Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Pili
Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu aliwaumba watu hawa wawili na kuwashughulikia kama mtu na mwandani Wake. Akiwa ndiye mwanafamilia pekee wao, Mungu aliangalia kuishi kwao na pia akakidhi mahitaji yao ya kimsingi. Hapa, Mungu anajitokeza kama mzazi wa Adamu na Hawa. Huku Mungu akifanya haya, binadamu haoni namna ambavyo Mungu alivyo mkuu; haoni mamlaka ya juu zaidi ya Mungu, hali Yake ya mafumbo, na hasa haoni hasira au adhama Yake.
Kile anachoona tu ni unyenyekevu wa Mungu, upendo Wake, kujali Kwake binadamu na jukumu Lake na utunzaji Wake kwake yeye. Mwelekeo na njia ambayo Mungu alishughulikia Adamu na Hawa ni sawa na namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyoonyesha hali ya kuwajali watoto wao binafsi. Ni kama pia namna ambavyo wazazi wa kibinadamu wanavyopenda, kuangalia, na kutunza watoto wao binafsi wa kiume na kike—halisia, namna ya kuonekana, na kushikika.”
Chanzo: Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” Sehemu ya Pili
Sikiliza zaidi: Usomaji-wa-Maneno-ya-Mwenyezi-Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni