9/16/2018

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kuwafundisha Wanangu (I)

Maneno ya Mungu Huniongoza Kujifunza Jinsi ya Kuwafundisha Wanangu (I)

Xiaoxue, Malesia
Nina wana wawili wa kiume na wameachana na mwaka mmoja. Ili kuwalea kuwa watu waliostaarabika, wenye tabia nzuri, watu wema ambao wataweza watajijengea jina katika jamii na kufanikiwa, walipokuwa na umri wa miaka miwili, nilijadiliana na mume wangu juu ya kuwatafutia shule nzuri ya chekechea. Baada ya ziara kadhaa, maulizo na kulinganisha, tulichagua shule ya chekechea ya Kiingereza kwa sababu waliweka umuhimu juu ya ubora wa tabia au akili na uwezo wa watoto, ambao ulifanana na mtazamo wangu juu ya kufundisha watoto. Ingawa ada za masomo zilikuwa za juu kiasi, alimradi watoto waliweza kuendeleza vizuri na kupata elimu bora, lilikuwa la thamani kutumia pesa zaidi kidogo.

Kanisa la Mwenyezi Mungu, ushuhuda, Umeme wa Mashariki


Wanangu walipokua hatua kwa hatua, nilitambua kwamba hawakuwa na busara na utii kama nilivyokuwa nimetarajia. Kinyume chake, walikuwa wadhalimu na waasi mno. Kwa mfano, nilipowapeleka kwa jengo la maduka, walipoona kitu walichopenda, walikichukua tu na kama sikuwanunulia, wangelala sakafuni na kulia na kufanya fujo. Walipocheza na watoto wengine, kama waliona kitu ambacho walipenda, wangekinyakua kutoka kwa hao watoto. Kama hao watoto wengine hawakuwapa hicho, wangewapiga. Nikiona wanangu wakiwa vigeugeu na wadhalimu sana, niliwakaripia kwa nguvu kila wakati. Hata hivyo, hilo halikukosa ufanisi tu, lakini wanangu waliendelea kutokuwa watiifu zaidi na zaidi. Mara nilipowakaripia, wangetupa nguo na viatu vyao katika jaa la taka. Walipokasirika, wangechukua mkasi na kukatakata nguo zao, mashuka ya kulalia na mito. Nilihisi huzuni sana kuhusu hili. Wanangu wangewezaje kuwa wenye kiburi na tabia mbaya hivyo? Nilipendekeza wabadilishae shule lakini mume wangu hakukubali. Alisema kuwa watoto wanafaa kukua kwa kawaida na kwa hiari. Mtazamo wa mume wangu kwa wanangu ulinikasirisha sana: Mtoto bora sana analelewa, sio kuachwa aendelee kienyeji. Ni nani anayejua jinsi watakavyokuwa ukiwaacha kukua kwa kujitegemea! Lakini bila kujali jinsi nilivyomshawishi, mume wangu bado alisisitiza maoni yake. Nilihisi huzuni mno kumwona mume wangu kama baba akiwa mtu asiyewajibika hivyo. Kama tungeendelea jinsi hii, watoto wetu wangekuwaje katika siku za baadaye! Nilivyozidi kufikiri juu ya hili, ndivyo nilivyozidi kuwa na wasiwasi, na sikujua cha kufanya. Nilihisi kuchanganyikiwa kwa mintarafu ya cha kufanya kuhusu elimu ya wanangu na nilihisi kuteseka na mwenye wasiwasi.
Katika mwezi wa Machi ya mwaka wa 2017, niliikubali injili ya ufalme wa Mwenyezi Mungu. Siku moja katika mwezi wa Juni mwaka huo, niliona kuwa maneno ya Mwenyezi Mungu yalisema: “Mbali na kuzaliwa na kulea watoto, jukumu la kila mzazi katika maisha ya mtoto ni kuweza kuwapatia tu mazingira rasmi ya kukulia ndani, bila malipo yoyote isipokuwa kule kuamuliwa kabla kwa Muumba ambako kunachukua mwelekeo katika hatima ya mtu huyu husika. Hakuna anayeweza kudhibiti ni mustakabali gani ambao mtu atakuwa nao; huwa umeamuliwa kabla na mapema sana, na hata wazazi wa mtu hawawezi kubadilisha hatima yake. Kulingana na mambo ya hatima, kila mtu yuko huru na kila mtu anayo hatima yake. Kwa hivyo hakuna wazazi wa mtu yeyote wanaweza kuiondoa hatima ya mtu katika maisha au kusisitizia ushawishi wowote ule mdogo katika wajibu ambao mtu huendeleza maishani. Inaweza kusemekana kwamba, familia ambayo mtu ameamuliwa kuzaliwa ndani, na mazingira ambayo mtu atakulia ndani, ni yale masharti ya awali ya kutimiza kazi maalum ya mtu maishani” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilipoona maneno ya Mungu nilitambua kwamba ingawa sisi ni wazazi wa watoto, sisi huwazaa tu, kuwalea na kuwapa mazingira ya kukulia. Kwa mintarafu ya jinsi mustakabali wao utakavyokuwa, aina gani ya jukumu watakalochukua na ni miito gani watakayotimiza, haya yote yako mikononi mwa Mungu. Ni Mungu ambaye husimamia majaliwa yao na ambaye huamua mustakabali wao, sio wazazi wao. Kitu cha pekee ninachoweza kufanya ni kumwomba Mungu, kuwaaminia wanangu kwa Mungu na kutumaini kwamba Mungu atawaongoza kukua. Pia nilitafakari juu ya jinsi nilivyowashughulikia wanangu. Daima nilikuwa nikitumia uwezo wangu kuwadhibiti kwa nguvu na kuweka mkazo kwa wanangu na wakati wowote nilipowaona wanangu wakikosa kutii, ningewapiga, nikidhani kuwa ningebadili tabia zao mbaya na kuboresha akili zao kwa njia hii. Lakini sio tu kwamba wanangu hawakugeuka kuwa wasikivu na wa busara, kwa kweli walikuwa wakaidi zaidi na zaidi. Sasa inaonekana kama sikuelewa ukweli na sikujua utawala na mipango ya Mungu, hivyo singeweza kuwaelimisha wanangu, sembuse kuwaruhusu wakue kwa afya. Ninafaa kubadilisha utaratibu wangu wa kuwaelimisha na kuwatendea kwa mtazamo sahihi. Baada ya hili, wanangu walipofanya makosa, nilizungumza nao kwa uvumilivu na kuwafanya wajue makosa yao wenyewe. Nilipowaona wakiinamisha vichwa vyao na kuacha kuzungumza, sikuwakaripia tena. Wakati mwingine walikuwa watundu mno na ningewaadhibu kidogo na kuwataka kuukabili ukuta na kutafakari juu ya matendo yao. Hatua kwa hatua, nikagundua kuwa walikuwa watulivu zaidi kuliko hapo awali na kwamba hawakuwapiga tena watoto wengine na ni mara chache walitukana na kutoa matusi. Nilipowaona wanangu wakianza kuendeleza vizuri, nilijihisi mwenye shukurani sana na nilijua kwamba haya yote yalikuwa ni kwa sababu ya maneno ya Mungu na kwa dhati nilimshukuru Mungu!
Katika mwezi wa Novemba mwaka wa 2017, wakati mwanangu wa kwanza wa kiume alipokuwa karibu kumaliza shule ya chekechea na kuendelea kwa darasa la kwanza, mume wangu nami tulimchagulia shule maarufu ya msingi, tukitarajia kuwa angesoma kwa bidii na kufanikisha matokeo mazuri siku za baadaye. Katikati ya mwezi wa Julai, tulimpeleka mtoto wetu kufanya majaribio ya kuingia shule mapema . Baada ya mitihani, mkuu wa shule aliniita na kusema kuwa pointi za  mwanangu zilikuwa mbaya sana katika idadi kubwa ya watoto na kwamba hangeweza kuendelea sambamba na darasa la kwanza. Pia alisema kuwa wangeandaa majaribio ya pili. Niliposikia habari hii, nilijihisi kutotulia kidogo, lakini mume wangu nami bado tulimpeleka mtoto wetu kufanya tena mtihani wa kuingia shule. Matokeo ya mtihani yalipotangaza, nilipigwa na bumbuwazi: Mwanangu alikuwa amekaa muda wa miaka tatu katika shule ya chekechea lakini alikuwa hajajifunza chochote. Hakuweza hata kusoma au kuandika alfabeti na hakuelewa kujumlisha na kutoa hesabu ya tarakimu moja. Mwanangu alikuwa karibu kuanza darasa la kwanza na matokeo yake yalikuwa mabaya sana bila kutarajiwa—singeweza kuamini matokeo hayo. Mkuu wa shule pia alinikaripia na kusema: “Je, una shughuli nyingi sana? Ingawa unatoka China, Kichina cha mtoto wako ni kibaya sana; wewe humfundishaje?” Karipio hilo la mkuu wa shule lilinifanya nione aibu sana. Ilikuwa ni mara ya kwanza ambapo nilihisi kushindwa kama mama. Nilihisi aibu mno kiasi kwamba sikutaka kumwona mtu yeyote na nilitaka sana kujificha.
Niliporudi nyumbani alasiri hiyo, mume wangu alinitaka nimtafutie mwanangu shule ya chekechea kwa haraka. Mara niliposikia jambo hili, hasira niliyoiweka ndani mara moja iliibuka na nilishindwa kuzuia ghadhabu na kuanza kukasirikia tena wanangu. Niliwaambia walale haraka na kisha nikakimbia kwa chumba kidogo peke yangu, nikafunga madirisha na mapazia, nikalala kitandani na kutofikiria chochote. Hivi ndivyo nilivyolala kama nimechanganyikiwa. Mpaka saa kumi na mbili jioni hiyo, nilihisi kufadhaika sana na sikuweza kuyazuia machozi. Sikuwa hata na motisha ya kupika mlo mkuu wa siku. Nikiwa nimekabiliwa na matokeo kama hayo, nafaa kufanya nini? Katika kuteseka, nilipiga magoti mbele ya Mungu na kuomba: “Mungu! Siwezi kuvumilia. Ninahisi maumivu mengi katika moyo wangu. Tafadhali Unipe nuru na uniongoze kuelewa mapenzi Yako. Niko tayari kutenda ukweli na kukuridhisha.” Kisha nikafikiria maneno ya Mungu: “Siku zote kutakuwepo na kitalifa fulani kati ya ndoto za mtu na uhalisia ambao lazima mtu akabiliane nao; mambo siku zote hayawi vile ambavyo mtu angetaka yawe, na watu wanapokumbwa na uhalisi kama huu hawawezi kutimiza hali ya kutosheka au kuridhika. Baadhi ya watu wataenda hadi kiwango chochote cha kufikirika, wataweza kutia bidii za kipekee na kujitolea pakubwa kwa minajili ya riziki na mustakabali wao, katika kujaribu kubadilisha hatima yao wenyewe. Lakini hatimaye, hata kama wataweza kutambua ndoto na matamanio yao kupitia kwa njia ya bidii yao wenyewe, hawawezi kubadilisha hatima zao, na haijalishi watajaribu vipi kwa njia ya ukaidi hawatawahi kuzidi kile ambacho hatima yao imewapangia. Licha ya tofauti katika uwezo, kiwango cha akili, na hiari ya kutenda, watu wote ni sawa mbele ya hatima, jambo ambalo halileti utofauti kati ya wakubwa na wadogo, wale wa kiwango kile cha juu na cha chini, wanaotukuzwa na wakatili. Ile kazi ambayo mtu anafuatilia, kile anachofanya mtu ili kuzumbua riziki, na kiwango kipi cha utajiri ambacho mtu amelimbikiza katika maisha yake vyote haviamuliwi na wazazi wa mtu, vipaji vya mtu, jitihada za mtu au malengo ya mtu, vyote vinaamuliwa kabla na Muumba” (“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili). Kutoka kwa maneno ya Mungu nilielewa ghafla kuwa sio watu ambao wana uamuzi wa mwisho juu ya majaliwa na kudura yetu na kwamba hauwezi kubadilishwa na mtu yeyote. Inategemea ustadi wa Mungu na majaaliwa. Bila kujali jinsi lengo la mtu na tamaa zilivyo kubwa ama ni jinsi gani malengo na matumaini yao yalivyo mazuri kabisa, hayabadilishi ustadi wa Mungu na mipango ya kudura ya watu hata kidogo. Nani anayejua ni watu wangapi ambao wamefuatilia mafanikio na cheo cha juu, lakini daima hugonga mwamba. Mwishowe, wao bado hukaa maisha yao yote wakiwa kama watu wa kawaida. Watu wengi wanataka kufanya kazi kwa bidii kwa kutegemeza jitihada zao wenyewe na kuishi maisha ya furaha, lakini wao hujitahidi maisha yote na hushindwa kufanikisha hili. Na kadhalika. Ukweli huu unaweza kuonekana karibu nasi mara nyingi. Mimi hufikiria kuhusu jinsi nilivyokuwa hivi pia wakati nilipokuwa nikiwafundisha wanangu. Kuanzia wakati wanangu walizaliwa, nilizingatia hasa maendeleo na elimu yao na nilitumaini kuwa wangekuwa watu waliostaarabika, wenye tabia njema na wazuri. Ili kufanikisha tamaa zangu, nilitoa matakwa makali kwao na kujaribu nilivyoweza kuwatafutia shule nzuri, lakini ingawa nilikuwa na wasiwasi sana na kuhisi nimechoka sana, hatimaye utendaji wa mwanangu haukuwa mzuri kama nilivyotarajia. Ni kwa kusoma maneno ya Mungu tu ndipo nilipokuja kuelewa hili: Mafanikio ya kitaaluma ya watoto, ni aina gani za kazi walizo nazo, watakachofanya katika siku za baadaye, riziki yao na jinsi ubinadamu wao ulivyo hauwekwi kwa msingi wa elimu ya shule na malezi. Haya yote yameamuliwa na ustadi wa Mungu na majaaliwa. Kazi yetu kama wazazi ni kujaribu tu tuwezavyo kuwaelimisha watoto wetu. Kwa mintarafu ya majaliwa yao katika siku za baadaye na ikiwa wanaweza kuwa na vipaji au la, ni Mungu peke yake aliye na uamuzi wa mwisho. Daima niliwafundisha wanangu kulingana na matakwa yangu mwenyewe na kuwafanya wanangu kuendelea kulingana na mapenzi yangu. Si huko ni kuutoroka ustadi wa tu Mungu? Haya pia ni maonyesho ya kutomtii Mungu! Baada ya kuyaelewa mapenzi ya Mungu, nilimwomba Yeye: “Mungu, ninaelewa kwamba mustakabali wa mwanangu uko mikononi Mwako. Sitawaelimisha wanangu tena kwa njia yangu mwenyewe kama ninavyotaka, na niko tayari kabisa kukuaminia Wewe wanangu, kukutegemea Wewe na kuutii ustadi na mipango Yako.” Baada ya kuomba, nilihisi nguvu ndani ya moyo wangu na moyo wangu ukawa thabiti.
Asubuhi iliyofuata, nilienda kumtafutia mwanangu shule. Niliendelea kumwomba Mungu njiani na kuomba kwamba Mungu angeniongoza. Niliangalia shule mbili siku hiyo. Nilipoiangalia shule ya pili, kwa kweli niliipenda na nilihisi kwamba hii shule ilikuwa imesanifishwa sana. Baada ya watoto kufika shuleni, walifanya mazoezi ya asubuhi na pia wakasimulia hadithi zao wenyewe. Ilihisi ya kawaida sana. Watoto walikwenda shuleni kutoka mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni, hivyo nilikuwa na muda zaidi wa kuhudhuria mikutano. Nilihisi furaha sana na mwanangu pia alikuwa na furaha sana alipoiona shule hiyo. Kwa hiyo niliamua kumruhusu mwanangu kwenda kwa shule hii. Baada ya hapo, nilifanikiwa kukamilisha taratibu za kuingia za mwanangu na aliandikishwa rasmi siku hiyo.
kutoka kwa Ushuhuda wa Injili
Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu, Kujua Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni