Maneno ya Mungu | Sura ya 105
Kwa sababu ya kanuni za maneno Yangu, kwa sababu ya utaratibu wa kazi Yangu, watu hunikana; hili ndilo kusudi Langu la kuzungumza kwa muda mrefu (imezungumzwa kuhusu wazao wote wa joka kubwa jekundu). Ni njia ya hekima ya kazi Yangu; ni hukumu Yangu ya joka kubwa jekundu; huu ni mkakati Wangu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuuelewa kikamilifu. Katika kila kipindi muhimu, yaani, katika kila awamu ya mpito ya mpango Wangu wa usimamizi, baadhi ya watu lazima waondolewe; wanaondolewa kulingana na utaratibu wa kazi Yangu.