4/21/2019

sauti ya Mungu | Kazi katika Enzi ya Sheria

sauti ya Mungu | Kazi katika Enzi ya Sheria

Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. 

4/20/2019

Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa

Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa.

4/19/2019

Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Jinsi Hatua ya Pili ya Kazi ya Ushindi Huzaa Matunda

Hatua ya kazi ya watenda-huduma ni hatua ya kwanza ya kazi ya ushindi; kwa sasa hii ni hatua ya pili ya kazi ya ushindi. Kwa nini ukamilifu unajadiliwa katika kazi ya ushindi? Ni kuujenga msingi kwa ajili ya siku za baadaye—kwa sasa hii ni hatua ya mwisho katika kazi ya kushinda, na baada ya hii, kazi ya kuwakamilisha watu itaanza rasmi wakati watakuwa wanapitia dhiki kuu. Jambo la msingi sasa ni ushindi; hata hivyo, hii pia ni hatua ya kwanza ya kukamilisha, kukamilisha ufahamu na utii wa watu, ambayo kwa kweli bado yanajenga msingi wa kazi ya kushinda. Kama unataka kukamilishwa, lazima uwe na uwezo wa kusimama imara katikati ya mateso ya siku za baadaye na uziweke nguvu zako zote katika kupanua hatua yenye kufuata ya kazi. 

4/18/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Siku hizi watu wengi hawatilii maanani mafunzo yapi yanayopaswa kusomwa wakati wa upatano na wengine. Nimegundua kuwa wengi wenu hawawezi kujifunza mafunzo hata kidogo wakati wa ushirikiano na wengine. Wengi wenu mnashikilia maoni yenu mwenyewe, na wakati mnafanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na yeye anatoa yake, moja uhusiano na mingine, bila kushirikiana kabisa. Mnajihusisha tu katika kutoa umaizi wenu wenyewe wa ndani, unaingia tu katika kuachilia huru “mizigo” ndani yenu, si kutafuta uzima hata kidogo. Inaonekana kwamba unafanya tu kazi hiyo kwa kutimiza wajibu, daima ukiamini kwamba unapaswa kufuata njia yako mwenyewe bila kujali jinsi watu wengine walivyo, na kwamba unapaswa kushiriki jinsi Roho Mtakatifu anavyokuongoza, bila kujali jinsi watu wengine walivyo.

4/17/2019

Maneno ya Kristo Alipokuwa Akitembea MakanisaniⅠ | Sisitiza Uhalisi Zaidi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu inayofaa zaidi makusudi ya Mungu. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu. Yaani, watu wengi zaidi hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango wa usimamizi wa Mungu. Hadi leo, watu wengi zaidi bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa. Bado hawajui chochote kuhusu umuhimu mahususi wa kumwamini Mungu, na aidha hawana ufahamu wowote wa kazi muhimu kabisa ya Mungu katika mpango Wake wa usimamizi. 

4/16/2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Pili


Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Pili


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho
1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini
2. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Mbalimbali Wenye Imani

4/15/2019

"Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)" Sehemu ya Kwanza


"Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)" Sehemu ya Kwanza


Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho
1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini