wa hewani, walikuwa ndio wapenzi wa viumbe vyote. Hivi punde ndio wangekuwa kiunganishi kati ya mbingu na ardhi, na wangepitisha ujumbe kwa viumbe vyote…. Waliimba, wakawa wanapaapaa kwa furaha kotekote, walileta vifijo, vicheko, na uchangamfu kwenye ulimwengu huu uliojaa utupu hapo mwanzoni…. Walitumia kuimba kwao kwa uwazi, kuvutia, na kutumia maneno yaliyokuwa ndani ya mioyo yao kusifu Muumba kwa maisha aliyowapa. Walicheza kwa uchangamfu ili kuonyesha utimilifu na miujiza ya uumbaji wa Muumba, na wangejitolea maisha yao yote kushuhudia agano la mamlaka ya Muumba kupitia kwenye maisha maalum ambayo Alikuwa amewapa …
Licha ya kama vilikuwa majini, au mbinguni, kwa amri ya Muumba, wingi huu wa viumbe hivi hai ulikuwepo katika mipangilio tofauti ya maisha, na kwa amri ya Muumba, vilikusanyika pamoja kulingana na aina zao mbalimbali—na sheria hii, kanuni hii, ilikuwa isiyoweza kubadilishwa na viumbe vyovyote. Havikuwahi kuthubutu kwenda nje ya mipaka viliyowekewa na Muumba, na wala visingeweza kufanya hivyo. Kama walivyoamriwa na Muumba, waliishi na kuzaana, na kutii kwa umakinifu mkondo wa maisha na sheria walizowekewa na Muumba, na kwa kufahamu wakafuata amri Zake zisizotamkwa na matamshi na maelekezi ya kimbinguni Aliyowapa, kutoka hapo hadi leo. Walizungumza na Muumba kwa njia yao wenyewe maalum, na wakashukuru maana ya Muumba, na wakatii amri Zake. Hakuna kati yao aliyewahi kukiuka mamlaka ya Muumba, na ukuu na amri Yake juu yao ilitekelezwa ndani ya fikira Zake; hakuna maneno yaliyotolewa, lakini mamlaka yaliyokuwa ya kipekee kwa Muumba yalidhibiti viumbe vyote kwa kimya ambacho hakikumiliki matumizi yoyote ya lugha, na iliyokuwa tofauti na mwanadamu. Utiliaji mkazo wa mamlaka Yake kwa njia hii maalum ulimshawishi binadamu kupata maarifa mapya, na kuufanya ufasiri mpya wa mamlaka ya kipekee ya Mungu. Hapa, lazima Niwaambie kwamba kwenye siku hii mpya, ule utiliaji mkazo wa mamlaka ya Muumba ulionyesha kwa mara nyingine ule upekee wa Muumba.
Kinachofuata, wacha tuangalie sentensi ya mwisho ya fungu hili la maandiko:
“Mungu akaona kwamba ni vizuri.”Unafikiri hii inamaanisha nini? Hapa, tunapata kuziona hisia za Mungu. Mungu alitazama viumbe vyote Alivyokuwa ameumba vikiumbika na kusimama wima kwa sababu ya matamshi Yake, na kwa utaratibu vikianza kubadilika. Wakati huu, Mungu alikuwa ametosheka na mambo mbalimbali Aliyoyaumba kwa matamshi Yake, na vitendo mbalimbali Alivyokuwa ametimiza? Jibu ni kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Wewe unaona nini hapa? Kinawakilisha nini kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri”? Kusema hivi kunaashiria nini? Kunamaanisha kwamba Mungu alikuwa na nguvu na hekima ya kukamilisha kile Alichokuwa amepangilia na kushauri, kukamilisha shabaha Alizokuwa ameweka wazi ili kuzikamilisha. Baada ya Mungu kukamilisha kila kazi, je, Alijutia chochote? Jibu lingali kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Kwa maneno mengine, Hakujutia chochote, lakini Alitosheka. Ni nini maana ya Yeye kutojutia chochote? Tunaelezewa kwamba Mpango wa Mungu ni mtimilifu, kwamba nguvu na hekima Zake ni timilifu, na hiyo ni kutokana tu na mamlaka Yake kwamba utimilifu kama huo unaweza kukamilishwa. Wakati binadamu anapotekeleza kazi, je, anaweza, kama Mungu, kuona kwamba kazi hiyo ni nzuri? Je, kila kitu anachofanya binadamu kinaweza kukamilika na kuwa timilifu? Je, binadamu anaweza kukamilisha kitu mara moja na kikawa hivyo daima dawamu? Kama vile tu binadamu anavyosema, “hakuna kitu kilicho timilifu, kinaweza tu kuwa bora zaidi,” hakuna kitu ambacho binadamu hufanya kinaweza kufikia utimilifu. Wakati Mungu alipoona kwamba kile Alichokuwa amefanya na kutimiza kilikuwa kizuri, kila kitu kilichoumbwa na Mungu kiliwekwa kwa matamshi Yake, hivi ni kusema kwamba, wakati “Mungu akaona kwamba ni vizuri,” kila kitu Alichoumba kikachukua mfumo wa kudumu, kikaainishwa kulingana na aina, na kikapewa mahali maalum, kusudio, na kazi, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu. Vilevile, wajibu wao miongoni mwa viumbe vyote na safari ambayo lazima waabiri kwenye usimamizi wa Mungu wa viumbe vyote, ulikuwa tayari umeamriwa na Mungu, na usingebadilishwa. Hii ilikuwa sheria ya kimbinguni iliyotolewa na Muumba kwa viumbe vyote.
“Mungu akaona kwamba ni vizuri,”matamshi haya mepesi, yasiyopongezwa, yanayopuuzwa mara nyingi, ndiyo matamshi ya sheria ya kimbinguni na maelekezo ya kimbinguni kwa viumbe vyote kutoka kwa Mungu. Ni mfano mwingine halisi wa mamlaka ya Muumba, mfano ambao ni wa kimatendo zaidi na unaojitokeza zaidi. Kupitia kwa matamshi Yake, Muumba hakuweza tu kufaidi kila kitu Alichoweka wazi ili kufaidi, na kutimiza kila kitu Alichoweka wazi ili kutimiza, lakini pia Aliweza kudhibiti mikononi Mwake, kila kitu Alichokuwa ameumba, na kutawala kila kitu Alichokuwa ameumba kulingana na mamlaka Yake, na, vilevile, kila kitu kilikuwa cha mfumo na cha kawaida. Viumbe vyote viliishi na kufa pia kwa matamshi Yake na, vilevile, kwa mamlaka Yake, vilikuwepo katikati ya sheria Aliyokuwa ameiweka wazi, na hakuna kiumbe kilichoachwa! Sheria hii ilianza punde tu “Mungu alipoona kuwa ni vyema,” na itakuwepo, itaendelea, na kufanya kazi kwa minajili ya mpango wa Mungu wa usimamizi mpaka siku ile itabatilishwa na Muumba! Upekee wa mamlaka ya Muumba ulionyeshwa si tu katika uwezo Wake wa kuumba viumbe vyote na kuamuru viumbe vyote kuwepo, lakini pia katika uwezo Wake wa kutawala na kushikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na kupatia maisha na nguvu kwa viumbe vyote, na, vilevile, katika uwezo Wake kusababisha, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu, viumbe vyote ambavyo Angeumba katika mpango Wake ili kuonekana na kuwepo katika ulimwengu ulioumbwa na Yeye kwa umbo timilifu, na kwa muundo wa maisha timilifu, na wajibu timilifu. Na ndivyo pia ilivyoonyeshwa kwa njia ambayo fikira za Muumba hazikutegemea vizuizi vyovyote, hazikuwekewa mipaka ya muda, nafasi, au jiografia. Kama mamlaka Yake, utambulisho wa kipekee wa Muumba utabakia vilevile milele hata milele. Mamlaka yake siku zote yatakuwa uwakilishi na ishara ya utambulisho Wake wa kipekee, na mamlaka Yake yatakuwepo milele sambamba na utambulisho Wake!
Kwenye Siku ya Sita, Muumba Aongea, na Kila Aina ya Kiumbe Hai Akilini Mwake Chajitokeza, Kimoja Baada ya Kingine
Bila kuchoka, kazi ya Muumba ya kuumba viumbe vyote ilikuwa imeendelea kwa siku tano, na punde tu baada ya hapo ndipo Muumba alipokaribisha siku ya sita ya uumbaji Wake wa viumbe vyote. Siku hii ilikuwa mwanzo mwingine mpya, na siku nyingine isiyo ya kawaida. Nini, basi, kilikuwa mpango wa Muumba mkesha wa siku hii mpya? Ni viumbe vipi vipya ambavyo Angezalisha, je, Angeviumba? Sikiliza, hii ndiyo sauti ya Muumba….
“Naye Mungu aksema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri.” (Mwa 1:24-25). Viumbe hai gani ndivyo vinavyojumuishwa hapa? Maandiko yanasema: ng'ombe, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye siku hii hakukuweko tu na aina zote za viumbe hai kwenye nchi, lakini pia vyote vilikuwa vimeainishwa kulingana na aina, na, vilevile, “Mungu akaona ya kuwa ni vizuri.”
Kama tu kwenye siku zile tano za awali, na kwa sauti sawa, kwenye siku ya sita Muumba akashurutisha kuzaliwa kwa viumbe hai Alivyotamani, na vikajitokeza kwenye nchi, kila kimoja kulingana na aina yake. Wakati Muumba anapotekeleza mamlaka Yake, hakuna matamshi Yake yanayotamkwa bure bilashi, na kwa hivyo, kwenye siku ya sita, kila kiumbe hai ambacho Alikuwa amenuia kuumba kikajitokeza wakati ule Aliochagua. Muumba aliposema “Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake,”nchi ilijawa mara moja na maisha, na juu ya ardhi kukaibuka pumzi za aina zote za viumbe hai…. Kwenye jangwa lenye nyasi za kijani, ng’ombe wanene, wakichezesha mikia yao huku na kule, walijitokeza mmoja baada ya mwengine, kondoo waliokuwa wakitoa milio walikusanyika kwa makundi, na farasi waliotoa milio wakaanza kurukaruka…. Mara moja, nchi pana tambarare yenye utulivu ikajaa uhai…. Kujitokeza kwa mifugo hii mbalimbali kulikuwa mandhari ya kupendeza kwenye nchi ile tambarare iliyotulia, na kujitokeza huko kukaleta nguvu zisizo na mipaka …. Wangekuwa wenza wa nchi ile tambarare, na wenyeji wakuu wa nchi ile tambarare, kila mmoja akitegemea mwengine; na vilevile ndivyo pia wangekuwa walezi na walinzi wa ardhi hizi, ambazo zingekuwa makao yao ya kudumu, na ambazo zingewapa kila kitu walichohitaji, chanzo cha ukuzwaji wa milele kwa minajili ya kuwepo kwao …
Kwenye siku iyo hiyo ambayo mifugo hii mbalimbali ilijitokeza, kwa tamko la Muumba, wadudu wengi pia walijitokeza, mmoja baada ya mwengine. Hata ingawaje ndio waliokuwa viumbe hai wadogo zaidi miongoni mwa viumbe vyote, nguvu zao za uhai zilikuwa bado uumbaji wa kimiujiza wa Muumba, na hawakuwasili wakiwa wamechelewa sana…. Baadhi yao walipigapiga mabawa yao madogo, huku wengine wakitambaa polepole; baadhi waliruka juu kwa juu, wengine wakapepesuka; wengine walichimba wakienda mbele, huku wengine wakirudi nyuma kwa haraka; wengine walienda upandeupande, wengine wakaruka juu na chini…. Wote walishughulika kwa kujaribu kujitafutia makao: Baadhi walisukumana na kujipata kwenye nyasi, baadhi walianza kuyachimba mashimo ardhini, baadhi wakapaa hadi kwenye miti, wakiwa wamejificha kwenye msitu…. Ingawaje walikuwa wadogo kwa ukubwa, hawakuwa radhi kuvumilia mateso ya njaa, na baada ya kupata makao yao binafsi, walikimbia kutafuta chakula ili kuweza kujilisha. Baadhi yao walipanda juu ya nyasi ili wale ncha zake laini, baadhi yao walikamata uchafu kwenye vinywa vyao na kuanza kulisha matumbo yao, wakila kwa bidii na kwa furaha (kwao, hata uchafu ulikuwa mlo wenye ladha); wengine walikuwa wamejificha misituni, lakini hawakusita kupumzika, kwani majimaji ndani ya majani yale ya kijani kolevu cha kumetameta yaliwapa mlo wenye utomvu mwingi…. Baada ya wao kushiba, bado wadudu hawakusita kufanya shughuli zao; ingawa walikuwa wadogo kwa kimo, walimilikiwa na nishati ya ajabu pamoja na uchangamfu usio na mipaka, na kwa viumbe vyote wao ndio walikuwa amilifu zaidi na wenye bidii zaidi. Hawakuwahi kuwa wazembe, na hawakuhusika katika mapumziko yoyote. Baada ya kushiba, bado walifanya kazi na wakafanyiza miili yao bidii kwa minajili ya siku zao za usoni, wakiwa wamejishughulisha na kukimbia hapa na pale kwa minajili ya kesho yao ili waweze kuishi…. Kwa utaratibu waliweza kuimba nyimbo zenye midundo tofauti ili kuhimizana na kusihi kila mmoja wao aendelee na kazi. Waliweza pia kuongeza furaha kwenye nyasi, miti, na kila inchi ya udongo, huku wakifanya kila siku, na kila mwaka kuwa wa kipekee…. Wakiwa na lugha zao binafsi na kwa njia zao wenyewe, walipitisha taarifa kwa viumbe vyote vilivyokuwa ardhini. Na wakitumia mkondo wao binafsi maalum wa maisha, waliweka alama katika viumbe vyote, na baadaye wakaacha alama…. Walikuwa na uhusiano wa karibu sana na mchanga, nyasi, na misitu, na walipatia mchanga nguvu na uthabiti, vivyo hivyo kwenye nyasi, na misitu na wakaweza kuleta ushawishi na salamu za Muumba kwa viumbe hai vyote …
Mtazamo wa Muumba ulienea kotekote kwenye viumbe vyote ambavyo Alikuwa ameumba na wakati huu kwa muda huo macho Yake yalitulizia misitu na milima, akili Yake ikigeuka. Huku matamshi Yake yakitamkwa wazi kwenye misitu mingi, na juu ya milima, kulionekana aina ya viumbe fulani vilivyokuwa tofauti na vyovyote vile vilivyokuwa vimekuja hapo awali: Walikuwa wanyama wa mwitu waliotamkwa kwa kinywa cha Mungu. Walikuwa wamepitiliza muda mrefu ajabu, walitikisa vichwa vyao na kupigapiga mikia yao, huku kila mmoja wao akiwa na uso wake pekee. Baadhi yao walikuwa na manyoya mengi, baadhi yao walikuwa wamejikinga, baadhi yao walikuwa na meno ya sumu, baadhi yao walikuwa wanakenua, baadhi yao walikuwa na shingo-ndefu, baadhi yao walikuwa na mkia—mfupi, baadhi walikuwa na macho— mapana, baadhi walikuwa na mtazamo wa woga, baadhi walikuwa wamejiinamia ili wale nyasi, baadhi walikuwa na damu midomoni mwao, baadhi walikuwa wakidundadunda kwa miguu miwili, baadhi walikuwa wakirukaruka kwa kwato nne, baadhi walikuwa wakiangalia mbele juu ya mti, baadhi walikuwa wamejilalia tu wakisubiria misituni, baadhi walikuwa wakitafuta vyumba vya chini kwa chini ili kupumzika, baadhi walikuwa wakikimbiakimbia na kuonyesha furaha ya kipekee kwenye nchi tambarare, baadhi walikuwa wakinyatianyatia kwenye misitu…; baadhi walikuwa wakinguruma, baadhi walikuwa wakitoa milio mikali, baadhi walikuwa wakibweka, baadhi walikuwa wakilia…; baadhi walikuwa na sauti nyororo, baadhi walikuwa na sauti ya kati, baadhi walikuwa na sauti nzito, baadhi walikuwa na sauti safi na yenye mdundo wa kimuziki…; baadhi walikuwa wa kuogofya, na baadhi walikuwa warembo, na baadhi walikuwa wakitisha, baadhi walikuwa wa kuvutia, baadhi walikuwa wa kutishia, baadhi walikuwa wasio na hatia ila wachangamfu…. Mmoja baada ya mwengine, wote walikuja. Tazama namna walivyotembea, kwenye uhuru, wasijue chochote kuhusu wenzao waliokuwa kando yao, wasitake hata kuchukua muda kutazamana…. Kila mmoja akiwa na maisha fulani waliyopewa na Muumba, na umwitu wao binafsi, na ukatili, walionekana kwenye misitu na pia juu ya milima. Viumbe vya kudharauliwa kati ya vyote, na vyenye kuamrisha kabisa—ni nani aliyewafanya kuwa mabingwa wa kweli wa milimani na misituni? Kutoka muda ambao Kuonekna kwao kuliamriwa na Muumba, waliweza “kuweka madai” hayo katika misitu, na “kuweka madai” kwenye milima, kwani Muumba alikuwa tayari amepangilia mipaka yao na Akaamua upana wa uwepo wao. Hawa ndio waliokuwa mabwana wa kweli wa milimani na misitu, na ndiyo maana walikuwa na umwitu mwingi na kwa hivyo wenye dharau. Waliitwa “wanyama wa mwituni” kimsingi kwa sababu, kati ya viumbe vyote, ndio waliokuwa wasiowezekana, wenye unyama, na wasiofugwa. Wasingeweza kufugwa, hivyo basi wasingeweza kulelewa na wasingeishi kwa amani na mapatano na mwanadamu au kufanya kazi kwa niaba ya mwanadamu. Ni kwa Sababu hawakuweza kufugwa, hawakuweza kumfanyia kazi mwanadamu, ndiyo maana iliwalazimu kuishi kwa umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kusongelewa na mwanadamu. Na ilikuwa kwa sababu waliishi umbali fulani kutoka kwa mwanadamu, na wasingeweza kukaribiwa na mwanadamu ndiposa waliweza kutimiza wajibu wao waliopewa na Muumba: kuilinda milima na misitu. Ule umwitu wao uliilinda milima na kulinda misitu, na ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi na wenye hakikisho la uwepo wao na utekelezaji wao. Wakati uo huo, umwitu wao uliendeleza na kuhakikisha usawazisho miongoni mwa viumbe vyote. Kuwasili kwao kulileta msaada na ukitaji mizizi kwenye milima na misitu; kuingia kwao kuliweza kuingiza nguvu na uthabiti zaidi kwenye milima ile mitupu na misitu mitupu. Kuanzia hapa kwenda mbele, milima na misitu ikawa ni makao yao ya kudumu, na wasingewahi kupoteza maskani yao, kwa sababu milima na misitu ilionekana na ikawepo kwa ajili yao, na wanyama wa mwituni wangetimiza wajibu wao na kufanya kila kitu ambacho wangeweza ili kuilinda. Kwa hivyo, pia, wanyama wa mwituni wangeweza kutii kwa umakinifu kule kusihiwa na Muumba ili waweze kushikilia eneo lao, na kuendelea kutumia asili yao ya kinyama ili kuendeleza usawazisho wa viumbe vyote vilivyoanzishwa na Muumba, na kuonyesha waziwazi mamlaka na nguvu za Muumba!
Katika Mamlaka ya Muumba, Viumbe Vyote ni Timilifu
Viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, vikiwemo vile vilivyoweza kusonga na vile visingeweza kusonga, kama vile ndege na samaki, kama vile miti na maua, na hata ikiwemo mifugo, wadudu na wanyama wa mwituni, wote walioumbwa kwenye siku ya sita—wote walikuwa wazuri mbele ya Mungu, na, vilevile, machoni mwa Mungu, viumbe hivi, kulingana na mpango Wake, vilikuwa vimetimiza kilele cha utimilifu, navyo vilikuwa vimefikia viwango ambavyo Mungu alitaka kutimiza. Hatua kwa hatua, Muumba alifanya kazi Aliyonuia kufanya kulingana na mpango Wake. Kimoja baada ya kingine, vitu hivi Alivyonuia kuumba vilijitokeza, na kujitokeza kwa kila kiumbe kulikuwa onyesho la Mamlaka ya Muumba, na uthibitishaji wa mamlaka Yake, na kwa sababu ya uthibitishaji huu, viumbe vyote visingeweza kufanya chochote kingine ila kushukuru kwa neema ya Muumba na riziki ya Muumba. Huku vitendo hivi vya kimiujiza vya Mungu vikijionyesha, ulimwengu huu ulijaa, vipande kwa vipande, ukiwa na viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, na ukabadilika kutoka kwa fujo na giza hadi kwa wazi na uangavu, kutoka kwenye utulivu wa kutisha hadi kwa uchangamfu na nguvu zisizokuwa na mipaka. Miongoni mwa viumbe vyote vya uumbaji, kutoka kwa wale wakubwa hata wadogo, toka kwa wadogo hata kwa wale wadogo zaidi, hakuna hata kiumbe kimoja ambacho hakikuumbwa kupitia kwa Mamlaka na nguvu za Muumba, na kukawa na upekee na haja ya ndani kwa ndani na thamani ya uwepo wa kila kiumbe. Licha ya tofauti zao katika maumbo na muundo, lazima viumbe hivi vingeumbwa na Muumba ili viwepo chini ya mamlaka ya Muumba. Wakati mwingine watu wataona mdudu, yule aliye na sura mbaya kabisa na watasema, “Mdudu yule ni sura mbaya kweli, hakuna vile ambavyo kiumbe chenye sura mbaya kama hicho kinaweza kuwa kiliumbwa na Mungu—hakuna njia ambayo Angeumba kitu chenye sura mbaya hivyo.” Mtazamo wa kijinga ulioje! Kile wanachofaa kusema ni, “ingawaje mdudu huyu ana sura mbaya sana, aliumbwa na Mungu, na kwa hivyo, lazima awe na kusudio lake la kipekee.” Kwenye fikira za Mungu, Alinuia kupatia kila mojawapo ya sura, na kazi na matumizi aina zote, katika viumbe mbalimbali vilivyo na uhai Alivyoumba, na hivyo basi hamna kati ya viumbe hivyo ambavyo Mungu aliumba vilivyoumbwa vikiwa vimefanana. Kuanzia sura yao ya nje hadi mkusanyiko wao wa ndani, kuanzia katika mazoea yao ya kuishi hadi mahali pa kuishi—kila kiumbe ni tofauti. Ng’ombe wana sura ya ng’ombe, punda wana sura ya punda, paa ana sura ya paa, na ndovu wana sura ya ndovu. Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi kinachovutia zaidi na ni kipi kinachotisha zaidi kwa sura? Je, unaweza kusema ni kiumbe kipi chenye manufaa zaidi na uwepo wa kile ambacho hakihitajiki sana? Baadhi ya watu wanapenda namna ambavyo ndovu hufanana, lakini hakuna anayetumia ndovu kutayarisha mashamba ya kupanda: baadhi ya watu wanapenda namna simba na chui mkubwa mwenye milia walivyo, kwani sura inavutia zaidi miongoni mwa viumbe vyote, lakini je, unaweza kuwafuga nyumbani? Kwa ufupi, kuhusiana na viumbe vyote, binadamu anafaa kurejelea mamlaka ya Muumba, hivi ni kusema kwamba, rejelea mpangilio uliochaguliwa na Muumba katika viumbe vyote; huu ndio mtazamo wenye hekima zaidi. Mtazamo tu wa kutafutiza, na wa kuwa mtiifu, kwa nia ama makusudio ya mwanzo ya Muumba ndio ukubalifu wa kweli na hakika wa mamlaka ya Muumba. Ni vyema kwa Muumba, kwa hivyo ni sababu gani ambayo binadamu atakuwa nayo ya kusema kwamba si vyema?
Hivyo basi, viumbe vyote vilivyo katika mamlaka ya Muumba vitaweza kuchezesha mdundo mpya wa ukuu wa Muumba, vitaanza utangulizi mwema kwa minajili ya kazi Yake kwenye siku mpya, na kwa muda huu Muumba ataufungua ukurasa mpya katika kazi ya usimamizi Wake! Kulingana na sheria ya mimea ya machipuko, kukomaa kwa kiangazi, mavuno ya mapukutiko, na hifadhi ya kipupwe iliyochaguliwa na Muumba, viumbe hivi vyote vitaweza kutilia mkazo mpango wa usimamizi wa Muumba na vitakaribisha siku yao mpya, mwanzo mpya, na mkondo mpya wa maisha, na hivi karibuni vitu vitaweza kuzaana katika mfululizo usioisha ili kuweza kukaribisha kila siku katika ukuu wa mamlaka ya Muumba ...
Hakuna Kiumbe Chochote Kati ya Vile Vilivyoumbwa na Vile Ambavyo Havikuumbwa Kinaweza Kubadilisha Utambulisho wa Muumba
Tangu Alipoanza uumbaji wa viumbe vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni njia gani Alitumia, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, viumbe vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwenye muda kabla ya mwanadamu kuumbwa ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba viumbe vyote kwa minajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwenye viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, nuru, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, zikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila mojawapo kilipewa maisha kwa matamshi ya Muumba, na kila kiumbe mojawapo kilizaana kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimojawapo kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawaje hawakupokea pumzi za Muumba, bado walionyesha maisha na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa mifumo na miundo yao mbalimbali; ingawaje hawakupokea uwezo wa kuongea aliopewa mwanadamu na Muumba, kila kimojawapo kilipokea njia ya kuelezea maisha yao ambayo walipewa na Muumba, na ambayo ilitofautiana na ile lugha ya Mwanadamu. Mamlaka ya Muumba hayatoi tu nguvu za maisha kwenye vifaa vinavyoonekana kuwa tuli, ili visiwahi kutoweka, lakini, vilevile, hupatia silika ya kuzaana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, vitaweza kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatilia mkazo mamlaka Yake haikubaliani kwa lazima na mtazamo wa mambo makubwamakubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka ya umbo lolote; Anaweza kuamuru utendaji mambo katika ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya maisha na kifo cha viumbe vyote, na, vilevile, Anaweza kushughulikia viumbe vyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala viumbe vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya pekee ya Muumba miongoni mwa viumbe vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu ya maisha tunayoishi, na hayatawahi kusita, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kubadilisha utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote-ambacho hakikuumbwa. Chukulia wajumbe na malaika wa Mungu kwa mfano. Hawamiliki nguvu za Mungu, isitoshe hawamiliki mamlaka ya Muumba, na sababu ambayo hawana nguvu na mamlaka ya Mungu ni kwa sababu hawamiliki ile hali halisi ya Muumba. Vile viumbe ambavyo havikuumbwa, kama vile wajumbe na malaika wa Mungu, ingawaje vinaweza kufanya baadhi ya mambo kwa niaba ya Mungu, haviwezi kuwakilisha Mungu. Ingawaje wanamiliki nguvu fulani zisizomilikiwa na binadamu, hawamiliki mamlaka ya Mungu, hawamiliki mamlaka ya Mungu ya kuumba viumbe vyote, na kuamuru viumbe vyote, na kushikilia kuwa na ukuu juu ya viumbe vyote. Na kwa hivyo upekee wa Mungu hauwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa, na vilevile, mamlaka na nguvu za Mungu haviwezi kusawazishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Kwenye Biblia, je, umewahi kusoma kuhusu mjumbe yeyote wa Mungu aliyeumba viumbe vyote? Na kwa nini Mungu hakuwahi kutuma mmojawapo wa wajumbe Wake au malaika kuumba viumbe vyote? Kwa sababu hawakumiliki mamlaka ya Mungu, na kwa hivyo hawakumiliki uwezo wa kutekeleza mamlaka ya Mungu. Sawa tu na viumbe vyote, viumbe vyote visivyoumbwa viko chini ya ukuu wa Muumba, na chini ya mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo, kwa njia ile ile, Muumba pia ni Mungu wao na pia ndiye Mtawala wao. Miongoni mwa kila mmoja wao—haijalishi kama wao ni sharifu au kina yahe, wenye nguvu nyingi au kidogo—hakuna hata mmoja anayeweza kuzidi mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo miongoni mwao, hakuna hata mmoja wao anayeweza kubadilisha utambulisho wa Muumba. Hawatawahi kuitwa Mungu, na hawatawahi kuweza kuwa Muumba. Huu ni ukweli na hoja zisizobadilika!
Kupitia ushirika uliotajwa hapo juu, je, tunaweza kusema yafuatayo: Muumba na Kiongozi wa viumbe vyote tu, Yule anayemiliki mamlaka ya kipekee na nguvu za kipekee, ndiye Anayeweza kuitwa Mungu Mwenyewe wa kipekee? Wakati huu, unaweza kuhisi kwamba swali kama hilo ni la kina sana. Wewe, kwa muda huu, huwezi kulielewa, na huwezi kung'amua kiini cha ndani na kwa hivyo kwa muda huu unahisi kwamba ni swali gumu kujibu. Kwa hivyo, Nitaendelea na ushirika Wangu. Kinachofuata, Nitakuruhusu kutazama vitendo halisi vya dhana nyingi za mamlaka na nguvu zinazomilikiwa na Mungu pekee, na hivyo basi Nitakuruhusu kuelewa kwa kweli, kushukuru, na kujua upekee wa Mungu, na maana ya mamlaka ya kipekee ya Mungu.
2. Mungu Hutumia Matamshi Yake Kuanzisha Agano na Binadamu
Mwa 9:11-13 Na nitaweka agano langu na ninyi, wala miili yote haitaondolewa tena na maji ya gharika; wala hakutakuwa na gharika tena kuiharibu dunia. Naye Mungu akasema, Hii ni alama ya agano ambayo naifanya kati ya Mimi na ninyi na viumbe vyote vyenye uhai vilivyo nanyi, kwa vizazi vya kudumu: naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.
Baada ya Kuumba Viumbe Vyote, Mamlaka ya Muumba Yanathibitishwa na Kuonyeshwa kwa Mara Nyingine Tena Kwenye Agano la Upinde wa Mvua
Mamlaka ya Muumba siku zote yanaonyeshwa na kutekelezwa miongoni mwa viumbe vyote, Naye hatawali tu hatima ya viumbe vyote, lakini pia Anatawala mwanadamu, kiumbe maalum ambacho Aliumba kwa mikono Yake mwenyewe, na kinachomiliki muundo tofauti wa uhai na kinachopatikana kwa mfumo tofauti wa uhai. Baada ya kuumba viumbe vyote, Muumba hakusita kuonyesha mamlaka na nguvu Zake; kwake Yeye, mamlaka ambayo Alishikilia ukuu juu ya viumbe vyote na hatima ya mwanadamu kwa ujumla, ilianza rasmi tu pale ambapo mwanadamu alizaliwa kwa kweli kutoka kwenye mkono Wake. Alinuia kusimamia mwanadamu, kutawala mwanadamu, Alinuia kumwokoa mwanadamu, Alinuia kufaidi mwanadamu kwa kweli, kufaidi mwanadamu ambaye angetawala viumbe vyote, na Alinuia kumfanya mwanadamu kama huyo kuishi chini ya mamlaka Yake, na kujua mamlaka Yake, na kutii mamlaka Yake. Hivyo basi, Mungu akaanza kuonyesha rasmi mamlaka Yake miongoni mwa binadamu kwa kutumia matamshi Yake, na Akaanza kutumia mamlaka Yake kutambua matamshi Yake. Bila shaka, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa mbele katika sehemu zote wakati wa mchakato huu; Nimeweza kuchukua tu baadhi ya mifano mahususi, inayojulikana ambayo unaweza kuelewa na kujua upekee wa Mungu na kuelewa na kujua upekee wa mamlaka ya Mungu.
Kunao mfanano kati ya fungu kwenye Mwanzo 9:11-13 na Mafungu yaliyo hapo juu yanayohusu rekodi za Mungu kuumba ulimwengu, ilhali kunayo pia tofauti. Mfanano ni upi? Mfanano umo katika matumizi ya matamshi na Mungu kuweza kufanya kile ambacho Alinuia, na tofauti ni kwamba, fungu hili ni mazungumzo ya Mungu na binadamu, ambapo Alianzisha agano na binadamu, na Akamwambia binadamu kuhusu kile ambacho kilikuwa ndani ya agano hilo. Utiliaji mkazo huu wa mamlaka ya Mungu ulitimizwa wakati wa mazungumzo Yake na Mungu, hivi ni kusema kwamba, kabla ya uumbaji wa mwanadamu, maneno ya Mungu yalikuwa maagizo, na amri ambavyo vilitolewa kwa viumbe ambavyo Alinuia kuumba. Lakini sasa kulikuwa na mtu wa kusikiliza matamshi ya Mungu, na hivyo basi matamshi Yake yalikuwa ya mazungumzo na binadamu, na pia himizo na onyo kwa binadamu, na zaidi, kulikuwa na amri zilizotolewa kwa viumbe vyote vilivyokuwa na mamlaka Yake.
Ni hatua gani ya Mungu imerekodiwa katika fungu hili? Inarekodi agano ambalo Mungu alianzisha na binadamu baada ya Yeye kuangamiza ulimwengu kwa gharika, linamwambia binadamu kwamba Mungu asingesababisha maangamizo katika ulimwengu tena, na kwamba, hadi mwisho huu, Mungu aliumba ishara—na ishara hii ilikuwa nini? Kwenye Maandiko inasemekana kwamba“naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.”Haya ni matamshi ya asili yaliyotamkwa na Muumba kwa mwanadamu. Aliposema matamshi haya, upinde wa mvua ulionekana mbele ya macho ya binadamu, ambapo ulibakia mpaka leo. Kila mmoja ameuona upinde wa mvua kama huo, na unapouona, je, unajua namna unavyojitokeza? Sayansi haiwezi kuthibitisha haya, au kutafuta chanzo chake, au kutambua mambo yanayosababisha upinde huu wa mvua. Hiyo ni kwa sababu, upinde wa mvua ni ishara ya agano lilioanzishwa kati ya Muumba na binadamu; hauhitaji msingi wowote wa kisayansi, haukuumbwa na binadamu, wala binadamu hawezi kuubadilisha. Ni maendelezo ya mamlaka ya Muumba baada ya Yeye kuongea matamshi Yake. Muumba alitumia mbinu fulani Yake mwenyewe kutii agano lake na binadamu na ahadi Yake, na hivyo basi matumizi Yake ya upinde wa mvua kama ishara ya agano ambalo Alianzisha ni maelekezo na sheria ya kimbinguni yatakayobakia milele hivyo, haijalishi kama ni kuhusiana na Muumba au mwanadamu aliyeumbwa. Ilhali sheria hii isiyobadilika ni, lazima isemwe, maonyesho mengine ya kweli ya mamlaka ya Muumba kufuatia uumbaji Wake wa viumbe vyote, na lazima isemwe kwamba mamlaka na nguvu za Muumba havina mipaka; matumizi Yake ya upinde wa mvua ni ishara ya maendelezo na upanuzi wa mamlaka ya Muumba. Hiki kilikuwa kitendo kingine kilichotekelezwa na Mungu kwa kutumia matamshi Yake, na kilikuwa ni ishara ya agano ambalo Mungu alikuwa ameanzisha na mwanadamu kwa kutumia matamshi. Alimwambia binadamu kuhusu kile ambacho Aliamua kuleta, na kwa njia gani kingekamilishwa na kutimizwa, na kwa njia hii suala liliweza kutimizwa kulingana na matamshi kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na leo, miaka elfu kadhaa baada ya Yeye kuongea matamshi haya, binadamu angali bado anaweza kuangalia upinde wa mvua uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Kwa sababu ya matamshi hayo yaliyotamkwa na Mungu, kitu hiki kimebakia bila ya kusongezwa na kubadilishwa mpaka hadi leo. Hakuna anayeweza kuuondoa upinde huu wa mvua, hakuna anayeweza kubadilisha sheria zake, na upo kimsingi kutokana na matamshi ya Mungu. Haya kwa hakika ni mamlaka ya Mungu. “Mungu ni mzuri tu kama matamshi Yake, na matamshi Yake yataweza kukamilishwa, na kile ambacho kimekamilishwa kinadumu milele.” Matamshi kama haya kwa kweli yanaonyeshwa waziwazi hapa, na ni ishara na sifa wazi kuhusu mamlaka na nguvu za Mungu. Ishara au sifa kama hiyo haimilikiwi na au kuonekana katika viumbe vyovyote vile vilivyoumbwa, wala kuonekana kwenye viumbe vyovyote vile ambavyo havikuumbwa. Inamilikiwa tu na Mungu wa kipekee, na inapambanua utambulisho na hali halisi inayomilikiwa tu na Muumba kutoka ile ya viumbe. Wakati uo huo, ni ishara na sifa pia ambayo mbali na Mungu Mwenyewe, haitawahi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa.
Uanzishaji wa agano Lake Mungu na binadamu kilikuwa ni kitendo chenye umuhimu mkubwa, na ambao Alinuia kutumia ili kuwasilisha hoja kwa binadamu na kumwambia binadamu mapenzi Yake, na hadi hapa, Alitumia mbinu ya kipekee, kwa kutumia ishara maalum ya kuanzisha agano na binadamu, ishara ambayo ilikuwa ahadi ya agano ambalo Alikuwa ameanzisha na binadamu. Kwa hivyo, je, uanzishaji wa agano hili ulikuwa ni tukio kubwa? Na tukio hili lilikuwa kubwa vipi? Hii haswa ndiyo inayoonyesha namna ambavyo agano hili lilivyo maalum: si agano lililoanzishwa kati ya binadamu mmoja na mwengine, au kundi moja na jingine, au nchi moja na nyingine, lakini agano lililoanzishwa kati ya Muumba na wanadamu kwa ujumla, na litabakia halali mpaka siku ambayo Muumba atakomesha mambo yote. Mtekelezaji wa agano hili ni Muumba, na mwendelezaji pia ni Muumba. Kwa ufupi, uzima wa agano la upinde wa mvua ulioanzishwa pamoja na mwanadamu ulikamilishwa na kutimizwa kulingana na mazungumzo kati ya Muumba na mwanadamu, na umebakia vivyo hivyo mpaka leo. Ni nini kingine ambacho viumbe vinaweza kufanya mbali na kujinyenyekeza, na kutii, na kusadiki, na kushukuru, na kutolea ushuhuda, na kusifu mamlaka ya Muumba? Kwani hamna yeyote yule isipokuwa Mungu wa pekee anayemiliki nguvu za kuanzisha agano kama hilo. Kujitokeza kwa upinde wa mvua mara kwa mara, kunatangaza kwa mwanadamu na kumtaka azingatie agano lile kati ya Muumba na mwanadamu. Katika kujitokeza kwingine kwa agano kati ya Muumba na binadamu, kile kinachoonyeshwa kwa mwanadamu si upinde wa mvua au agano lenyewe, lakini ni mamlaka yenyewe yasiyobadilika ya Muumba. Kujitokeza kwa upinde wa mvua, mara kwa mara, kunaonyesha yale matendo ya kipekee na ya kimiujiza ya Muumba yanayopatikana kwenye sehemu zilizofichwa, na, wakati uo huo ni onyesho muhimu la mamlaka ya Muumba ambayo hayatawahi kufifia, na wala kubadilika. Je, hili si onyesho la dhana nyingine ya mamlaka ya kipekee ya Muumba?
3. Baraka za Mungu
Mwa 17:4-6 Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwa wewe.
Mwa 18:18-19 Kuona kwamba Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye? Kwani namjua, kuwa atawatawala watoto wake na nyumba yake kufuata yeye, na wataishika njia ya Yehova, kufanya haki na hukumu; ili Yehova aweze kumletea Ibrahimu yale ambayo amemwambia.
Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kujipitia, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.
Ayu 42:12 Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike.
Njia na Sifa za Kipekee za Matamshi ya Muumba Ni Ishara ya Utambulisho na Mamlaka ya Kipekee ya Muumba
Wengi hupenda kutafuta, na kufaidi, baraka za Mungu, lakini si kila mmoja anayeweza kufaidi baraka hizi, kwani Mungu anazo kanuni Zake binafsi, na Yeye hubariki binadamu kulingana na njia Zake binafsi. Ahadi ambazo Mungu hutoa kwa binadamu, na kiwango cha neema ambacho Yeye humpa binadamu, vyote vinatolewa kulingana na fikira na vitendo vya binadamu. Na kwa hivyo ni nini huonyeshwa kupitia kwa baraka za Mungu? Huwa zinatwambia nini? Wakati huu, hebu tuweke kando mazungumzo kuhusu ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki, au kanuni anazofuata Mungu katika kubariki binadamu. Badala yake, hebu tuangalie baraka za Mungu kwa binadamu kwa kusudio la kujua mamlaka ya Mungu, kutoka kwenye mtazamo wa kujua mamlaka ya Mungu.
Mafungu manne ya maandiko yaliyotajwa hapo juu yote ni rekodi kuhusu baraka za Mungu kwa binadamu. Yanatupa ufafanuzi wenye maelezo kuhusu wapokeaji wa baraka za Mungu, kama vile Ibrahimu na Ayubu, vilevile yanatupa sababu zinazoelezea kwa nini Mungu alitoa baraka Zake, na ni nini kilichokuwa kwenye baraka hizi. Ile sauti na njia ya matamshi ya Mungu, mtazamo na mahali ambapo Alitamka, huturuhusu kushukuru kwamba Yule anayetoa baraka na mpokeaji wa baraka kama hizo ni wenye utambulisho, hadhi, na hali halisi tofauti kabisa. Sauti na njia ambayo matamshi haya yanatolewa, na mahali ambapo yalitamkwa, vinaonyesha upekee wao kwa Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba. Anayo mamlaka na uwezo, pamoja na heshima ya Muumba, na adhama isiyovumilia shaka kutoka kwa binadamu yeyote.
Kwanza hebu tuangalie Mwa 17:4-6:“Na kuhusu mimi, tazama, agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa baba yao mataifa mengi. Nalo jina lako halitakuwa Abramu tena, ila jina lako litaitwa Ibrahimu; kwa kuwa nimekufanya uwe baba yao mataifa mengi. Na Mimi nitafanya uwe na uzao ulio mwingi mno, na nitayaunda mataifa kutoka kwako, nao wafalme watatoka kwa wewe.”Matamshi haya ndiyo yaliyokuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, pamoja na baraka za Mungu kwa Ibrahimu: Mungu angemfanya Ibrahimu baba wa mataifa, Angemfanya kuwa na uzao mwingi, na Angemfanya kuwa na mataifa mengi, nao wafalme wangetoka kwake. Je, unayaona mamlaka ya Mungu katika maneno haya? Na unayaonaje mamlaka kama hayo? Ni dhana gani ya hali halisi ya mamlaka ya Mungu unayoona? Kutoka kwa usomaji wa makini wa maneno haya, si vigumu kutambua kwamba mamlaka na utambulisho wa Mungu vyote vimefichuliwa waziwazi na maneno ya matamshi ya Mungu. Kwa mfano, Mungu anaposema “agano langu liko na wewe, na wewe utakuwa … kuwa nimekufanya … Mimi nitafanya uwe…,” kauli kama vile “wewe utakuwa” na “nitayaunda,” ambazo maneno yake yanasheheni thibitisho la utambulisho na mamlaka ya Mungu, kwa upande mmoja ni onyesho la uaminifu wa Muumba; kwa upande mwingine, ni maneno maalum yaliyotumiwa na Mungu, anayemiliki utambulisho wa Muumba—pamoja na kuwa sehemu ya msamiati uliozoeleka. Kama mtu atasema anatumai kuwa mtu mwengine atazidisha uzao, kwamba mataifa yatatokana na wao, na kuwa wafalme watatoka miongoni mwao, basi hiyo bila shaka ni aina ya tamanio, na si ahadi wala baraka. Na hivyo, hawathubutu kusema “Mimi nitakufanya kuwa hivi na hivi, kufanya hivi na hivi,” kwani wanajua kwamba hawamiliki nguvu kama hizo; si juu yao, na hata kama watasema maneno kama hayo, maneno yao yatakuwa matupu, na ya kipuzi, yanayoendeshwa na matamanio na maono yao. Je, yupo yeyote anayethubutu kuongea kwa sauti kuu kama hiyo ilhali wanahisi kwamba hawawezi kutimiza matamanio yao? Kila mtu hutamani mema yafikie kizazi chake, na kutumai kwamba kitafanikiwa na kufurahia ufanisi mkubwa. Ni utajiri upi mkubwa utakaokuwepo kama mmoja wao angekuwa mfalme mkuu! Kama mmoja angekuwa gavana ingekuwa vizuri, pia—mradi tu wawe ni watu muhimu! Haya yote ni matamanio ya watu wote, lakini watu wanaweza kutamani tu baraka juu ya kizazi chao, na hawawezi kutimiza au kufanya ahadi zao zozote kuwa kweli. Katika mioyo yao, kila mtu anajua waziwazi kwamba wao hawamiliki nguvu za kutimiza mambo kama hayo, kwani kila kitu chao ni zaidi ya udhibiti wao, na hivyo basi watawezaje kuamuru hatima ya wengine? Sababu inayomfanya Mungu kusema mambo kama haya ni kwa vile Mungu anamiliki mamlaka kama hayo, na Anaweza kutekeleza na kutambua ahadi zote Anazotoa kwa ajili ya binadamu, na kufanya baraka zote Anazomwombea binadamu kuwa kweli. Binadamu aliumbwa na Mungu, na ili Mungu aweze kumuumba mtu atakayezidi kwa uzao ni jambo ambalo litakuwa rahisi sana; kufanya kizazi cha mtu kufanikiwa kutahitaji neno moja tu kutoka Kwake. Hatawahi kufanya kazi Mwenyewe na kutoa jasho kwa ajili ya kitu kama hicho, au kushughulisha akili Yake, au kujifunga mafunda mbalimbali; hii ndiyo nguvu halisi ya Mungu, mamlaka halisi ya Mungu.
Baada ya kusoma “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye”kwenye Mwanzo 18:18, je, unaweza kuhisi mamlaka ya Mungu hapo? Unaweza kuhisi hali isiyokuwa ya kawaida ya Muumba? Unaweza kuhisi hali ya mamlaka ya juu ya Muumba? Maneno ya Mungu yana uhakika. Mungu hasemi maneno kama hayo kwa sababu ya, au kwa kuwakilisha, ujasiri Wake katika ufanisi; hayo ni, badala yake, ithibati ya mamlaka ya matamshi, na ni amri inayotimiza maneno ya Mungu. Kunazo semi mbili ambazo unafaa kutilia maanani hapa. Wakati Mungu anaposema“Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye,”kunayo dalili ya kutoeleweka kwenye maneno haya? Kunayo dalili yoyote ya wasiwasi? Kunayo dalili yoyote ya woga? Kwa sababu ya matamshi “ataweza kwa hakika” na “atakuwa” kwenye matamshi ya Mungu, dalili hizi, ambazo zinapatikana tu kwa binadamu na mara nyingi zinajionyesha ndani yake, hazijawahi kupata uhusiano wowote na Muumba. Hakuna mtu angethubutu kutumia maneno kama haya wakati akiwatakia wengine mema, hakuna yule angethubutu kubariki mwengine apate taifa kubwa na lenye nguvu kwa uhakika kama huo, au kutoa ahadi kwamba mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia kwake. Maneno ya Mungu yanapokuwa na uhakika zaidi, ndipo yanathibitisha kitu fulani—na kitu hicho ni nini? Yanathibitisha kuwa Mungu anayo mamlaka kama hayo, kuwa mamlaka Yake yanaweza kutimiza mambo haya, na kwamba ufanisi wake ni lazima. Mungu alikuwa na uhakika katika moyo Wake, bila kusita kokote, kwa kila kitu Alichombariki Ibrahimu. Aidha, uzima wa haya utakamilishwa kulingana na maneno Yake, na hakuna nguvu ingeweza kubadilisha, kuzuia, kuharibu, au kutatiza kukamilika kwake. Licha ya kilichotendeka, hakuna kitu ambacho kingebatilisha au kuathiri kutimia na kukamilika kwa matamshi ya Mungu. Huu ndio uzito wenyewe wa maneno yaliyotamkwa kutoka kinywa cha Muumba, na mamlaka ya Muumba ambayo hayavumilii kanusho la binadamu! Baada ya kuyasoma maneno haya, ungali unahisi shaka? Maneno haya yalitamkwa kutoka kinywa cha Mungu, na kunazo nguvu, adhama na mamlaka katika maneno ya Mungu. Uwezo na mamlaka kama haya, na kutozuilika kwa kukamilika kwa hoja, haviwezi kufikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa na haviwezi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa. Muumba pekee ndiye anaweza kuongea na binadamu kwa sauti na mkazo kama huo, na hoja zimethibitisha kuwa ahadi Zake si maneno matupu, au majigambo ya kupitisha wakati, lakini ni maonyesho ya mamlaka ya kipekee yasiyoweza kupitwa na mtu, kitu, au kifaa chochote.
Ni nini tofauti kati ya maneno yanayotamkwa na Mungu na yale yanayotamkwa na binadamu? Unaposoma maneno haya yaliyotamkwa na Mungu, unahisi nguvu za maneno ya Mungu, na mamlaka ya Mungu. Je, unahisi vipi unaposikia watu wakitamka maneno kama hayo? Je, unafikiria kuwa wao wana kiburi kupindukia, na ni wenye kujigamba na kujionyesha? Kwani hawana nguvu hizi, hawamiliki mamlaka kama haya, na hivyo basi hawawezi kabisa kutimiza mambo kama hayo. Kwamba wao wana hakika kabisa kuhusu ahadi zao, yaonyesha tu kutojali kwa matamshi yao. Kama mtu anasema maneno kama hayo, basi bila shaka watakuwa wenye kiburi, na waliozidisha ujasiri wao, huku wakijifichua kama mfano wa pekee wa tabia ya malaika mkuu. Maneno haya yalitoka kinywani mwa Mungu; je, unahisi dalili yoyote ya kiburi hapa? Je, unahisi ya kwamba matamshi ya Mungu ni mzaha tu? Matamshi ya Mungu ni mamlaka, Maneno ya Mungu ni hoja za kweli, na kabla hajatamka maneno kutoka kinywani Mwake, hivi ni kusema, wakati Anapofanya uamuzi wa kufanya kitu, tayari kitu hicho kimefanyika. Yaweza kusemwa kwamba kila kitu alichosema Mungu kwa Ibrahimu kilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, na ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu. Ahadi hii ilikuwa hoja iliyoanzishwa, pamoja na hoja iliyokamilika, na hoja hizi zilitimizwa kwa utaratibu kwa fikira za Mungu kulingana na mpango wa Mungu. Kwa hivyo, Mungu kusema maneno kama hayo haimaanishi kuwa Ana tabia ya kiburi, kwani Mungu anaweza kutimiza mambo kama hayo. Anazo nguvu na mamlaka, na ana uwezo wa kutimiza hoja hizi, na mafanikio yake kwa jumla yanapatikana ndani ya uwezo Wake. Wakati maneno kama haya yanapotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, yanakuwa ufunuo na maonyesho ya tabia ya kweli ya Mungu, ufunuo na maonyesho timilifu ya hali halisi na mamlaka ya Mungu, na hakuna kitu ambacho kinafaa zaidi na kizuri kama ithibati ya utambulisho wa Mungu. Namna, sauti, na mpangilio wa maneno ya matamshi kama hayo ndiyo alama haswa ya utambulisho wa Muumba, na vyote hivi vinalingana kwa njia timilifu na maonyesho na utambulisho wa Mungu, na ndani yao hakuna kusingizia, au kasoro; vyote hivi ni, onyesho timilifu na lililo kamili kabisa, la hali halisi na mamlaka ya Muumba. Lakini Kuhusu viumbe, havimiliki mamlaka haya, wala hali hii halisi, vilevile havimiliki nguvu inayotolewa na Mungu. Kama binadamu atasaliti tabia kama hiyo, basi hali hiyo itakuwa bila shaka mlipuko wa tabia yake iliyopotoka, na itaishia kwa athari ya kujihusisha visivyofaa na kiburi cha binadamu na maono yasiyo na mipaka, na kufichuliwa kwa nia haribifu za yuleyule ibilisi, Shetani, anayependa kudanganya watu na kuwashawishi kuweza kusaliti Mungu. Naye Mungu anachukuliaje kile ambacho kimefichuliwa kwa lugha kama hii? Mungu angesema kwamba ungependa kunyakua nafasi Yake na kwamba unapenda kumwiga Yeye na kumbadili Yeye. Wakati unaiga sauti ya matamshi ya Mungu, nia yako ni ya kubadilisha mahali pa Mungu katika mioyo ya watu, kujitwalia mwanadamu ambaye anamilikiwa kwa haki na Mungu. Huyu ni Shetani, wazi na bila kukuficha; haya ni matendo ya vizazi vya malaika mkuu visivyovumilika Mbinguni! Miongoni mwenu, kunao wowote waliowahi kuiga Mungu kwa njia fulani kwa kuongea maneno machache, kwa nia ya kupotosha na kudanganya watu na kuwafanya watu kuhisi kuwa maneno na matendo ya mtu huyu yana mamlaka na nguvu za Mungu, kama kwamba hali halisi na utambulisho wa mtu huyo ni vya upekee, na hata ni kana kwamba sauti ya mtu huyu ni sawa na ile ya Mungu? Umewahi kufanya jambo kama hili? Umewahi kuiga sauti ya Mungu kwenye matamshi yako, kwa miondoko iliyodai kuwakilisha tabia za Mungu, ikiwa pamoja na uwezo na mamlaka ya kudhaniwa? Je, wengi wenu huwa mara nyingi mnatenda, au kupanga kutenda kwa njia kama hiyo? Sasa, unapoona kwa kweli, kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, na kutazama kile ulichokuwa ukikifanya, na ulichokuwa ukifichua kujihusu, je, unahisi vibaya? Je, unatambua hali yako ya kutoheshimu na kuwa na utovu wa haya? Baada ya kuchambua tabia na hali halisi ya watu kama hawa, je, inaweza kusemekana kuwa wao ndio walaaniwa wa jahanamu? Yaweza kusemekana kuwa kila mtu anayefanya mambo kama haya anajiletea udhalilishaji? Je, unatambua uzito wa asili yake? Na uzito wake ni wa kiasi kipi? Nia ya watu wanaotenda mambo kwa njia hii ni kuiga Mungu. Wanataka kuwa Mungu, na kuwafanya watu kuwaabudu kama Mungu. Wanataka kuondoa nafasi ya Mungu katika mioyo ya watu, na kutupilia mbali yule Mungu anayefanya kazi miongoni mwa binadamu, ili kutimiza nia ya kuwadhibiti watu, na kuwateketeza watu, na kuwamiliki watu hao. Kila mmoja anayo matamanio na maono kama hayo yaliyofichika akilini, na kila mmoja anaishi katika hali halisi potovu na ya kishetani kama hiyo na anaishi katika asili ya kishetani ambapo yumo katika uadui na Mungu, na anamsaliti Mungu, na anapenda kuwa Mungu. Kufuatia Ushirika Wangu katika mada hii ya Mungu, bado ungependa au ungetamani kujifanya wewe ni Mungu, au kuiga Mungu? Na bado unatamani kuwa Mungu? Ungali unapenda kuwa Mungu? Mamlaka ya Mungu hayawezi kuigwa na binadamu, na utambulisho na hadhi ya Mungu haiwezi kuigizwa na binadamu. Ingawaje unaweza kuiga sauti ambayo Mungu huongea nayo, huwezi kuiga hali halisi ya Mungu. Ingawaje unaweza kusimama mahali pa Mungu na kujifanya kuwa Mungu, hutawahi kuweza kufanya kile ambacho Mungu ananuia kukifanya, na hutawahi kutawala na kuamuru viumbe vyote. Katika macho ya Mungu, utabakia kuwa kiumbe kidogo, na haijalishi ni vipi ambavyo mbinu na uwezo wako ulivyo mkubwa, haijalishi ni vipaji vingapi unavyo, uzima wako wewe umetawaliwa na Muumba. Ingawaje unaweza kusema maneno fulani ya kijeuri, hilo haliwezi kuonyesha kuwa unayo hali halisi ya Muumba, wala kuwakilisha ya kwamba unamiliki mamlaka ya Muumba. Mamlaka na nguvu za Mungu ni hali halisi ya Mungu Mwenyewe. Hayakufunzwa wala kusomwa, au kuongezewa kutoka nje, lakini ni hali ya asili ya Mungu Mwenyewe. Na kwa hivyo uhusiano kati ya Muumba na viumbe hauwezi katu kubadilishwa. Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia.
Mamlaka ya Muumba Hayawekewi Mipaka ya Muda, Nafasi, au Jiografia, na Mamlaka ya Muumba Hayakadiriki
Hebu tutazame Mwanzo 22:17-18. Hili ni fungu jingine lililozungumziwa na Yehova Mungu, Alisema kwa Ibrahimu, “Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.”Yehova Mungu alimbariki Ibrahimu mara nyingi ili uzao wake uweze kuzidishwa—na kuzidishwa hadi kiwango gani? Hadi kiwango kilichozungumziwa katika Maandiko: “kama nyota za mbinguni na mchanga ulio pwani.” Hii ni kusema kwamba Mungu alipenda kumpa Ibrahimu uzao uliokuwa mwingi kama nyota za mbinguni, na tele kama mchanga wa pwani. Mungu aliongea akitumia taswira, na kutoka kwenye taswira hii si vigumu kuona kwamba Mungu asingempa tu Ibrahimu uzao elfu moja, mbili, au hata elfu nyingi, lakini idadi isiyohesabika, iliyotosha kuwa uzao wa mataifa mengi ya dunia, kwani Mungu alimwahidi Ibrahimu kuwa atakuwa baba wa mataifa mengi. Na je, idadi hiyo iliamuliwa na binadamu au iliamuliwa na Mungu? Je, binadamu anaweza kudhibiti uzao kiasi gani atakaokuwa nao? Je, inategemea yeye? Haitegemei binadamu kujua kama atakuwa na uzao mbalimbali au la, sikwambii uzao mwingi kama “nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani.” Ni nani asiyetamani uzao wake kuwa mwingi kama nyota? Kwa bahati mbaya mambo huwa hayaendi namna unavyotaka. Licha ya vile mwanadamu anaweza kuwa na mbinu au kuweza kufanya jambo fulani, haitegemei binadamu; hakuna anayeweza kusimama nje ya kile ambacho kimeamriwa na Mungu. Kiasi ambacho Atakuruhusu, hicho ndicho utakachokuwa nacho: Kama Mungu atakupa kidogo, basi hutawahi kuwa na kingi, na kama Mungu Atakupa kingi haina faida wewe kuchukia kingi hicho ulichonacho. Je, hayo si kweli? Haya yote yanategemea Mungu, si binadamu! Binadamu hutawaliwa na Mungu, na hakuna yule anayeachwa!
Wakati Mungu alisema “nitazidisha mithili,” hili lilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, sawa na agano la upinde wa mvua, lingeweza kutimizwa milele hadi milele, na pia ilikuwa ahadi iliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu. Mungu pekee ndiye anayefuzu na kuweza kufanya ahadi hii kutimia. Bila kujali kama binadamu anaisadiki au la, bila kujali kama binadamu aikubali au la, na bila kujali namna binadamu anavyoitazama, na namna anavyoichukulia, haya yote yataweza kutimizwa, hadi mwisho wa maelezo ya agano hili, kulingana na matamshi yaliyotamkwa na Mungu. Matamshi ya Mungu hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko katika mapenzi au dhana za binadamu, na hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mtu yeyote, kitu au kifaa. Viumbe vyote vitaweza kutoweka lakini matamshi ya Mungu yatabaki milele hadi milele. Kinyume cha mambo ni, siku ambapo viumbe vyote vitatoweka ndiyo siku ile ile ambayo matamshi ya Mungu yataweza kutimizwa kabisa, kwani Yeye ndiye Muumba, na Anamiliki mamlaka ya Muumba, na nguvu za Muumba, na Anadhibiti vitu na viumbe vyote na nguvu zote za maisha; na Anaweza kusababisha kitu kutoka kule kusikokuwa na kitu, au kitu kuwa kile kisichokuwepo, na Anadhibiti mabadiliko ya viumbe vyote vilivyo na uhai na vile vilivyokufa, na kwa hivyo kwake Mungu, hakuna kinachokuwa rahisi kuliko kuzidisha uzao wa mtu. Haya yote yanaonekana ya kufikiria tu akilini mwa binadamu, sawa na hadithi za uwongo, lakini kwa Mungu, kile Anachoamua kufanya, na kuahidi kufanya, si cha kufikiria tu akilini wala si hadithi za uwongo. Badala yake ni hoja ambayo Mungu tayari ameiona, na ambayo kwa kweli itaweza kutimizwa. Je, unashukuru kuyasikia haya? Je, hoja hizi zinathibitisha kwamba uzao wa Ibrahimu ulikuwa mwingi? Na ulikuwa mwingi kiasi kipi? Mwingi kiasi cha “nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani” kama ilivyosemwa na Mungu? Je, uliweza kuenea kotekote katika mataifa na maeneo, kwenye kila sehemu ya ulimwengu? Na ni nini kilichotimiza hoja hii? Iliweza kutimizwa kutokana na mamlaka ya matamshi ya Mungu? Kwa miaka kadhaa ifikayo mamia au elfu baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, matamshi ya Mungu yaliendelea kutimizwa, na bila kusita yakaendelea kuwa hoja; huu ndio uwezo wa matamshi ya Mungu, na ithibati ya mamlaka ya Mungu. Wakati Mungu alipoumba viumbe vyote hapo mwanzo, Mungu alisema na hebu kuwe na nuru, na kukawa na nuru. Tokeo hili lilifanyika haraka sana, lilitimizwa kwa muda mfupi sana, na hakukuwa na kuchelewa kokote kuhusu kukamilika na kutimizwa kwake; athari za matamshi ya Mungu zilitokea papo hapo. Vyote vilikuwa onyesho la mamlaka ya Mungu, lakini wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Aliruhusu binadamu kuuona upande mwingine wa mamlaka ya Mungu, na Akaruhusu binadamu kuona mamlaka ya Muumba yasiyokadirika, na zaidi, Akaruhusu binadamu kuona upande halisi, bora zaidi wa mamlaka ya Muumba.
Punde tu matamshi ya Mungu yanapotamkwa, mamlaka ya Mungu yanachukua usukani wa kazi hii, na hoja iliyoahidiwa kwa kinywa cha Mungu kwa utaratibu huanza kugeuka na kuwa uhalisi. Miongoni mwa viumbe vyote, mabadiliko huanza kufanyika katika kila kitu kutokana na hayo, sawa na vile, kwenye mwanzo wa msimu wa mchipuko, nyasi hugeuka kuwa kijani, maua huchanua, macho ya maua yanachanua kutoka mitini, ndege wanaanza kuimba, nao batabukini wanaanza kurejea, nayo mashamba yanaanza kujaa watu…. Wakati wa msimu wa machipuko unapowadia viumbe vyote hupata nguvu, na hiki ndicho kitendo cha miujiza cha Muumba. Wakati Mungu anapokamilisha ahadi zake, viumbe vyote mbinguni na ardhini vinapata nguvu mpya na kubadilika kulingana na fikira za Mungu—na hakuna kiumbe ambacho kinaachwa. Wakati kujitolea au kuahidi kunapotamkwa kutoka kwa Mungu, viumbe vyote vinatimiza wajibu wake, na vinashughulikiwa kwa minajili ya kutimizwa kwake, na viumbe vyote vinaundwa na kupangiliwa chini ya utawala wa Mungu, na vinaendeleza wajibu wao maalum, na kuhudumu kazi zao husika. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya Muumba. Unaona nini katika mambo haya? Unajuaje mamlaka ya Mungu? Kunao upana wa mamlaka ya Mungu? Kuna kipimo cha muda? Je, inaweza kusemekana kuwa na kimo fulani, au urefu fulani? Je, inaweza kusemekana kuwa na ukubwa au nguvu fulani? Je, inaweza kupimwa kwa vipimo vya binadamu? Mamlaka ya Mungu hayawakiwaki yakizima, hayaji yakienda, na hakuna mtu anayeweza kupima namna ambavyo mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, wakati Mungu anabariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutaruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za maisha zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Kila onyesho la mamlaka Yake ni onyesho timilifu la maneno kutoka kwenye kinywa Chake, na linaonyeshwa kwa vitu vyote, na kwa mwanadamu. Zaidi ya hayo, kila kitu kinachokamilishwa na mamlaka Yake ni bora zaidi ya kulinganishwa, na hakina dosari kamwe. Yaweza kusemekana kwamba fikira Zake, matamshi Yake, mamlaka Yake, na kazi zote Anazozikamilisha, zote ni picha nzuri isiyolinganishwa, na kwa viumbe, lugha ya binadamu haiwezi kuelezea umuhimu na thamani yake. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanakoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au hata ni vipi ambavyo mageuzi makubwa yamekuwa makubwa katika harakati zao za kuishi kwenye mazingira yao—haya yote yanajulikana kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Haijalishi ni muda upi umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kama vile ndio mwanzo yametamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutambua kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia—kwa mfano, muda, jiografia, kabila, na kadhalika—ahadi hii itakamilishwa, na kutambuliwa, na, zaidi, kukamilishwa kwake na kutambuliwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba upana wa mamlaka ya Mungu na nguvu vinatosha kudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote. Mungu aliumba nuru, lakini hiyo haimaanishi kuwa Mungu anasimamia tu nuru, kwamba Yeye anasimamia maji tu kwa sababu Aliyaumba maji, na kwamba kila kitu kingine hakina uhusiano na Mungu. Je, hii siyo suitafahamu? Ingawaje baraka za Mungu kwa Ibrahimu zilikuwa zimefifia polepole kutoka kwenye kumbukumbu ya binadamu baada ya miaka mia kadhaa, kwake Mungu, ahadi hii ilibaki vilevile. Ilikuwa kwenye mchakato wa kukamilishwa, na haikuwahi kusitishwa. Binadamu hakuwahi kujua au kusikia namna ambavyo Mungu alisisitiza mamlaka Yake, namna ambavyo vitu vyote vilivyoundwa na kupangiliwa, na ni hadithi ngapi za ajabu zilifanyika miongoni mwa vitu vyote vya uumbaji wa Mungu kwenye kipindi hiki cha muda, lakini kila kipande kizuri cha onyesho la mamlaka ya Mungu na ufunuo wa matendo Yake vilipitishwa na kutukuzwa miongoni mwa viumbe vyote, viumbe vyote vilijitokeza na kuongea kuhusu vitendo vya kimiujiza vya Muumba, na kila mojawapo ya hadithi iliyosimuliwa sana kuhusu ukuu wa Muumba juu ya viumbe vyote itaweza kutangazwa na viumbe vyote daima dawamu. Mamlaka ambayo Mungu anatawala viumbe vyote, na nguvu za Mungu, vinaonyesha viumbe vyote kwamba Mungu anapatikana kila pahali wakati wote. Wakati unashuhudia upekee wa mamlaka na nguvu za Mungu, utaona kwamba Mungu anapatikana kila mahali na nyakati zote. Mamlaka na nguvu za Mungu haviwekewi mipaka ya muda, jiografia, nafasi, au mtu yeyote, jambo au kitu. Upana wa mamlaka na nguvu za Mungu unazidi mawazo ya binadamu; haufikiriki kwa binadamu, hauwaziki kwa binadamu, na hautawahi kujulikana na binadamu.
Baadhi ya watu wanapenda kujijazia na kujifikiria, lakini, mawazo ya binadamu yanaweza kufikia wapi? Yanaweza kuzidi ulimwengu huu? Je, mwanadamu ana uwezo wa kujijazia na kufikiria uhalali na usahihi wa mamlaka ya Mungu? Je, kule kujijazia na kujifikiria kwa binadamu kunaweza kuruhusu yeye kufikia maarifa ya mamlaka ya Mungu? Vinaweza kufanya binadamu kushukuru kwa kweli na kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Mungu? Hoja zinathibitisha kwamba uingiliaji kati na kufikiria kwa binadamu ni zao tu la akili za binadamu, na hakutoi hata msaada kidogo au manufaa kidogo kwa maarifa ya binadamu kuhusu mamlaka ya Mungu. Baada ya kusoma makala ya kidhahania ya kisayansi, baadhi wanaweza kufikiria mwezi, na vile nyota zilivyo. Ilhali hii haimanishi kwamba binadamu anao ufahamu wowote wa mamlaka ya Mungu. Kufikiria kwa binadamu ni huku tu: kufikiria. Kuhusiana na hoja za mambo haya, hivi ni kusema kwamba, kwa kurejelea muunganiko wao kwa mamlaka ya Mungu, hana ung'amuzi wowote. Na je, ikiwa umeenda hadi mwezini? Je, hii inaonyesha kuwa unao ufahamu wa pande nyingi kuhusu mamlaka ya Mungu? Je, inaonyesha kwamba wewe unaweza kufikiria upana wa mamlaka na nguvu za Mungu? Kwa sababu huko kuingilia kati na kufikiria kwa mwanadamu hakuwezi kumruhusu kujua mamlaka ya Mungu, je, binadamu anafaa kufanya nini? Chaguo lenye hekima zaidi ni kutojijazia au kutojifikiria, ambapo ni kusema kwamba binadamu asiwahi kutegemea kufikiria na kutegemea uingiliaji kati inapohusu kujua mamlaka ya Mungu. Ni nini ambacho Ningependa kukwambia hapa? Maarifa ya mamlaka ya Mungu, nguvu za Mungu, utambulisho binafsi wa Mungu, na hali halisi ya Mungu haviwezi kutimizwa kwa kutegemea kufikiria kwako. Kwa vile huwezi kutegemea kufikiria ili kujua mamlaka ya Mungu, basi ni kwa njia gani unaweza kutimiza maarifa ya kweli ya mamlaka ya Mungu? Kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kupitia ushirika, na kupitia kwa uzoefu wa maneno ya Mungu, utaweza kuwa na hali halisi ya kujua kwa utaratibu na uthibitishaji wa mamlaka ya Mungu na hivyo basi utafaidi kuelewa kwa utaratibu na maarifa yaliyoongezeka. Hii ndiyo njia tu ya kutimiza maarifa ya mamlaka ya Mungu; hakuna njia za mkato. Kukuuliza kutofikiria si sawa na kukufanya uketi kimyakimya ukisubiri maangamizo, au kukusitisha dhidi ya kufanya kitu. Kutotumia akili zako kuwaza na kufikiria kunamaanisha kutotumia mantiki ya kujijazia, kutotumia maarifa kuchambua, kutotumia sayansi kama msingi, lakini badala yake kufurahia, kuhakikisha, na kuthibitisha kuwa Mungu unayemsadiki anayo mamlaka, kuthibitisha kwamba Yeye anashikilia ukuu juu ya hatima yako, na kwamba nguvu Zake nyakati zote zinathibitisha kuwa Yeye Mungu Mwenyewe ni wa kweli, kupitia kwa matamshi ya Mungu, kupitia ukweli, kupitia kwa kila kitu unachokabiliana nacho maishani. Hii ndiyo njia pekee ambayo mtu yeyote anaweza kutimiza ufahamu wa Mungu. Baadhi ya watu husema kwamba wangependa kupata njia rahisi ya kutimiza nia hii, lakini unaweza kufikiria kuhusu njia kama hiyo? Nakwambia, hakuna haja ya kufikiria: Hakuna njia nyingine! Njia ya pekee ni kujua kwa uangalifu na bila kusita na kuhakikisha kile Mungu anacho na alicho kupitia kwa kila neno Analolielezea na Analolifanya. Hii ndiyo njia pekee ya kujua Mungu. Kwani kile Mungu anacho na alicho, na kila kitu cha Mungu, si cha wazi na tupu—lakini cha kweli.
Hoja ya Udhibiti wa Muumba na Utawala Juu ya Vitu Vyote na Viumbe Vilivyo Hai Inazungumzia Uwepo wa Kweli wa Mamlaka ya Muumba
Vilevile, baraka za Yehova Mungu kwa Ayubu zimerekodiwa katika Kitabu cha Ayubu. Ni nini ambacho Mungu alimpa Ayubu? “Kwa hivyo Yehova akabariki mwisho wa baadaye wa Ayubu zaidi kuliko mwanzo wake: kwa sababu alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na elfu moja ya jozi za ng’ombe, na elfu moja ya punda wa kike” (Ayubu 42:12). Kutoka kwenye mtazamo wa binadamu, ni vitu gani alivyopewa Ayubu? Je, vilikuwa rasilimali ya binadamu? Akiwa na rasilimali hizi, je, Ayubu angeweza kuwa tajiri sana kwenye kipindi hicho? Na aliwezaje kumiliki rasilimali kama hizo? Ni nini kilisababisha utajiri wake? Bila shaka ilikuwa ni shukrani kwa baraka ya Mungu ambapo Ayubu alifanikiwa kumiliki. Namna ambavyo Ayubu alitazama rasilimali hizi, na vipi alivyochukulia baraka za Mungu, si jambo ambalo tutalizungumzia hapa. Tunapokuja katika baraka za Mungu watu wote hutamani, mchana na usiku, kubarikiwa na Mungu, ilhali binadamu hana udhibiti wowote kuhusiana na idadi ngapi ya rasilimali anaweza kufaidi katika maisha yake yote, au kama anaweza kupokea baraka kutoka kwa Mungu—na hii ni hoja isiyopingika! Mungu anayo mamlaka, na nguvu za kumpatia mwanadamu rasilimali yoyote, kumruhusu binadamu kupata tamko lolote la baraka, ilhali kuna kanuni ya baraka za Mungu. Ni aina gani ya watu ambao Mungu hubariki? Watu Anaowapenda, bila shaka! Ibrahimu na Ayubu walibarikiwa wote na Mungu, ilhali baraka walizopokea hazikuwa sawa. Mungu alibariki Ibrahimu kwa vizazi vingi kama mchanga na nyota. Wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Alisababisha vizazi vya mtu mmoja, taifa moja, kuwa na nguvu na ufanisi. Katika haya mamlaka ya Mungu yalitawala mwanadamu, ambaye alipumua pumzi za Mungu miongoni mwa viumbe vyote na viumbe vyenye uhai. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, huyu mwanadamu aliweza kupenyeza na kuwepo kwa kasi, na ndani ya upana, ulioamuliwa na Mungu. Haswa, uwezo wa taifa hili, kima cha upanuzi, na matarajio ya maisha vyote vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Mungu, na kanuni ya haya yote ilitokana kwa ujumla kwa ahadi ambazo Mungu alimpa Ibrahimu. Hivi ni kusema kwamba, licha ya hali zozote zile, ahadi za Mungu zingeendelea mbele bila kizuizi na kuweza kutambuliwa kulingana na uwepo wa mamlaka ya Mungu. Katika ahadi ambayo Mungu alimpa Ibrahimu, licha ya misukosuko ya ulimwengu, licha ya umri, licha ya majanga yanayovumiliwa na mwanadamu, vizazi vya Ibrahimu visingeweza kukabiliwa na hatari ya maangamizo, na taifa lao lisingefifia na kutokomea. Baraka ya Mungu kwa Ayubu, hata hivyo, ilimfanya kuwa tajiri wa kupindukia. Kile Mungu alichompa kilikuwa mseto wa viumbe hai, vinavyopumua, maelezo yake yalikuwa—idadi yao, kasi yao ya kuzaa, kima cha kuishi, kiwango cha mafuta kwenye viumbe hivyo, na kadhalika—vilidhibitiwa pia na Mungu. Ingawaje viumbe hivi hai havikumiliki uwezo wa kuongea, navyo pia vilikuwa sehemu ya mipangilio ya Muumba, na kanuni za mipangilio ya Mungu zilikuwa kulingana na baraka ambayo Mungu aliahidi Ayubu. Katika baraka ambazo Mungu alimpa Ibrahimu na Ayubu, ingawaje kile kilichokuwa kimeahidiwa kilikuwa tofauti, mamlaka ambayo Muumba alitumia kutawala viumbe vyote na viumbe vilivyo na uhai yalikuwa yale yale. Kila maelezo ya mamlaka na Nguvu za Mungu yameonyeshwa kwenye ahadi Zake tofauti na baraka zake kwa Ibrahimu na Ayubu, kwa mara nyingine zaonyesha binadamu kwamba mamlaka ya Mungu ni zaidi ya kufikiria kwa binadamu. Maelezo haya yanamwambia binadamu kwa mara nyingine kwamba kama angetaka kujua mamlaka ya Mungu, basi hii itawezekana tu kupitia kwa maneno ya Mungu na kuweza kupitia kazi ya Mungu.
Mamlaka ya Mungu ya ukuu juu ya viumbe vyote huruhusu binadamu kuweza kuona ukweli kwamba: Mamlaka ya Mungu hayapo tu katika matamshi “Mungu akasema, na Kuwepo na nuru, na kukawa na nuru, na, Kuwepo na anga, na kukawa na anga, na, Kuwepo na ardhi, na kukawa na ardhi,” lakini, vilevile namna Alivyofanya nuru ile kuendelea kuwepo, kulizuia anga dhidi ya kutoweka na Akaiweka ardhi milele ikiwa kando na maji, pamoja na maelezo ya namna Alivyotawala na kusimamia viumbe: nuru, anga, na ardhi. Nini kingine unachoona katika baraka za Mungu kwa mwanadamu? Ni wazi, kwamba baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, nyayo za Mungu hazikusita, kwani Alikuwa tu ameanza kuonyesha mamlaka Yake, na Alinuia kuhakikisha kwamba kila mojawapo ya matamshi Yake yangekuwa uhalisia, na kuhakikisha kuwa kila mojawapo ya maelezo ambayo Alizungumza yanatokea kuwa kweli, na kwa hivyo kwenye miaka iliyofuata, Aliendelea kufanya kila kitu Alichonuia. Kwa sababu Mungu anayo mamlaka, pengine inaonekana kwa binadamu kwamba Mungu huongea tu, na Hahitaji kuinua hata kidole chake ili mambo yote yaweze kutimizwa. Kufikiria hivyo, ni, lazima Niseme, mzaha! Kama utachukua mtazamo wa upande mmoja wa Mungu kuanzisha agano na binadamu kwa kutumia maneno, na ukamilishaji wa kila kitu na Mungu kwa kutumia maneno, na huwezi kuona ishara na hoja mbalimbali ambazo mamlaka ya Mungu yanatawala juu ya kila kitu, basi ufahamu wako kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni mdogo mno na wa mzaha! Kama binadamu anafikiria Mungu kuwa hivyo, basi, lazima isemwe, maarifa ya binadamu kuhusu Mungu yameendeshwa hadi kwenye shimo la mwisho, na sasa yamefika mwisho wenyewe, kwani Yule Mungu ambaye binadamu anafikiria kuhusu ni mashine tu ya kutoa amri, na si Mungu anayemiliki mamlaka. Je, umeona nini kupitia kwenye mifano ya Ibrahimu na Ayubu? Je, umeuona upande halisia wa mamlaka na nguvu za Mungu? Baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, Mungu hakubakia mahali Alipokuwa, wala Yeye kuwaweka wajumbe Wake kazini huku Akisubiri kuona matokeo yake yatakuwa yapi. Kinyume cha mambo ni kuwa, pindi Mungu alipotamka maneno Yake, akiongozwa na mamlaka ya Mungu, mambo yote yalianza kukubaliana na kazi ambayo Mungu alinuia kufanya, na kulikuwepo na watu waliokuwa wamejitayarisha, vitu, na vifaa ambavyo Mungu alihitaji. Hivi ni kusema kwamba, punde tu maneno hayo yalipotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, mamlaka ya Mungu yalianza kutumika kotekote kwenye ardhi nzima, na Akaweka wazi mkondo ili kuweza kukamilisha na kutimiza ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu na Ayubu, huku Akifanya pia mipango na matayarisho yote kuhusiana na kila kitu kilichohitajika kwa kila awamu Aliyopanga kutekeleza. Kwa wakati huu, hakuwashawishi tu wafanyakazi Wake, lakini pia na viumbe vyote vilivyokuwa vimeumbwa na Yeye. Hivyo ni kusema kwamba upana ambao mamlaka ya Mungu yalitiliwa maanani haukujumuisha tu wajumbe, lakini, vilevile, vitu vyote, vilivyoshawishiwa ili kutii ile kazi ambayo Alinuia kukamilisha; hizi ndizo zilizokuwa tabia mahususi ambazo mamlaka ya Mungu yalitumiwa. Katika kufikiria kwako, baadhi ya watu wanaweza kuwa na ufahamu ufuatao kuhusiana na mamlaka ya Mungu: Mungu anayo mamlaka, na Mungu anao uwezo, na hivyo basi Mungu anahitaji kubaki katika mbingu ya tatu, au Anahitajika tu kubakia mahali maalum, na hahitajiki kufanya kazi yoyote fulani, na uzima wa kazi ya Mungu unakamilishwa katika fikira Zake. Baadhi wanaweza kusadiki kuwa, ingawaje Mungu alibariki Ibrahimu, Mungu hakuhitajika kufanya kitu chochote, na ilitosha kwake Yeye kutamka tu matamshi Yake. Je, hivi ndivyo ilivyofanyika kweli? Bila shaka la! Ingawaje Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, mamlaka Yake ni ya kweli na halisia, si matupu. Uhalisi na ukweli wa mamlaka ya Mungu na nguvu hufichuliwa kwa utaratibu, kuwekwa ndani ya uumbaji Wake wa vitu vyote, na udhibiti wa vitu vyote, na katika mchakato ambao Anaongoza na kusimamia wanadamu. Kila mbinu, kila mtazamo na kila maelezo ya ukuu wa Mungu juu ya wanadamu na vitu vyote, na kazi yote ambayo Amekamilisha, vilevile ufahamu Wake kuhusu vitu vyovyote—vinathibitisha kwa kweli kwamba mamlaka na nguvu za Mungu si maneno matupu. Mamlaka na nguvu Zake vyote vinaonyeshwa na kufichuliwa kila mara, na katika mambo yote. Maonyesho haya na ufunuo vyote vinazungumzia uwepo wa kihalisia wa mamlaka ya Mungu, kwani Yeye ndiye anayetumia mamlaka na nguvu Zake kuendeleza kazi Yake, na kuamuru vitu vyote, na kutawala vitu vyote kila wakati, na nguvu na mamlaka Yake, vyote haviwezi kubadilishwa na malaika, au wajumbe wa Mungu. Mungu aliamua ni baraka gani Angempa Ibrahimu na Ayubu—uamuzi ulikuwa wa Mungu. Hata ingawaje wajumbe wa Mungu waliweza kumtembelea Ibrahimu na Ayubu wao binafsi, vitendo vyao vilikuwa kulingana na amri za Mungu, na kulingana na mamlaka ya Mungu, na pia walikuwa wakifuata ukuu wa Mungu. Ingawaje binadamu anawaona wajumbe wa Mungu wakimtembelea Ibrahimu, na hashuhudii Yehova Mungu binafsi akifanya chochote kwenye rekodi za Biblia, kwa hakika Yule Mmoja tu ambaye anatilia mkazo nguvu na mamlaka ni Mungu Mwenyewe, na hali hii haivumilii shaka yoyote kutoka kwa binadamu yeyote! Ingawaje umewaona malaika na wajumbe wakimiliki nguvu nyingi, na wametenda miujiza, au wamefanya baadhi ya mambo yaliyoagizwa na Mungu, vitendo vyao ni kwa minajili tu ya kukamilisha agizo la Mungu, na wala si tu kuonyesha mamlaka ya Mungu—kwani hakuna binadamu au kifaa kilicho na, au kinachomiliki, mamlaka ya Muumba ya kuumba vitu vyote na kutawala vitu vyote. Na kwa hivyo hakuna binadamu au kifaa chochote kinaweza kutumia au kuonyesha mamlaka ya Muumba.
Mamlaka ya Muumba Hayabadiliki na ni Yasiyokosewa
Ni nini umeona katika sehemu hizi tatu za maandiko? Je, umeona kuwa kuna kanuni ambayo Mungu hutumia mamlaka Yake? Kwa mfano, Mungu aliutumia upinde wa mvua kuanzisha agano na binadamu, ambapo Aliuweka upinde wa mvua katika mawingu ili kumwambia binadamu kuwa Yeye Hatawahi tena kutumia gharika kuangamiza ulimwengu. Je, upinde wa mvua tunaouona leo, bado ndio uleule uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu? Je, asili na maana yake vimebadilika? Bila shaka, havijabadilika. Mungu alitumia mamlaka Yake ili kutekeleza kitendo hiki, nalo agano Aliloanzisha na binadamu limeendelea hadi leo, na muda ambao agano hili litabadilishwa, bila shaka, ni uamuzi wa Mungu. Baada ya Mungu kutamka “Mimi nauweka upinde wangu wa mvua mawinguni,” siku zote Mungu alifuata agano hili, Alilifuata hadi leo. Unaona nini katika haya? Ingawaje Mungu anayamiliki mamlaka na nguvu, Anayo bidii sana na Anafuata kanuni katika vitendo Vyake, na Anashikilia maneno Yake. Bidii Yake na kanuni za vitendo Vyake, vinaonyesha namna Muumba asivyoweza kukosewa na namna ambavyo mamlaka ya Muumba yalivyo magumu kushindwa. Ingawaje Anamiliki mamlaka ya juu, na kila kitu kinatawaliwa na Yeye, na japokuwa Anazo nguvu za kutawala vitu vyote, Mungu hajawahi kuharibu mpango Wake au kutatiza mpangilio Wake mwenyewe, na kila wakati Anapotumia mamlaka Yake, ni kulingana na umakinifu unaohitajika kwenye kanuni Zake mwenyewe na hasa kwa kufuata kile kilichotamkwa kutoka kwenye kinywa Chake, na kufuata hatua na majukumu ya mpango Wake. Sina haja ya kusema kwamba kila kitu kinachotawaliwa na Mungu pia kinatii kanuni ambazo mamlaka ya Mungu yanatumika, na hakuna mwanadamu au kitu kisichojumuishwa kwenye mipangilio ya mamlaka Yake, wala hakuna anayeweza kubadilisha kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumika. Kwenye macho ya Mungu, wale wanaobarikiwa hupokea utajiri mzuri unaoletwa na mamlaka Yake, na wale wanaolaaniwa hupokea adhabu yao kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, hakuna binadamu au kitu ambacho hakijumuishwi, kwenye utumiaji wa mamlaka Yake, wala hakuna kinachoweza kubadilisha kanuni hizi ambazo mamlaka Yake yanatumiwa. Mamlaka ya Muumba hayabadilishwi kwa mabadiliko ya aina yoyote ile, na, vilevile, kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumiwa hazibadiliki kwa sababu yoyote ile. Mbingu na ardhi vyote vinaweza kupitia misukosuko mingi, lakini mamlaka ya Muumba hayatabadilika; vitu vyote vitatoweka, lakini mamlaka ya Muumba hayatawahi kutoweka. Hiki ndicho kiini cha mamlaka ya Muumba ambayo hayabadiliki na ni yasiyokosewa, na huu ndio upekee wenyewe wa Muumba!
Maneno yaliyo hapa chini ni lazima katika kujua mamlaka ya Mungu, na maana yake yametolewa kwenye ushirika ulio hapa chini. Hebu tuendelee kuyasoma Maandiko.
4. Amri ya Mungu kwa Shetani
Ayubu 2:6 Naye Yehova akasema kwa Shetani, Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.
Shetani Hajawahi Kuthubutu Kukiuka Mamlaka ya Muumba, na Kwa Sababu Hiyo, Vitu Vyote Vinaishi kwa Mpangilio
Hili ni dondoo kutoka katika Kitabu cha Ayubu, na “yeye” katika maneno haya inaashiria Ayubu. Ingawaje imeandikwa kwa muhtasari, sentensi hii inaelezea masuala mengi. Inafafanua mabadilishano fulani kati ya Mungu na Shetani kwenye ulimwengu wa kiroho, na inatwambia kuwa kiini cha maneno ya Mungu kilikuwa Shetani. Pia inarekodi kile kilichozungumziwa mahususi na Mungu. Maneno ya Mungu yalikuwa amri na shurutisho kwa Shetani. Maelezo mahususi ya shurutisho hili ni kuhusiana na kuyaokoa maisha ya Ayubu na pale ambapo Mungu aliweka masharti namna ambavyo Shetani alifaa kumshughulikia Ayubu—Shetani alilazimika kuyaokoa maisha ya Ayubu. Kitu cha kwanza tunachojifunza kutoka kwenye sentensi hii ni kwamba matamshi haya yalitamkwa na Mungu kwa Shetani. Kulingana na maandishi ya asili ya Kitabu cha Ayubu, yanatwambia usuli wa matamshi kama hayo: Shetani alipenda kumshutumu Ayubu, na hivyo lazima angepokea huo mkataba wa Mungu kabla hajamtia majaribuni. Wakati alipokubali ombi la Shetani kumjaribu Ayubu, Mungu aliweza kumtajia Shetani sharti lifuatalo: “Tazama, yeye yuko katika mkono wako; lakini uuhifadhi uhai wake.”Ni nini asili ya maneno haya? Ni wazi kwamba ni amri, ni shurutisho. Baada ya kuelewa asili ya maneno haya, unafaa, bila shaka, pia kung’amua kwamba Aliyetoa shurutisho hili ni Mungu, na kwamba aliyepokea amri hii, na akaitii, ni Shetani. Sina haja ya kusema kwamba katika shurutisho hili, uhusiano kati ya Mungu na Shetani uko wazi kwa yeyote ambaye anasoma maneno haya. Bila shaka, huu ndio uhusiano kati ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, na tofauti kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani, iliyoelezwa kwenye rekodi za mabadilishano ya mazungumzo ya Mungu na Shetani katika Maandiko, na, hadi leo, ni mfano mahususi na rekodi ya maandishi ambapo binadamu anaweza kujifunza tofauti kuu kati ya utambulisho na hadhi ya Mungu na Shetani. Wakati huu, lazima Niseme kwamba, rekodi ya maneno haya ni waraka muhimu sana katika ufahamu wa binadamu juu ya hadhi na utambulisho wa Mungu, na inatoa taarifa muhimu kwa maarifa ya mwanadamu kuhusu Mungu. Kupitia mabadilishano haya ya Mungu na Shetani katika ulimwengu wa kiroho, binadamu anaweza kuelewa dhana moja mahususi katika mamlaka ya Muumba. Maneno haya ni ushuhuda mwingine wa kuonyesha mamlaka ya kipekee ya Muumba.
Kwa nje, ni mabadilishano kati ya Yehova Mungu na Shetani. Hali yao halisi ni kwamba, mtazamo ambao Yehova Mungu anaongea, na nafasi ambayo Anazungumzia, ni ya juu zaidi kuliko ya Shetani. Hivyo ni kusema kwamba Yehova Mungu anamwamuru Shetani na sauti ya kushurutisha, na Anamwambia Shetani ni nini anafaa afanye na kile hafai kufanya, kwamba tayari Ayubu yu mikononi mwake, na yuko huru kumfanya Ayubu vyovyote atakavyo—lakini asiyachukue maisha ya Ayubu. Ujumbe hapa ni, ingawaje Ayubu alikuwa amewekwa kwenye mikono ya Shetani, maisha yake hayakuchukuliwa na Shetani; hakuna anayeweza kuchukua maisha ya Ayubu kutoka mikononi mwa Mungu isipokuwa Mungu amruhusu. Mtazamo wa Mungu unafafanuliwa waziwazi katika amri hii kwa Shetani, na amri hii pia inajionyesha na kufichua msimamo ambao Yehova Mungu anazungumza na Shetani. Katika haya, Yehova Mungu hashikilii tu hadhi ya Mungu aliyeumba nuru, na hewa, na vitu vyote na viumbe hai, au ya Mungu anayeshikilia ukuu juu ya vitu vyote na viumbe hai, lakini pia ya Mungu ambaye anaamuru mwanadamu, na kuamuru Jahanamu, Mungu ambaye anadhibiti maisha na kifo cha viumbe vyote hai. Katika ulimwengu wa kiroho, ni nani mbali na Mungu ambaye angethubutu kutoa shurutisho kama hilo kwa Shetani? Na ni kwa nini Mungu binafsi Alitoa shurutisho Lake kwa Shetani? Kwa sababu maisha ya binadamu, pamoja na yale ya Ayubu, yanadhibitiwa na Mungu. Mungu hakumruhusu Shetani kujeruhi au kuchukua maisha ya Ayubu, hivyo ni kusema kwamba kabla ya Mungu kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, Mungu bado alikumbuka kutoa shurutisho maalum kama hilo, na kwa mara nyingine Akamwamuru Shetani asiyachukue maisha ya Ayubu. Shetani hajawahi kuthubutu kukiuka mamlaka ya Mungu, na, vilevile, amesikiliza kwa umakinifu siku zote na kutii shurutisho na amri mahususi za Mungu, asiwahi thubutu kuzivunja, na, bila shaka asithubutu kubadilisha kwa hiari shurutisho zozote za Mungu. Hiyo ndiyo mipaka ambayo Mungu amemwekea wazi Shetani, na hivyo Shetani hajawahi thubutu kuvuka mipaka hiyo. Huu si uwezo wa mamlaka ya Mungu? Je, huu si ushuhuda wa mamlaka ya Mungu? Wa namna ya kuwa mbele ya Mungu, na namna ya kumtazama Mungu, Shetani anao ung'amuzi bora zaidi kuliko mwanadamu, hivyo, katika ulimwengu wa kiroho, Shetani anaona hadhi na mamlaka ya Mungu vizuri sana, na anatambua sana ule uwezo wa mamlaka ya Mungu na kanuni zinazotilia mkazo kwenye mamlaka Yeye. Hathubutu, kamwe, kutozitilia maanani kanuni hizo, wala hathubutu kukiuka kanuni hizo kwa vyovyote vile, au kufanya chochote ambacho kinakiuka mamlaka ya Mungu, na hathubutu kukabiliana na hasira ya Mungu kwa njia yoyote. Ingawaje ni mwovu na mwenye kiburi kiasili, Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka na viwango alivyowekewa na Mungu. Kwa miaka milioni, ametii kwa umakinifu mipaka hii, ametii kila amri na shurutisho lililotolewa na Mungu na hajawahi kuthubutu kukanyaga juu ya alama. Ingawaje ni mwenye kijicho, Shetani ni “mwerevu” zaidi kuliko mwanadamu aliyepotoka; anajua utambulisho wa Muumba, na anajua mipaka yake. Kutokana na vitendo vya Shetani vya kunyenyekea tunaweza kuona kwamba mamlaka na nguvu za Mungu ni maelekezo ya mbinguni ambayo hayawezi kukiukwa na Shetani, na kwamba yanatokana na upekee na mamlaka ya Mungu ndiposa viumbe vyote vinabadilika na kuzalisha katika njia ya mpangilio, kwamba mwanadamu anaweza kuishi na kuongezeka kupitia ndani ya mkondo ulioanzishwa na Mungu, huku hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuuharibu mpango huu, na hakuna mtu au kifaa kinachoweza kubadilisha sheria hii—kwani vyote vinatoka kwenye mikono ya Muumba na kwenye mpangilio na mamlaka ya Muumba.
Mungu Pekee, Ambaye Anao Utambulisho wa Muumba, Anamiliki Mamlaka ya Kipekee
Ule utambulisho wa pekee wa Shetani umesababisha watu wengi kuonyesha shauku thabiti kwenye maonyesho yake ya dhana mbalimbali. Kunao hata watu wengi wajinga wanaosadiki kwamba, kama vile Mungu, Shetani anamiliki mamlaka, kwani shetani anaweza kuonyesha miujiza, na anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kufanya. Kwa hivyo, mbali na kumwabudu Mungu, mwanadamu pia anahifadhi nafasi kwenye moyo wake, na hata humwabudu Shetani kama Mungu. Watu hawa wote ni wa kusikitikiwa na kuchukiwa. Ni wa kusikitikiwa kwa sababu ya kutojua kwao, na wa kuchukiwa kwa sababu ya hali yao ya uasi wa kidini na hali halisi ya maovu ya ndani kwa ndani. Wakati huu Nahisi kwamba ni muhimu niwafahamishe kuhusu maana ya mamlaka, yanaashiria nini, na yanawakilisha nini. Kwa mazungumzo ya jumla, Mungu Mwenyewe ni mamlaka, mamlaka Yake yaanashiria mamlaka ya juu na hali halisi ya Mungu, na mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanawakilisha hadhi na utambulisho wa Mungu. Kwa hiyo, je, Shetani huthubutu kusema kwamba yeye ni Mungu? Je, Shetani huthubutu kusema kwamba aliumba viumbe vyote, na anashikilia ukuu juu ya viumbe vyote? Bila shaka la! Kwani hawezi kuumba viumbe vyote; mpaka leo, hajawahi kuumba chochote kilichoumbwa na Mungu, na hajawahi kuumba chochote kilicho na maisha. Kwa sababu hana mamlaka ya Mungu, hatawahi endapo itawezekana kumiliki hadhi na utambulisho wa Mungu, na hili linaamuliwa na hali yake halisi. Je, anazo nguvu sawa na Mungu? Bila shaka hana! Tunaita nini vitendo vya Shetani, na miujiza inayoonyeshwa na Shetani? Je, ni nguvu? Vitendo hivi vinaweza kuitwa mamlaka? Bila shaka la! Shetani huelekeza wimbi la maovu, na misukosuko, uharibifu, na kuchachawiza kila dhana ya kazi ya Mungu. Kwa miaka elfu kadhaa iliyopita, mbali na kupotosha na kunyanyasa mwanadamu, na kumjaribu na kumdanganya binadamu hadi kufikia kiwango cha uovu, na ukataaji wa Mungu, ili binadamu aweze kutembea kwenye bonde la kivuli cha mauti, je, Shetani amefanya chochote ambacho kinastahili hata kumbukumbu ndogo zaidi, pongezi au sherehe ndogo zaidi kutoka kwa binadamu? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, binadamu angepotoshwa naye? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angepata madhara kutokana nayo? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angemwacha Mungu na kugeukia mauti? Kwa sababu Shetani hana mamlaka au nguvu, ni nini ambacho tunafaa kuhitimisha kuhusu hali halisi ya kila kitu anachofanya? Kunao wale wanaofafanua kila kitu ambacho Shetani hufanya kama ujanja mtupu, ilhali Nasadiki kwamba ufafanuzi kama huo haufai sana. Je, Matendo maovu ya kupotosha mwanadamu ni ujanja mtupu tu? Nguvu za maovu ambazo Shetani alimnyanyasia Ayubu, na tamanio lake kali la kumnyanyasa na kumpotosha, lisingewezekana kutimizwa kupitia kwa ujanja mtupu tu. Tukiangalia nyuma, tunaona kwamba, mara moja, kondoo na ng’ombe wa Ayubu walitawanyishwa kila pahali kotekote kwenye milima na vilima, walikuwa hawapo tena; kwa muda mfupi tu, utajiri mwingi wa Ayubu ukatoweka. Je, yawezekana kwamba haya yote yalitimizwa kupitia kwa ujanja mtupu tu? Asili ya yale yote ambayo Shetani hufanya yanalingana na kuingiliana na istilahi mbaya kama vile kudhoofisha, kukatiza, kuharibu, kudhuru, maovu, hali ya kuwa na kijicho, na giza, na kwa hivyo matukio haya yote ambayo si ya haki na ni maovu yanahusiana na kuunganika kwenye vitendo vya Shetani, na hayawezi kutenganishwa na ile hali halisi ya uovu wa Shetani. Haijalishi ni vipi ambavyo Shetani “alivyo na nguvu”, haijalishi ni vipi Shetani alivyo mwenye kuthubutu na haijalishi ni vipi uwezo wake ulivyo mwingi katika kusababisha madhara, haijalishi ni vipi anavyotumia mbinu zenye mseto-mpana ambazo zinapotosha na kudanganya binadamu, haijalishi ni vipi alivyo mwerevu kupitia kwenye ujanja na njama zake ambazo anadhalilisha binadamu, haijalishi ni vipi anavyoweza kujibadilisha katika mfumo ule aliomo, hajawahi kuweza kuumba kiumbe chochote kimoja, hajawahi kuweza kuweka wazi sheria au kanuni za uwepo wa viumbe vyote, na hajawahi kutawala na kudhibiti kifaa chochote, kiwe ni chenye uhai au kisichokuwa na uhai. Kotekote kwenye upana mkubwa wa ulimwengu, hakuna hata mtu au kifaa kimoja kilichotokana na Shetani, au kilichopo kwa sababu ya Shetani; hakuna hata mtu au kifaa kimoja ambacho kimetawaliwa na Shetani, au kudhibitiwa na Shetani. Kinyume cha mambo ni kwamba, hana budi kuishi katika utawala wa Mungu lakini, vilevile, lazima atii shurutisho na amri zote za Mungu. Bila ruhusa ya Mungu, ni vigumu sana kwa Shetani kugusa hata tone la maji au chembechembe ya mchanga kwenye ardhi; bila ruhusa ya Mungu, Shetani hana hata hiari ya kusongea mchwa wanaojiendea zao kwenye ardhi—sikwambii hata mwanadamu, aliyeumbwa na Mungu. Kwenye macho ya Mungu, Shetani ni duni zaidi ya yungiyungi kwenye mlima, hadi kwenye ndege wanaopaa hewani, hadi kwenye samaki walio baharini, hadi kwenye funza kwenye juu ya nchi. Wajibu wake miongoni mwa viumbe vyote ni kuhudumia viumbe vyote, na kufanyia kazi mwanadamu, na kuhudumia kazi ya Mungu na mpango Wake wa usimamizi. Licha ya vile anavyoonea wenzake kijicho katika asili yake, na vile ambavyo hali yake halisi ya maovu ilivyo, kitu ambacho Shetani anaweza kufanya tu ni kuweza kukubaliana kwa wajibu kuhusiana na kazi yake: kuwa mwenye huduma kwa Mungu, na kuwa mjalizo kwa Mungu. Hiki ndicho kiini na nafasi ya Shetani. Hali yake halisi haijaungana na maisha, haijaungana na nguvu, haijaungana na mamlaka; ni kitu cha kuchezea tu kwenye mikono ya Mungu, mtambo tu kwenye huduma ya Mungu!
Baada ya kuelewa uso wa kweli wa Shetani, watu wengi bado wangali hawajaelewa ni nini maana ya mamlaka, hivyo basi wacha Mimi nikuelezee! Mamlaka yenyewe yanaweza kufafanuliwa kama nguvu za Mungu. Kwanza, inaweza kusemekana kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni vizuri. Havina uunganisho wowote na kitu chochote kibaya, na havina uhusiano wowote na viumbe vyovyote vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Nguvu za Mungu zinaweza kuumba viumbe vya mfumo wowote ulio na uzima na nguvu, na haya yote yanaamuliwa na uzima wa Mungu. Mungu ni uzima, kwa hivyo Yeye ndiye chanzo cha viumbe hai vyote. Vilevile, mamlaka ya Mungu yanaweza kufanya viumbe vyote kutii kila neno la Mungu, yaani kuumbika kulingana na matamshi yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na kuishi na kuzaana kwa amri ya Mungu, ambapo baadaye Mungu anatawala na kuamuru viumbe vyote hai, na hakutakuwa na kupotoka kokote, daima dawamu. Hakuna mtu au kifaa kilicho na mambo haya; Muumba tu ndiye anayemiliki na aliye na nguvu kama hizo, na hivyo basi yanaitwa mamlaka. Huu ndio upekee wa Muumba. Kwa hivyo, haijalishi kama ni neno lenyewe “mamlaka” au hali halisi ya mamlaka haya, kila mojawapo linaweza tu kuhusishwa na Muumba kwa sababu ni ishara ya utambulisho na hali halisi ya kipekee ya Muumba; na inawakilisha utambulisho na hadhi ya Muumba, mbali na Muumba, hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuhusishwa na neno “mamlaka” Huu ni ufasiri wa mamlaka ya kipekee ya Muumba.
Ingawaje Shetani alimwaangalia Ayubu kwa macho ya kutamani mali yake, bila ya ruhusa ya Mungu hakuthubutu kugusa hata unywele mmoja wa mwili wa Ayubu. Ingawaje ni mwenye uovu na unyama wa ndani, baada ya Mungu kutoa shurutisho Lake kwake, Shetani hakuwa na chaguo lakini kutii shurutisho la Mungu. Na kwa hivyo, hata ingawaje Shetani alionekana kana kwamba ameshikwa na kichaa sawa na mbwamwitu miongoni mwa kondoo alipomjia Ayubu, hakuthubutu kusahau mipaka aliyowekewa wazi na Mungu, hakuthubutu kukiuka shurutisho za Mungu, na kwa hayo yote, Shetani hakuthubutu kutoka kwenye kanuni ya maneno ya Mungu—je, hii si kweli? Kutokana na mtazamo huu wa maisha, tunaona kwamba Shetani hathubutu kuvunja matamshi yoyote yale ya Yehova Mungu. Kwake Shetani, kila neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu ni shurutisho, na sheria ya kimbinguni, na maonyesho ya mamlaka ya Mungu—kwani nyuma ya kila neno la Mungu kunadokezwa adhabu ya Mungu kwa wale wanaokiuka maagizo ya Mungu, na wale wasiotii na wanaopinga sheria za kimbinguni. Shetani anajua wazi kwamba kama atakiuka shurutisho za Mungu, basi lazima akubali athari za kukiuka mamlaka ya Mungu na kupinga sheria za kimbinguni. Na sasa athari hizi ni zipi? Sina haja ya kusema kwamba, athari hizi bila shaka, ni adhabu kutoka kwa Mungu. Vitendo vya Shetani kwake Ayubu vilikuwa tu mfano mdogo wa yeye kumpotosha binadamu, na wakati ambapo Shetani alipokuwa akitekeleza vitendo hivi, ile mipaka ambayo Mungu Aliweka na amri Alizotoa kwake Shetani vilikuwa tu mfano mdogo wa kanuni zinazotokana na kila kitu anachofanya. Aidha, wajibu na nafasi ya Shetani katika suala hili ulikuwa tu mfano mdogo wa wajibu na nafasi yake katika kazi ya usimamizi wa Mungu, na utiifu kamili wa shetani kwa Mungu wakati alipomjaribu Ayubu, ulikuwa tu mfano mdogo wa namna ambavyo Shetani hakuthubutu kuweka hata upinzani mdogo kwa Mungu katika kazi ya usimamizi wa Mungu. Ni onyo gani ambalo mifano hii midogo inakupa? Miongoni mwa mambo yote, akiwemo Shetani, hakuna mtu au kitu kinachoweza kukiuka sheria na kanuni za mbinguni zilizowekwa wazi na Muumba, na hakuna mtu au kitu kinachothubutu kukiuka sheria na kanuni hizi za mbinguni, kwani hakuna mtu au kifaa kinaweza kubadilisha au kuepuka adhabu ambayo Mungu anawawekea wale wanaokosa kumtii. Ni Muumba tu anayeweza kuanzisha sheria na kanuni za kimbinguni, ni Muumba tu aliye na nguvu za kuanza kuzitekeleza na nguvu za Muumba ndizo haziwezi kukiukwa na mtu au kitu chochote. Haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba, mamlaka haya yako juu zaidi miongoni mwa mambo yote, na kwa hivyo haiwezekani kusema kwamba “Mungu ndiye mkubwa zaidi naye Shetani ni nambari mbili.” Isipokuwa Muumba anayemiliki mamlaka ya kipekee, hakuna Mungu mwengine.
Je, sasa unayo maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu? Kwanza, kunayo tofauti kati ya mamlaka ya Mungu yaliyotajwa hivi punde na nguvu za binadamu? Na tofauti ni nini? Baadhi ya wanadamu husema kwamba hakuna ulinganifu wowote kati ya haya mawili. Hayo ni kweli! Ingawaje watu husema kwamba hakuna ulinganisho kati ya haya mawili, kwenye fikira na dhana za binadamu, nguvu za binadamu mara nyingi zinadhaniwa kuwa mamlaka, huku haya mawili yakilinganishwa mara nyingi sako kwa bako. Ni nini kinachoendelea hapa? Je, watu hawafanyi kosa kubadilisha bila ya kuwa waangalifu kitu kimoja na kingine? Vitu hivi viwili havina uhusiano wowote na hakuna ulinganisho wowote kati yavyo, ilhali watu bado hawawezi kuelewa. Je, haya yatatuliwe vipi? Kama ungependa kwa kweli kupata suluhu, njia ya pekee ni kuelewa na kujua mamlaka ya kipekee ya Mungu. Baada ya kuelewa na kujua mamlaka ya Muumba, hutataja kwa mkupuo mmoja nguvu za binadamu na mamlaka ya Mungu.
Nguvu za binadamu zinarejelea nini? Kwa ufupi, ni uwezo au mbinu inayowezesha tabia potoshi, matamanio na malengo ya binadamu kuweza kupanuliwa au kutimizwa hadi kiwango cha juu zaidi. Je, haya yatumike kumaanisha mamlaka? Haijalishi ni vipi ambavyo malengo na matamanio ya binadamu yalivyo makubwa au yenye faida, mtu huyu hawezi kusemekana amemiliki mamlaka; kama amezidi sana, haya majivuno na ufanisi ni maonyesho tu ya upumbavu wa Shetani miongoni mwa binadamu, kama imezidi sana, ni upuzi ambao shetani anaendeleza kama babu yake mwenyewe ili kutimiza maono yake ya kuwa Mungu.
Unatazama vipi haswa mamlaka ya Mungu sasa? Kwa vile sasa maneno haya yamezungumziwa kwenye ushirika, unafaa kuwa na maarifa mapya kuhusu mamlaka ya Mungu. Na kwa hivyo Nakuuliza: Mamlaka ya Mungu yanaashiria nini? Je, yanaashiria ule utambulisho wa Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria nguvu za Mungu Mwenyewe? Je, yanaashiria hadhi ya kipekee ya Mungu Mwenyewe? Miongoni mwa mambo yote, ni katika kitu gani umeona mamlaka ya Mungu? Uliyaona vipi? Kwa mujibu wa ile misimu minne inayopitiwa na binadamu, je, mtu yeyote anaweza kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya machipuko, kiangazi, mapukutiko na kipupwe? Wakati wa machipuko, miti huweza kuchomoza na kuchanua; katika kiangazi, inafunikwa na majani; katika mapukutiko inazaa matunda na katika kipupwe majani yanaanguka. Je, yupo anayeweza kubadilisha sheria hii? Je, hii inaonyesha dhana moja ya mamlaka ya Mungu? Mungu alisema“Iwe Nuru,”na ikawa nuru. Je, nuru hii ingali ipo? Nuru hii inakuwepo kwa ajili ya nini? Inakuwepo kwa sababu ya maneno ya Mungu, bila shaka, na kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Je, hewa iliyoumbwa na Mungu bado ipo? Je, hewa ambayo binadamu anapumua inatoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kuchukua vitu vinavyotoka kwa Mungu? Je, kuna yeyote anayeweza kubadilisha hali yao halisi na kazi? Kuna yeyote anayeweza kutibua mpangilio wa usiku na mchana kama ulivyopangwa na Mungu, na sheria ya usiku na mchana kama ilivyoamrishwa na Mungu? Je, shetani anaweza kufanya kitu kama hicho? Hata kama hulali wakati wa usiku, na unachukulia usiku kuwa wakati wa mchana, basi bado ni wakati wa usiku; unaweza kubadilisha mazoea yako ya kila siku, lakini huwezi kubadilisha sheria ya mabadilishano kati ya usiku na mchana—na ukweli huu hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote, au sio? Kuna yeyote anayeweza kumfanya simba kulima ardhi kama afanyavyo ng'ombe? Je, yupo yeyote anayeweza kubadilisha ndovu kuwa punda? Je, yupo anayeweza kubadilisha kuku akapaa hewani kama tai? Je, yupo anayeweza kumfanya mbwamwitu kula nyasi kama kondoo? Je, yupo anayeweza kumfanya samaki aliye majini kuishi kwenye ardhi kavu? Na kwa nini hamna? Kwa sababu Mungu aliwaamuru kuishi ndani ya maji, na kwa hivyo wanaishi ndani ya maji. Kwenye ardhi kavu hawataweza kuishi kwani watakufa; hawawezi kukiuka vipimo vya amri ya Mungu. Vitu vyote vina sheria na kipimo cha kuwepo kwao, na kila mojawapo kina silika zake binafsi. Haya yameamriwa na Muumba, na hayawezi kubadilishwa na kupitishwa na binadamu yeyote. Kwa mfano, simba siku zote ataishi jangwani, umbali fulani kutoka kwenye jumuia ya binadamu, na hatawahi kuwa mtulivu na mwaminifu kama vile ngo'mbe alivyo na anavyoishi na kumfanyia binadamu kazi. Ingawaje ndovu na punda ni wanyama, na wote wana miguu minne, na ni viumbe vinavyopumua hewa, ni aina tofauti, kwani waligawanywa kwenye aina tofauti na Mungu, kila mmoja wao anazo silika zake binafsi, na hivyo hawatawahi kubadilishana. Ingawaje kuku ana miguu miwili, na mbawa kama vile alivyo tai, hatawahi kuweza kupaa hewani; kama amejaribu sana anaweza tu kupaa hadi kwenye mti—na hili linaamuliwa na silika yake. Sina haja kusema, haya yote ni kwa sababu ya amri za mamlaka ya Mungu.
Katika maendeleo ya mwanadamu leo, sayansi ya mwanadamu inaweza kusemekana kwamba inanawiri, na mafanikio ya uchunguzi wa kisayansi wa binadamu unaweza kufafanuliwa kama wa kuvutia. Uwezo wa kibinadamu, lazima isemwe, unazidi kukua mkubwa zaidi, lakini kunao ushindi mmoja wa kisayansi ambao mwanadamu hajaweza kufanya: Mwanadamu ameunda ndege, vibebaji vya ndege, na hata bomu la atomiki, mwanadamu ameenda angani, ametembea mwezini, amevumbua Intaneti, na ameishi maisha ya kiwango cha juu ya teknolojia, ilhali mwanadamu hawezi kuumba kiumbe hai kinachopumua. Silika za kila kiumbe kilicho hai na sheria ambazo zinatawala kuishi kwake na mzunguko wa maisha na kifo wa kila kiumbe kilicho hai—vyote hivi haviwezekani na havidhibitiki na sayansi ya mwanadamu. Wakati huu, lazima isemekane kwamba haijalishi ni viwango gani vya juu zaidi vitakavyofikiwa na sayansi ya binadamu, haviwezi kulinganishwa na fikira zozote za Muumba na haiwezekani kutambua miujiza ya uumbaji wa Muumba na uwezo wa mamlaka Yake. Kunazo bahari nyingi sana juu ya nchi, ilhali hazijawahi kukiuka mipaka yao na kuja kwenye ardhi kwa nguvu, na hiyo ni kwa sababu Mungu aliwekea mipaka kila mojawapo ya bahari hizo; zilikaa popote pale Aliziamuru kukaa; na bila ya ruhusa ya Mungu haziwezi kusongasonga ovyo. Bila ya ruhusa ya Mungu, haziwezi kuingiliana, na zinaweza kusonga tu pale ambapo Mungu anasema hivyo, na pale ambapo zinaenda na kubakia ni suala na uamuzi wa mamlaka ya Mungu.
Ili kuweka wazi zaidi, “mamlaka ya Mungu” yanamaanisha kwamba ni wajibu wa Mungu. Mungu anayo haki ya kuamua namna ya kufanya kitu na kinafanywa kwa vyovyote vile Anavyopenda. Sheria ya vitu vyote ni wajibu wa Mungu, na wala si wajibu wa binadamu; na wala haiwezi kubadilishwa na binadamu. Haiwezi kusongeshwa kwa mapenzi ya binadamu, lakini inaweza badala yake kubadilishwa kwa fikira za Mungu, na hekima ya Mungu, na amri za Mungu, na hii ni kweli ambayo haiwezi kukataliwa na binadamu yeyote. Mbingu na nchi na viumbe vyote, ulimwengu, mbingu yenye nyota, misimu minne ya mwaka, ile inayoonekana na isiyoonekana kwa binadamu—yote haya yapo, yanafanya kazi, na kubadilika, bila ya kosa hata dogo, chini ya mamlaka ya Mungu, kulingana na shurutisho za Mungu, kulingana na amri za Mungu, na kulingana na sheria za mwanzo wa uumbaji. Si hata mtu mmoja au kifaa kimoja kinaweza kubadilisha sheria zao, au kubadilisha mkondo wa asili ambao sheria hizi zinafanya kazi; zilianza kutumika kwa sababu ya mamlaka ya Mungu, na zitaangamia kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ya Mungu. Sasa kwa sababu haya yote yamesemwa, je, unahisi kwamba mamlaka ya Mungu ni ishara ya utambulisho na ishara ya Mungu? Je, mamlaka ya Mungu yanaweza kumilikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au ambacho hakijaumbwa? Yanaweza kuigwa, kughushiwa, au kubadilishwa na mtu yeyote, na kitu chochote, au kifaa chochote.
Utambulisho wa Muumba ni wa Kipekee, na Hufai Kufuata lile Wazo la Imani ya Kuabudu Miungu Wengi
Ingawaje mbinu na uwezo wa Shetani ni kubwa zaidi kuliko zile za binadamu, ingawaje anaweza kufanya mambo ambayo hayawezi kufanywa na binadamu, bila kujali kama waonea wivu au unatamani kile ambacho Shetani anafanya, bila kujali kama unachukia au unachukizwa na kile anachofanya, bila kujali kama unaweza au huwezi kuona hicho, bila kujali ni kiwango kipi ambacho Shetani anaweza kutimiza au ni watu wangapi anaweza kudanganya ili wakamwabudu na kumtolea kafara, na bila kujali ni vipi unavyomfafanua, haiwezekani wewe kusema kwamba Shetani anayo mamlaka na nguvu za Mungu. Unafaa kujua kwamba Mungu ni Mungu, tunaye Mungu mmoja tu, na zaidi ya yote unafaa kujua kwamba ni Mungu tu aliye na mamlaka, na kwamba Anazo nguvu za kudhibiti na kutawala viumbe vyote. Eti kwa sababu Shetani anao uwezo wa kudanganya watu, na anaweza kujifanya kuwa Mungu, na anaweza kuiga ishara na miujiza inayofanywa na Mungu, amefanya mambo sawa na yale ya Mungu, wewe unasadiki kimakosa kwamba Mungu si wa kipekee, kwamba tunayo miungu mingi, kwamba tofauti yao ni kule kuwa tu na mbinu nyingi au chache zaidi, na kwamba kunazo tofauti katika upana na nguvu zinazoonyeshwa. Unapima ukubwa wao katika mpangilio wa kuwasili kwao, na kulingana na umri wao, na unasadiki kwa njia isiyofaa kwamba kunayo miungu mingine mbali na Mungu, na unafikiri kwamba nguvu na mamlaka ya Mungu si ya kipekee. Kama unazo fikira kama hizo, kama hutambui upekee wa Mungu, husadiki ni Mungu pekee anayemiliki mamlaka na kama utatii tu imani ya kuabudu miungu wengi, basi Nasema kwamba wewe ni duni kabisa kuliko viumbe vyote, wewe ni mfano halisi na wa kweli wa Shetani, na wewe ni mtu kamili wa maovu! Je, unaelewa kile Ninachojaribu kufunza kwa kusema maneno haya? Haijalishi ni muda gani, mahali au maelezo ya ziada kuhusu wewe, haifai kuchanganya Mungu na mtu yeyote mwengine, kitu au kifaa. Haijalishi unavyohisi kwamba mamlaka ya Mungu na hali halisi ya Mungu Mwenyewe havijulikani wala kuweza kufikiwa, haijalishi ni kiwango kipi cha matendo na maneno ya Shetani yanavyokubaliana na utambuzi na kufikiria kwako, haijalishi ni vipi ambavyo mambo haya yanakutosheleza wewe, usiwe mjinga, usichanganye dhana hizi, usikatae uwepo wa Mungu, usikatae utambulisho na hadhi ya Mungu, usimsukume Mungu nje ya mlango na kumleta Shetani kuchukua nafasi ya “Mungu” aliye ndani ya moyo wako na kuwa Mungu wako. Sina shaka kwamba una uwezo wa kufikiria athari za kufanya hivyo!
Ingawaje Binadamu Amepotoka, Angali Anaishi Chini ya Ukuu wa Mamlaka ya Muumba
Shetani amekuwa akipotosha mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Ameleta kiwango kisichosemezeka cha maovu, amedanganya vizazi baada ya vizazi, na ametenda uhalifu wa kuchukiza ulimwenguni. Amedhulumu binadamu, amedanganya binadamu, ameshawishi binadamu ili ampinge Mungu, na ametenda vitendo vya maovu ambavyo vimetatiza na kuharibu mpango wa Mungu mara kwa mara. Ilhali, chini ya mamlaka ya Mungu, viumbe vyote na viumbe vyenye uhai vinaendelea kutii kanuni na sheria zilizowekwa wazi na Mungu. Yakilinganishwa na mamlaka ya Mungu, asili ovu ya Shetani na kuenea kwake ni vitu vibaya mno, vinakera mno na ni vya kuleta aibu na ni vidogo mno na vinyonge. Hata ingawaje Shetani anatembea miongoni mwa viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, hawezi kutekeleza mabadiliko madogo zaidi kwa watu, vitu, na vifaa vilivyoamriwa na Mungu. Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia viumbe vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku zingali zinabadilishana nafasi zao bila kusita; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nao batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao; wadudu aina ya nyenje kwenye mchanga wanaimba kwelikweli kwenye siku za kiangazi; nyenje kwenye nyasi wanaimba kwa sauti ya polepole huku wakikaribisha msimu wa mapukutiko, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia pweke; fahari za simba wakijitosheleza wenyewe kwa kuwinda; nao kunguni wa kaskazini wa ulaya hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni yanafanyika kwa muda wa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kusalia. Wanaishi katika ruzuku na kustawishwa na Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi. Ingawaje mwanadamu, anayeishi miongoni mwa viumbe vyote amepotoka na kudanganywa na shetani, angali hawezi kupuuza maji yaliyoumbwa na Mungu, hewa iliyoumbwa na Mungu, na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na binadamu angali bado anaishi na kuzaana kwenye anga hii iliyoumbwa na Mungu. Silika za mwanadamu zingali hazijabadilika. Binadamu angali anategemea macho yake kuona, masikio yake kusikia, ubongo wake kufikiria, moyo wake kuelewa, miguu na viganja vyake kutembea, mikono yake kufanya kazi, na kadhalika; silika zote ambazo Mungu alimpa binadamu ili aweze kukubali toleo la Mungu limebakia hivyo bila kubadilishwa, welekevu ambao binadamu alitumia kushirikiana na Mungu bado haujabadilika, welekevu wa mwanadamu wa kutenda wajibu wa kiumbe kilichoumbwa haujabadilishwa, mahitaji ya kiroho ya mwanadamu hayajabadilika, tamanio la mwanadamu kuweza kujua asili zake halijabadilika, hamu ya mwanadamu kuweza kuokolewa na Muumba haijabadilika. Hizi ndizo hali za sasa za mwanadamu, anayeishi katika mamlaka ya Mungu, na ambaye amevumilia maangamizo mabaya yaliyoletwa na Shetani. Ingawaje mwanadamu amepitia unyanyasaji wa Shetani, na yeye si Adamu na Hawa tena kutoka mwanzo wa uumbaji, badala yake amejaa mambo ambayo yana uadui na Mungu kama vile maarifa, fikira na kadhalika, na amejaa tabia ya kishetani iliyopotoka, kwenye macho ya Mungu, mwanadamu yungali bado mwanadamu yule yule Aliyemuumba. Mwanadamu angali anatawaliwa na kupangiwa na Mungu, na angali anaishi ndani ya mkondo uliowekwa wazi na Mungu, na kwa hivyo kwenye macho ya Mungu, mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani amefunikwa tu na uchafu na tumbo linalonguruma, na miitikio ambayo ni ya kujikokota kidogo, kumbukumbu ambayo si nzuri kama ilivyokuwa, na mwenye umri ulioongezeka kidogo—lakini kazi na silika zote za binadamu bado hazijapata madhara kamwe. Huyu ndiye mwanadamu ambaye Mungu ananuia kuokoa. Mwanadamu huyu anahitaji tu kusikia mwito wa Muumba na kusikia sauti ya Muumba, naye atasimama wima na kukimbia kutafuta ni wapi sauti imetokea. Mwanadamu huyu lazima tu aweze kuona umbo la Muumba naye hatakuwa msikivu wa kila kitu kingine, ataacha kila kitu, ili kuweza kujitolea mwenyewe kwa Mungu, na hata atayatenga maisha yake kwa ajili Yake. Wakati moyo wa mwanadamu unapoelewa maneno hayo ya moyoni kutoka kwa Muumba, mwanadamu atakataa Shetani na atakuja upande wake Muumba; wakati mwanadamu atakuwa ametakasa kabisa uchafu kutoka kwenye mwili wake, na amepokea kwa mara nyingine toleo na ukuzaji kutoka kwa Muumba, basi kumbukumbu la mwanadamu litarejeshwa, na kwa wakati huu mwanadamu atakuwa amerejea kwa kweli katika utawala wa Muumba.
Desemba 14, 2013
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili
Kuhusu Sisi: Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni