9/10/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 107


Wakati maneno Yangu ni makali kwa kiwango fulani, watu wengi huondoka kwa sababu ya maneno Yangu. Ni wakati huu hasa ambapo wazaliwa Wangu wa kwanza wanafichuliwa. Nimesema kuwa Sitafanya lolote, lakini Nitatumia tu maneno Yangu kutimiza mambo yote. Ninatumia maneno Yangu kuwaangamiza wote ambao Ninawachukia, na pia Ninatumia maneno Yangu kuwakamilisha wazaliwa Wangu wa kwanza. (Maneno Yangu yatakaponenwa, ngurumo saba zitatoa sauti, na wakati huo wazaliwa Wangu wa kwanza pamoja na Mimi tutabadili sura na kuingia katika ulimwengu wa kiroho.) Niliposema Roho Wangu hufanya kazi binafsi, Nilichomaanisha ni kuwa maneno Yangu hutimiza yote, na kupitia kwa hili mtu anaweza kuona kwamba Mimi ni mwenyezi.

9/07/2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 106

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Kristo | Sura ya 106


Wale wasioyajua maneno Yangu, wale wasioujua ubinadamu Wangu wa kawaida, na wale wanaokataa uungu Wangu wote wataangamizwa hadi wasikuwepo. Hakuna atakayeachiliwa kutokana na hili, na wote lazima wapitie hili kwa sababu ni amri Yangu ya utawala, na ndicho kifungu kikali zaidi cha amri Yangu. Wale wasioyajua maneno Yangu ni wale ambao wamesikiliza yale ambayo Nimesema wazi, ilhali bado hawayajui, kwa maneno mengine wale ambao hawaelewi masuala ya kiroho (kwa kuwa Sijaumba sehemu hii ya mwili kwa ajili ya wanadamu, Sihitaji mengi kutoka kwao; Nahitaji tu kwamba wasikilize maneno Yangu na kisha wayaweke katika matendo).

9/04/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 105

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu


Maneno ya Mungu | Sura ya 105

Kwa sababu ya kanuni za maneno Yangu, kwa sababu ya utaratibu wa kazi Yangu, watu hunikana; hili ndilo kusudi Langu la kuzungumza kwa muda mrefu (imezungumzwa kuhusu wazao wote wa joka kubwa jekundu). Ni njia ya hekima ya kazi Yangu; ni hukumu Yangu ya joka kubwa jekundu; huu ni mkakati Wangu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuuelewa kikamilifu. Katika kila kipindi muhimu, yaani, katika kila awamu ya mpito ya mpango Wangu wa usimamizi, baadhi ya watu lazima waondolewe; wanaondolewa kulingana na utaratibu wa kazi Yangu.

9/01/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 104

Sauti ya Mungu | Sura ya 104

Watu, matukio na vitu vyote nje Yangu vitakufa na kuwakatika hali ya kutokuwepo, ilhali watu, matukio na vitu vyote vilivyo ndani Yangu vitapata kila kitu kutoka Kwangu na kuingia katika utukufu pamoja na Mimi, kuingia katika Mlima Wangu Sayuni, makazi Yangu, na kuishi pamoja kwa amani nami milele. Niliumba vitu vyote mwanzoni na Nitamaliza kazi Yangu mwishowe, na pia Nitatawala milele kama Mfalme.

8/29/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 103

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 103

Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami. Wale wasiosikiza kile Ninachosema na hawatendi maneno Yangu wanahukumiwa vikali na kupokea laana ya ghadhabu Yangu.

8/26/2019

Wimbo Mpya wa Dini 2019 | “Zingatia Majaliwa ya Binadamu” | Wokovu wa Mungu (Lyrics Video)



 Wimbo Mpya wa Dini 2019 | “Zingatia Majaliwa ya Binadamu” | Wokovu wa Mungu  (Lyrics Video)

Mungu awahimiza makabila yote, mataifa na nyanja zote:
Sikizeni sauti Yake, muione kazi Yake; 
mzingatie hatima ya wanadamu;
mfanye Mungu Mtakatifu na Mheshimiwa,
Mkuu na wa pekee wakuabudiwa,
ulimwengu wote, na wanadamu, waishi chini ya baraka Yake Mungu,
kama vizazi vya Ibrahimu, walivyoishi na ahadi ya Yehova,
kama viumbe vya Mungu, Adamu na Hawa, walivyoishi bustani Edeni.

8/23/2019

Wimbo wa Sifa "Upendo wa Kweli wa Mungu" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitles)



Wimbo wa Kuabudu "Upendo wa Kweli wa Mungu" | Haleluya! Msifuni Mungu! (Korean Song Swahili Subtitles)

Leo naja mbele ya Mungu tena, 
naona uso Wake wa kupendeza.
Leo naja mbele ya Mungu tena, 
nimeacha siku zangu za zamani za kuzurura nyuma yangu.
Leo naja mbele ya Mungu tena, 
kufurahia neno Lake kunanijaza na furaha.
Leo naja mbele ya Mungu tena, 
moyo wangu una mengi ya kusema.