Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II" Sehemu ya Pili
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Mungu Anawajali tu Wale Wanaoweza Kutii Maneno Yake Na Kufuata Amri Zake
Mungu ni Mwenye Wingi wa Rehema Kwa Wale Anaowajali, na Mwenye Hasira Kali kwa Wale Anaowachukia na Kukataa
Watu Wa Siku Za Mwisho Wanaiona tu Hasira Ya Mungu Katika Maneno Yake, na Hawaipitii kwa Kweli Hasira Ya Mungu
Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu
Mwenyezi Mungu anasema: “Katika simulizi za Biblia, kulikuwepo na watumishi kumi wa Mungu kule Sodoma? La, hakukuwepo! Kulikuwepo na jiji lililostahili kusamehewa na Mungu? Mtu mmoja tu kwenye jiji hilo—Loti—ndiye aliye wapokea wajumbe wa Mungu. Matokeo ya haya ni kwamba kulikuwa na mtumishi mmoja tu wa Mungu kwenye jiji, na hivyo basi Mungu hakuwa na chaguo ila kumwokoa Loti na kuliangamiza jiji la Sodoma. Mabadilishano haya kati ya Ibrahimu na Mungu yanaweza kuonekana kuwa rahisi tu, lakini yanaonyesha kitu fulani kikuu: Kuna kanuni za vitendo vya Mungu, na kabla ya kufanya uamuzi Atachukua muda mrefu akiangalia na kutafakari; kabla ya wakati kuwa sawa, bila shaka Hatafanya au kukimbilia hitimisho zozote. Mabadilishano kati ya Ibrahimu na Mungu yanatuonyesha kwamba uamuzi wa Mungu wa kuangamiza Sodoma haukuwa mbaya hata kidogo, kwani Mungu alijua tayari kwamba kwenye jiji hakukuwa na watu arubaini wenye haki, na wala thelathini wenye haki, wala ishirini. Hawakuwa hata kumi. Mtu mwenye haki pekee kwenye jiji alikuwa Loti. Yote yaliyofanyika ndani ya Sodoma na hali zake ziliangaliwa na Mungu, na zilizoeleka kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Hivyo, uamuzi Wake usingekosa kuwa sahihi. Kinyume na haya, tukilinganisha uweza wa Mungu, binadamu hajali katu, ni mjinga na asiyejua neno, asiyeona mbali katu. Haya ndiyo tunayoona katika mabadilishano kati ya Ibrahimu na Mungu. Mungu amekuwa akiwasilisha mbele tabia Yake kuanzia mwanzo hadi leo. Hapa, vilevile, kuna pia tabia ya Mungu tunayofaa kuona. Nambari ni rahisi, na hazionyeshi chochote, lakini hapa kuna maonyesho muhimu sana ya tabia ya Mungu. Mungu asingeangamiza jiji kwa sababu ya watu hamsini wenye haki. Je, haya ni kutokana na rehema ya Mungu? Ni kwa sababu ya upendo na uvumilivu Wake? Je mmeuona upande huu wa tabia ya Mungu? Hata kama kungekuwa na wenye haki kumi pekee, Mungu asingeangamiza jiji hili kwa sababu ya watu hawa kumi wenye haki. Je, haya yanaonyesha uvumilivu na upendo wa Mungu au la? Kwa sababu ya rehema, uvumilivu, na kujali kwa Mungu kwa wale watu wenye haki, Asingeliangamiza jiji hili. Huu ndio uvumilivu wa Mungu. Na hatimaye, ni matokeo gani tunayoyaona? Wakati Ibrahimu aliposema, “Iwapo watapatikana huko watu kumi,” Mungu akasema, “Sitauharibu kwa sababu yao.” Baada ya hapo, Ibrahimu hakusema tena—kwani ndani ya Sodoma hakukuwa na wenye haki kumi aliowarejelea, na hakuwa na chochote ziada cha kusema, na kwa wakati huo alielewa ni kwa nini Mungu alikuwa ameamua kuangamiza Sodoma. Katika haya, ni tabia gani ya Mungu unayoiona? Ni aina gani ya utatuzi ambayo Mungu alifanya? Yaani, kama jiji hili lisingekuwa na wenye haki kumi, Mungu asingeruhusu uwepo wake, na bila shaka Angeliangamiza. Je hii si hasira ya Mungu? Je, hasira hii inawakilisha tabia ya Mungu? Je, hii tabia ni ufunuo wa kiini cha haki cha Mungu? Je, huu ni ufunuo wa kiini cha haki ya Mungu, ambacho binadamu hafai kukosea? Baada ya kuthibitisha kwamba hakukuwa na wenye haki kumi kule Sodoma, Mungu alikuwa na hakika ya kuliangamiza jiji, na angewaadhibu vikali watu walio ndani ya hilo jiji, kwani walimpinga Mungu, na kwa sababu walikuwa wachafu na waliopotoka.”
Sikiliza zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni