12/25/2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | "Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani" Mambo Muhimu 5 | Wimbo wa Kuabudu

Wimbo wa Kwaya ya Injili | "Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani" Mambo Muhimu 5: Tumaini la Milenia Hatimaye Latimia | Wimbo wa Kuabudu

Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?
Miongoni mwa wanadamu, ni nani aishiye katika uchungu na ambaye amevumilia maelfu ya miaka ya upotovu wa Shetani, ambaye hatamani—hana hamu—ya kuwasili kwa Mungu? Je, ni waumini na wafuasi wangapi wa Mungu katika enzi zote, ambao chini ya ushawishi wa Shetani, wamevumilia taabu na dhiki, mateso na kutengwa? Ni nani asiyetumaini kuwa ufalme wa Mungu utakuja hivi karibuni? Baada ya kuonja furaha na masikitiko ya binadamu, ni nani kati ya wanadamu asiyetamani ukweli na haki vimiliki kati ya wanadamu?
Ufalme wa Mungu utakapokuja, siku inayosubiriwa kwa hamu na mataifa na watu wote hatimaye itafika! Wakati huu, mandhari kati ya vitu vyote mbinguni na duniani yatakuwa yapi? Maisha katika ufalme yatakuwa mazuri kiasi gani? Zikiwa na "Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani," sala za milenia zitatimia!

12/23/2019

Latest Swahili Praise and Worship Song | "Tuna Bahati Kukutana na Kuja kwa Mungu" | Tenzi ya Rohoni

Latest Swahili Praise and Worship Song | "Tuna Bahati Kukutana na Kuja kwa Mungu" | Tenzi ya Rohoni

Tuna bahati kukutana na kuja kwa mungu, twaisikia sauti Yake.
Tuna bahati kukutana na kuja kwa mungu, tunahudhuria sikukuu ya Mwanakondoo.
Tunamjua Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaona matendo Yake ya ajabu.
Tunaelewa siri ya maisha ya mwanadamu, maneno ya Mwenyezi Mungu ni ya thamani zaidi.
Tunakula na kunywa maneno ya Mungu, na tunaishi mbele Yake,
tusitafute tena huku na kule.
Tunapopitia hukumu ya Mungu, ingawa tunaweza kuteseka, tunatakaswa.
Tunapata ukweli na njia ya uzima wa milele.
Tukitafuta kumpenda Mungu, hatutawahi kujuta.

Maisha haya yamebarikiwa sana, tunakuwa watu wanaompenda Mungu.
Maisha haya yamebarikiwa sana, tunasifiwa na Mungu.
Kutimiza wajibu wetu, kushuhudia kwa Mungu,
na kufuatilia ukweli kuna maana zaidi.
Nani anaweza kuwa na bahati zaidi?
Nani anaweza kubarikiwa zaidi?
Mungu anatupa ukweli na uzima, lazima tuishi kwa ajili ya Mungu.
Lazima tuishi kwa ajili ya Mungu, lazima tuishi kwa ajili ya Mungu.
Tunapata ukweli na tunashuhudia kwa Mungu ili kulipa upendo wa Mungu.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

12/21/2019

Latest Swahili Worship Song 2019 | "Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa"

Latest Swahili Worship Song 2019 | "Kwa Kuwa Mungu Anamwokoa Mwanadamu, Atamwokoa Kabisa"

I
Kwa kuwa Mungu alimuumba mwanadamu, Atamwongoza;
kwa kuwa Anamwokoa mwanadamu, Atamwokoa na kumpata kabisa;
kwa kuwa anamwongoza mwanadamu, Atamfikisha katika hatima sahihi.
Kwa kuwa Alimuumba mwanadamu na Anamsimamia,
ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu.
Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba.
Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu,
mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.

II
Kwa sababu ni Mungu anayemfanyia mwanadamu kazi, mwanadamu ana hatima
na hatima yake hivyo inahakikishwa, hatima yake inahakikishwa.
Yale ambayo mwanadamu hufuatilia na kutamani ni matarajio aliyo nayo
anapofuata tamaa badhirifu za kimwili,
badala ya hatima, hatima inayotazamiwa na mwanadamu.
Yale ambayo Mungu amemwandalia mwanadamu, kwa upande mwingine,
ni baraka na ahadi zinazomngoja mwanadamu atakapotakaswa,
ambayo Mungu alimwandalia baada ya kuiumba dunia.
Hizo baraka na ahadi hazichafuliwi na fikira
ya mwanadamu na mawazo, au chaguo lake au mwili.
Hii hatima haijaandaliwa kwa mtu mahsusi, mtu mahsusi,
lakini ni mahali pa mapumziko kwa kila mwanadamu.
Hii ndiyo hatima inayofaa, hatima inayofaa kwa mwanadamu.

III
Ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu.
Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba.
Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu,
mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.
Ni lazima awajibikie matarajio na jalaa ya mwanadamu.
Ni hii ndiyo kazi inayofanywa na Muumba.
Ingawa kazi ya ushindi inafanikishwa ikiondoa matarajio ya jamii ya wanadamu,
mwishowe, mwanadamu bado ataletwa katika
hatima sahihi ambayo Mungu amemwandalia.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

12/19/2019

Wimbo wa Kwaya ya Injili | "Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani" Mambo Muhimu 3: Mbingu na Dunia Mpya Baada ya Maafa | Wimbo wa Kuabudu

Wimbo wa Kwaya ya Injili | "Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani" Mambo Muhimu 3: Mbingu na Dunia Mpya Baada ya Maafa | Wimbo wa Kuabudu

Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?

Miongoni mwa wanadamu, ni nani aishiye katika uchungu na ambaye amevumilia maelfu ya miaka ya upotovu wa Shetani, ambaye hatamani—hana hamu—ya kuwasili kwa Mungu? Je, ni waumini na wafuasi wangapi wa Mungu katika enzi zote, ambao chini ya ushawishi wa Shetani, wamevumilia taabu na dhiki, mateso na kutengwa? Ni nani asiyetumaini kuwa ufalme wa Mungu utakuja hivi karibuni? Baada ya kuonja furaha na masikitiko ya binadamu, ni nani kati ya wanadamu asiyetamani ukweli na haki vimiliki kati ya wanadamu?

Ufalme wa Mungu utakapokuja, siku inayosubiriwa kwa hamu na mataifa na watu wote hatimaye itafika! Wakati huu, mandhari kati ya vitu vyote mbinguni na duniani yatakuwa yapi? Maisha katika ufalme yatakuwa mazuri kiasi gani? Zikiwa na “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani,” sala za milenia zitatimia!

12/15/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" (Dondoo 3)

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu" (Dondoo 3)

Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Kwa kuchukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu Wake, unaanza safari yako katika maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeunda, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake mwenyewe, kwa maana yule Anayetawala kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa akitenda kazi Yake kwa njia hii, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mifuatano ya mabadiliko katika mambo yote na njia ambazo yanasongea. Pamoja na vitu vyote vingine, mwanadamu polepole na bila kujua anastawishwa na utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote vingine, mwanadamu bila kujua, anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yake yote yanatazamwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, viwe hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu huongoza vitu vyote.

12/13/2019

Matamshi ya Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

       Matamshi ya Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yanayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake. Hayo ndiyo binadamu wote wanayaamini. Aina hii ya imani kwa Mungu haitaruhusu binadamu kupatwa na kukamilishwa Naye kwa uhakika. Kwa kweli, si kwamba neno la Mungu ni pungufu, badala yake uwezo wa binadamu wa kupokea neno Lake ni duni mno. Inaweza kusemwa karibu binadamu wote hutenda kulingana na nia za Mungu. Badala yake, imani yao kwa Mungu ni kwa mujibu wa nia zao wenyewe, fikra za kidini zilizowekwa, na desturi. Ni wachache wanaopitia mabadiliko baada ya kulikubali neno la Mungu na kuanza kutenda kwa mujibu wa mapenzi Yake. Badala yake, wanaendelea katika imani yao potovu. Wakati mwanadamu anaanza kuamini katika Mungu, anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za kawaida za dini, na anaishi na kuhusiana na wengine kwa misingi ya falsafa yake ya maisha. Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu tisa kati ya kila watu kumi. Ni wachache sana wanaounda mpango mwingine na kuanza mwanzo mpya baada ya kuanza kumwamini Mungu. Hakuna anayeona au kuweka katika vitendo neno la Mungu kama ukweli.