Watu! Furahini!
Katika nuru Yangu, watu wanaona nuru tena. Katika neno Langu, watu wanapata vitu vya raha. Nimekuja kutoka Mashariki nami Natoka huko. Wakati ambapo utukufu Wangu unang'aa, mataifa yote yanaangaziwa, vitu vyote vinaletwa katika nuru, hakuna kitu kinachobaki katika giza. Katika ufalme, maisha ya watu wa Mungu pamoja na Mungu ni ya furaha isiyolinganishwa.