12/14/2018

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni|Utangulizi

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki


Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni|Utangulizi 


Mnamo Februari 11, mwaka wa 1991, Mungu alitoa tamko Lake la kwanza katika kanisa ambalo lilikuwa na athari isiyo ya kawaida kwa kila mmoja wa watu walioishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu wakati huo. Tamko hili lilitaja yafuatayo: “Makazi ya Mungu yameonekana” na “Mkuu wa ulimwengu, Kristo wa siku za mwisho—Yeye ni Jua linalong’aa.” Kwa maneno haya ya maana sana, watu hawa wote waliletwa katika ulimwengu mpya. Wale wote waliosoma tamko hili walihisi maelezo ya kazi mpya, kazi kuu ambayo Mungu alikuwa karibu kuanzisha.

12/13/2018

"Ndoto Yangu ya Ufalme wa Kibinguni" (1) - Jinsi ya Kufuatilia Ili Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni (1)


        Utambulisho

Waumini wengi wa Bwana wanahisi kwamba almradi tukiyafuata maneno ya Bwana, tukitenda unyenyekevu na uvumilivu, na kufuata mfano wa Paulo kwa kujitolea, kutumia rasilmali na kufanya kazi kwa ajili ya Bwana, tutayaridhisha mapenzi ya Mungu. Na tutaletwa katika ufalme wa mbinguni Bwana atakaporudi. Hata hivyo, je, tumewahi kufikiria iwapo jitihada kama hizi kweli zitastahili sifa za Bwana na ruhusa ya kuingia katika ufalme wa mbinguni? Kama sivyo, tunapaswa kufuatilia kupata sifa ya Bwana na kuletwa katika ufalme wa mbinguni vipi?

Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki Hutoka wapi? Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu

12/12/2018

Neno la Mwenyezi Mungu | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

Neno la Mwenyezi Mungu | Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)


      Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu; hii ni kwa kuwa asili potovu ya mwanadamu inatokana kabisa na Shetani na asili ya mwanadamu imemilikiwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, na aidha haishi katika mwanga.

12/11/2018

Neno la Mwenyezi Mungu|Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo

Neno la Mwenyezi Mungu|Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo


Wale miongoni mwa ndugu na dada ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika Imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi hawatashindwa tu kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomuasi Mungu.

12/10/2018

Video za Kikristo | "Kaa Mbali na Shughuli Zangu" | Christ Is My Lord and My God

Video za Kikristo | "Kaa Mbali na Shughuli Zangu" | Christ Is My Lord and My God


Li Qingxin ni mhubiri katika kanisa la nyumba nchini Uchina ambaye amekuwa mwaminifu kwa Bwana kwa miaka mingi.  Siku zote kwa shauku kubwa anaifanya kazi ya Bwana ya kuieneza injili, akisubiri kwa uangalifu kuja kwa Bwana ili amlete hadi kwenye ufalme wa mbinguni. Katika miaka ya hivi majuzi, Li Qingxin amegundua kwamba vikundi na makanisa mbalimbali yamekuwa na ukiwa zaidi. Umeme wa Mashariki, hata hivyo, limekuwa la kusisimua zaidi, licha ya shutuma na mateso mengi yenye mhemko kutoka kwa serikali ya Kikomunisti ya Uchina na jamii ya dini. Kondoo wazuri zaidi na zaidi na kondoo viongozi wa madhehebu na vikundi mbalimbali wamekubali Umeme wa Mashariki.

12/09/2018

Best Swahili Full Christian Movie | "Wimbo wa Ushindi" | Preaching the Gospel of the Last Days


Best Swahili Full Christian Movie | "Wimbo wa Ushindi" | Preaching the Gospel of the Last Days


Kazi ya hukumu ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho imevuma katika kila farakano na kikundi. Kufuatia kuenea kwa injili ya ufalme, maneno ya Mwenyezi Mungu yanakubaliwa na kuenezwa na watu zaidi na zaidi, waumini wa kweli katika Mungu ambao wana kiu ya Yeye kuonekana wamekuwa wakirudi mmoja kwa mmoja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.

12/08/2018

Neno la Mwenyezi Mungu|Asili na Utambulisho wa Mwanadamu

Neno la Mwenyezi Mungu|Asili na Utambulisho wa Mwanadamu


Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi. Mimi Siwalaumu mwanadamu, wala Siwaangamizi kwa ukatili au kuwatolea kuadibu kusiko na huruma, kwani uovu haukuwa wa wanadamu kiasili.