3/17/2019

Neno la Mungu | Sura ya 32

Mwanga ni nini? Katika siku za nyuma kwa kweli mliuona mbadiliko wa kazi ya Roho Mtakatifu kama mwanga. Kuna mwanga wa kweli wakati wote, unaojumuisha ninyi kupata kile Mungu alicho kupitia kwa kunikaribia na kushirikiana na Mimi; kuwa na utambuzi katika maneno ya Mungu na kufahamu mapenzi ya Mungu katika maneno Yake—yaani, mnapokula na kunywa, mnahisi Roho wa maneno ya Mungu na kupokea maneno ya Mungu ndani yenu; kuelewa kile Alicho huku mkipitia na kupokea mwangaza wa Mungu huku mkizungumza na Yeye; na pia kupewa nuru na kuwa na utambuzi mpya katika maneno ya Mungu wakati wote huku mkifikiria na kutafakari. Ukielewa neno la Mungu na uhisi mwanga mpya, basi hutakuwa na nguvu katika huduma yako?

3/16/2019

Neno la Mungu | Sura ya 31

Ninawapenda wale wote wanaonitaka Mimi kwa dhati. Mkilenga kunipenda, hakika Nitawabariki kwa kiasi kikubwa. Je, mnaelewa nia Zangu? Katika nyumba Yangu, hakuna tofauti kati ya hali ya juu na chini.

3/15/2019

Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I” Sehemu ya Pili



Neno la Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu I” Sehemu ya Pili


Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. Lengo lake ni nini?

Maonyesho ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza


Maonyesho ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Amri ya Yehova Mungu kwa Mwanadamu
Nyoka Anamshawishi Mwanamke

3/13/2019

Neno la Mungu | Sura ya 30

Amkeni, ndugu! Amkeni, kina dada! Siku Yangu haitakawishwa; wakati ni uhai, na kuushika wakati ni kuokoa uhai! Wakati hauko mbali sana! Mkifanya mitihani ya kuingia katika chuo kikuu na msipite, mnaweza kujaribu tena na mubukue kwa ajili ya mtihani. Hata hivyo, siku Yangu haitakuwa na ucheleweshaji kama huo. Kumbuka! Kumbuka! Ninakuhimiza kwa maneno haya mazuri. Mwisho wa dunia unafunguka mbele ya macho yenu wenyewe, majanga makubwa yanakaribia upesi; Je, maisha yenu ni muhimu au kulala, kula, kunywa, na kuvaa kwenu ndivyo muhimu? Wakati umekuja wa ninyi kufikiria kwa makini mambo haya. Msiwe wenye shaka tena na msiogope kuwa na uhakika!

3/12/2019

Neno la Mungu | Sura ya 29

Je, ulijua kwamba wakati uko karibu? Hivyo kwa muda mfupi wa hivi karibuni utanitegemea Mimi na kuyatupilia mbali mambo yote kutoka kwako ambayo hayalingani na tabia Yangu: upumbavu, upole wa kuonyesha hisia, mawazo yasiyo wazi, moyo wa upole, nia hafifu, upuuzi, hisia zilizotiwa madoido mengi, kuchanganyikiwa na ukosefu wa utambuzi. Haya lazima yatupiliwe mbali upesi iwezekanavyo. Mimi ndimi mwenyezi Mungu! Mradi tu uko radhi kushirikiana na Mimi, Nitayatibu yote yanayokuuguza. Mimi ni Mungu anayeangalia ndani kabisa ya mioyo ya watu, Naujua magonjwa yako yote na kule ambako dosari zako ziko.

3/11/2019

Neno la Mungu | Sura ya 28

Unaona kwamba muda ni mfupi sana na kazi ya Roho Mtakatifu inavurumisha mbele, ikikusababisha kupata baraka kubwa hivi, kumpokea Mfalme wa ulimwengu, Mwenyezi Mungu, ambaye ni Jua ling’aalo, Mfalme wa ufalme—hii yote ni neema na huruma Yangu. Kuna nini kinachoweza kuwepo kinachoweza kukutoa kwa upendo Wangu? Tafakari kwa makini, usijaribu kuepa, subiri kwa ustahamilivu mbele Yangu kila wakati na usiwe ukizurura nje daima. Moyo wako lazima ukae karibu na moyo Wangu, na bila kujali kile kinachoweza kukufikia usifanye vitu bila kufikiri au kiholela.