Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Adhimu-na-Zenye-Taadhima. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Adhimu-na-Zenye-Taadhima. Onyesha machapisho yote

12/25/2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | "Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani" Mambo Muhimu 5 | Wimbo wa Kuabudu


Wimbo wa Kwaya ya Injili | "Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani" Mambo Muhimu 5: Tumaini la Milenia Hatimaye Latimia | Wimbo wa Kuabudu

Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?
Miongoni mwa wanadamu, ni nani aishiye katika uchungu na ambaye amevumilia maelfu ya miaka ya upotovu wa Shetani, ambaye hatamani—hana hamu—ya kuwasili kwa Mungu? Je, ni waumini na wafuasi wangapi wa Mungu katika enzi zote, ambao chini ya ushawishi wa Shetani, wamevumilia taabu na dhiki, mateso na kutengwa? Ni nani asiyetumaini kuwa ufalme wa Mungu utakuja hivi karibuni? Baada ya kuonja furaha na masikitiko ya binadamu, ni nani kati ya wanadamu asiyetamani ukweli na haki vimiliki kati ya wanadamu?
Ufalme wa Mungu utakapokuja, siku inayosubiriwa kwa hamu na mataifa na watu wote hatimaye itafika! Wakati huu, mandhari kati ya vitu vyote mbinguni na duniani yatakuwa yapi? Maisha katika ufalme yatakuwa mazuri kiasi gani? Zikiwa na "Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani," sala za milenia zitatimia!


12/01/2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote"


I Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safari ya maisha. Vyovyote vilivyo msingi wako ama safari iliyo mbele yako, hakuna anayeweza kuepuka utaratibu na mpango ambao Mbingu imeweka, na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake, kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote ndiye ana uwezo wa kazi kama hii. II Tangu siku ambayo mwanadamu alikuja kuwepo Mungu amekuwa imara katika kazi Yake, Akisimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na kusonga kwa vitu vyote. Kama vitu vyote, mwanadamu kwa kimya na bila kujua anapokea uboreshaji wa utamu, mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya utaratibu wa mkono wa Mungu. III Moyo na roho ya mwanadamu viko mkononi mwa Mungu, na maisha yote ya mwanadamu yanatazamwa machoni mwa Mungu. Bila kujali kama unaamini katika hili ua la, chochote na vitu vyote, viishivyo au vilivyokufa, vitageuka, vibadilike, vifanywe upya, na kupotea kulingana na fikira za Mungu. Hivi ndivyo Mungu hutawala juu ya vitu vyote. kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Iliyotazamwa Mara Nyingi