Je, Umekuwa Hai Tena?
Mwenyezi Mungu alisema: Baada ya kutimiza kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, na umefanywa mkamilifu, ingawa utakuwa huwezi kunena unabii, wala siri zozote, utakuwa unaishi kulingana na kufichua taswira ya mwanadamu. Mungu alimuumba mwanadamu, baada ya hapo mwanadamu akaharibiwa na Shetani, na uharibifu huu umewafanya watu wawe maiti—na hivyo, baada ya kuwa umebadilika, utakuwa tofauti na maiti hizi. Ni maneno ya Mungu ndiyo yanatoa uzima kwa roho za watu na kuwasababisha kuzaliwa upya, na roho za watu zinapozaliwa upya, watakuwa hai tena.
Neno "wafu" linarejelea maiti ambazo hazina roho, kwa watu ambao roho zao zimekufa. Roho za watu zinapowekewa uhai, wanakuwa hai tena. Watakatifu waliozungumziwa awali huashiria watu ambao wamekuwa hai, wale ambao walikuwa chini ya ushawishi wa Shetani lakini wakamshinda Shetani. Wateule wa China wamestahimili ukatili na mateso na ulaghai wa joka kuu jekundu, ambalo limewaacha wakiwa wameharibika kiakili na kuwachwa wakiwa hawana hata ujasiri wa kuishi. Hivyo, kuamsha roho zao kunapaswa kuanza na hulka zao. Kidogo kidogo, katika hulka yao roho yao itaamshwa. Siku moja, watakapokuwa hai tena, hakutakuwa na vizuizi zaidi, na vyote vitasonga mbele bila tatizo. Kwa sasa, hii inabakia kuwa bado haijafanikiwa. Kuishi kwa kudhihirisha kwa watu wengi kunajumuisha mazingira ya kifo, wamezungukwa na hali ya kifo, na wamepungukiwa sana. Maneno ya baadhi ya watu yanabeba kifo, matendo yao yanabeba kifo, na takribani kila kitu wanachoishi kwa kudhihirisha ni kifo. Ikiwa leo, watu wanamshuhudia Mungu waziwazi, basi kazi hii itashindwa, maana bado hawajakuwa hai tena kikamilifu, na kuna wafu wengi sana miongoni mwenu. Leo, baadhi ya watu wanauliza kwa nini Mungu haonyeshi ishara na maajabu ili kwamba aweze kusambaza kazi Yake miongoni mwa nchi za Wamataifa. Wafu hawawezi kuwa na ushuhuda wa Mungu; walio hai wanaweza, lakini watu wengi leo ni wafu, wengi wao wanaishi katika kifungo cha kifo, wanaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hawawezi kupata ushindi—na hivyo wanawezaje kuchukua ushuhuda wa Mungu? Wanawezaje kueneza kazi ya injili?
Wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, ni wale ambao wanaishi katikati ya kifo, ni wale ambao wametawaliwa na Shetani. Bila kuokolewa na Mungu, na kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, watu wanakuwa hawana uwezo kukwepa athari ya kifo, hawawezi kuwa hai. Wafu hawa hawawezi kuwa ushuhuda kwa Mungu, wala hawawezi kutumiwa na Mungu, wala kuingia katika ufalme. Mungu anahitaji ushuhuda wa walio hai, na sio wafu, na Anaomba kwamba walio hai wafanye kazi kwa ajili Yake, na sio wafu. "Wafu" ni wale ambao wanampinga na kumwasi Mungu, ni wale ambao ni mbumbumbu katika roho na hawaelewi maneno ya Mungu, ni wale ambao hawaweki ukweli katika matendo na hawana utii hata kidogo kwa Mungu, na ni wale wamemilikiwa na Shetani na kunyanyaswa na Shetani. Wafu wanajionyesha wenyewe kwa kusimama kwa kuupinga ukweli, kwa kumwasi Mungu, na kwa kuwa duni, wa kudharaulika, kuwa waovu, katili, wadanganyifu, na kudhuru kwa siri. Ingawa watu wa namna hiyo wanakula na kunywa maneno ya Mungu, hawana uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu; wanaishi, lakini ni wafu wanaotembea, ni maiti zinazopumua. Wafu hawawezi kabisa kumridhisha Mungu, wala kumtii kikamilifu. Wanaweza tu kumdanganya, kusema maneno ya makufuru juu Yake, na kumsaliti, na yote wanayoyaishi kwa kudhihirisha hufichua asili ya Shetani. Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Baada ya hapo ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi. Mwanadamu wa asili aliyeumbwa na Mungu alikuwa hai, lakini kwa sababu ya uharibifu wa Shetani maisha ya mwanadamu yapo katikati ya kifo, na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo watu hawa wamekuwa wafu ambao hawana roho, wamekuwa ni maadui ambao wanampinga Mungu, wamekuwa nyenzo ya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu wote walio hai ambao wameumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda wake, na Amempoteza mwanadamu, ambaye Alimuumba na ndiye kiumbe pekee aliye na pumzi Yake. Ikiwa Mungu ataamua kurejesha ushuhuda Wake, na kuwarejesha wale ambao waliumbwa kwa mkono wake lakini ambao wamechukuliwa mateka na Shetani, basi ni lazima awafufue ili waweze kuwa viumbe hai, na ni lazima awaongoe ili kwamba waweze kuishi katika nuru Yake. Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake. Mungu anawaokoa wale ambao wanaweza kuwa hai tena, ambao wanaweza kuuona wokovu wa Mungu, ambao wanaweza kuwa watii kwa Mungu, na wapo tayari kumtafuta Mungu. Anawaokoa wale ambao wanamwamini Mungu aliyepata mwili, na wanaamini katika kuonekana Kwake. Baadhi ya watu wanaweza kuwa hai tena, na baadhi hawawezi; inategemea na asili yao kama inaweza kuokolewa au la. Watu wengi wamesikia sana kuhusu maneno ya Mungu lakini bado hawaelewi mapenzi ya Mungu, wameyasikia maneno mengi sana ya Mungu lakini bado hawawezi kuyaweka katika vitendo, hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ukweli wowote na pia kwa kukusudia kabisa wanaingilia kazi ya Mungu. Hawawezi kufanya kazi yoyote kwa ajili ya Mungu, hawawezi kujitolea chochote Kwake, na pia wanatumia kwa siri pesa za kanisa, na kula katika nyumba ya Mungu bure. Watu hawa ni wafu, na hawataokolewa. Mungu anawaokoa wale ambao wapo katika kazi Yake. Lakini kuna sehemu ya watu hao ambao hawawezi kupokea wokovu Wake; ni idadi ndogo tu ndiyo inaweza kupokea wokovu Wake, maana watu wengi ni wafu sana, ni wafu sana kiasi kwamba hawawezi kuokolewa, wameharibiwa kabisa na Shetani, na kwa asili, wamekuwa hatari sana. Wala idadi ndogo hiyo ya watu haikuweza kumtii Mungu kikamilifu. Hawakuwa wale ambao walikuwa waaminifu kabisa kwa Mungu tangu mwanzo, au wale ambao walikuwa na upendo wa hali ya juu kabisa kwa Mungu toka mwanzo; badala yake, wamekuwa watiifu kwa Mungu kwa sababu ya kazi Yake ya ushindi, wanamwona Mungu kwa sababu ya upendo wake mkuu, kuna mabadiliko katika tabia zao kwa sababu ya tabia ya Mungu ya haki, na wanamjua Mungu kwa sababu ya kazi Yake, ambayo ni halisi na ya kawaida. Bila kazi hii ya Mungu, haijalishi watu hawa ni wazuri kiasi gani bado wangebaki kuwa wa Shetani, bado wangekuwa ni wa kifo, bado wangekuwa wafu. Kwamba, leo, watu hawa wanaweza kupokea wokovu wa Mungu ni kwa sababu kabisa wanaweza kushirikiana na Mungu.
Kwa sababu ya utiifu wao kwa Mungu, walio hai wanaweza kuchukuliwa na Mungu na kuishi katika ahadi Zake, na kwa sababu ya upinzani wao kwa Mungu, wafu watachukiwa zaidi na kukataliwa na Mungu na kuishi katikati ya adhabu na laana Zake. Hiyo ndiyo tabia ya haki ya Mungu, na haiwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Kwa sababu ya utafutaji wao wenyewe, watu wanapokea kibali cha Mungu na kuishi katika nuru; kwa sababu ya hila zao za kutisha, watu wanalaaniwa na Mungu, na kushuka chini katika adhabu; kwa sababu ya matendo yao maovu, watu wanaadhibiwa na Mungu; na kwa sababu ya kutamani kwao sana na utii wao, watu wanapokea baraka za Mungu. Mungu ni mwenye haki: Anawabariki walio hai, na kuwalaani waovu, ili kwamba siku zote wanakuwa katikati ya kifo, na kamwe hawataishi katika nuru ya Mungu. Mungu atawachukua walio hai kwenda katika ufalme Wake, Atawachukua walio hai kwenda katika baraka Zake milele. Wafu Atawaangusha katika kifo cha milele; wao ni wahusika wa uharibifu Wake, na siku zote watakuwa kwa Shetani. Mungu hamtendei mtu yeyote bila haki. Wale wote ambao kweli wanamtafuta Mungu hakika watabaki katika nyumba ya Mungu, na wale wote ambao hawamtii Mungu, na wale ambao hawana ulinganifu Naye hakika wataishi katika adhabu Yake. Pengine huna uhakika kuhusu kazi ya Mungu katika mwili—lakini siku moja mwili wa Mungu hautapangilia hatima ya mwanadamu moja kwa moja; badala yake, Roho Wake, atapanga mwisho wa mwanadamu, na wakati huo watu watajua kwamba mwili wa Mungu na Roho Wake ni kitu kimoja, kwamba mwili Wake hauwezi kufanya kosa, na hata Roho Wake hawezi kabisa kufanya kosa. Na hatimaye, hakika atawachukua wale ambao watakuwa hai tena na kuwapeleka katika ufalme Wake, hakuna zaidi, wala pungufu, na wale wafu ambao hawakutoka wakiwa hai watatupwa katika shimo la Shetani.
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni