Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne
Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. ... Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa.
Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu. ... Katika Macho ya Mungu, ingawaje Ayubu alikuwa bado Ayubu wa hapo awali, imani, utiifu na kumcha Mungu kwake kulikuwa kumemletea Mungu utoshelezi kamilifu. Wakati huu, Mungu alitarajia Ayubu kuweza kutimiza, alikuwa amegeuka kuwa mtu aliyestahili kuitwa ‘mtimilifu na mnyofu’ mbele ya macho ya Mungu. Vitendo vyake vya haki vilimruhusu yeye kumshinda Shetani na kuwa makini katika ushuhuda wake kwa Mungu. Hivyo, pia, matendo yake ya haki yalimfanya kuwa mtimilifu, na kuruhusu thamani ya maisha yake kuimarishwa, kuzidishwa zaidi kuliko awali, na kumfanya yeye kuwa mtu wa kwanza kutoweza kushambuliwa au kujaribiwa zaidi na Shetani. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishtakiwa na kujaribiwa na Shetani; kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alikabidhiwa Shetani; na kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishinda na kumlemea Shetani, na kuweza kusimama imara katika ushuhuda wake. Kuendelea mbele, Ayubu akawa binadamu wa kwanza ambaye hangewahi tena kukabidhiwa Shetani, kwa kweli alikuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na akaishi kwenye nuru, katika baraka za Mungu bila ya kupelelezwa au kuangamizwa na Shetani.… Alikuwa amekuwa binadamu wa kweli katika macho ya Mungu, alikuwa ameachiliwa huru. …”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni