7/21/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 95

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 95
Watu hufikiri kila kitu kuwa rahisi sana, wakati kwa kweli hali siyo hivyo. Ndani ya kila kitu kuna siri zilizofichwa, na vile vile hekima Yangu na mipango Yangu. Hakuna utondoti usioangaliwa, na yote yanapangwa na Mimi Mwenyewe. Hukumu ya siku kuu inawafikia wale wote wasionipenda kwa kweli (kumbuka, hukumu ya siku kuu inalenga kila mtu anayepokea jina hili) na kuwasababisha kulia na kusaga meno.

7/19/2019

Matamshi ya Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”



Matamshi ya Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilimali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa. Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.

7/16/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 94

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 94

Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni.

7/13/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 93

Sauti ya Mungu | Sura ya 93

Ukweli unatimizwa mbele ya macho ya mtu na mambo yote yametimizwa. Kazi Yangu inapata hatua, ikipanda juu kama roketi iliyofyatuliwa, ambayo hakuna mtu aliwahi kutarajia. Ni baada ya vitu kufanyika ndipo mtaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu. Watoto wa joka kubwa jekundu si wa pekee na lazima wafanywe kushuhudia matendo Yangu ya ajabu kwa macho yao wenyewe. Usidhani kwamba Sitakutelekeza, sasa kwa kuwa una uhakika kunihusu baada ya kuona matendo Yangu—si rahisi hivyo!

7/10/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 92

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 92
Kila mmoja anaweza kuuona uweza Wangu na hekima Yangu ndani ya maneno Ninayoyazungumza na mambo Ninayoyatenda. Popote Ninapokwenda, kazi Yangu iko pale. Hatua Zangu haziko nchini China pekee, bali muhimu zaidi, ziko katika mataifa yote ya dunia. Ya kwanza kulipokea jina hili, hata hivyo, ni mataifa saba tu ambayo yamezungumziwa hapo awali, kwani hizi ni hatua za kazi Yangu, na hivi karibuni mtaweza kufahamu kabisa kuihusu na mtaielewa kabisa.

7/07/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 91

Sauti ya Mungu | Sura ya 91

Roho Wangu huongea na kutamka sauti Yangu daima—wangapi kati yenu wanaweza kunijua Mimi? Kwa nini lazima Nipate mwili na kuja kati yenu? Hili ni fumbo kubwa. Ninyi mnanifikiria kuhusu Mimi na kunitamani sana siku nzima, na mnanisifu, kunifurahia na kunila na kuninywa kila siku, na ilhali leo bado hamnijui Mimi. Ninyi ni wajinga na vipofu kweli! Jinsi gani mnavyonijua kidogo! Ni wangapi kati yenu wanaweza kufikiria kuhusu mapenzi Yangu?

7/06/2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu  | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo.