12/31/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (5)

Mwenyezi Mungu alisema, Ilikuwa kwamba hakuna aliyejua Roho Mtakatifu, na hasa hawakujua njia ya Roho Mtakatifu ilikuwa gani. Ndio maana watu kila mara walifanya upumbavu mbele ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba karibu watu wote wanaoamini katika Mungu hawamjui Roho, lakini tu wana aina ya imani iliyochanganyikiwa.

12/30/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (4) 

Mwenyezi Mungu alisema, Kwamba watu wanaweza kugundua kupendeza kwa Mungu, kutafuta njia ya kumpenda Mungu katika enzi hii, na kwamba wako radhi kukubali mafunzo ya ufalme wa leo—hii yote ni neema ya Mungu na hata zaidi, ni Yeye ndiye anawainua wanadamu.

12/29/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (3)

Mwenyezi Mungu alisema, Katika maisha Yangu, Niko radhi kila mara kujitolea Mwenyewe kwa Mungu kabisa, mwili na fikra. Kwa njia hii, hakuna lawama kwa dhamiri Yangu na Naweza kupata kiasi kidogo cha amani. Mtu anayeandama uzima ni lazima kwanza aukabidhi moyo wake wote kwa Mungu kabisa. Hili ni sharti la mwanzo. Ningependa ndugu na dada Zangu wamwombe Mungu pamoja

12/28/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (2) 

Mwenyezi Mungu alisema, Labda ndugu na dada zetu wana muhtasari kidogo wa utaratibu, hatua, na mbinu za kazi ya Mungu katika China bara, lakini Mimi huhisi kila mara kwamba ni heri kuwa na kumbukumbu au muhtasari kidogo wa ndugu na dada zetu. Ninatumia tu nafasi hii kusema machache ya kile kilicho moyoni Mwangu; Sizungumzi juu ya chochote nje ya kazi hii.

12/27/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (1)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (1)


Mwenyezi Mungu alisema, Katika maisha yake, hakuna mtu anayejua ni aina gani ya vipingamizi ataenda kukutana navyo, wala hajui ni aina gani ya kusafishwa ambayo atapata mara kwa mara. Kwa wengine ni katika kazi yao, kwa wengine ni katika matazamio yao ya siku za baadaye, kwa wengine ni katika familia yao ya asili, na kwa wengine ni katika ndoa yao.

12/26/2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)



Mwenyezi Mungu alisema, Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu.

12/25/2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)

Kwa kipindi hiki chote, tumezungumza juu ya mambo mengi yanayohusiana na kumjua Mungu na hivi karibuni tulizungumza kuhusu kitu fulani muhimu sana juu ya mada hii: Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote. Wakati uliopita tulizungumza juu ya vipengele vichache vya mazingira kwa ajili ya kuendelea kuishi ambayo Mungu aliyatengeneza kwa ajili ya binadamu, vilevile Mungu kuandaa kila aina ya riziki ya lazima kwa ajili ya watu katika maisha yao.

12/24/2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII


Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)

Mwenyezi Mungu alisema, Tuendelee na mada ya mawasiliano ya wakati uliopita. Je, mnaweza kukumbuka ni mada gani tuliwasiliana wakati uliopita? (Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote.) Je, “Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote” ni mada mnayohisi ikiwa mbali sana nanyi? Mtu fulani anaweza kuniambia wazo kuu la mada hii tuliyowasiliana wakati uliopita?

12/23/2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu


















Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII


Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu


Mnapomaliza maombi yenu, je, mioyo yenu inahisi utulivu katika uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Ikiwa moyo wa mtu unaweza kutulizwa, ataweza kusikia na kuelewa neno la Mungu na ataweza kusikia na kuuelewa ukweli. Ikiwa moyo wako hauwezi kutulizwa, ikiwa moyo wako siku zote unayoyoma, au siku zote unafikiria juu ya mambo mengine, utaathiri kuja kwako pamoja kusikia neno la Mungu.

12/22/2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI


Utakatifu wa Mungu (III)

Mwenyezi Mungu alisema, Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu.

12/21/2017

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V


Utakatifu wa Mungu (II)

Habari za jioni kila mtu! (Habari ya jioni Mwenyezi Mungu!) Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu “Upendo Safi Bila dosari.”)
Kiitikio: “Upendo” unarejelea hisia safi bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, hakuna mpango, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna chaguo na hakuna chochote kichafu.

12/20/2017

Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Maono ya Kazi ya Mungu (2)


Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote. Leo, hakuna mtu anayezungumza maneno haya, na vitu kama vile vimepitwa na wakati. Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. 

12/19/2017

Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote


Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Uyahudi. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyotoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Wanaisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Wanaisraeli pekee.

12/18/2017

Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi?


Watu wamemwamini Mungu kwa muda mrefu, ilhali wengi wao hawaelewi maana ya neno “Mungu”. Wanafuata tu bila kufahamu vema. Hawajui sababu ya ni kwa nini binadamu anafaa kumwamini Mungu ama Mungu ni nini hasa. Iwapo watu wanajua tu kumfuata na kuamini Mungu, na hawajui Mungu ni nini, wala hawamwelewi Mungu, si huo ni mzaha mkuu ulimwenguni?

12/17/2017

Maneno kwa Vijana na Wazee|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Maneno kwa Vijana na Wazee|Mwenyezi Mungu


Nimetekeleza kazi nyingi sana duniani na Nimetembea kati ya wanadamu kwa miaka mingi sana. Ilhali watu kwa nadra sana huwa na ufahamu wa sura Yangu na tabia Yangu, na watu wachache wanaweza kuelezea kikamilifu kazi Ninayofanya. Watu wanakosa mengi sana, daima wanakosa ufahamu wa kile Ninachokifanya, na mioyo yao daima iko tayari kana kwamba wanaogopa sana Nitawaleta katika hali nyingine na kisha kuwapuuza.

12/16/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”


Kwa maelfu kadhaa ya miaka, mwanadamu ametamani kuweza kushuhudia kufika kwa Mwokozi. Mwanadamu ametamani kumtazama Yesu Mwokozi katika wingu jeupe Anaposhuka, yeye binafsi, kati ya wale ambao wamengoja na kumtamani kwa maelfu ya miaka. Mwanadamu ametamani Mwokozi arejee na kuungana na watu, yaani, ili Yesu Mwokozi Arudi kwa watu ambao wamekuwa mbali Naye kwa maelfu ya miaka. 

12/15/2017

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu


Leo, tutawasiliana hasa jinsi watu wanavyostahili kumhudumia Mungu katika imani yao Mungu, masharti yanayopaswa kutimizwa na kinachopaswa kufahamika na watu wanaomhudumia Mungu, na mikengeuko ipi iliyoko katika huduma yako. Unapaswa kufahamu haya yote. Masuala haya yanagusia jinsi unavyomwamini Mungu, jinsi unavyotembea katika njia ya kuongozwa na Roho Mtakatifu, na jinsi mambo yako yote yanavyopangwa na Mungu, na yatakuwezesha kujua kila hatua ya kazi ya Mungu ndani yako.

12/14/2017

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu


Kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu haitengani na mwanadamu, kwa kuwa mwanadamu ni chombo cha kazi hii na kiumbe wa pekee aliyeumbwa na Mungu anayeweza kutoa ushuhuda kwa Mungu. Maisha ya mwanadamu na shughuli zake zote havitengani na Mungu, na vyote vinaongozwa na mkono wa Mungu, na inaweza kusemwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuishi bila Mungu. 

12/13/2017

Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu


















Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu


Mwenyezi Mungu alisema, Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kutimiza kwa ujumla mahitaji Yangu, kwa hiyo lazima Nilenge suala moja kwa moja na kuwafafanulia moyo na akili Zangu. Tukichukulia kwamba uwezo wenu wa utambuzi na ufahamu wenu vyote ni duni sana, karibu mmekosa kabisa kujua tabia na dutu Yangu, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuhusu haya. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani.

12/12/2017

Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu


Enzi ya zama ishaenda, na enzi mpya imefika. Mwaka baada ya mwaka na siku baada ya siku, Mungu amefanya kazi nyingi. Alikuja duniani, kisha Akaondoka. Mzunguko kama huu umeendelea kwa vizazi vingi. Siku ya leo, Mungu anaendelea kama mbeleni kufanya kazi Anayopaswa kufanya, kazi ambayo bado Hajaikamilisha, kwani hadi leo, bado Hajaingia mapumzikoni.

12/11/2017

Maonyo Matatu | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,  Mwenyezi Mungu

Maonyo Matatu


Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote.

12/10/2017

Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?


Huenda ikawa safari yako ya imani katika Mungu imekuwa ndefu zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda kwa maisha yako umestahimili ugumu mwingi miaka hii yote; au labda haujapitia ugumu na badala yake umepokea neema nyingi. Kuna uwezekano pia kuwa hujapitia ugumu wala kupokea neema, na badala yake

12/09/2017

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kiini Cha Kristo ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba Wa Mbinguni


Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote.

12/08/2017

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili



Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. 

12/07/2017

Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea


Watu wengi wanamwamini Mungu kwa ajili ya hatima yao ya baadaye au kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Kwa wale ambao hawajapitia ushughulikiaji wowote, imani kwa Mungu ni kwa ajili ya kuingia mbinguni, ili kupata tuzo. Sio ili kufanywa wawe na ukamilifu, au kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu. Ambayo ni kusema kwamba watu wengi hawamwamini Mungu ili watimize majukumu yao, au kukamilisha wajibu wao.

12/06/2017

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu


Kazi ya Mungu katika mwili inajumuisha sehemu mbili. Mara ya kwanza Alipofanyika kuwa mwili, watu hawakumwamini au kumfahamu na kumsulubisha Yesu msalabani. Mara ya pili, pia, watu pia hawakuamini ndani Yake, wala kumfahamu, na kwa mara nyingine wakamsulubisha Kristo msalabani. Je, si mwanadamu ni adui wa Mungu? Kama mwanadamu hamjui Yeye, mwanadamu anawezaje kuwa mwandani wa Mungu? Na anawezaje kuwa amehitimu kumshuhudia Mungu? Kumpenda Mungu, kumtumikia Mungu, kumtukuza Mungu—je, huu si udanganyifu?

12/05/2017

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

 Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?


Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake.

12/04/2017

Kuhusu Majina na Utambulisho | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kuhusu Majina na Utambulisho


Iwapo unataka kufaa kwa ajili ya matumizi na Mungu, lazima uijue kazi ya Mungu; lazima uijue kazi Aliyofanya awali (katika Agano Jipya na la Kale), na, zaidi ya hayo, lazima uijue kazi Yake ya leo. Ndiyo kusema, ni lazima uzitambue hatua tatu za kazi ya Mungu ya zaidi ya miaka 6,000. Ukiulizwa ueneze injili, basi hutaweza kufanya hivyo bila kuijua kazi ya Mungu.

12/03/2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo


Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya binadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji.

12/02/2017

Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu


Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, "Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika.

12/01/2017

Je, Utatu Mtakatifu Upo?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Je, Utatu Mtakatifu Upo?


Ni baada tu ya ukweli wa Yesu kuwa mwili kutokea ndipo mwanadamu alipogundua hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho Mtakatifu. Hii ndiyo dhana ya kawaida aliyonayo mwanadamu, kwamba kuna Mungu wa aina hii mbinguni: Utatu ambao ni Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, wote katika nafsi moja. Wanadamu wote wana fikra hizi: Mungu ni Mungu mmoja, ila Anajumuisha sehemu tatu, kile ambacho wale wote waliofungwa kwa huzuni katika hizi dhana za kawaida wanachukulia kuwa kuna Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu.