10/31/2017

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Kunayo siri kubwa moyoni mwako. Huwezi kuijua hapo kwa sabubu umekuwa ukiishi katika ulimwengu usio na mwanga unaoangaza. Moyo wako na roho yako vimechukuliwa mateka na yule mwovu. Macho yako yamefunikwa na giza; huwezi kuliona jua likiangaza angani, wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yatiririkayo kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako na kila kitu ambacho Mwenye Uweza alikupatia. Umeingia katika bahari ya uchungu isiyokuwa na mwisho, pasipo uwezo wa kukuokoa, hukuna tumaini la kuishi, umeachwa ukipambana na kuzunguka zunguka. … Tokea wakati huo, umekuwa hatarini kuteswa na yule mwovu, uko mbali na baraka za Mwenye Uweza, mbali na kukimu kwa Mwenye Uweza, na unaenenda katika njia ambayo huwezi kurudi tena. Kuitwa mara milioni hakutaweza kuamsha moyo wako na roho yako. Umelala fofofo mikononi mwa yule mwovu, aliyekulaghai na kukuingiza katika ulimwengu usio na kikomo, pasipo mwelekeo, wala alama za kukuongoza katika njia. Tokea hapo umepoteza utakaso wako wa kwanza, hali yako ya kutokuwa na hatia, na kuanza kuukimbia uso wa Mwenye Uweza. Yule mwovu anauendesha moyo wako katika kila jambo na anakuwa maisha yako. Humwogopi tena, wala humwepuki tena, humshuku tena. Badala yake, unamchukulia kama Mungu wa moyo wako. Unaanza kumtunza, na kumuabudu, mnaambatana pamoja kama kivuli chake, mmejipa kwa kila mmoja katika maisha na mauti. Hujui lolote kabisa kuhusu asili yako, kwa nini upo, au kwa nini unakufa. Unamtazama Mwenye Uweza kama asiyejulikana; hujui mwanzo Wake, achilia mbali yale yote Aliyokutendea. Kila kitu kutoka Kwake kimekuwa chukizo kwako. Huyatunzi wala kujua thamani yake. Unatembea na yule mwovu, tokea siku ile ulipoanza kupokea chakula kutoka kwa Mwenye Uweza. Wewe na yule mwovu mmepita katika maelefu ya miaka ya dhoruba na tufani. Wewe pamoja naye, mnampinga Mungu, ambaye alikuwa chanzo cha maisha yenu. Hutubu, wala kujua kwamba umefikia hatua ya maangamizi. Unasahau kwamba yule mwovu amekujaribu, amekutesa; unasahau asili yako. Vivyo hivyo, yule mwovu amekuwa akikuharibu hatua baada ya hatua, hata mpaka sasa. Moyo wako na roho yako vimekufa ganzi na vimeoza. Hulalamiki tena juu ya dhiki ya dunia, huamini tena kwamba dunia si ya haki. Wala hujali tena juu ya uwepo wa Mwenye Uweza. Hii ni kwa sababu umemchukulia mwovu kuwa baba yako wa kweli, na huwezi kutengana naye. Hii ndiyo siri iliyomo moyoni mwako.
Alfajiri inapofika, nyota ya asubuhi huonekana mashariki. Ni nyota ambayo haijawahi kuwepo hapo awali. Inaliangaza anga lililo bado na nyota na kuwasha nuru iliyozimwa katika mioyo ya watu. Watu hawako wapweke tena, kwa sababu ya nuru hii, nuru inayokuangazia wewe na watu wengine. Lakini wewe bado umelala fofofo gizani. Huwezi kuisika sauti, wala kuiona nuru, umeshindwa kutambua ujio wa mbingu mpya na nchi mpya, enzi mpya. Kwa sababu baba yako anakuambia, “Mwanangu, usiamke, bado ni mapema. Nje kuna baridi, kaa ndani, usije ukachomwa macho yako kwa mkuki na upanga.” Unaamini katika ushawishi wa baba yako pekee, maana unaamini kwamba baba yako yupo sahihi kwa sababu baba ana umri mkubwa kuliko wewe, na kwamba baba anakupenda sana. Ushawishi na upendo wa namna hiyo vinakufanya usiamini hadithi kwamba kuna nuru ulimwenguni, na hujali tena kama ulimwenguni kuna ukweli. Wala huthubutu kutumainia ukombozi kutoka kwa Mwenye Uweza. Umeridhika kuwa katika hali hiyo, hutumainii tena ujio wa nuru, na wala hutazamii tena kuja kwa Mwenye Uweza anayesifika. Machoni mwako, yote yaliyo mazuri hayawezi kufufuliwa, wala kuendelea kukuwepo. Machoni huoni kesho wala majaliwa ya mwanadamu. Unalikwamilia vazi la baba yako, uko tayari kuteseka pamoja naye, ukiogopa kumpoteza msafiri mwenzako na mwelekeo wa safari yenu ndefu. Ulimwengu huu mkubwa na wenye giza umewafanya wengi wenu, kuwa majasiri na watu wa kujitahidi sana katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya ulimwengu huu. Umewafanya “mashujaa” wengi ambao hawaogopi kifo kabisa. Zaidi ya hayo, umetengeneza makundi ya watu waliokufa ganzi na wanadamu waliopooza ambao hawaelewi makusudi ya kuumbwa kwao. Macho ya Mwenye Uweza humwangazia mwanadamu aliyepo katika mateso makali, anasikia vilio vya wanaoteseka, anaona kutokuwa na aibu kwa wale wanaoteseka, na anahisi hali ya mwanadamu ya kukosa msaada na shida za mwanadamu aliyepoteza wokovu. Mwanadamu anakataa utunzaji Wake, na wanakwenda katika njia zao wenyewe, na wanakwepa macho Yake yanayowatazama. Wanaona ni afadhali waonje uchungu wa kilindi cha bahari, pamoja na adui. Kutanafusi kwa Mwenye Uweza hakiwezi kusikika tena. Mikono ya Mwenye Uweza haiko tayari kumgusa tena mwanadamu huyu wa kuhuzunisha. Anarudia kazi Yake, akirejesha na kupoteza, mara tena na tena. Tokea wakati huo, Yeye anachoka, na kujihisi mchovu, na hivyo Anasitisha kazi Anayoifanya, na Anaacha kuzunguka zunguka kwa watu. ... Watu hawajui kabisa kama kuna mabadiliko haya, hawaelewi kuja na kuondoka huku, huzuni na kukatishwa tamaa kwa Mwenye Uweza.
Yote yaliyopo hapa duniani yanabadilika upesi kwa mawazo ya Mwenye Uweza, kwa macho Yake. Mambo ambayo mwanadamu hajawahi kuyasikia yanaweza kuja kwa ghafla. Na bado, vitu vyote ambavyo mwanadamu amekuwa akivimiliki, vitapotea pasipo yeye kujua. Hakuna anayeweza kutambua mahali alipo Mwenye Uweza, na zaidi, hakuna anayeweza kuhisi uwepo na ukuu wa nguvu za uzima za Mwenye Uweza. Kuzidi Kwake uwezo wa binadamu kuko ndani ya jinsi Anavyoweza kuelewa yale ambayo wanadamu hawezi. Ukuu wake upo katika jinsi ni Yeye anayekataliwa na mwanadamu na bado Anamwookoa mwanadamu. Yeye anajua maana ya uzima na mauti. Aidha, Anajua kanuni za maisha kwa ajili ya mwanadamu, ambaye Alimuumba Yeye. Yeye ndiye msingi wa uwepo wa mwanadamu na Ndiye Mkombozi wa mwanadamu katika ufufuo. Yeye huishusha mioyo yenye furaha kwa kuipatia huzuni na kuiinua mioyo yenye huzuni kwa kuipatia furaha. Hii yote ni kwa ajili ya kazi Yake, na mpango Wake.
Mwanadamu, ambaye aliacha kupokea uzima wake kutoka kwa Mwenye Uweza, hajui ni kwa nini anaishi, na bado anaogopa kifo. Hukuna usaidizi, wala msaada, lakini mwanadamu bado anasita kufumba macho yake, akiyakabili yote bila woga, kuishi katika maisha yasiyokuwa na maana katika ulimwengu ndani ya miili isiyokuwa na utambuzi wa roho. Unaishi hivyo, pasipo tumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na malengo. Kuna Mmoja tu aliye Mtakatifu katika hadithi hii ambaye atakuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa kuumia na wanasubiri kwa shauku kubwa kuja Kwake. Imani hii haiwezi kutambulika kufikia sasa kwa watu ambao hawana utambuzi. Hata hivyo, watu watu bado wanaitaka sana. Mwenye Uweza ana rehema kwa watu hawa wanaoteseka sana. Wakati huo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na utambuzi, maana lazima Asubiri sana jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kuchunguza, kuuchunguza moyo na roho yako. Anataka kukuletea chakula na maji na kukuamsha, ili usipate kiu na kupata njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuona huzuni katika ulimwengu huu, usifadhaike, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yupo pembeni mwako Anakuangalia, anakusubiri uweze kumrudia. Anasubiri siku ambayo kumbukumbu zako zitarejea: kuwa na utambuzi wa ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, kwa namna fulani na mahala fulani umepotea, umeanguka barabarani ukiwa hujitambui, halafu pasipo kujua unakuwa na “baba.” Halafu tena unatambua kuwa Mwenye Uweza amekuwa akiangalia, akisubiri kurejea kwako muda huu wote. Anangoja kwa uchungu, akisubiri mwitikio pasipo jibu. Kusubiri kwake hakuna gharama na ni kwa ajili ya moyo na roho ya wanadamu. Pengine kusubiri huku hakuna mwisho, na pengine kusubiri huku kumefikia mwisho wake. Lakini unapaswa kujua kabisa moyo wako na roho yako viko wapi sasa.
Mei 28, 2003

kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni