7/05/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X  Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu


3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu


Mwenyezi Mungu anasema,"Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache.

7/04/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 90

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 90

Wote walio vipofu lazima waondoke kutoka Kwangu na wasiwepo kwa muda zaidi hata kidogo, kwani wale ambao Nataka ni wale ambao wanaweza kunijua, wanaoweza kuniona na wanaoweza kupata vitu vyote kutoka Kwangu. Na wanaoweza kweli kupata vitu vyote kutoka Kwangu ni nani? Hakika kuna wachache sana wa mtu wa aina hii na hakika watapata baraka Zangu. Nawapenda watu hawa na Nitawachukua mmoja baada ya mwingine kuwa wasaidizi Wangu wakuu, kuwa maonyesho Yangu, na Nitayafanya mataifa yote na watu wote wanisifu bila kukoma, wakishangilia bila kukoma kwa ajili yao wenyewe. 

7/03/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 89

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mungu | Sura ya 89
Sio rahisi kuwa sawa na makusudi Yangu kwa kila kitu unachofanya; sio jambo la kujilazimisha kudanganya, lakini inategemea ikiwa Nilikujalia na akili Yangu kabla ya kuumbwa kwa dunia, ambalo lilikuwa jukumu Langu. Hiki sio kitu watu wanachoweza kufanya. Nitampenda ninayempenda, na yeyote Ninayesema ni mzaliwa wa kwanza hakika ni mzaliwa wa kwanza, hii ni sawa kabisa. Unaweza kutaka kudanganya, lakini huku kutakuwa bure tu! Unadhani Sikutambui? Je, kuwa na tabia nzuri mbele Yangu inatosha?

7/02/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 88

Sauti ya Mungu | Sura ya 88

Watu hawawezi tu kuwaza kiasi ambacho mwendo Wangu umezidisha kasi: Ni ajabu ambayo imetokea isiyoeleweka kwa mwanadamu. Tangu uumbaji wa dunia, mwendo Wangu umeendelea na kazi Yangu haijawahi kusimama. Ulimwengu wote hubadilika siku kwa siku na watu pia wanabadilika mara kwa mara. Hizi zote ni kazi Zangu, mipango Yangu yote na hata zaidi, usimamizi Wangu—hakuna mtu anayejua au kuelewa hivi vitu.

7/01/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 87

Maneno ya Mungu | Sura ya 87

Lazima uharakishe hatua na ufanye kile Nataka kufanya. Hii ni kusudi Langu lenye hamu kwenu. Inawezekana kuwa kwa wakati huu bado hamjaelewa maana ya maneno Yangu? Inawezekana kuwa bado hamjui kusudi Langu? Nimezungumza wazi zaidi na zaidi, na kusema mengi zaidi, lakini, je, ninyi hamjajitahidi kujaribu kuelewa maana ya maneno Yangu? Shetani, usifikiri kwamba unaweza kuharibu mpango Wangu!

6/30/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 86

Sauti ya Mungu | Sura ya 86

Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia. 

6/29/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85

Mimi huwatumia watu tofauti kufanikisha mapenzi Yangu. Laana Zangu hufanikishwa kwa wale Ninaowaadibu na baraka Zangu kufanikishwa kwa wale ambao Ninawapenda. Ambao sasa hukutana na baraka Zangu na ambao hupitia laana Zangu kwa neno Langu moja na tamko Langu. Unajua kuwa yeyote Ninayekuwa mzuri kwake sasa hakika atakutana na baraka Zangu wakati wote (kumaanisha kuwa wale wanaokuja kunijua polepole, wanaokuwa na uhakika kunihusu polepole, wale walio na mwanga mpya na ufunuo na walio na uwezo wa kwenda mwendo sawa na wa kazi Yangu).