Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Kuwapata Wale Wanaomjua Mungu na Wanaweza Kumtolea Ushuhuda Ndilo Tamanio la Mungu Lisilobadilika
Kuwapata Wale Wanaomjua Mungu na Wanaweza Kumtolea Ushuhuda Ndilo Tamanio la Mungu Lisilobadilika
Wakati huohuo Alipokuwa akijizungumzia Mwenyewe, Mungu alizungumza pia na Ibrahimu, lakini mbali na kusikiliza baraka ambazo Mungu alimpa, Ibrahimu aliweza kuyaelewa matamanio ya kweli ya Mungu katika maneno Yake yote wakati huo?
Hakuweza! Na hivyo, kwa wakati huo, wakati Mungu alipoapa kwa nafsi Yake Mwenyewe, moyo Wake ulikuwa bado pweke na wenye huzuni. Hakukuwepo hata na mtu mmoja wa kuweza kuelewa au kufahamu kile Alichonuia na Alichopangilia. Wakati huo, hakuna—akiwemo Ibrahimu—aliyeweza kuongea na Yeye kwa ujasiri, isitoshe hakuna yule aliyeweza kushirikiana na Yeye katika kufanya kazi ambayo lazima Angefanya. Juujuu, Mungu alikuwa Amempata Ibrahimu na Alipata mtu ambaye angetii maneno Yake. Lakini kwa hakika, maarifa ya mtu huyu kuhusu Mungu yalikuwa kidogo mno. Hata ingawaje Mungu alikuwa amembariki Ibrahimu, moyo wa Mungu ulikuwa bado hujatosheka. Inamaanisha nini kwamba Mungu hakuwa ametosheka? Inamaanisha kwamba usimamizi Wake ulikuwa tu umeanza, inamaanisha kwamba watu Aliotaka kupata, watu Aliotamani kuona, watu Aliopenda, walikuwa bado mbali na Yeye; Alihitaji muda, Alihitaji kusubiri, Alihitaji kuwa na subira. Kwani kwa wakati huo, mbali na Mungu Mwenyewe, hakuna yeyote yule aliyejua kile Alichohitaji au kile Alichotaka kupata, au kile Alichotamani. Na hivyo basi, Kwa wakati uohuo aliokuwa akihisi sana furaha Mungu pia alihisi kuwa mwenye uzito wa moyo. Bado Hakusitisha hatua Zake, na Aliendelea kupanga hatua inayofuata ya kile ambacho lazima Afanye.
Unaona nini katika ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu? Mungu alimpa baraka kuu Ibrahimu kwa sababu tu ya yeye kusikiliza maneno ya Mungu. Ingawaje, juujuu, hali hii yaonekana ya kawaida na suala ambalo bila shaka, ndani yake tunauona moyo wa Mungu: Mungu hasa anathamini utiifu wa binadamu kwake Yeye, na hutunzwa mno na uelewa wa binadamu kuhusu Yeye na uaminifu wake Kwake. Mungu anathamini kiasi kipi uaminifu huu? Huenda usielewe ni kiasi kipi ambacho Yeye Anauthamini, na huenda hata kusiwe na yeyote anayeutambua. Mungu alimpa Ibrahimu mwana, na wakati mwana huyo alipokua, Mungu alimwomba Ibrahimu kumkabidhi mtoto wake Kwake. Ibrahimu alifuata amri ya Mungu kwa umakinifu, alitii neno la Mungu na uaminifu wake ulimpendeza Mungu na ukathaminiwa sana na Mungu. Mungu aliuthamini kiasi kipi? Na kwa nini Akauthamini sana? Kwa wakati ambao hakuna aliyefahamu maneno ya Mungu au kuuelewa moyo Wake, Ibrahimu alifanya kitu kilichotikisa mbingu na kutetemesha ardhi, na kikafanya Mungu kuhisi hali fulani ya kutosheka kwa mara ya kwanza, kikamletea Mungu furaha ya kumpata mtu ambaye aliweza kutii maneno Yake. Uradhi na furaha hii ilitoka kwa kiumbe aliyeumbwa kwa mkono ya Mungu, na ndiyo iliyokuwa “sadaka” ya kwanza ambayo binadamu aliwahi kumpa Mungu na ambayo ilithaminiwa sana na Mungu, tangu binadamu kuumbwa. Mungu alikuwa na wakati mgumu kusubiria sadaka hii, na Aliichukulia kama zawadi ya kwanza muhimu zaidi kutoka kwa binadamu, ambaye Alikuwa amemuumba. Hii ilionyesha Mungu tunda la kwanza la jitihada Zake, na gharama ambayo Alikuwa amelipia na ikamruhusu Yeye kuliona tumaini kwa wanadamu. Baadaye, Mungu alikuwa na hata tamanio kubwa zaidi la kundi la watu kama hao wa kushinda na Yeye kumchukulia Yeye kwa uaminifu, kumtunza Yeye kwa uaminifu. Mungu alitamani hata kwamba Ibrahimu angeendelea kuishi, kwani Alipenda kuwa na moyo kama huo ukiandamana na Yeye na kuwa na Yeye Alipoendelea na usimamizi Wake. Haijalishi ni nini alichotaka Mungu, yalikuwa tu ni matakwa, wazo tu—kwani Ibrahimu alikuwa tu binadamu aliyeweza kumtii Yeye, na wala hakuwa na uelewa au maarifa hata madogo zaidi kuhusu Mungu. Yeye alikuwa mtu aliyepungukiwa pakubwa na viwango vya mahitaji ya Mungu kwa binadamu: kumjua Mungu, kuweza kushuhudia Mungu, na kuwa na akili sawa na Mungu. Na hivyo, hangeweza kutembea na Mungu. Katika sadaka ya Ibrahimu ya Isaka, Mungu aliuona uaminifu na utiifu huu wa Ibrahimu, na Akaona kwamba alikuwa amestahimili jaribio la Mungu kwake yeye. Hata ingawaje Mungu aliukubali uaminifu na utiifu wake, bado hakustahili kuwa mwandani wa Mungu, wa kuwa mtu aliyemjua Mungu, na kumwelewa Mungu, na alifahamishwa kuhusu tabia ya Mungu; alikuwa mbali sana na kuwa na akili sawa na Mungu na vilevile kuweza kutekeleza mapenzi ya Mungu. Hivyo basi, katika moyo Wake, Mungu alikuwa bado mpweke na mwenye wasiwasi. Kwa kadri Mungu alipokuwa mpweke na mwenye wasiwasi zaidi, ndipo Yeye alipohitaji zaidi kuendelea na usimamizi Wake haraka iwezekanavyo, na kuweza kuchagua na kulipata kundi la watu wa kukamilisha mpango Wake wa usimamizi na kutimiza mapenzi Yake haraka iwezekanavyo. Hili ndilo lilikuwa tamanio lenye hamu kubwa la Mungu, na limebakia vilevile kuanzia mwanzo kabisa hadi leo. Tangu Alipomuumba binadamu hapo mwanzo, Mungu ametamani kuwa na kundi la washindi, kundi ambalo litatembea na Yeye na linaweza kuelewa, kufahamu na kujua tabia Yake. Mapenzi haya ya Mungu hayajawahi kubadilika. Haijalishi ni muda gani bado Atasubiria, haijalishi barabara iliyo mbele ni ngumu kiasi gani, hata malengo Anayoyatamani yawe mbali kiasi kipi, Mungu hajawahi kubadilisha au kukata tamaa katika matarajio Yake kuhusu binadamu. Kwa vile nimeyasema haya, unatambua chochote kuhusu mapenzi ya Mungu? Pengine kile ulichotambua hakina uzito sana—lakini kitajitokeza kwa utaratibu!
Kwenye kipindi sawa na kile cha Ibrahimu, Mungu pia aliliangamiza jiji. Jiji hili liliitwa Sodoma. Bila shaka, watu wengi wanaijua hadithi ya Sodoma, lakini hakuna yeyote aliyejua fikira za Mungu zilikuwa usuli wa kuangamiza Kwake jiji hili.
Na hivyo leo, kupitia mazungumzo yake Mungu na Ibrahimu hapa chini, tutajifunza fikira Zake wakati huo, huku pia tukijifunza kuhusu tabia Yake. Kinachofuata, hebu tusome vifungu vya maandiko.
B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma.
(Mwa 18:26) Kisha BWANA akasema, Nikipata katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, basi Nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
(Mwa 18:29) Na akazungumza tena naye, akasema, Huenda wakapatikana humo arobaini. Akasema, Sitafanya hivyo.
(Mwa 18:30) Akamwambia, labda watapatikana huko thelathini. Naye akasema, Sitafanya hivyo.
(Mwa 18:31) Kisha akasema, huenda wakaonekana huko ishirini. Naye akasema, Sitauharibu.
(Mwa 18:32) Naye akasema, huenda wakaonekana huko kumi. Naye akasema, Sitauharibu.
Hizi ni dondoo chache Nilizochagua kutoka kwenye Biblia. Dondoo hizi si kamilifu, za matoleo ya awali. Kama mngependa kuziona hizo, mnaweza kuzitafuta kwenye Biblia nyinyi wenyewe; ili kuokoa muda, Nimeiacha sehemu ya maudhui asilia. Hapa Nimechagua tu vifungu na sentensi mbalimbali kuu, huku nikiziacha sentensi mbalimbali ambazo hazina umuhimu katika ushirika wetu wa leo. Katika vifungu na maudhui yote tunayotumia katika ushirika, zingatio letu haliyaendei maelezo ya hadithi na mwenendo wa binadamu katika hadithi hizi; badala yake, tunazungumzia tu fikira za Mungu na mawazo Yake wakati huo. Katika fikira na mawazo ya Mungu, tutaiona tabia ya Mungu, na kutoka katika kila kitu alichofanya Mungu, tutaweza kumuona Mungu Mwenyewe wa kweli—na katika haya tutaweza kutimiza malengo yetu.
Juni 13, 2014
Tanbihi:
a. Maandishi asilia yanasoma “vitendo.”
b. Maandishi asilia yameacha “kichwa cha.”
c. Maandishi asilia yameacha “kupotezwa kwa.”
d. Maandishi asilia yameacha “ yaliyokuwa yameenda.”
e. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni