7/24/2018

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Kutotikisika kwa Uadilifu wa Ayubu Kunaleta Aibu Kwake Shetani na Kusababisha Shetani Kutoroka kwa Wasiwasi

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II - Kutotikisika kwa Uadilifu wa Ayubu Kunaleta Aibu Kwake Shetani na Kusababisha Shetani Kutoroka kwa Wasiwasi

Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kutotikisika kwa Uadilifu wa Ayubu Kunaleta Aibu Kwake Shetani na Kusababisha Shetani Kutoroka kwa Wasiwasi

Na ni nini ambacho Mungu alifanya wakati Ayubu alipopitia mateso haya? Mungu aliangalia, na kutazama, na Akasubiri matokeo. Wakati Mungu Alipokuwa akiangalia na kutazama, Alihisi vipi? Alihisi kuwa mwenye huzuni, bila shaka. Lakini, kutokana na huzuni Yake, Aliweza kujuta ruhusa Yake kwa Shetani ya kumjaribu Ayubu? Jibu ni, La, Asingefanya hivyo. Kwani Yeye alisadiki kwa dhati kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alikuwa amempa Shetani tu fursa ya kuthibitisha uhaki wa Ayubu mbele ya Mungu, na kufichua maovu yake Shetani na hali ya kudharauliwa kwake binafsi. Ilikuwa, zaidi ya hapo, fursa ya Ayubu kutolea ushuhuda utakatifu wake na kumcha Mungu kwake na kujiepusha na maovu mbele ya watu wa ulimwengu, Shetani, na hata wale wanaomfuata Mungu. Je, matokeo ya mwisho yalithibitisha kwamba ukadiriaji wa Mungu kuhusu Ayubu ulikuwa sahihi na bila makosa? Je, Ayubu alimshinda kweli Shetani? Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: “Nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile.”Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe.” Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, kwamba Anaweza kuangalia kwenye akili ya binadamu, na yanathibitisha kwamba kuidhinisha kwake kwa Ayubu hakuna kosa, kwamba binadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. “…BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe.”Maneno haya ni ushuhuda wa Ayubu kwa Mungu. Yalikuwa maneno haya ya kawaida yaliyomfanya Shetani kuogopa, yaliyoleta aibu kwake na kumsababisha kutoroka kwa wasiwasi, na, vilevile, yaliyomfunga pingu Shetani na kumuacha bila rasilimali zozote. Hivyo, pia, ndivyo maneno haya yalivyomfanya Shetani kuhisi matendo ya kustaajabisha na yenye nguvu ya Yehova Mungu, na kumruhusu kuelewa haiba kubwa na isiyo ya kawaida ya yule ambaye moyo wake ulitawaliwa na njia ya Mungu. Zaidi, yalionyesha Shetani nguvu za kipekee zilizoonyeshwa na mtu mdogo asiyekuwa na umuhimu wowote katika kutii njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu Shetani hivyo basi alishindwa kwenye shindano la kwanza. Licha ya utambuzi wake “uliopatikana kwa hali ngumu,” Shetani hakuwa na nia ya kumwachilia Ayubu, wala hakukuwa na badiliko lolote katika asili yake ya unafiki. Shetani alijaribu kuendelea kumshambulia Ayubu, na kwa mara nyingine tena akamjia Mungu …
Kisha, hebu tuyasome maandiko kuhusu mara ya pili ambapo Ayubu alijaribiwa.
3. Shetani Amjaribu Ayubu Mara Nyingine Tena (Majipu Mabaya Yaupiga Mwili wa Ayubu)
a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu
(Ayubu 2:3) BWANA akamwuliza Shetani, je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.
(Ayubu 2:6) BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini uutunze uhai wake.
b. Maneno Yaliyotamkwa na Shetani
(Ayubu 2:4-5) Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele ya uso wako.
c. Namna Ayubu Anavyoshughulikia Majaribio
(Ayubu 2:9-10) Kisha mkewe akamwambia, Je, Wewe bado unashikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ufe. Lakini yeye akamwambia, Wewe unazungumza kama mmoja wa wanawake wapumbavu wanavyozungumza. Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika yote haya Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
(Ayubu 3:3) ) Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba.
...

Juni 13, 2014
Tanbihi:
a. Maandishi asilia yanasoma “vitendo.”
b. Maandishi asilia yameacha “kichwa cha.”
c. Maandishi asilia yameacha “kupotezwa kwa.”
d. Maandishi asilia yameacha “ yaliyokuwa yameenda.”
e. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili


Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kujua Umeme wa Mashariki, Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni