7/23/2018

8. Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa

8. Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa

Wang Lan, Beijing
Agosti 6, Mwaka wa 2012
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mafuriko makubwa zaidi tangu miaka sitini yalipitia kijijini mwetu kwa nguvu mno. Maafa yalianguka kutoka mbinguni, maji ya mafuriko yalichanganya matope na mawe na kuharibu kijiji chote. Nyumba nyingi ziliharibiwa na maji na maporomoko ya matope.

7/22/2018

5 Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu

Smiley face



Watu Wote Wanaishi Katika Mwanga wa Mungu


Utambulisho

I
Sasa kwa kushangilia sana, utakatifu wa Mungu na haki vinakua ulimwenguni kote, ikitukuka sana kati ya wanadamu wote. Miji ya mbinguni inacheka, falme za dunia zinacheza.

7/21/2018

Video ya Kiswahili ya Ushuhuda wa Kikristo "Mungu Ndiye Nguvu ya Maisha Yangu"



Video ya Kiswahili ya Ushuhuda wa Kikristo "Mungu Ndiye Nguvu ya Maisha Yangu"


Utambulisho

Fang Jin ni Mkristo. Alikamatwa na serikali ya CCP kwenye mkusanyiko. Ili kumlazimisha kuwataja ndugu zake wa kike na kiume na kumsaliti Mungu, polisi walimnyima chakula, maji na usingizi kwa siku saba mchana na siku sita usiku, na kusababisha kila aina ya mateso ya kinyama juu yake: mapigo makali, kuning’inizwa, kuchuchumaa, kudhihakiwa na kufedheheshwa.

7/20/2018

Nitampenda Mungu Maisha Yangu Yote | "Mpendwa Wangu, Tafadhali Nisubiri" (Video Rasmi ya Muziki)



Nitampenda Mungu Maisha Yangu Yote | "Mpendwa Wangu, Tafadhali Nisubiri" (Video Rasmi ya Muziki)


Utambulisho

Juu ya miti, nikiukwea mwezi wa amani. Kama mpendwa wangu, wa haki na mzuri.
Ee mpendwa wangu, Uko wapi? Sasa mimi nina machozi. Je, Wanisikia nikilia?
Wewe Ndiwe hunipa upendo. Wewe Ndiwe Unayenitunza.
Wewe Ndiwe unayeniwaza daima, Wewe Ndiwe unayeyatunza maisha yangu.

7/19/2018

1. Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

1. Mwenyezi Mungu Amenipa Fursa ya Pili Katika Maisha

Ndugu wawili wa kawaida, Beijing
Agosti 15, 2012
Julai 21, mwaka wa 2012 ilikuwa siku isiyosahaulika sana kwangu, pamoja na kuwa siku muhimu zaidi ya maisha yangu.

Siku hiyo, mvua kubwa ilikuwa ikinyesha katika Wilaya ya Fangshan jijini Beijing—ilikuwa kubwa kuliko yoyote iliyowahi kuonekana pale katika miaka sitini na mmoja. Muda mfupi baada ya saa 4 jioni, nilitoka nje mtaani ili kuangalia na nikaona kuwa maji yalikuwa kila mahali. Gari la familia yetu lilikuwa tayari limeelea, na sababu ya pekee gari hilo kutosombwa na mkondo wa maji ilikuwa kwamba lilizuiwa na kitu mbele yake kilicholizuia kusonga. Maono hayo yalinifanya kuwa na wasiwasi sana, hivyo kwa haraka nilimpigia mume wangu simu, ambaye pia ni muumini, lakini sikuweza kumpata kwa simu bila kujali ni mara ngapi nilijaribu. Kisha, badala ya kutafuta mapenzi ya Mungu, niliharakisha kurudi nyumbani kumwita mume wangu kwa haraka.

7/18/2018

2. Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe

2. Nguvu ya Maisha Ambayo Haiwezi Kuzimwa Kamwe

Dong Mei, Mkoa wa Henan
Mimi ni mtu wa kawaida. Niliishi maisha ya kawaida. Kama wengi wanaotamani sana mwanga, nilijaribu njia nyingi kutafuta maana ya kweli ya uwepo wa wanadamu, nikijaribu kuyapa maisha yangu umuhimu zaidi. Mwishowe, juhudi zangu zote zilikuwa bure. Lakini baada ya kuwa na bahati ya kutosha kukubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, mabadiliko ya muujiza yalitokea katika maisha yangu. Yalileta rangi zaidi katika maisha yangu, na nilikuja kuelewa kwamba ni Mungu pekee ni Mtoa wa kweli wa roho na maisha ya wanadamu. Nilikuwa na furaha kwamba hatimaye nilikuwa nimepata njia sahihi ya maisha. Hata hivyo, huku nikitekeleza wajibu wangu wakati mmoja nilikamatwa kiharamu na kuteswa kikatili na serikali ya CCP. Kutoka kwa hili, safari ya maisha yangu ilipata uzoefu ambao kamwe sitasahau ...

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

7/17/2018

Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu"



Mwabudu Mungu kwa Roho na Ukweli | Muziki wa Akapela "Tokeo Lililofikiwa kwa Kumjua Mungu"


Utambulisho


Mpaka siku moja,
utahisi kuwa Muumba sio fumbo tena,
kwamba Muumba hajawahi kufichwa kutoka kwako,
kwamba Muumba hajawahi kuificha sura Yake kutoka kwako,
kwamba Muumba hayuko mbali na wewe hata kidogo,
kwamba Muumba siye Yule unayemtamania katika mawazo yako
lakini kwamba huwezi kumfikia na hisia zako,
kwamba Anasimama kwa kweli kama mlinzi kulia na kushoto kwako,
Akiruzuku maisha yako, na kudhibiti majaliwa yako, kudhibiti majaliwa yako.
Hayuko katika upeo wa mbali, wala hajajificha juu mawinguni.
Yuko kando yako, akiwa na mamlaka juu ya kila kitu chako,
Yeye ni kila kitu ulicho nacho, na Yeye ni kitu pekee ulicho nacho.