11/25/2019

“Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari” – Kufichua Fumbo la Kupata Mwili | Swahili Gospel Film Clip 3/6



Ingawa watu wanaomwamini Bwana wote wanajua kwamba Bwana Yesu ni Mungu aliyepata mwili, hata hivyo hakuna kweli anayeweza kuelewa ukweli wa kupata mwili. Imetabiriwa katika Biblia kwamba Bwana atakuja tena katika mwili kuzungumza na kufanya kazi katika siku za mwisho. Kama hatumjui Mungu mwenye mwili, basi hatuna namna ya kukaribisha kuja kwa mara ya pili kwa Bwana. Hivyo, kumjua Mungu mwenye mwili ni muhimu katika kukaribisha kurudi kwa Bwana. Tunapaswaje basi kumjua Mungu mwenye mwili?

11/22/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kuijua Kazi ya Mungu Leo"



Mwenyezi Mungu anasema, "Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho."

11/21/2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli”



Mwenyezi Mungu anasema, “Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote. Enzi nzee ikipita, itabadilishwa na enzi mpya, na mara tu kazi nzee imekamilika, kazi mpya itaendeleza usimamizi wa Mungu. ... Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.”

11/19/2019

“Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari” – Je, Kuna Msingi Katika Biblia wa Kurudi kwa Bwana Kupitia Kupata Mwili? | Swahili Gospel Film Clip 2/6



Watu wengi katika kukaribisha kuja kwa mara ya pili kwa Bwana wanaweka umuhimu tu katika unabii ulio katika Maandiko kwamba Bwana atashuka kutoka mawinguni kuja tena huku wakipuuza unabii kwamba kuja kwa pili kwa Bwana ni kupitia kupata mwili. Wanatangaza kuwa ya uongo njia yoyote ambayo inashuhudia kuja kwa mara ya pili kwa Bwana kama Mungu kuwa mwili. Je, ufahamu wao na kutenda kwao kunapatana na Maandiko? Kuhusu kurudi kwa Bwana kupitia kupata mwili, je, kumetabiriwaje hasa katika Maandiko?

Video Husika:

11/17/2019

“Sauti Nzuri Ajabu” – Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia? | Filamu za Injili (Movie Clip 1/5)


“Sauti Nzuri Ajabu” – Je, Ni Vipi Unabii wa Kurudi kwa Bwana Yesu Unatimia? | Filamu za Injili (Movie Clip 1/5)
  Watu wengi katika ulimwengu wa kidini hufuata unabii unaosema kwamba Bwana atashuka akiwa juu ya wingu na wanamsubiria Yeye kuja kwa njia hiyo kisha kuwanyakua hadi kwenye ufalme wa mbinguni, lakini wanapuuza unabii mbalimbali wa Bwana kuhusu kuja kwa siri: "Tazama, mimi nakuja kama mwizi" (Ufunuo 16:15). "Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha" (Mathayo 25:6). Hivyo unabii huu mbalimbali wa kurudi kwa Bwana unatimizwa vipi? Na tunafaa kuwa vipi wanawali wenye hekima ambao wanakaribisha kurudi kwa Bwana? 
     Video Husika:

Swahili Gospel Movie "Ivunje Laana" | Mungu ni Wokovu Wangu

"Wimbo wa Ushindi" (6) - Njia Inayoongoza kwenye Utakaso na Wokovu

11/14/2019

1. Bwana Yesu Mwenyewe alitabiri ya kwamba Mungu angepata mwili katika siku za mwisho na kuonekana kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi

Aya za Biblia za Kurejelea:
Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja” (Luka 12:40).
Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa” (Mathayo 24:37).
Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia” (Mathayo 24:27).
Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24-25).
Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha” (Mathayo 25:6).
Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).
Na nikapinduka ili kuiona sauti hiyo iliyonizungumzia. Na baada ya kupinduka, nikatazama vinara saba vya taa vilivyokuwa vya dhahabu; Na hapo katikati ya hivyo vinara saba vya taa nilimwona mtu aliyefanana na Mwana wa Adamu, aliyekuwa amevalia nguo iliyofika katika miguu yake, na kifuani alikuwa amefungwa kanda ya dhahabu. Kichwa chake na nywele zilikuwa nyeupe mithili ya sufu, nyeupe mithili ya theluji; na macho yake yalikuwa mithili ya ulimi wa moto; Na miguu yake mithili ya shaba safi, kama kwamba ilikuwa imechomwa ndani ya tanuru; na sauti yake ilikuwa mithili ya sauti ya maji mengi. Na katika mkono wake wa kulia kulikuwa na nyota saba: na alitoa kinywani mwake upanga mkali wenye sehemu mbili za makali: nao uso wake ulikuwa mithili ya jua liangazavyo kupitia nguvu zake yeye” (Ufunuo 1:12-16).
Maneno Husika ya Mungu:
Yesu alisema kwamba Angewasili kama Alivyoondoka, lakini unajua maana halisi ya maneno Yake? Je, angeweza kwa kweli kukwambia? Unajua tu kwamba Atawasili kama Alivyoondoka juu ya wingu, lakini unajua hasa jinsi Mungu Mwenyewe hufanya kazi Yake? Ikiwa ungeweza kuona kweli, basi maneno ya Yesu yanapaswa kuelezwa vipi?  Alisema: Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika siku za mwisho, Yeye Mwenyewe hatajua, malaika hawatajua, wajumbe wa mbinguni hawatajua, na watu wote hawatajua. Baba tu ndiye atakayejua, yaani, Roho pekee ndiye atajua Hata Mwana wa Adamu Mwenyewe hajui, lakini wewe unaweza kuona na kujua? Ikiwa ungekuwa na uwezo wa kujua na kuona kwa macho yako mwenyewe, je, maneno hayo hayakusemwa bure? Na Yesu alisema nini wakati huo? “Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa. Basi kutakuwa na watu wawili shambani; mmoja wao atachukuliwa, na mwingine kuachwa. … Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu.” Wakati siku hiyo itakapofika, Mwana wa Adamu Mwenyewe hataijua. Mwana wa Adamu inahusu umbo la Mungu lililopata mwili wa Mungu, ambaye atakuwa mtu wa kawaida. Hata Mwana wa Adamu mwenyewe hajui, kwa hiyo wewe ungejuaje?
kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

11/10/2019

2019 Swahili Gospel Worship song | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" (Lyrics Video)




2019 Swahili Gospel Worship song | "Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu" (Lyrics Video)


I
Kama washiriki wa jamii ya wanadamu,
kama wafuasi wa Kristo wa dhati,
ni wajibu wetu, ni jukumu letu
kutoa akili zetu na miili yetu
kwa kutimiza agizo la Mungu.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

II
Ikiwa akili na miili yetu haiko kwa ajili ya
agizo la Mungu au njia ya mwanadamu ya haki,
roho zetu hazitastahili waliokufa kishahidi
kwa ajili ya agizo la Mungu,
zaidi haistahili kwa Mungu
anayetupa kila kitu.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu yote ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.
Kwa maana asili yetu, ilitoka kwa Mungu,
na twaishi, kwa ajili ya ukuu Wake.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya