11/04/2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” Sehemu ya Pili



Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu ni Bwana wa kanuni zinazoudhibiti ulimwengu, Anadhibiti kanuni zinazoongoza kuishi kwa vitu vyote, na pia Anadhibiti ulimwengu na vitu vyote kiasi kwamba vinaweza kuishi pamoja; Anaifanya ili kwamba visikwishe au kutoweka ili kwamba binadamu aendelee kuishi, binadamu anaweza kuishi katika mazingira hayo kupitia uongozi wa Mungu. Kanuni hizi zinazoongoza vitu vyote zipo chini ya utawala wa Mungu, na binadamu hawawezi kuingilia na hawawezi kuzibadilisha; ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anajua kanuni hizi na ni Yeye pekee ndiye anazisimamia.”
Video Husika:

     Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu




11/01/2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Wimbo wa Kusifu na Kuabudu

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Mtazamo Kimbele Uliorefushwa


Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?

10/28/2019

Neno la Mungu | "Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?"

Neno la Mungu | "Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?"


Mwenyezi Mungu anasema, "Historia inaendelea mbele, na pia kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu yanaendelea kubadilika. Haingewezekana kwa Mungu kudumisha hatua moja ya kazi kwa miaka elfu sita, kwani kila mwanadamu anajua kwamba Yeye daima ni mpya na kamwe si mzee. Hangeweza kuendelea kuendeleza kazi sawa na kusulubiwa, na mara moja, mara mbili, mara tatu…. kupigwa misumari kwa msalaba. Huu ni mtazamo wa mwanadamu mjinga. Mungu haendelezi kazi sawa, na kazi Yake daima inabadilika na daima ni mpya, jinsi kila siku Nazungumza nanyi maneno mapya na kufanya kazi mpya. Hii ndiyo kazi Ninayofanya, umuhimu wake ukiwa kwa maneno 'mpya' na 'ajabu.' 'Mungu habadiliki, na Mungu daima Atakuwa Mungu'; usemi huu hakika ni ukweli. Kiini cha Mungu hakibadiliki, Mungu daima ni Mungu, na Hawezi kamwe kuwa Shetani, lakini haya hayathibitishi kwamba kazi Yake ni ya daima na kabambe kama kiini Chake. Unatangaza kwamba Mungu yuko hivyo, lakini ni jinsi gani basi unaweza kueleza kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si mzee? Kazi ya Mungu inaendelea kuenea, na mapenzi ya Mungu yanaendelea kujitokeza na kufanywa kujulikana na mwanadamu."

10/24/2019

Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV


Mandhari iliyochorwa katika Biblia “Amri ya Mungu kwa Adamu” ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu, uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao. Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure; Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru, huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu. Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake. Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo, yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga. Kutoka wakati wa kwanza Mungu alipowaumba wanadamu, Mungu aliwaweka chini ya uangalizi Wake. Ni uangalizi wa aina gani huo? Ni jukumu Lake kumlinda mtu na kumchunga mtu. Anamtumainia mtu kuamini katika, kuamini katika na kuyatii maneno Yake. Hiki ndicho kitu cha kwanza ambacho Mungu alikitarajia kwa wanadamu. Akiwa na tumaini hili la kwanza, Mungu aliyasema maneno yafuatayo: “Matunda ya kila mti wa bustani mwaweza kuyala: Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, msiyale, msiyale: kwa maana siku mtakapoyala matunda ya mti huo hakika mtakufa.” Maneno haya rahisi, yakisimamia mapenzi ya Mungu, yaonyesha kuwa kumjali mtu kulikuwa tayari katika moyo Wake. Hivyo, kwa maneno haya rahisi, tunaona kilicho moyoni mwa Mungu. Je, kuna upendo katika moyo Wake? Si kuna utunzaji na dhima? Upendo na utunzaji wa Mungu ni jambo ambalo linaweza kuonekana na kuhisiwa. Kama wewe ni mtu wa dhamiri na una ubinadamu, utajihisi vuguvugu, ukitunzwa na kupendwa, utajihisi mwenye heri na furaha. Unapoyahisi mambo haya, utatenda vipi mintarafu ya Mungu? Utakuwa mwaminifu Kwake? Upendo wa staha, upendo wa staha hutakua katika moyo wako? Moyo wako utasogea karibu na Yeye? Kutokana na haya tunaona, jinsi upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa mtu. Lakini hata muhimu zaidi kuliko hili ni kwamba mtu anaweza kuuhisi na kuuelewa upendo wa Mungu. kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

10/23/2019

Swahili Christian Video "Miaka 17? Hakika!" | The Power of Faith in God


"Kijana! Je, unajua kwamba Chama cha Kikomunisti ni kikana Mungu na kiko kinyume na imani katika Mungu? Katika China, kuna Mungu yupi kwako kuamini? Mungu huyu wako yuko wapi?" "Usifikiri kwamba kwa sababu wewe ni mdogo, tutakuwa wenye huruma kwako! Ukiendelea kumwamini Mungu, utaishia kufa!" Wakiwa na fimbo za umeme mikononi, polisi wa Kikomunisti wa China wanamvamia kijana huyu ambaye amejawa na mavilio ya damu.

10/19/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni” (Dondoo 1)



Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe. Basi iwe ubinadamu Wake au uungu, yote hujiwasilisha kwa mapenzi ya Baba wa mbinguni. Kiini cha Kristo ni Roho, yaani, uungu. Kwa hivyo, chemichemi Yake ni ile ya Mungu Mwenyewe; Dutu hii haitapinga kazi Yake Mwenyewe, na Yeye hangeweza kufanya kitu chochote kinachoharibu kazi Yake Mwenyewe, wala milele Yeye kutamka maneno yoyote ambayo yanakwenda kinyume na mapenzi Yake Mwenyewe. Kwa hiyo, Mungu mwenye mwili kamwe hangefanya kazi yoyote ambayo inasumbua usimamizi Wake Mwenyewe. Hili ndilo ambalo binadamu wote wanapaswa kuelewa. Kiini cha kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya usimamizi wa Mungu Mwenyewe. Vile vile, kazi ya Kristo ni kuokoa binadamu na ni kwa ajili ya mapenzi ya Mungu. Kutokana na kwamba Mungu Anapata mwili, Anatambua dutu Yake ndani ya mwili Wake, kama kwamba mwili Wake ni wa kutosha kufanya kazi Yake. Kwa hivyo, kazi zote za Roho wa Mungu zinabadilishwa na kazi ya Kristo wakati wa kupata mwili, na kwenye msingi wa kazi zote wakati wa kupata mwili ni kazi ya Kristo. Haiwezi kuchanganyika na kazi yoyote ile kutoka enzi nyingine yoyote. Na kwa kuwa Mungu Anakuwa mwili, Yeye Anafanya kazi katika utambulisho wa mwili Wake; kwa kuwa Yeye hukuja katika mwili, kisha Yeye humaliza katika mwili kazi hiyo Anayoazimia kufanya. Iwe ni Roho wa Mungu au ni Kristo, wote ni Mungu Mwenyewe, na Anafanya kazi hiyo Anayoazimia kufanya na hufanya huduma hiyo Anayopaswa kufanya.

10/16/2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Mtazamo Kimbele Uliorefushwa

Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?
Miongoni mwa wanadamu, ni nani aishiye katika uchungu na ambaye amevumilia maelfu ya miaka ya upotovu wa Shetani, ambaye hatamani—hana hamu—ya kuwasili kwa Mungu? Je, ni waumini na wafuasi wangapi wa Mungu katika enzi zote, ambao chini ya ushawishi wa Shetani, wamevumilia taabu na dhiki, mateso na kutengwa? Ni nani asiyetumaini kuwa ufalme wa Mungu utakuja hivi karibuni? Baada ya kuonja furaha na masikitiko ya binadamu, ni nani kati ya wanadamu asiyetamani ukweli na haki vimiliki kati ya wanadamu?
Ufalme wa Mungu utakapokuja, siku inayosubiriwa kwa hamu na mataifa na watu wote hatimaye itafika! Wakati huu, mandhari kati ya vitu vyote mbinguni na duniani yatakuwa yapi? Maisha katika ufalme yatakuwa mazuri kiasi gani? Zikiwa na “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani,” sala za milenia zitatimia!
Iliyotazamwa Mara Nyingi:
Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Wimbo wa Kusifu na Kuabudu
Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu