3/19/2018

Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wanaweza kupangwa kwa makundi, ambayo hubainishwa kwa roho zao. Watu wengine wana roho za binadamu, na wao huchaguliwa kwa njia iliyoamuliwa kabla. Ndani ya roho ya binadamu kuna sehemu iliyoamuliwa kabla. Watu wengine hawana roho; wao ni pepo ambao wamepenyeza. Hawajaamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu. Ingawa wamekuja ndani, hawawezi kuokolewa, na hatimaye wataondolewa na pepo. Inaamuliwa na asili ya ndani ya mtu huyo iwapo ataikubali kazi ya Mungu, au njia ipi atakayochukua au iwapo ataweza kubadilika baada ya kuikubali. Watu wengine hawana la kufanya ila kupotea. Roho zao huamua kwamba wao ni aina hii ya kitu; hawawezi kubadilika. Kuna watu ambao Roho Mtakatifu hukoma kufanya kazi kwa sababu watu hawa hawajachagua njia sahihi. Wakirudi Roho Mtakatifu huenda bado akafanya kazi Yake, lakini wakishikilia kutorudi basi wamemalizika kabisa. Kuna kila aina za hali. Ni jinsi gani mtu anapaswa kufahamu, ni jinsi gani mtu anapaswa kujua tabia ya haki ya Mungu? Ni jinsi gani mtu huja kuijua haki hii? Mtu mwenye haki hupokea baraka za Mungu, na mtu mwovu hupatwa na laana za Mungu. Hivyo ndivyo haki ya Mungu ilivyo, sivyo? Je, hivi ndivyo ilivyo? Nitawauliza ninyi, ikiwa mtu mwenye haki hajapokea baraka za Mungu, na hawezi kupata baraka za Mungu, na ikiwa Mungu hambariki, na mtu mwovu kinyume chake ni tajiri katika mali ya familia, ana watoto wengi, na kila kitu kinaendelea kwa urahisi na kwa mafanikio, je, hii ni haki ya Mungu? Ndiyo! Ni jinsi gani tunaeleza hili? Kuna msemo kwamba Mungu huwatuza wema na kuwaadhibu waovu, na kwamba kila mtu hupokea adhabu kulingana na matendo yake. Je, msemo huu ni sahihi? Sasa kuna jambo kama hili: Mtu anayemwabudu Mungu anauawa au analaaniwa na Mungu, au Mungu hajawahi kumbariki au kumzingatia, na ibada zaidi inapuuzwa. Kisha kuna mtu mwovu ambaye Mungu hajawahi kumbariki wala kumuadhibu, lakini yeye ni tajiri katika mali ya familia, ana watoto wengi, na kila kitu kinaendelea kwa urahisi na kwa mafanikio. Watu wengine husema: "Mungu si mwenye haki. Sisi humwabudu Yeye, ilhali hatujapokea baraka Zake. Mtu mwovu, kwa hali yoyote, ambaye hajamwabudu Yeye lakini alimpinga Yeye, ni bora kuliko sisi katika kila jambo, yuko juu kuliko tulivyo. Mungu si mwenye haki!" Je, jambo hili linawaruhusu ninyi kuona nini? Kati ya mifano miwili ambayo Nimetoa, ni upi unaeleza kwa mfano haki ya Mungu? Watu wengine husema: "Yote miwili ni haki ya Mungu!" Mbona weseme hivi? Ufahamu ambao watu wanao kuhusu tabia ya Mungu ni wenye kosa. Kujua kote kwa mwanadamu kuko ndani ya fikira na mtazamo wake, kutokana na msimamo wa biashara, au kutokana na mtazamo wa mazuri na maovu au sahihi na isiyo sahihi, au kutokana na mtazamo wa mantiki. Ukijishughulisha na kumjua Mungu huku unashikilia mitazamo hii, hakutakuwa na njia yoyote ya wewe kupatana na Mungu, na bado utampinga Mungu, na kulalamika. Kulikuwa na ombaomba aliyeonekana kuwa mpumbavu. Yeye alijua tu kumwabudu Mungu, lakini Mungu alimpuuza tu, Mungu hakumbariki. Labda mnafikiri, "Hata kama Mungu hatambariki katika ulimwengu ujao, bila shaka Mungu atambariki katika ahera na kumtuza mara elfu kumi zaidi. Je, hilo halitamfanya Mungu kuwa mwenye haki? Mtu huyo tajiri, anafurahia baraka mara mia, na katika maisha ya baadaye anafishwa. Je, hii pia si haki ya Mungu?" Ni vipi ambavyo mtu anapaswa kufahamu haki? Chukua, kwa mfano, kuijua kazi ya Mungu. Kama Mungu angefanya tu kazi mpaka Enzi ya Neema, na hakutekeleza hatua hii ya mwisho ya kazi, na watu wote wakafishwa, je, upendo wa Mungu uko ndani ya hili? Tuseme kwamba mtu anayemwabudu Mungu anatupwa ndani ya ziwa la moto wa jahanamu, na mtu mwingine asiyemwabudu Mungu au asiyemjua Mungu, na Mungu anamruhusu mtu huyo kubaki, ni vipi ambavyo tutalishughulikia hili? Je, kuna haki ndani ya hili? Kile watu husema ni kuhusu tu kujua mafundisho ya dini. Uhalisi unapopitiwa huwa kuna kuchangayikiwa. Mbona isemekane kwamba Mungu anampenda mwanadamu, na kwamba Mungu ni mwenye haki? Hiki ni kitu ambacho lazima mtu akifahamu kwa ukamilifu. Kulingana na dhana za binadamu, mazuri hutuzwa na maovu huadhibiwa, watu waovu hawatakiwi kupokea tuzo, na wale wasiofanya maovu yoyote wanapaswa wote kupokea tuzo, na kubarikiwa, kwa sababu Mungu ni mwenye haki. Inaonekana kwamba watu wanapaswa kupokea wanachostahili, na kwamba Mungu husemekana kuwa mwenye haki tu watu wanapopokea wanachostahili. Itakuwaje iwapo mtu hatapata sehemu yake? Je, unapaswa basi kusema kwamba Mungu si mwenye haki? Tuseme kwamba watu katika enzi hii wangeona maelezo katika kitabu yanayosema kwamba Mungu aliumba kabila la wanadamu katika enzi iliyotangulia. Baada ya kupita maelfu ya miaka, Mungu anaona kwamba watu wamekuwa wapotovu kupindukia, na Yeye hana hali ya moyo ya kuwaokoa na kwa hivyo anawaangamiza. Ni vipi ambavyo ungeliangalia jambo hili? Je, ungesema kwamba Mungu hana upendo? Kama wanavyoona watu, Mungu aliwaangamiza watu katika enzi iliyotangulia, hivyo Mungu hakuwa na upendo. Ufahamu wa Mungu si kusema hiki au kile kumhusu Mungu kulingana na vile binadamu huvitazama vitu. Hakuna ukweli katika njia ambayo binadamu huvitazama vitu. Lazima uone kiini cha Mungu ni nini, tabia ya Mungu ni gani. Watu hawapaswi kuona kiini cha Mungu kulingana na mambo yaliyo nje ya kile ambacho Mungu amefanya au ameshughulikia. Kabila la binadamu lenyewe limepotoshwa na Shetani. Kimsingi halijui asili yake ni nini, au kabila la binadamu lililopotoshwa ni nini mbele ya Mungu, na jinsi linapaswa kushughulikiwa. Fikiria juu ya Ayubu, mtu mwenye haki aliyebarikiwa na Mungu. Hii ni haki ya Mungu. Ayubu anapitia majaribu, na Shetani anaweka dau na Yehova: Kwa nini Ayubu anakuabudu Wewe? Ni kwa sababu Wewe humpa tuzo kama hizi. Ukiondoa vitu hivyo vyote kutoka kwake, je, bado atakuabudu Wewe? Yehova Mungu akasema, "Maadamu hutauchukua uhai wake, unaweza kufanya chochote upendacho." Shetani alimwendea Ayubu na baadaye Ayubu alipitia majaribu. Kila kitu alichokuwa nacho kilichukuliwa, na watoto wake wakafa. Je, tabia ya haki ya Mungu iko ndani ya majaribu ya Ayubu? Ndiyo! Wapi? Huwezi kueleza, sivyo? Hata kama wewe ni mtu mwenye haki, Mungu bado ana haki ya kukujaribu, na kukuruhusu kuwa shahidi wa Mungu. Tabia ya Mungu ni yenye haki. Yeye humtendea kila mtu kwa hali sawa, ambayo haimaanishi kwamba kwa sababu mtu mwenye haki anaweza kustahimili majaribu kwamba hatakiwi kuyapitia, kwamba mtu mwenye haki anatakiwa kuhifadhiwa. Sio hivyo. Ana haki ya kukujaribu. Haya ni maonyesho ya tabia Yake ya haki. Mwishowe, baada ya Ayubu kupitia majaribu na kuwa na ushuhuda wa Yehova, Yeye alimbariki hata zaidi ya hapo awali, Akimbariki maradufu na bora zaidi. Zaidi ya hayo, Yehova alionekana mbele yake, na Akanena naye katika upepo, kama kwamba Ayubu alimwona Yeye ana kwa ana. Hii ni baraka aliyopewa, sio? Hii ni haki ya Mungu. Itakuwaje ikiwa ni kinyume? Yehova alimwona Ayubu akiyakubali majaribu haya, akiwa na ushuhuda Wake mbele ya Shetani, na kumuaibisha Shetani. Lakini Yehova aligeuka na kuondoka, akimpuuza. Ayubu hakupata baraka baadaye. Je, haki ya Mungu iko ndani ya hili? Bila kujali iwapo Ayubu alibarikiwa baada ya majaribu au la, au iwapo Yehova alijitokeza mbele yake au la, haya yote yana makusudi mema ya Mungu. Kujitokeza mbele yake ni haki ya Mungu, na kutojitokeza mbele yake pia ni haki ya Mungu. Kama sehemu ya viumbe, ni kwa msingi gani ambao wewe humtaka Mungu akufanyie jambo? Mwanadamu hastahili kumtaka Mungu amfanyie jambo. Kumtaka Mungu akufanyie jambo ni hali isiyo na busara kabisa. Mungu atafanya kile Anachotaka, na Mungu ana haki ya kutofanya jambo hilo kwa njia hii. Ana haki ya kuyashughulikia mambo haya Yeye mwenyewe. Tabia Yake mwenyewe ni yenye haki. Haki kamwe sio adilifu na ya maana, kugawa moja mara mbili, kukufidia wewe kulingana na kiasi cha kazi unayofanya au kukulipa kwa kiasi cha kazi ambayo umeifanya. Hii si haki ya Mungu. Unaamini kwamba kila mtu hufanya sehemu yake, na mgawanyo kulingana na kazi iliyofanywa, na kwamba kila mtu hupokea haki yake kulingana na matokeo ya kazi yake; hii yenyewe ndio haki. Tuseme Mungu angemwangamiza Ayubu baada ya Ayubu kuwa na ushuhuda Wake. Mungu ni mwenye haki hapa, pia. Kwa nini tuseme kwamba Yeye ni mwenye haki? Kusema kwamba Mungu ni mwenye haki katika kufanya hili, kwa nini tuseme jambo kama hili? Haki ni kitu ambacho ikiwa jambo fulani linalingana na dhana za watu, watu husema Mungu ni mwenye haki, ambalo ni rahisi kiasi, lakini ikiwa watu hawaoni kwamba linalingana na dhana zao, ikiwa ni jambo ambalo watu hawawezi kulifahamu, hilo lingehitaji juhudi kubwa ya watu kulieleza hilo kama haki. Kama angemwangamiza Ayubu wakati huo, watu hawangesema kwamba Mungu alikuwa mwenye haki. Hata kama kungekuwa na watu ambao wangesema alikuwa mwenye haki, wangesema hivyo kwa kutotaka: "Yehova Mungu yuko sawa...." Kwa kweli ikiwa watu wanaangamizwa na Mungu, iwapo wamepotoshwa au la, je, ni lazima Mungu awaeleze sababu za kuwaangamiza watu? Je, Anapaswa kuwaeleza watu msingi Wake wa kuwaangamiza? Hakungekuwa na haja, sivyo? Je, inahitajika kulingana na kuwahifadhi watu wenye maana, na kumtoa mtu asiye na maana? Haihitaji. Machoni pa Mungu mtu mpotovu anaweza kushughulikiwa vile Apendavyo. Kwa hali yoyote inavyofanywa ni ya kufaa; yote ni katika mpango Wake. Ikiwa haifurahishi machoni Pake, wewe huna maana baada ya kuwa na ushuhuda na ukatolewa, je, hii ni haki? Ni haki. Ingawa katika uhalisi hili si rahisi kufahamu, lazima uwe na ufahamu kwa jumla. Niambie, je, Mungu kumwangamiza Shetani ni haki? Iwapo angemhurumia Shetani? Labda huthubutu kusema? Ni vipi ambavyo ni haki? Kiini cha Mungu ni haki. Ingawa si rahisi kufahamu yale afanyayo Mungu, yote Afanyayo ni yenye haki. Ni kawaida kwamba watu hawafahamu, hakuna kosa kuhusu hilo. Unaona kwamba Mungu alipomtoa Petro kwa Shetani, vile Petro alijibu: "Mwanadamu hawezi kuelewa maana ya kile unachofanya, lakini yote ambayo Wewe hufanya yana makusudi yako mema. Kuna haki ndani ya hayo yote. Ninawezaje kukosa kutamka sifa kwa ajili ya matendo Yako ya hekima?" Sasa unapaswa kutambua kwamba Mungu hamwondoi Shetani mara moja, ili kwamba mwanadamu aweze kuona jinsi Shetani amewapotosha watu, na jinsi Mungu amewaokoa watu. Ni baada tu ya mwanadamu kuweza kuona kiasi cha Shetani kumpotosha mwanadamu, jinsi orodha ya Shetani ya uhalifu inafika mbinguni ndipo Mungu hatimaye atamwondoa Shetani, ili watu waweze kuona kwamba humo mna haki ya Mungu na tabia Yake. Kila jambo afanyalo Mungu ni haki. Ingawa huwezi kulitambua, hupaswi kufanya hukumu jinsi upendavyo. Likionekana kwako kuwa bila mantiki, au kama una dhana kulihusu, na kisha useme kwamba Mungu si mwenye haki, hili ni la kukosa busara kabisa. Sasa hivi Nimetoa mifano michache mibaya ili mtofautishe, nanyi hamthubutu kuzungumza. Unaona kwamba Petro alipata kwamba mambo mengine hayafahamiki, ilhali alikuwa na hakika kwamba hekima ya Mungu ilikuwa hapa, kwamba makusudi mema ya Mungu yalikuwa katika hilo lote. Mwanadamu hawezi kuelewa kila jambo. Kuna mambo mengi sana yasiyoeleweka. Kujua tabia ya Mungu kwa kweli si jambo rahisi.
Watu wengine walichoma vitabu na waliadhibiwa moja kwa moja. Watu wengine walitangaza Mungu kuwa mwenye hatia na waliadhibiwa. Kuna mifano mingi ya aina hii. Waumini wapya wanapoyasikia mambo haya hawawezi kuyakubali, wakiwa na dhana. Mungu huona kwamba wewe ni mshenzi na hukosa kukuzingatia. Je, unadhani kwamba hawezi kulielewa? Ikiwa waumini wa muda mrefu wako hivi, halikubaliki, bila kujali ni miaka mingapi wameshirikiana na au kumfuata Yeye. Waumini wapya ni mafidhuli na wenye kiburi, hivyo Yeye hakutilii wewe maanani. Kutakuja kuwa na siku ambapo utajigundulia mwenyewe. Ikiwa utafuata kwa miaka mingi na bado uwe na dhana ambazo hutaachilia, ukibeza, ukidhihaki, ukidharau, na kutawanya mawazo kila mahali, unapaswa kushughulikiwa kwa adhabu. Katika mambo mengine unasamehewa kwa kuwa mpumbavu na mjinga, lakini iwapo unajua na bado unatenda kwa njia hiyo kwa makusudi, na husikilizi kwa vyovyote vile, basi utapata adhabu. Unajua tu upande wa Mungu wenye huruma kwa watu. Usisahau kwamba Mungu pia ana upande usiovumilia kosa kutoka kwa watu.
kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni