12/06/2019

Maonyesho ya Mungu | "Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" | Only Those Who Know God Can Be Perfected

Maonyesho ya Mungu | "Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" | Only Those Who Know God Can Be Perfected

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. ... Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.”

Iliyotazamwa Mara Nyingi:

Je, Biblia ndiye Bwana, au ni Mungu? | "Bwana Wangu Ni Nani" ( Filamu za Injili )


12/03/2019

“Ivunje Laana” – Bwana Atakaporudi, Ataonekanaje kwa Wanadamu? | Swahili Gospel Movie Clip 2/6

Siku za mwisho tayari zimefika, na waumini wengi wanatamani Bwana arudi na kuwachukua kwenda katika ufalme wa mbinguni. Lakini unajua Bwana atakavyoonekana kwetu Atakaporudi? Je, kweli itakuwa kama tunavyofikiria, kwamba Ataonekana wazi, moja kwa moja Akishuka juu ya wingu? Mwenyezi Mungu alisema, "Je, ungependa kumwona Yesu? Je, ungependa kuishi na Yesu? Je, ungependa kusikia maneno yaliyonenwa na Yesu?… Yesu Atarejea kwa namna gani? Mnaamini kuwa Yesu Atarudi juu ya wingu jeupe, lakini Nawauliza: wingu hili jeupe linaashiria nini? Na kwa kuwa wafuasi wengi wa Yesu wanangoja kurejea Kwake, Atashuka miongoni mwa watu wapi?" "Mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. … Itaashiria mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi, na utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna uashirio wa ukweli tu" (Neno Laonekana katika Mwili).
Iliyotazamwa Mara Nyingi:
Video za Kikristo "Kuamka Kutoka kwa Ndoto" | Kufichua Fumbo la Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni "Wimbo wa Ushindi" (6) - Njia Inayoongoza kwenye Utakaso na Wokovu


12/01/2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote"


I Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safari ya maisha. Vyovyote vilivyo msingi wako ama safari iliyo mbele yako, hakuna anayeweza kuepuka utaratibu na mpango ambao Mbingu imeweka, na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake, kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote ndiye ana uwezo wa kazi kama hii. II Tangu siku ambayo mwanadamu alikuja kuwepo Mungu amekuwa imara katika kazi Yake, Akisimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na kusonga kwa vitu vyote. Kama vitu vyote, mwanadamu kwa kimya na bila kujua anapokea uboreshaji wa utamu, mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya utaratibu wa mkono wa Mungu. III Moyo na roho ya mwanadamu viko mkononi mwa Mungu, na maisha yote ya mwanadamu yanatazamwa machoni mwa Mungu. Bila kujali kama unaamini katika hili ua la, chochote na vitu vyote, viishivyo au vilivyokufa, vitageuka, vibadilike, vifanywe upya, na kupotea kulingana na fikira za Mungu. Hivi ndivyo Mungu hutawala juu ya vitu vyote. kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Iliyotazamwa Mara Nyingi

11/28/2019

Wimbo wa Maneno ya Mungu Mungu Hutumaini Mtu Anaweza Kumjua na Kumwelewa

Kanisa la Mwenyezi Mungu


I
Tangu uhusiano wa kwanza wa Mungu na mwanadamu,
Amekuwa akifichua kwao
Kiini Chake na vile Alivyo na Alicho nacho,
bila kukoma, kila wakati.
Kama watu katika enzi wanaweza kuona au kuelewa,
Mungu huzungumza na kufanya kazi
ili kuonyesha tabia Yake na kiini.

11/25/2019

“Njia ya Kwenda katika Ufalme wa Mbinguni ni Yenye Hatari” – Kufichua Fumbo la Kupata Mwili | Swahili Gospel Film Clip 3/6



Ingawa watu wanaomwamini Bwana wote wanajua kwamba Bwana Yesu ni Mungu aliyepata mwili, hata hivyo hakuna kweli anayeweza kuelewa ukweli wa kupata mwili. Imetabiriwa katika Biblia kwamba Bwana atakuja tena katika mwili kuzungumza na kufanya kazi katika siku za mwisho. Kama hatumjui Mungu mwenye mwili, basi hatuna namna ya kukaribisha kuja kwa mara ya pili kwa Bwana. Hivyo, kumjua Mungu mwenye mwili ni muhimu katika kukaribisha kurudi kwa Bwana. Tunapaswaje basi kumjua Mungu mwenye mwili?

11/22/2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kuijua Kazi ya Mungu Leo"



Mwenyezi Mungu anasema, "Kwa upande mmoja, Mungu katika mwili katika siku za mwisho Anaondoa nafasi iliyochukuliwa na Mungu asiye yakini katika dhana za mwanadamu, ili taswira ya Mungu asiye yakini isiwepo kabisa katika moyo wa mwanadamu. Kwa kutumia maneno Yake halisi na kazi Yake halisi, Anazunguka katika nchi zote, na kazi Anayoifanya miongoni mwa wanadamu ni halisi kabisa na ya kawaida, kana kwamba mwanadamu anakuja kujua uhalisia wa Mungu na Mungu asiye yakini Anapoteza nafasi Yake moyoni mwake. Kwa upande mwingine, Mungu Anatumia maneno yaliyozungumzwa na mwili Wake ili kumfanya mwanadamu mkamilifu, na kukamilisha vitu vyote. Hii ndiyo kazi ambayo Mungu Ataikamilisha wakati wa siku za mwisho."

11/21/2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli”



Mwenyezi Mungu anasema, “Baada ya kazi ya Yehova, Yesu Alipata mwili ili Afanye kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Kazi Yake haikutekelezwa kivyake, ila ilijengwa juu ya misingi ya kazi ya Yehova. Ilikuwa kazi ya enzi mpya baada ya Mungu kukamilisha Enzi ya Sheria. Vivyo hivyo, baada ya kazi ya Yesu kukamilika, Mungu bado Aliendeleza kazi Yake ya enzi iliyofuata, kwa sababu usimamizi wote wa Mungu huendelea mbele siku zote. Enzi nzee ikipita, itabadilishwa na enzi mpya, na mara tu kazi nzee imekamilika, kazi mpya itaendeleza usimamizi wa Mungu. ... Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.”