1/30/2018

Tamko la Kumi na Tisa | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Tamko la Kumi na Tisa | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Ni shughuli sahihi ya mwanadamu kuchukua maneno Yangu kama msingi wa maisha yake. Mwanadamu lazima aanzishe fungu lake binafsi katika kila sehemu ya maneno Yangu; kutofanya hivyo kutakuwa kuuliza matata, kutafuta maangamizo yake mwenyewe. Binadamu haunijui, na kwa sababu ya hili, badala ya kuleta maisha yake Kwangu badala, anachofanya ni kujipanga tu mbele Yangu na takataka mikononi mwake, na hivyo kujaribu kuniridhisha. Lakini, mbali na kuridhishwa na mambo yalivyo, Naendelea kutoa matakwa kwa binadamu. Napenda sifa za mwanadamu, lakini Nachukia wizi wake. Wanadamu wote wana mioyo iliyojaa ulafi; ni kama moyo wa binadamu unadhibitiwa na Shetani, na mwanadamu hawezi kuponyoka na kutoa moyo wake Kwangu. Ninapozungumza, mwanadamu husikiza sauti Yangu kwa makini; lakini Ninapokoma kuzungumza, anaaza tena “biashara” yake na kusitisha kabisa kuyajali maneno Yangu, ni kama maneno Yangu ni duni kwa biashara yake. Sijawahi kuwa mzembe kwa binadamu, na bado Nimekuwa pia mvumilivu na mkarimu kwa binadamu. Na hivyo, kwa sababu ya huruma Yangu, binadamu wote wamekuwa wenye kiburi, wasio na maarifa na tafakari ya binafsi, na wanatumia vibaya uvumilivu Wangu ili kunidanganya. Hakuna mmoja kati yao anayenijali kwa dhati, na hakuna mmoja kweli ananithamini kama kitu apendacho moyoni mwake; ni wakati tu walipo na wakati wa ziada ndipo wanaponitambua kwa kiwango duni. Juhudi ambazo Nimetumia kwa mwanadamu tayari ni zaidi ya kipimo. Ninamfanyia mwanadamu aina ya pekee ya kazi, na mbali na haya, Nimempaa mzigo wa ziada, ili, ndani ya kile Ninacho na kile Nilicho, mwanadamu anaweza kupata maarifa na kupitia mabadiliko. Simtaki mwanadamu awe mtumiaji tu, lakini Namtaka awe mzalishaji anayeweza kumshinda Shetani. Ingawa Sidai chochote kutoka kwa mwanadamu, hata hivyo Nina viwango vya matakwa Ninayoyatoa, kwani kuna madhumuni kwa yale Ninayoyafanya, na pia Ninatenda kulingana na kanuni: Sichezi kiholela, anavyodhani mwanadamu, wala Siundi mbingu na dunia na mambo mengi ya uumbaji kwa ghafla na bila mpango. Kwa kazi Zangu, mwanadamu anapaswa kuwa na uwezo wa kuona kitu, kupata kitu. Hapaswi kutumia vibaya uchangamfu wa ujana wake, ama kutunza maisha yake kama vazi ambalo linakusanya vumbi; badala yake, anapaswa kujilinda vikali, kuchukua kutoka kwa fadhila Yangu kwa ajili ya starehe yake mwenyewe, hadi, kwa sababu Yangu, hawezi kumrudia Shetani, na kwa sababu Yangu anamshambulia Shetani. Si Ninachomwulizia mwanadamu ni rahisi hivi? 
Mwangaza hafifu unapoanza kuonekana Mashariki, watu wote ulimwenguni kwa sababu hii wanaupa kipaumbele mwangaza ulio Mashariki. Bila kujawa na usingizi, wanadamu huenda kuchunguza chanzo cha mwangaza wa mashariki, lakini kwa sababu ya vikwazo vya uwezo wa binadamu, hakuna anayeweza kuona mahali unapotokea mwangaza. Wakati yote yaliyo ulimwenguni yameangaziwa kabisa, mwanadamu atazinduka kutoka usingizi na ndoto, na hapo tu ndipo atakapotambua kwamba siku Yangu inawadia polepole duniani. Binadamu wote wanasherehekea kwa sababu ya ujio wa mwangaza, na kwa sababu ya haya hawalali tena, na si wapumbavu tena. Chini ya mng’aro wa mwangaza Wangu, binadamu wote wanakuwa na uwazi wa akili na mtazamo, na ghafla wanakuwa na furaha ya maisha. Chini ya kifuniko cha ukungu, Nawalinda wanadamu. Wanyama wote wako katika mapumziko; kwa sababu ya ujio wa mwangaza hafifu, kila kitu katika uumbaji kinafahamu kwamba maisha mapya yanakaribia. Kwa sababu hii, wanyama pia wanatoka nje ya mapango yao, kutafuta chakula. Mimea, bila shaka, si tofauti, na kwa mng’aro wa mwangaza majani yao ya kijani yanang’aa, yakisubiri kutakasa sehemu yao binafsi Kwangu wakati Niko duniani. Wanadamu wote wanataka ujio wa mwangaza, lakini bado wanahofia ujio wake, na wasiwasi kwamba ubaya wao hutafichika tena, kwani mwanadamu yu uchi kabisa, na hajafunikwa. Watu wangapi wanahofia, kwa sababu ya ujio wa mwangaza, na kwa sababu mwangaza umetokea, wako katika hali ya mshtuko? Watu wangapi, baada ya kuuona mwangaza, wamejawa majuto yasiyo na mipaka, wakichukia uchafu wao, lakini, bila uwezo wa kubadilisha ukweli uliotimia, wanaweza tu kunisubiri kutamka hukumu. Watu wangapi, wakisafishwa na mateso gizani, wanapoona mwangaza wanapigwa ghafla na umuhimu wake mkubwa, na hatimaye kukumbatia mwangaza karibu na vifua vyao, wakiogopa kuupoteza tena? Watu wangapi, badala ya kutupwa nje ya uzingo na kutoka kwa ghafla kwa mwanga, wanaendelea tu na kazi ya kila siku, kwa sababu wamekuwa vipofu kwa miaka mingi, na hivyo hawana habari kwamba mwangaza umekuja, wala hawaridhishwi nao. Katika mioyo ya wanadamu, Mimi siko juu, wala chini. Wanadamu hawajali iwapo Nipo au la, kama kwamba maisha ya mwanadamu hayawezi kuwa na upweke zaidi iwapo Sipo, na iwapo Nipo, hayatafaidika na furaha. Kwa sababu wanadamu hawanithamini, raha Ninayowapa ni chache. Lakini punde tu binadamu unaponiabudu kidogo, basi pia Nitafanya mabadiliko kwa mtazamo Wangu kwa binadamu. Kwa sababu hii, wakati tu binadamu unapofahamu sheria hii, ndipo tu wanadamu watakapokuwa na bahati ya kujitolea Kwangu na kudai vitu vilivyo mikononi Mwangu. Hakika pendo la mwanadamu Kwangu halifungwi tu na maslahi yake mwenyewe? Hakika imani yake Kwangu haifungwi tu kwa mambo Ninayompa? Inaweza kuwa kwamba, isipokuwa tu yeye kuona mwangaza Wangu, mwanadamu hawezi kunipenda kwa dhati kwa njia ya imani yake? Hakika nguvu za mwanadamu na afya hazizuiliwi na hali ya leo? Inaweza kuwa kwamba mwanadamu anahitaji ujasiri ili anipende?
Kutegemea kuwepo Kwangu, mambo mengi ya uumbaji yanakubali kwa utiifu mahali yanamoishi, na katu, bila ya nidhamu Yangu, hayajihusishi na uasherati bila kujali. Kwa hivyo, milima inakuwa mipaka kati ya mataifa ulimwenguni, maji yanakuwa vikwazo vya kuwatenga watu kati ya nchi, na hewa inapuliza kutoka kwa mwanadamu mmoja hadi mwingine katika uwanda wa dunia. Binadamu tu huwezi kweli kutii matakwa ya mapenzi Yangu; hii ndiyo maana Nasema kwamba, kwa viumbe vyote, mwanadamu pekee ni ndiye wa kundi la wasiotii. Mwanadamu hajawahi kweli kunitii, na kwa sababu hii wakati wote Nimemweka chini ya nidhamu kali. Iwapo katikati ya binadamu, itakuja kuwa kwamba utukufu Wangu umetandaa ulimwengu nzima, basi hakika Nitachukua utukufu Wangu wote na kuufanya uwe wazi mbele ya mwanadamu. Kwa sababu katika uchafu wake mwanadamu hafai kutazama utukufu Wangu, kwa maelfu ya miaka Sijawahi kujitokeza hadharani, lakini Nimebakia mafichoni; kwa sababu hii utukufu Wangu hujawahi kuwa wazi mbele ya mwanadamu, na mwanadamu daima amezama kwa shimo la kina la dhambi. Nimeusamehe udhalimu wa binadamu, lakini wanadamu hawajui jinsi ya kujihifadhi, na badala yake daima wanajiweka wazi kwa dhambi, kuruhusu dhambi kuwajeruhi. Huu si ukosefu wa mwanadamu wa kujiheshimu na kujipenda? Katikati ya binadamu, kuna kweli yeyote anayeweza kupenda? Ibada ya mwanadamu inaweza kuwa na uzito wa wakia ngapi? Hakuna bidhaa safi zilizochanganywa na kinachoitwa uhalisi wake? Si ibada yake imeungana kabisa na mkanganyiko? Ninachohitaji ni upendo wa mwanadamu usiogawanyika. Mwanadamu hanijui, na ingawa anaweza kupata kunijua, hatanipa moyo wake wa ukweli na dhati. Kwa mwanadamu, Sidai kile asichotaka kupeana. Akinipa ibada yake, Nitaikubali bila pingamizi; lakini asiponiamini, na kukataa kujitoa hata kidogo Kwangu, badala ya kukasirika juu ya hayo, Nitamwondoa tu kwa njia ingine na kumtuma kwa nyumba inayomfaa. Radi, inayovingirika angani, inamwangusha chini mwanadamu, milima ya juu, inapoanguka, inamzika; wanyama pori kwa njaa yao wanamla kwa ulafi; na bahari, zinapobingirika, zinazingira kichwa chake. Binadamu wanapojishughulisha na migogoro ya mauaji ya jamii, wanadamu wote watatafuta maangamizo yao katika majanga yatokayo katikati ya binadamu.
Ufalme unapanuka miongoni mwa binadamu, unachipua miongoni mwa binadamu, unasimama miongoni mwa binadamu; hakuna nguvu inayoweza kuharibu ufalme Wangu. Kwa watu Wangu walio katika ufalme wa leo, nani kati yenu si mwanadamu miongoni mwa wanadamu? Nani kati yenu yu nje ya hali ya ubinadamu? Wakati hatua Yangu ya kwanza mpya itatangazwa kwa wengi; binadamu utaguswa vipi? Mmeona na macho yenu hali ya mwanadamu; hakika bado hamna matumaini ya kudumu milele kwa dunia hii? Sasa Natembea ng’ambo katikati ya watu Wangu, Naishi katikati ya watu Wangu. Leo, walio na pendo la kweli Kwangu, watu kama hawa wamebarikiwa; wamebarikiwa wanaonitii, hakika watabaki katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonijua, hakika watakuwa na mamlaka katika ufalme Wangu; wamebarikiwa wanaonitafuta, hakika watatoroka vifungo vya Shetani na kufurahia baraka ndani Yangu; wamebarikiwa wanaoweza kujiacha, hakika wataingia katika milki Yangu, na kurithi fadhila ya ufalme Wangu. Wanaokimbia kimbia kwa ajili Yangu Nitawaadhimisha, wanaopata gharama kwa ajili Yangu Nitawakumbatia kwa furaha, wanaonitolea sadaka Nitawapa starehe. Wanaopata raha ndani ya maneno Yangu, Nitawabariki; hakika watakuwa nguzo zinazoshikilia mwamba kwa ufalme Wangu, hakika watakuwa na fadhila isiyo na kifani kwa nyumba Yangu, na hakuna anayeweza kulinganishwa nao. Mmewahi kuzikubali baraka mlizopewa? Mmewahi kutatufa ahadi mlizopewa? Hakika, chini ya mwongozo wa mwangaza Wangu, mtapenya utawala wa nguvu za giza. Hakika, katikati ya giza, hamtaupoteza mwangaza unaowaongoza, katikati ya giza. Hakika mtakuwa bwana wa viumbe vyote. Hakika mtakuwa washindi mbele ya Shetani. Hakika, wakati wa maangamizi ya ufalme wa joka kubwa jekundu, mtasimama miongoni mwa umati mkubwa kushuhudia ushindi Wangu. Hakika mtakuwa shujaa na imara katika nchi ya Sinimu. Kupitia mateso mnayoyavumilia, mtarithi baraka zinazotoka Kwangu, hakika mtaangaza ndani ya ulimwengu wote kwa utukufu Wangu.
Machi 19, 1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

1/29/2018

Maono ya Kazi ya Mungu (1)

more
Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,  Mwenyezi Mungu

Maono ya Kazi ya Mungu (1)

Yohana alimfanyia Yesu kazi kwa miaka saba, na tayari alikuwa ameandaa njia Yesu alipofika. Kabla ya haya, injili ya ufalme wa mbinguni iliyohubiriwa na Yohana ilisikika kotekote katika nchi, hivyo ilienea kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa Uyahudi, na kila mtu alimwita nabii. Wakati huo, Mfalme Herode alitamani kumuua Yohana, lakini hakuthubutu, kwani watu walimheshimu sana Yohana, na Herode aliogopa kwamba kama angemuua Yohana wangemuasi. Kazi iliyofanywa na Yohana ilikita mizizi miongoni mwa watu wa kawaida, na aliwafanya Wayahudi kuwa waumini.

1/28/2018

Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja


Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa. Kutoka hapa kuendelea, Mungu hakupumzika tena lakini badala yake Alianza kufanya kazi miongoni mwa binadamu.

1/27/2018

Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Kristo ndiye Chanzo cha Uhai na Vile Vile Bwana wa Biblia


Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Kristo ndiye Chanzo cha Uhai na Vile Vile Bwana wa Biblia


      Biblia imejaa maneno ya Mungu na vile vile uzoefu na ushuhuda kutoka kwa mwanadamu ambao unaweza kutupa uhai na ni yenye manufaa sana kwetu. Bwana Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima: Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, bado ataishi: Na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele.” (Yohana 11:25-26).

1/26/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sura ya 18

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

 Kanisa la Mwenyezi MunguSura ya 18


Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oh, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope! Ah, ya kwamba binadamu wote Niliouumba hatimaye umerudiwa na uhai tena katika mwanga, kupata msingi wa kuwepo, na kuacha kupambana katika tope!

1/25/2018

Upendo wa Mungu | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Swahili Gospel Music Video


Upendo wa Mungu | "Kama Nisingeokolewa na Mungu" | Swahili Gospel Music Video


Kama nisingeokolewa na Mungu, ningekuwa bado nazurura ulimwenguni humu,
nikipambana kwa bidii na maumivu katika dhambi; kila siku huwa ya taabu isiyo na tarajio.
Kama nisingeokolewa na Mungu, bado ningekuwa nimepondwa chini ya miguu ya shetani,
kama nimenaswa katika dhambi na starehe zake, bila kujua maisha yangu yangekuwaje.
Kama nisingeokolewa na Mungu, nisingekuwa na baraka zangu leo,
wala kujua kwa nini sisi tuendelee kuishi ama maana ya maisha yetu.

1/24/2018

Mbingu Mpya na Nchi imeonekana | "Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu"


Mbingu Mpya na Nchi imeonekana | "Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu"


Ulimwengu na Eneo Kubwa Zamsifu Mungu
Ha … nyimbo ni nyingi na ngoma ni za madaha;
ulimwengu na miisho ya dunia zinakuwa bahari inayosisimka.
Ha … mbingu ni mpya na dunia ni mpya.
Eneo kubwa la ulimwengu limejaa kusifu; tunapiga ukelele na kuruka kwa shangwe.
Milima yajiunga na milima na maji mengi kujiunga na maji mengi, ndugu wote wa kiume na kike ni wandani.

1/23/2018

Tamko la Kumi na Saba|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Kumi na Saba


Mwenyezi Mungu alisema, Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya.

1/22/2018

Upendo wa Mungu na wokovu | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho




Upendo wa Mungu na wokovu | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza” Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho


Mwenyezi Mungu alisema, "Mwanadamu, ambaye aliacha kupokea uzima wake kutoka kwa Mwenye Uweza, hajui ni kwa nini anaishi, na bado anaogopa kifo. Hukuna usaidizi, wala msaada, lakini mwanadamu bado anasita kufumba macho yake, akiyakabili yote bila woga, kuishi katika maisha yasiyokuwa na maana katika ulimwengu ndani ya miili isiyokuwa na utambuzi wa roho. Unaishi hivyo, pasipo tumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na malengo. Kuna Mmoja tu aliye Mtakatifu katika hadithi hii ambaye atakuja kuwaokoa wale wanaoomboleza kwa kuumia na wanasubiri kwa shauku kubwa kuja Kwake. 

1/21/2018

Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Maana ya Kuwa Mwanadamu Halisi|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu huenda hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho na pia huenda hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda wale walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini, adui Yangu alipoungana katika vita na Mimi, Nilikuwa Nimeshamwambia kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kufanywa watoto wake na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake.

1/20/2018

Tamko la Kumi Na Sita|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Tamko la Kumi na Sita

Kuna mengi Mimi natamani kumwambia mwanadamu, mambo mengi sana ambayo lazima Nimwambie. Lakini uwezo wa mwanadamu wa kukubali una upungufu mwingi: Hana uwezo wa kuyaelewa kabisa maneno Yangu kulingana na kile Ninachokitoa, na anaelewa kipengele kimoja tu lakini haelewi vingine.

1/19/2018

Tamko la Kumi na Tano|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Tamko la Kumi na Tano

Mwanadamu ni kiumbe asiyejifahamu. Hata ingawa hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii.

1/18/2018

Sura ya 14|Kanisa la Mwenyezi Mungu


Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Sura ya 14|Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Mwenyezi Mungu alisema, Katika enzi zote, hakuna mwanadamu ameingia katika ufalme na hivyo hakuna aliyefurahia neema ya Enzi ya Ufalme, hakuna aliyeona Mfalme wa ufalme. Ingawa chini ya nuru ya Roho Wangu watu wengi wametabiri uzuri wa ufalme, wanajua tu nje ya ufalme, sio umuhimu wa ndani. Leo, ufalme ujapo kuwepo rasmi duniani, binadamu wote bado hujui kinachopaswa kukamilishwa, ulimwengu ambao binadamu hatimaye ataletwa ndani, wakati wa Enzi ya Ufalme.

1/17/2018

Tamko la Kumi na Tatu|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Tamko la Kumi na Tatu

Mwenyezi Mungu alisema, Dhamira Zangu kadhaa zimefichwa ndani ya matamshi ya sauti Yangu. Ila mwanadamu hajui na hafahamu chochote kuhusu haya, huku akiendelea kuyapokea na kuyafuata maneno Yangu kutoka nje bila kung’amua roho Yangu na kuelewa mapenzi Yangu kutoka ndani ya maneno Yangu.

1/16/2018

Drama yenye Muziki ya Sifa za Ufalme–Kila Taifa Humwabudu Mungu wa Vitendo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Mungu anasema: “Je, hukutamani sana kumwona Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kumwelewa Mungu aliye mbinguni? Je, hukutamani sana kuona hatima ya mwanadamu? Atakueleza hizi siri zote ambazo hakuna mwanadamu ameweza kukuambia, na hata Atakuelezea kuhusu ukweli usioelewa. Yeye ndiye lango la kuingia katika ufalme, na mwongozo wako katika enzi mpya”(Neno Laonekana katika Mwili).

1/15/2018

Tamko La Kumi Na Mbili | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Tamko la Kumi na Mbili

Mwenyezi Mungu alisema, Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangaziwa, na nyota zote zinaanza kubadilika. Inaonekana kana kwamba jamii nzima ya binadamu imesafishwa na kupangwa vizuri. Chini ya mng’aro wa mwale huu wa mwangaza kutoka Mashariki, wanadamu wote wanafichuliwa katika maumbo yao ya awali, macho yaking’aa, yakizuiwa kwa kuchanganyikiwa; na hawawezi hata kidogo kuficha sifa zao mbaya.

1/14/2018

Sura ya 11 | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Sura ya 11 | Kanisa la Mwenyezi Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo, anapaswa kuangalia matendo Yangu ya ajabu. Mnahisi aje wakati wa kuwasili kwa ufalme duniani? Wakati Wanangu na watu Wangu wanarudi katika kiti Changu cha enzi, Naanza rasmi hukumu mbele ya kiti kikuu cheupe cha enzi.

1/13/2018

Tamko La Kumi|Kanisa la Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Tamko La Kumi

Mwenyezi Mungu alisema, Enzi ya Ufalme ni, hata hivyo, tofauti na nyakati za kale. Haihusu kile anachofanya mwanadamu. Badala yake, Mimi binafsi Natekeleza kazi Yangu baada ya kushuka duniani—kazi ambayo wanadamu hawawezi kuelewa wala kufanikisha.

1/12/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Sura ya 9

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 9 

Mwenyezi Mungu alisema, Kwa sababu kwamba wewe ni mmoja wa watu nyumbani Mwangu, na kwa sababu wewe ni mwaminifu katika Ufalme wangu, kila unachofanya lazima kifikie viwango Ninavyohitaji Mimi. Sisemi kwamba uwe tu kama wingu linalofuata upepo, bali uwe kama theluji inayong'aa, na uwe na hali kama yake na hata zaidi uwe na thamani yake. Kwa sababu Nilitoka katika nchi takatifu, si kama yungiyungi, ambalo lina jina tu na halina dutu kwa sababu lilikuja kutoka katika matope na si kutoka nchi takatifu.

1/11/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Nane

Mwenyezi Mungu alisema, Ufunuo Wangu unapofika kilele chake, na wakati hukumu Yangu inapomalizika, utakuwa wakati ambao watu Wangu wote wanafichuliwa na kufanywa wakamilifu. Nyayo zangu hukanyaga kila pembe ya ulimwengu katika hali ya kutafuta kwa kudumu wale wenye kupendeza nafsi Yangu na wanafaa kwa matumizi Yangu. Nani anaweza kusimama na kushirikiana na Mimi? Upendo wa mwanadamu Kwangu ni mdogo mno na imani yake Kwangu ni ndogo ajabu.

1/10/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

 Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Saba


Matawi yote ya magharibi yanapaswa kuisikiliza sauti Yangu:
Je, mmekuwa waaminifu Kwangu hapo awali? Je, mmekuwa mkiyasikia maneno Yangu mazuri ya ushauri? Je, mnayo matumaini ambayo ni halisi na yasiyo na mashaka? Utiifu wa mwanadamu, mapenzi yake, imani yake—hamna kipatikanacho ila kutoka Kwangu, hamna hata kimoja ila kilichotawazawa na Mimi.

1/09/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Sita 

Kwa masuala ya ndani ya roho, unapaswa kuwa makini kwa utaratibu; kwa maneno Yangu, unapaswa kuwa msikivu kwa makini. Unapaswa kulenga hali ambayo unaona Roho Yangu na nafsi Yangu ya mwili, maneno Yangu na nafsi Yangu ya mwili, kama kitu kimoja kizima kisichogawanyika, na kufanya kuwa binadamu wote wataweza kuniridhisha mbele Yangu. 

1/08/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Tamko la Tano


Wakati Roho Wangu anatoa sauti, Anaonyesha hali nzima ya tabia Yangu. Je, wewe unalifahamu hili? Kutolifahamu hili katika hatua hii itakuwa sawa na kunipinga moja kwa moja. Je umeona umuhimu ulioko humu? Je, unajua juhudi kiasi gani, kiasi gani cha nguvu, Ninatumia juu yako? Je, unaweza thubutu kuweka wazi kila ulichofanya mbele Yangu?

1/07/2018

Mungu ni upendo | "Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu" | Best Swahili Gospel Worship Song



Utambulisho

Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu
Sasa kwa kushangilia sana, utakatifu wa Mungu na haki
vinakua ulimwenguni kote,
ikitukuka sana kati ya wanadamu wote.
Miji ya mbinguni inacheka, falme za dunia zinacheza.
Ni nani asiyesherehekea? Ni nani asiyetoa machozi?
Wanadamu hawagombani wala kupigana makonde;
jua linaaangaza kotekote.

1/06/2018

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mnapaswa Kuweka Pembeni Baraka za Hadhi na Kuelewa Mapenzi ya Mungu kwa ajili ya Wokovu wa Mwanadamu


Kwa mwanadamu, haiwezekani kwa wana wa Moabu kuwa wakamilifu na hawajahitimu kufanywa hivyo. Wana wa Daudi, kwa upande mwingine, hakika wana matumaini na hakika wanaweza kufanywa kamili. Kwa sharti kwamba mtu ni mzawa wa Moabu, basi hawezi kufanywa kamili. Hata leo, bado hamjui umuhimu wa kazi inayofanyika miongoni mwenu; mpaka katika hatua hii ya sasa bado mnashikilia matumaini yenu ya baadaye katika mioyo yenu na hamtaki kuyaacha.

1/05/2018

Nampenda Mungu kwa Moyo Wangu Wote | "Nitampenda Mungu Milele" Video Rasmi ya Muziki


Utambulisho


Nitampenda Mungu Milele
Ee Mungu! Maneno Yako yameniongoza kurudi Kwako.
Nakubali mafunzo katika ufalme Wako mchana na usiku.
Majaribio mengi na maumivu, mateso mengi sana.
Mara nyingi nilimwaga machozi na kuhisi huzuni,
na mara nyingi nimeanguka katika mtego wa Shetani.
Lakini Hujawahi kuniacha.

1/04/2018

Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu | Drama ya Muziki “ Kwaya ya Injili ya Kichina Onyesho la 19” | Haleluya



Utambulisho


   Chini ya mbingu ya usiku yenye nyota, tulivu na kimya, kundi la Wakristo wanasubiri kwa ari kurudi kwa Mwokozi wakiimba na kucheza kwa muziki mchangamfu.Wanaposikia habari za furaha "Mungu amerejea" na "Mungu ametamka maneno mapya", wanashangaa na kusisimka. Wanafikiri: "Mungu ameonekana? Tayari ametokea?" Kwa udadisi na kutokuwa na uhakika, mmoja baada ya mwingine, wanaingia katika safari ya kuyatafuta maneno mapya ya Mungu.

1/03/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (8)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (8)

Mwenyezi Mungu alisema, Sote tunaweza kuona katika uzoefu wetu wa utendaji kwamba kuna nyakati nyingi ambazo Mungu binafsi ametufungulia njia ili tuwe tunakanyaga njia iliyo imara zaidi, ya kweli zaidi. Hii ni kwa sababu hii ndiyo njia ambayo Mungu alitufungulia tangu mwanzo wa wakati na imepitishwa kwa kizazi chetu baada ya makumi ya maelfu ya miaka.

1/02/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (7)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia… (7)

Mwenyezi Mungu alisema, Sote tunaweza kuona katika uzoefu wetu wa utendaji kwamba kuna nyakati nyingi ambazo Mungu binafsi ametufungulia njia ili tuwe tunakanyaga njia iliyo imara zaidi, ya kweli zaidi. Hii ni kwa sababu hii ndiyo njia ambayo Mungu alitufungulia tangu mwanzo wa wakati na imepitishwa kwa kizazi chetu baada ya makumi ya maelfu ya miaka.

1/01/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (6)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Njia... (6)

Mwenyezi Mungu alisema, Ni kwa sababu ya kazi ya Mungu ndio tumeletwa katika siku hii. Kwa hiyo, sisi sote ni wasaliaji katika mpango wa usimamizi wa Mungu, na kwamba tunaweza kubakizwa mpaka siku hii ni kutiwa moyo kwa hali ya juu kutoka kwa Mungu. Kulingana na mpango wa Mungu, nchi ya joka kuu jekundu inapaswa kuangamizwa, lakini Ninadhani kwamba labda Ameanzisha mpango mwingine, au Anataka kutekeleza sehemu nyingine ya kazi Yake.