1/06/2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 9

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 9


Nataka kukukumbusha kwamba huwezi kuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya neno Langu na kutokujali kwa aina yoyote hakukubaliki. Unapaswa kulisikiliza na kulitii na kutenda mambo kulingana na nia Zangu. Daima lazima uwe macho na kamwe usiwe na tabia ambayo ni ya kiburi na ya kujidai, na lazima kila wakati unitegemee Mimi ili kutupilia mbali tabia ya zamani ya asili ambayo hukaa ndani yako. Unapaswa daima kuwa na uwezo wa kudumisha hali ya kawaida mbele Yangu, na uwe na tabia thabiti Kuwaza kwako lazima kuwe kwa busara na wazi na hakupaswi kuyumbishwa au kudhibitiwa na mtu yeyote, tukio, au kitu.

1/05/2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 8

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 8


Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu.

1/04/2019

Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God


Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God


Maombi ni njia moja ya mwanadamu kushirikiana na Mungu,
kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu.
Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kuangaziwa na kuwa mwenye nguvu-nia.
Watu kama hao wanaweza kufanywa kamili hivi karibuni.
Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kuangaziwa na kuwa mwenye nguvu-nia.
Watu kama hao wanaweza kufanywa kamili hivi karibuni.

1/03/2019

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (6) : Mwenyezi Mungu Hutoa Njia ya Uzima wa Milele kwa Binadamu


"Nimewahi Treni ya Mwisho" (6) : Mwenyezi Mungu Hutoa Njia ya Uzima wa Milele kwa Binadamu


Mwishoni mwa Enzi ya Sheria, Wayahudi walishikilia kwa ukaidi sheria yao na kukataa kukubali kazi ya Bwana Yesu, ambayo iliwafanya waanguke katika giza na kupoteza wokovu wa Mungu. Sasa katika zile siku za mwisho, dunia nzima ya kidini inalinda tu jina la Bwana Yesu na kukataa kumkubali Mwenyezi Mungu, na hivyo kuisababisha kuwa na ukiwa zaidi na zaidi na kuwa jangwa lilisoweza kuzaa matunda. Kwa nini hasa iko hivi?

1/02/2019

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (5) : Matokeo Yanayofikiwa na Kazi ya Mungu Aliyepata Mwili


"Nimewahi Treni ya Mwisho" (5) : Matokeo Yanayofikiwa na Kazi ya Mungu Aliyepata Mwili


Bwana Yesu alitabiri kwamba katika zile siku za mwisho, ngano itatenganishwa na matawi, kondoo na mbuzi, na watumishi wema kutoka kwa watumishi waovu. Unajua jinsi unabii huu unatimizwa? Je, ungependa kujua njia ambayo Mungu anafanya kazi ya kutenganisha kila moja kwa aina yake katika zile siku za mwisho? Ikiwa unataka kupata ufahamu zaidi, tafadhali angalia video hii fupi!

 Tazama Video: Filamu za Injili

1/01/2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 7

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 7


Kuinuka kwa mazingira pande zetu zote huharakisha kurudi nyuma kwetu katika roho. Usitende kwa moyo mgumu, usipuuze kwa vyovyote vile kama Roho Mtakatifu Ana wasiwasi, usijaribu kuwa mjanja na usiwe na ridhaa kupita kiasi na kuridhika kibinafsi au kuzingatia sana matatizo yako mwenyewe; kitu pekee cha kufanya ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Huwezi kuyaacha maneno ya Mungu nyuma au kuyapa kisogo; lazima uyaelewae kwa makini, rudia kuomba-kusoma kwako, na uelewe maisha ndani ya maneno hayo.

12/31/2018

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 6

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 6

Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi.