12/17/2017

Maneno kwa Vijana na Wazee|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Maneno kwa Vijana na Wazee|Mwenyezi Mungu


Nimetekeleza kazi nyingi sana duniani na Nimetembea kati ya wanadamu kwa miaka mingi sana. Ilhali watu kwa nadra sana huwa na ufahamu wa sura Yangu na tabia Yangu, na watu wachache wanaweza kuelezea kikamilifu kazi Ninayofanya. Watu wanakosa mengi sana, daima wanakosa ufahamu wa kile Ninachokifanya, na mioyo yao daima iko tayari kana kwamba wanaogopa sana Nitawaleta katika hali nyingine na kisha kuwapuuza. Kwa hivyo, mtazamo wa watu Kwangu daima ni vuvuwaa pamoja na tahadhari kubwa sana. Hili ni kwa sababu watu wamekuja kwa wakati wa sasa bila kuelewa kazi Ninayofanya, na wao hasa hukanganywa na maneno ambayo Ninawaambia. Wao huyabeba maneno Yangu mikononi mwao, wasijue kama wanapaswa kujitahidi kuamini au kama wanapaswa kuyasahau kwa shaka. Hawajui kama wanapaswa kuyatia katika vitendo, au kama wanapaswa kungoja kuona. Hawajui kama wanapaswa kuachana na kila kitu na kisha kufuata kwa ujasiri, au kama wanapaswa kuendelea kuwa wa kirafiki na ulimwengu kama hapo awali. Ulimwengu wa ndani wa watu ni wenye utata sana, na wao ni wajanja sana. Kwa sababu watu hawawezi kuyaona kwa dhahiri maneno Yangu na hawawezi kuyaona kikamilifu, wengi wao wana wakati mgumu kuyatenda, na wana shida kuweka moyo wao mbele Yangu. Ninayaelewa kwa kina matatizo yenu. Udhaifu mwingi hauepukiki wakati mtu anapoishi ndani ya mwili, na vipengele vingi ya kuhusu mambo huwaletea shida. Mnalisha familia zenu, mnatumia siku zenu mkifanya kazi kwa bidii, na wakati hupita vigumu. Kuna shida nyingi za kuishi katika mwili—Sikatai hili, na bila shaka mahitaji Yangu kwenu yanalingana na shida zenu. Mahitaji katika kazi Ninayofanya yote yana msingi katika kimo chenu halisi. Labda wakati watu walipokuwa wakifanya kazi zamani mahitaji yao kwenu yalichanganywa na dalili za uziada, lakini mnapaswa kujua kwamba Sijawahi kuwa na mahitaji ya ziada kwenu katika yale Ninayosema na kutenda. Yote yanahitajika kulingana na asili ya watu, mwili, na kile wanachohitaji. Mnapaswa kujua, na Naweza kuwaambia kwa dhahiri sana, kwamba Sikupingi kufikiria fulani kwa maana kwa watu na asili zao za awali. Ni tu kwa sababu watu hawaelewi kwa kweli kile kilicho kiwango cha mahitaji Yangu kwao, wala hawaelewi maana ya asili ya maneno Yangu ambayo hadi sasa, watu bado wana wasiwasi na maneno Yangu, na hata chini ya nusu ya watu huyaamini maneno Yangu. Waliosalia ni wasioamini, na hata zaidi ni wale wanaopenda kunisikia "Nikisimulia hadithi." Aidha, kuna wengi ambao wanaoliona kama kiburudisho. Ninawapa onyo: Maneno Yangu mengi tayari yamefunguliwa kwa wale wanaoniamini Mimi, na wale ambao "wanafurahia" mandhari mazuri ya ufalme lakini wamefungiwa nje ya mlango wake tayari wameondolewa na Mimi. Je, nyinyi si magugu tu ambavyo yamechukiwa na kukataliwa na Mimi? Je, Mngeniaga vipi na kisha kukaribisha kurudi Kwangu kwa furaha? Nawaambieni, baada ya watu wa Ninawi kusikia maneno ya hasira ya Yehova, mara moja walitubu kwa magunia na majivu. Ilikuwa kwa sababu waliyaamini maneno Yake kwamba walijawa na woga na hofu na wakatubu kwa magunia na majivu. Na ingawa watu wa leo pia wanaamini maneno Yangu na hata zaidi kuamini kuwa Yehova amekuja tena kati yenu leo, mtazamo wenu sio chochote ila usioheshimu vitu vitakatifu, kana kwamba mnamwangalia tu Yesu aliyezaliwa Yudea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita na sasa Ameshuka katikati yenu. Ninaelewa kabisa udanganyifu ulio ndani ya mioyo yenu; wengi wenu hunifuata kutokana na udadisi na mmekuja kunitafuta kutokana na utupu. Wakati matakwa yenu ya tatu yanavunjwavunjwa—kwa ajili ya maisha ya amani na yenye furaha—udadisi wenu pia unatapanywa. Udanganyifu ulio ndani ya mioyo ya kila mmoja wenu wote hufunuliwa kupitia maneno na matendo yenu. Kusema kweli, nyinyi mnataka tu kujua kunihusu, hamwogopi; hamjali matamshi yenu, na mnazuia tabia zenu hata mara chache zaidi. Basi imani yenu iko vipi kwa kweli? Je, ni ya kweli? Mnatumia tu maneno Yangu kuondoa wasiwasi wenu na kupunguza uchoshi wenu, ili kujaza nafasi zilizobaki tupu katika maisha yako. Ni nani miongoni mwenu ambaye ameyatia katika vitendo? Nani ana imani ya kweli? Mnaendelea kupiga kelele kwamba Mungu ni Mungu ambaye huona ndani kabisa ya mioyo ya watu, lakini ni vipi Mungu mnayepiga kelele kuhusu mioyoni mwenu analingana na Mimi? Kwa kuwa mnapiga kelele kwa njia hii, basi kwa nini mnatenda kwa njia ile? Inawezea kuwa kwamba huu ndio upendo mnaotaka kunilipizia nao? Hakuna kiasi kidogo cha upendo kwenye midomo yenu, lakini ziko wapi dhabihu zenu, na matendo yenu mema? Isingalikua maneno yenu kuyafikia masikio Yangu, Ningaliwezaje kuwachukia sana? Ikiwa kweli mliniaminia, mngewezaje kuangukia hali kama hii ya dhiki? Mnazo sura za huzuni kwenye nyuso zenu kana kwamba mko kuzimu mkishtakiwa. Hamna uhai wowote, na mnanena kuhusu sauti yenu ya ndani kwa udhaifu; mmejawa hata na malalamiko na laana Mlipoteza imani katika yale Nifanyayo zamani na hata imani yenu ya asili imepotea, basi mnawezaje kufuata mpaka mwisho? Mnawezaje kuokolewa kwa njia hii?

Ingawa kazi Yangu ni yenye msaada mkubwa kwenu sana, maneno Yangu daima hushindwa kuwashawishi na kutofanikiwa ndani yenu. Ni vigumu kupata chombo cha kukamilishwa na Mimi na leo karibu Nimepoteza tumaini kwenu. Nimetafuta kati yenu kwa miaka kadhaa lakini ni vigumu kupata msiri. Ninahisi kama Sina imani ya kuendelea kufanya kazi ndani yenu, na Sina upendo kuendelea kuwapenda. Hili ni kwa sababu Nilikuwa Nimechukizwa kitambo na yale mafanikio yenu madogo ya kusikitisha; ni kana kwamba Sikuwahi kuzungumza kati yenu na Sikuwahi kufanya kazi ndani yenu. Mafanikio yenu yanachafua moyo sana—daima mmetiwa fedheha na karibu hamna thamani yoyote. Kwa nadra Ninapata mfano wa mwanadamu ndani yenu au kusikia harufu ya mwanadamu. Iko wapi harufu yenu mpya? Iko wapi gharama ambayo mmelipa kwa miaka mingi, na matokeo yako wapi? Hamjawahi kuyapata? Kazi Yangu sasa ina asili mpya, mwanzo mpya. Ninaenda kutekeleza mipango mikubwa na Ninataka kutekeleza kazi kubwa, ilhali bado mnavingirika katika matope kama hapo awali, kuishi katika maji machafu ya zamani, na kwa utendaji hamjatupa mashaka yenu ya awali. Kwa hivyo, bado hamjapata chochote kutoka kwa maneno Yangu. Bado hamjatupa pahali penu pa awali pa matope na maji machafu, na mnayajua maneno Yangu tu, lakini kwa kweli hamjaingia katika eneo la uhuru wa maneno Yangu, hivyo maneno Yangu hayajawahi kufunguliwa kwenu, na yako kama kitabu cha unabii ambacho kimefungwa kwa maelfu ya miaka. Ninaonekana kwenu katika maisha yenu lakini daima hamjui, na hamnitambui hata. Takriban nusu ya maneno Ninayoyasema ni hukumu ya nyinyi, na nusu yao ni ya ufanisi ili nyote mnavutwa mawazo. Nusu iliyobaki ni maneno ya kuwafundisha kuhusu maisha na jinsi ya kutenda, lakini ni kana kwamba hayapo kwenu, na kana kwamba nyinyi mnasikiliza maneno ya watoto wanaocheza, ambayo daima nyinyi huyatolea tabasamu iliyofichwa, na kisha hakuna kitu kinachofanywa. Hamjawahi kujishughulisha na mambo haya; daima mmefuata matendo Yangu kutokana na udadisi wenu ili kwamba sasa mmeanguka gizani na hamwezi kuuona mwanga—mnalia kwa huruma gizani. Kile Ninachotaka ni utiifu wenu, utiifu wenu usio na masharti na hata zaidi, Nahitaji kwamba muwe na hakika kabisa juu ya kila kitu Ninachosema. Hampaswi kukubali mtazamo wa kutokujali na hasa hampaswi kuuvumilia kwa kuchagua, ni wazi kwamba nyinyi daima hamjali maneno Yangu na kazi Yangu. Kazi Yangu inafanywa katikati yenu na Nimewapa maneno Yangu mengi, lakini mkinilaghai kwa njia hii, Ninaweza tu kutoa bure kile ambacho hamjapata na hamjatia katika vitendo kwa familia za Mataifa. Ni nini kati ya uumbaji hakipo mikononi Mwangu? Wengi wa wale kati yenu ni wa "wa miaka mingi sana" na hamna nguvu ya kukubali aina hii ya kazi Yangu. Nyinyi ni kama ndege wa Hanhao[a], mnaishi kwa shida, na hamjawahi kuyachukulia maneno Yangu kwa uzito. Vijana ni bure sana na wanajifurahisha sana na hata zaidi wanaipuuza kazi Yangu. Hawahisi kufurahia vyakula vitamu vya karamu Yangu; Wao ni kama ndege mdogo ambaye ameruka nje ya tundu lake kwenda mbali kabisa. Je, wazee na vijana wa aina hii wanawezaje kuwa na manufaa Kwangu? Wale wa umri uliosonga wako tayari kuyatumia maneno Yangu kama kiinua mgongo mpaka wakati wako katika makaburi yao, ili baada ya wao kufa nafsi zao zinaweza kwenda juu mbinguni, na hilo linatosha. Ndiyo sababu kwa sasa, wanathamini "tamanio kubwa" na "wanajiamini sana." Ingawa wamejawa uvumilivu kwa kazi Yangu, na wao ni waadilifu na wasiokubali kushindwa kama roho ya mtu mzee ambaye hataburutwa au kushindwa na mtu yeyote au kitu chochote kama tu ngome isiyoingilika, imani ya watu hawa siyo iliyojaa roho ya ushirikina ya maiti? Iko wapi njia yao? Kwao, njia yao siyo ndefu sana, ya mbali sana? Wangejuaje mapenzi Yangu? Hata kama imani yao ni ya kustahili kusifiwa, ni wangapi kati ya wazee hawa hawafuati kwa njia ya kuchanganyikiwa bali wanafukuzia maisha? Ni wangapi wanaofahamu kwa kweli umuhimu wa kweli wa kazi Yangu? Nia ya nani siyo kwamba waweze kunifuata katika ulimwengu huu leo, na katika siku za karibu za usoni hawatashuka kuzimu bali kuletwa kwatika eneo jingine na Mimi? Je, mnafikiri hatima yenu ni jambo rahisi sana? Ingawa nyinyi vijana wote ni kama simba wachanga, kwa nadra mnakuwa na njia ya kweli mioyoni mwenu. Ujana wenu hauwezi kupata zaidi ya kazi Yangu, lakini daima nyinyi husababisha chuki Changu kwenu. Ingawa nyinyi ni wachanga, ama mnakosa uhai au hamna tamaa ya makuu, daima nyinyi hamjihusishi na siku zenu zijazo; ni kana kwamba hamjali, na pia mnawaza sana. Ingeweza kusemwa kuwa uchangamfu, maadili, na msimamo yanayochukuliwa ambayo yanapaswa kupatikana kwa vijana hayawezi kabisa kupatikana kwenu; nyinyi, vijana wa aina hii, mnakosa msimamo na hamna uwezo wa kutofautisha kati ya sahihi na isiyo sahihi, mema na maovu, mazuri na mabaya. Haiwezekani kupata dalili zozote zenu ambazo ni mpya. Nyinyi karibu mmepitwa na wakati kabisa, na nyinyi, vijana wa aina hii, pia mmejifunza kukubali tu , kuwa bila mantiki. Hamwezi kamwe kutofautisha kwa dhahiri mazuri kutoka kwa mabaya, hamwezi kutofautisha kati ya ukweli na uongo katika masuala, kamwe hamjitahidi kupata ubora, wala hamwezi kusema nini ni sahihi na nini si sahihi, nini ni ukweli, na nini ni unafiki. Ndani yenu kunabakia mipulizo ya ghafla ya dini hata zaidi na hata mikubwa zaidi kuliko kwa watu wazee. Nyinyi hata ni wenye kiburi na msio na busara, nyinyi ni wa ushindani kabisa, na uchokozi wenu ni mzito sana—kijana wa aina hii anawezaje kumiliki ukweli? Mtu asiyeweza kuchukua msimamo anawezaje kushuhudia? Mtu asiye na uwezo wa kutofautisha kati ya yaliyo sahihi na yasiyo sahihi anawezaje kuitwa kijana? Mtu asiye na uhai, nguvu, utulivu, ubichi, utulivu na udhabiti wa kijana anawezaje kuitwa mfuasi Wangu? Mtu asiye na ukweli wowote wala hisia ya haki, lakini hupenda kucheza na kupigana anawezaje kufaa kuwa shahidi Wangu? Macho ambayo yamejaa uongo na chuki bila sababu kwa watu siyo wanayopaswa kuwa nayo vijana, na wale wanaotekeleza vitendo vya uharibifu, vinavyochukiza mno hawapaswi kuwa vijana. Hawapaswi kuwa bila maadili, matarajio, au tabia ya maendeleo ya shauku; hawapaswi kuvunjika moyo juu ya matarajio yao wala hawapaswi kupoteza matumaini maishani au kupoteza imani katika siku zijazo; wanapaswa kuwa na uvumilivu kuendelea na njia ya ukweli ambayo sasa wamechagua kufanikisha matamanio yao ya kutumia maisha yao yote kwa ajili Yangu; hawapaswi kuwa bila ukweli, wala kuficha unafiki na udhalimu, bali wanapaswa kusimama imara katika msimamo unaofaa. Hawapaswi tu kuzurura, bali wanapaswa kuwa na roho ya kuthubutu kujitolea mhanga na kujitahidi kwa ajili ya haki na ukweli. Vijana wanapaswa kuwa na ujasiri wa kutoshindwa na ukandamizaji wa nguvu za giza na kubadili umuhimu wa uwepo wao. Vijana hawapaswi kukubali shida bila kulalamika, bali wanapaswa wawe wazi na wa kusema bila kuficha na roho ya msamaha kwa ndugu wao. Bila shaka haya ni mahitaji Yangu ya kila mtu pamoja na ushauri Wangu kwa kila mtu. Hata zaidi, ni maneno Yangu ya kutuliza kwa vijana wote. Mnapaswa kutenda kulingana na maneno Yangu. Hasa vijana hawapaswi kuwa bila azimio la utambuzi katika masuala, na la kutafuta haki na ukweli. Yale mnayopaswa kufuata ni mambo yote mazuri na mema, na mnapaswa kupata uhalisi wa mambo yote mazuri, na pia kuwajibika juu yaa maisha yenu—hampaswi kuyachukulia kwa wepesi. Watu huja duniani na ni nadra kupatana na Mimi, na pia ni nadra kuwa na fursa ya kutafuta na kupata ukweli. Kwa nini msithamini wakati huu mzuri kama njia sahihi ya kutafuta katika maisha haya? Na ni kwa nini daima nyinyi hupuuza sana ukweli na haki? Kwa nini daima nyinyi hujikanyaga na kujiangamiza kwa ajili ya ule udhalimu na uchafu ambao huchezea watu? Na kwa nini mnajishughulisha na kile ambacho wadhalimu hufanya kama watu wazee? Kwa nini mnaiga njia za zamani za mambo ya kale? Maisha yenu yanapaswa kujaa haki, ukweli, na utakatifu; hayapaswi kupotoshwa sana hivi punde sana, na kuangushwa kuzimu. Je, hamhisi kwamba hili ni la kusikitisha sana? Je, hamhisi kwamba hili silo haki kwenu sana?
Watu wote wanapaswa kufanya kazi sahihi kabisa yenu na kuidhabihu juu ya madhabahu Yangu kama dhabihu bora zaidi, za kipekee ambazo mnanipa. Nyote mnapaswa kusimama imara katika msimamo wenu wenyewe na msipeperushwe peperushwe na kila upepo mwanana kama mawingu angani. Mnafanya kazi kwa bidii nusu ya maisha yenu, basi kwa nini msitafute hatima mnapaswa kuwa nayo? Mnafanya kazi kwa bidii kwa muda wa nusu ya maisha ilhali mnawaacha wazazi wenu walio kama nguruwena mbwa kukokota ukweli na umuhimu wa maisha yenu binafsi ndani ya kaburi. Je, huhisi kwamba halifai? Je, huhisi kuwa kuishi kwa njia hii ni maisha yasiyo na maana kabisa? Kutafuta ukweli na njia sahihi kwa njia hii mwishowe kutasababisha matatizo ili kuwa majirani ni wa wasiwasi na familia nzima haina furaha, na hupata misiba ya mauti—je, si wewe kuwa hivi ni maisha yasiyo na maana kabisa? Maisha ya nani yanaweza kuwa na bahati zaidi kuliko yako, na maisha ya nani yanaweza kuwa ya mzaha zaidi kuliko yako? Kunitafuta kwako si kwa ajili ya kupata furaha Yangu na kwa maneno ya faraja kwako? Lakini baada ya wewe kukimbia kimbia kwa nusu ya maisha na kisha kunichokoza mpaka Ninapojawa na hasira na kukupuuza au kutokusifu, basi si maisha yako yote ni bure? Na ungewezaje kuthubutu kwenda kuona roho za wale watakatifu katika enzi zote ambao wameondolewa toharani? Wewe hunijali na hatimaye unasababisha msiba wa mauti—ingekuwa bora zaidi kutumia fursa hii na kuwa na safari ya furaha kuvuka bahari kubwa mno na kisha kusikiza "utoaji" Wangu. Niliwaambia zamani kwamba wewe leo, kama usiyejali ilhali hutaki kuondoka, hatimaye ungeingizwa na kumezwa na mawimbi yaliyoinuliwa na Mimi. Je, kwa kweli mnaweza kujilinda wenyewe? Je, una imani kwamba mbinu yako ya sasa ya ukimbizaji itahakikisha kuwa unakamilishwa? Je, moyo wako si mgumu sana? Kufuata kwa aina hii, ukimbizaji wa aina hii, maisha ya aina hii, na tabia ya aina hii—jinsi gani vingeweza kupata sifa Yangu?
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni