Maonyesho ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Amri ya Yehova Mungu kwa Mwanadamu
Nyoka Anamshawishi Mwanamke
Mwenyezi Mungu anasema, “Hivi vifungu viwili ni dondoo kutoka kwa kitabu kipi cha Biblia? (Mwanzo.) Je, nyinyi nyote mnavijua vifungu hivi viwili? Hiki ni kitu kilichofanyika mwanzoni wakati binadamu kwanza aliumbwa; lilikuwa ni tukio halisi. Kwanza hebu tuangalie ni amri ya aina gani ambayo Yehova Mungu aliwapa Adamu na Hawa, kwani yaliyomo katika amri hii ni muhimu sana kwa mada yetu ya leo. “Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema….” Endelea kusoma kifungu kifuatacho. (“Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.”) Amri ya Mungu kwa mwanadamu katika kifungu hiki ina nini? Kwanza, Mungu anamwambia mwanadamu kile anachoweza kula, yakiwa ni matunda ya miti ya aina nyingi. Hakuna hatari na hakuna sumu, yote yanaweza kulika na kulika atakavyo mtu, bila wasiwasi wowote. Hii ni sehemu moja. Sehemu nyingine ni onyo. Onyo hili linamwambia mwanadamu mti ambao hawezi kula tunda kutoka—lazima asile tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Nini itafanyika akifanya hivyo? Mungu alimwambia mwanadamu: Ukilila hakika utakufa. Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? (Ndiyo.) Iwapo Mungu angekwambia jambo hili lakini hukuelewa kwa nini, ungelichukulia kama kanuni ama amri ya kufuatwa? Linapaswa kufuatwa, sivyo? Lakini iwapo mwanadamu anaweza ama hawezi kulifuata, maneno ya Mungu hayaachi shaka. Mungu alimwambia mwanadamu kwa uwazi kabisa kile anachoweza kula na kile asichoweza, na kile kitakachofanyika akila kile hapaswi kula. Umeona tabia yoyote ya Mungu katika haya maneno machache ambayo Alisema? Haya maneno ya Mungu ni ya ukweli? Kuna udanganyifu wowote? Kuna uongo wowote? (La.) Kuna chochote kinachotisha? (La.) Mungu kwa uaminifu, kwa kweli, kwa dhati Alimwambia mwanadamu kile anachoweza kula na kile asichoweza kula, wazi na dhahiri. Kuna maana iliyofichwa katika maneno haya? Maneno haya yanaeleweka kwa urahisi? Je, kuna haja yoyote ya dhana? (La.) Hakuna haja ya kukisia, sivyo? Maana yake ni wazi kwa mtazamo mmoja, na unaelewa punde tu unapoyaona. Ni wazi kabisa. Yaani, kile Mungu anataka kusema na Anachotaka kuonyesha kinatoka katika moyo Wake. Mambo ambayo Mungu anaonyesha ni safi, yanaeleweka kwa urahisi na ni wazi. Hakuna nia za siri ama maana zilizofichwa. Alizungumza moja kwa moja na mwanadamu, Akimwambia kile anachoweza kula na kile asichoweza kula. Hivyo ni kusema, kupitia maneno haya ya Mungu mwanadamu anaweza kuona kwamba moyo wa Mungu ni angavu, kwamba moyo wa Mungu ni wa kweli. Hakuna uwongo kabisa hapa, kukwambia kwamba huwezi kula kile kinacholika ama kukwambia “Ifanye na uone kitakachofanyika” na vitu ambavyo huwezi kula. Anamaanisha jambo hili? (La.) La. Chochote afikiriacho Mungu katika moyo Wake ndicho Anachosema. Nikisema Mungu ni mtakatifu kwa sababu Anaonyesha na kujifichua Mwenyewe ndani ya maneno haya kwa njia hii, unaweza kuhisi kana kwamba Nimefanya jambo lisilokuwa kubwa ama Nimenyoosha ufasiri Wangu mbali kiasi. Kama ni hivyo, usijali, hatujamaliza bado.”
Yaliyopendekezwa: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni