Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 95
Watu hufikiri kila kitu kuwa rahisi sana, wakati kwa kweli hali siyo hivyo. Ndani ya kila kitu kuna siri zilizofichwa, na vile vile hekima Yangu na mipango Yangu. Hakuna utondoti usioangaliwa, na yote yanapangwa na Mimi Mwenyewe. Hukumu ya siku kuu inawafikia wale wote wasionipenda kwa kweli (kumbuka, hukumu ya siku kuu inalenga kila mtu anayepokea jina hili) na kuwasababisha kulia na kusaga meno.
Sauti hii ya kuomboleza hutoka jahanamu na kutoka kuzimu; si watu wanaolia, ila ni pepo. Ni hukumu Yangu inayoleta kulia huku, inayoleta wokovu wa mwisho wa mpango Wangu wa usimamizi kwa ajili ya watu. Awali Nilikuwa na matumaini kiasi kwa watu fulani. Lakini kwa kuangalia sasa, ni lazima Nitelekeze watu hawa mmoja mmoja, kwa kuwa kazi Yangu imekuja kwa hatua hii na ni kitu ambacho hakuna mtu anaweza kubadili. Wale wote ambao si wazaliwa Wangu wa kwanza au watu Wangu lazima watelekezwe na lazima waondoke hapa! Lazima muelewe kwamba, nchini China, kando na wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu, wengine wote ni watoto wa joka kubwa jekundu na wanapaswa kutupwa. Nyote mnapaswa kuelewa, hata hivyo Uchina ni taifa ambalo limelaaniwa na Mimi, na watu Wangu wachache hapo ni wale wanaotoa huduma kwa kazi Yangu ya baadaye tu. Kulisema vingine, kando na wazaliwa Wangu wa kwanza, hakuna mtu mwingine—wote wataangamizwa. Usifikiri kwamba Mimi ni wa kuzidi kiasi sana katika matendo Yangu—hii ni amri Yangu ya utawala. Wale wanaopitia laana Zangu ni walengwa wa chuki Yangu, hili ni bila shaka. Sifanyi makosa yoyote; Nikimwona mtu asiyenipendeza Nitamwondoa, na hilo linatosha kuthibitisha kwamba wewe umelaaniwa na Mimi na ni dhuria ya joka kubwa jekundu. Acha Nikufahamishe tena, kuna wazaliwa Wangu wa kwanza Uchina pekee (kando na watu Wangu wanaotoa huduma) na hii ni amri Yangu ya utawala. Lakini wazaliwa Wangu wa kwanza ni wachache sana na wote wameamuliwa kabla na Mimi—Najua ninachokifanya. Siogopi uhasi wako na Siogopi kwamba utageuka na kuniuma, kwa kuwa Nina amri Zangu za utawala na Nina ghadhabu. Yaani, Ninashikilia maafa makuu mikononi Mwangu na Siogopi chochote, kwa kuwa Nachukulia vitu vyote kuwa vimetimizwa tayari, na wakati ambapo siku hiyo itafika Nitakushughulikia kabisa. Mtu hawezi kukamilishwa au kuadilishwa na mwanadamu na kugeuka kuwa mzaliwa Wangu wa kwanza, lakini badala yake inaamuliwa kabisa na majaaliwa Yangu. Yeyote Ninayesema ni mzaliwa wa kwanza ni mzaliwa wa kwanza; usilipiganie au kulinyakua. Vitu vyote vinaamuliwa na Mimi, Mungu mwenye uweza Mwenyewe.
Siku moja Nitawaruhusu nyote muone amri Zangu za utawala ni nini na ghadhabu Yangu ni nini (wote watanipigia magoti, wote wataniabudu, wote wataniomba msamaha na wote wataishi katika utii; sasa Naruhusu tu wazaliwa Wangu wa kwanza kuona sehemu yake). Nitawafanya watoto wote wa joka kubwa jekundu waone kwamba Nimechagua wengi kutolewa kafara (isipokuwa wazaliwa Wangu wa kwanza) ili kuwakamilisha wazaliwa Wangu wa kwanza, kwamba Nimelifanya joka kubwa jekundu kuangukia hila yake ya ujanja. (Katika mpango Wangu wa usimamizi, joka kubwa jekundu linatuma wale wanaonitolea huduma—ikiwa inajumuisha kila mtu isipokuwa wazaliwa Wangu wa kwanza—kukatiza mpango Wangu wa usimamizi; lakini limeanguka katika hila yake ya ujanja lenyewe, na wote wanatoa huduma kwa kazi Yangu. Hii ni sehemu ya maana ya kweli ya Mimi kuwahamasisha wote kunitolea huduma.) Leo, wakati ambapo vitu vyote vimetimizwa, Nitawatupa wote, kuwakanyaga chini ya miguu Yangu, na kupitia hili Nitalifedhehesha joka kubwa jekundu na kulifanya liaibike kabisa (wanajaribu kudanganya kupata baraka, lakini hawakuwahi kufikiria kwamba wangenitolea huduma)—hii ni hekima Yangu. Wanaposikia hili, watu hufikiri Sina hisia au rehema, na wanafikiri kwamba Sina ubinadamu. Kwa kweli Sina hisia au rehema kwake Shetani, na aidha Mimi ni Mungu Mwenyewe anayezidi sana uwezo wa ubinadamu. Unawezaje kusema Mimi ni Mungu aliye na ubinadamu? Hujui kwamba Mimi si wa dunia hii? Hujui kwamba Niko juu ya vitu vyote? Kando na wazaliwa Wangu wa kwanza, hakuna mtu kama Mimi, hakuna mtu aliye na tabia Yangu (si tabia ya binadamu ila tabia takatifu), na hakuna mtu anayemiliki sifa Zangu.
Wakati lango la dunia ya roho linafunguliwa, mtaona siri zote, kuwawezesha kuingia kabisa katika eneo huru, kuingia katika kumbatio Langu la upendo na kuingia katika baraka Zangu za milele. Mikono Yangu imewasaidia wanadamu daima. Lakini kuna sehemu ya wanadamu ambayo Nitaokoa na sehemu ambayo Sitaokoa. (Nasema “kusaidia” kwa sababu kama Singeisaidia dunia nzima, ingeaguka imeanguka kuzimu kitambo.) Oneni hili wazi! Huu ni mpango Wangu wa usimamizi. Na mpango Wangu wa usimamizi ni nini? Niliwaumba wanadamu, lakini Sikuwahi kupanga kumpata kila mtu, ila kupata tu sehemu ndogo ya wanadamu. Kwa hivyo mbona Niliwaumba watu wengi? Nimesema awali kwamba, Nikiwepo, yote ni ufunguliwaji na uhuru, na Ninafanya chochote Ninachotaka. Nilipowaumba wanadamu, ilikuwa tu ili waishi maisha ya kawaida na kisha kungetokea sehemu ndogo ya wanadamu ambao ni wazaliwa Wangu wa kwanza, wana Wangu na watu Wangu. Inaweza kusemwa kwamba watu, mambo na vyombo vyote—kando na wazaliwa Wangu wa kwanza, watu Wangu na wana Wangu—wote ni watendaji huduma na lazima wote waangamie. Kwa njia hii mpango Wangu mzima wa usimamizi utahitimishwa. Huu ni mpango Wangu wa usimamizi, ni kazi Yangu na ni hatua Zangu zinazoendelea mbele. Wakati ambapo kila kitu kimeisha Nitakuwa mapumzikoni kabisa. Wakati huo, kila kitu kitafanywa chema na kila kitu kitafanywa kitulivu na salama.
Hatua ya kazi Yangu ni yenye kasi sana kiasi kwamba hakuna mtu anayeweza kuifikiria. Inabadilika siku kwa siku na yeyote asiyeweza kwenda kwa mwendo sawa atapata hasara; mtu anaweza tu kushikilia mwanga mpya kila siku (ingawa amri Zangu za utawala, na maono na ukweli Ninaoshiriki havibadiliki kamwe). Kwa nini Nazungumza kila siku? Kwa nini siku zote Nakupa nuru? Je, unaelewa maana ya kweli ndani? Watu wengi bado sasa wanacheka na kufanya mzaha na hawawezi kuwa makini. Hawazingatii maneno Yangu kabisa, lakini wanahisi tu wasiwasi wa muda wanapoyasikia. Baadaye, maneno Yangu yanasahaulika punde na punde hawajui utambulisho wao wenyewe na wanakuwa wazembe. Je, unajua hadhi yako ni ipi? Iwapo mtu ananitolea huduma au anajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi kunasimamiwa na mikono Yangu tu na hakuna mtu anayeweza kubadili hili—ni lazima Nifanye hili Mwenyewe, lazima Niwachague na kuwajaalia Mimi Mwenyewe. Nani anathubutu kusema Mimi ni Mungu asiye na hekima? Kila neno Ninalosema na kila kitu Ninachofanya ni hekima Yangu. Nani anathubutu kukatiza usimamizi Wangu tena au kuharibu mipango Yangu? Bila shaka Sitamsamehe! Wakati uko mikononi Mwangu na Siogopi kucheleweshwa; Mimi siye Yule anayeamua wakati ambao mpango Wangu wa usimamizi utaisha? Hauamuliwi na wazo Langu moja tu? Ninaposema umeisha, umeisha, na unaisha Ninaposema uishe. Sina haraka na Nitafanya mipango ya kufaa. Mwanadamu lazima asiingilie kazi Yangu na ni lazima asinifanyie mambo kama apendavyo. Namlaani yeyote anayeingilia—hii ni mojawapo ya amri Zangu za utawala. Mimi Mwenyewe nafanya kazi Yangu na Simhitaji yeyote mwingine (Naruhusu wale watendaji huduma kutenda, vinginevyo hawangethubutu kutenda kwa haraka au bila kufikiri). Kazi yote inapangwa na Mimi, inaamuliwa na Mimi, kwa kuwa Mimi ndiye Mungu mmoja Mwenyewe.
Mataifa yote ya dunia yanapigana kwa ajili ya mamlaka na faida na kupigania ardhi, lakini usishtuke, vitu hivi vyote vinanihudumia. Na kwa nini Nasema vinanihudumia? Nafanya vitu bila jitihada. Kumhukumu Shetani kwanza Nawafanya wagombane miongoni mwao wenyewe na mwishowe kuwaleta kwa uangamizi na kuwafanya waanguke katika hila zao za ujanja (wanataka kupigana na Mimi kwa ajili ya mamlaka, lakini wanaishia kunihudumia). Nazungumza tu na kutoa maagizo Yangu na kila mtu atafanya kile Nitakachokwambia ufanye, au vinginevyo Nitakuangamiza mara moja. Vitu hivi vyote ni sehemu ya hukumu Yangu, kwa kuwa Naamuru vitu vyote, na vitu vyote vinaagizwa na Mimi. Yeyote anayefanya chochote anafanya hivyo pasipo kutaka, kufanya hivyo kwa mpango Wangu mwenyewe, na Natumai kwamba mnaweza kujaa hekima Yangu katika matukio ambayo yatafika karibuni. Msilivuruge, ila mnikaribie zaidi wakati mambo yanapowafikia; kuweni makini na kujihadhari zaidi katika mambo yote kuepuka kukosea kuadibu Kwangu, na kuepuka kuangukia hila za ujanja za Shetani. Mnapaswa kupata umaizi kutoka kwa maneno Yangu, mjue kile Nilicho, na kuona kile Ninacho. Ni lazima mfanye vitu kulingana na mitazamo Yangu ya maana na lazima msilivuruge. Fanyeni kile Ninachofanya, na mseme kile Ninachokisema. Nasema vitu hivi kwenu mapema ili mweze kuepuka kufanya makosa na kuepuka kujaribiwa. Na kile Nilicho na Ninacho ni nini? Kweli mnajua? Uchungu Ninaoupitia ni sehemu ya kile Nilicho, kwa kuwa ni sehemu ya ubinadamu Wangu wa kawaida, na kile Nilicho kinaweza kupatikana pia katika uungu Wangu kamili—mnajua hili? Kile Nilicho kinajumuishwa na vipengele viwili: Kipengele kimoja ni kile cha ubinadamu Wangu, ilhali kingine ni kile cha uungu Wangu kamili. Ni vipengele hivi viwili tu vikijumuishwa pamoja ndivyo vinamuunda Mungu Mwenyewe kamili. Kile ambacho uungu Wangu kamili ndicho pia kinajumuisha mambo mengi: Sizuiliwi na mtu, suala au jambo lolote; Navuka mipaka ya mazingira yote; Nimezidi mipaka ya wakati au nafasi au jiografia; Najua watu, masuala na vitu vyote kweli kama kiganja cha mkono Wangu; na bado Mimi ni nyama na mifupa, katika umbo linalogusika; Mimi bado ni mtu huyu machoni pa watu, lakini asili imebadilika—si nyama, ila ni mwili. Vitu hivi ni sehemu yake ndogo tu. Wazaliwa Wangu wa kwanza wote watakuwa hivi pia katika siku za baadaye; hii ni njia ambayo lazima itembelewe na wale ambao wamehesabika hawawezi kutoroka. Ninapokuwa nikifanya hili, wale wote ambao hawajajaaliwa watafukuzwa wote (kwa kuwa huku ni Shetani kunijaribu kuona kama maneno Yangu ni sahihi). Wale ambao wamejaaliwa hawawezi kulitoroka bila kujali wanapokwenda, na mtaona humo kanuni za hili tendo Langu. Kile Ninacho kinarejelea maarifa Yangu, hekima Yangu, werevu Wangu na kila neno Ninalosema. Ubinadamu Wangu na uungu Wangu unakimiliki. Yaani, yote ambayo yanafanywa na ubinadamu Wangu na vile vile kile ambacho kinafanywa na uungu Wangu ni kile Ninacho; hakuna anayeweza kuchukua vitu hivi au kuviondoa, Navimiliki, na hakuna anayeweza kuvibadili. Hii ndiyo amri Yangu ya utawala kali zaidi (kwani katika dhana za mwanadamu, vitu vingi Ninavyovifanya havipatani na dhana zao na haviwezi kueleweka na mwanadamu; hii ndiyo amri ambayo kila mtu huikosea kwa urahisi zaidi na pia ndiyo kali zaidi, kwa hivyo maisha yao humo lazima yapoteze). Nitasema tena, ni lazima mchukue mtazamo wa uangalifu sana kwa kile Ninachowasihi kufanya—ni lazima msiwe wazembe!
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Maneno Husika ya Mungu: Hukumu ya Siku za Mwisho | Ni vipi kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho humtakasa na kumwokoa wanadamu?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni