3/31/2018

Kulipa Gharama ili Kupata Ukweli ni Muhimu Sana

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kulipa Gharama ili Kupata Ukweli ni Muhimu Sana


Mwenyezi Mungu alisema, Sio rahisi kwa vijana kuendeleza kazi; wengi wao hawadumishi mwendo. Ni lazima moyo wako uwe mtulivu, lazima uweze kudumisha mwendo na uwe tayari kutumia muda kwake. Wengine hujiburudisha au kuwachezea wengine, lakini wewe unasema, "Siwezi, sina wakati.

3/30/2018

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu


Katika kipindi kile ambacho Petro alikuwa na Yesu, aliona sifa nyingi za kupendeza ndani ya Yesu, hali nyingi zenye za kustahili kuigwa, na nyingi ambazo zilimkimu. Ingawa Petro aliona nafsi ya Mungu ndani ya Yesu katika njia nyingi, na kuona sifa nyingi za kupendeza, mara ya kwanza hakumjua Yesu. Petro alianza kumfuata Yesu alipokuwa na umri wa miaka 20, na akaendelea kufanya hivyo kwa miaka sita. 

3/29/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Sita

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Sita

Binadamu wanapigwa bumbuazi kwa sababu ya matamshi ya Mungu wanapotambua kwamba Mungu amefanya kitendo kikubwa katika ulimwengu wa kiroho, kitu ambacho mwanadamu hawezi na ambacho Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anaweza kufanikisha. Kwa sababu hii, Mungu mara tena anawasilisha maneno ya huruma kwa wanadamu. Mioyo ya watu inapojaa ukinzani, ikishangaa: “Mungu ni Mungu asiye na huruma au upendo, lakini badala yake Mungu aliyejitolea kuwaangusha binadamu; kwa hiyo mbona Atuonyeshe huruma? Yawezekana kwamba Mungu kwa mara nyingine amehamia kwa utaratibu?” wakati ambapo fikira hii, wazo hili huumbika ndani ya akili zao, wao hung’ang’ana kulishinda kwa nguvu zao zote.

3/28/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Petro

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Petro


Petro ni mfano ambao Mungu aliutambulisha kwa wanadamu, na yeye ni mtu mashuhuri anayejulikana vizuri. Kwa nini mtu mnyonge kama huyo aliwekwa mahala kama mfano na Mungu na amesifiwa na vizazi vya baadaye? Bila shaka, ni wazi kwamba hili halitenganishwi na maonyesho yake na azimio lake la upendo kwa Mungu. 

3/27/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Nne


Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Nne


Ili kuwazuia watu wote kutiwa kiburi na kujisahau baada ya mabadiliko yao kutoka kwa ubaya hadi kwa uzuri, katika fungu la maneno la mwisho la matamshi ya Mungu, mara tu Mungu akishazungumza kuhusu matakwa yake ya juu zaidi kwa watu Wake—mara tu Mungu akishawaambia watu kuhusu mapenzi Yake katika hatua hii ya mpango wa usimamizi Wake—Mungu huwapa nafasi ya kuyatafakari maneno Yake, kuwasaidia kufanya uamuzi wa kuridhisha mapenzi ya Mungu mwishowe.

3/26/2018

Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

 Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?


Ninyi nyote mara nyingi mmepata uzoefu wa hali ya kuwa katika mkutano, na kuhisi kana kwamba huna chochote cha kuhubiri kuhusu—hatimaye unajilazimisha na unasema kitu cha juu juu. 

3/25/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I - Mungu Atumia upinde wa mvua kuasisi agano na mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I - Mungu Atumia upinde wa mvua kuasisi agano na mwanadamu


3. Mungu Atumia upinde wa mvua kuasisi agano na mwanadamu.
(Mwa 9:11-13) Na Nitalithibitisha agano langu nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika kuiharibu nchi. Na Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano Ninalofanya kati yangu na nyinyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, kwa vizazi vyote mpaka milele: Mimi Nauweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi.

3/24/2018

Mbingu Mpya na Nchi Mpya | Tamthilia ya Jukwaa "Kwaya ya Injili ya Kichina 13"


Mbingu Mpya na Nchi Mpya | Tamthilia ya Jukwaa "Kwaya ya Injili ya Kichina 13"

La … la … la … la … Wakati huu wa shangwe, wakati huu wa nderemo (du ba du ba), haki ya Mungu na utakatifu wa Mungu vimeenda ugenini kote ulimwenguni (ba ba ba …), na binadamu wote wanavisifu bila kikomo.

3/23/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Moja

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Moja

Sijawahi kuwa na nafasi ndani ya mioyo ya watu. Ninapowatafuta watu kweli, wao hufunga na kubana macho yao na kupuuza matendo Yangu, kana kwamba yote Nifanyayo ni jaribio la kuwafurahisha, kutokana na hilo wao daima huchukizwa na matendo Yangu.

3/22/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Safina ya Siku za Mwisho | “Siku za Nuhu Zimekuja” Swahili Gospel Video


Kanisa la Mwenyezi Mungu|Safina ya Siku za Mwisho | “Siku za Nuhu Zimekuja” Swahili Gospel Video 

Hebu tumwangalie mwanadamu wakati wa enzi ya Nuhu. Mtu alishiriki katika kila aina ya utendaji wa maovu akikosa kufikiria toba. Hakuna aliyesikiliza neno la Mungu. Ugumu na uovu wao uliamsha hasira ya Mungu na mwishoni, walimezwa na maafa ya mafuriko makuu. Nuhu na familia yake ya watu nane pekee ndio walisikiliza neno la Mungu na walikuwa na uwezo wa kuishi.

3/21/2018

Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Yote kuhusu Mjadala wa “Iwapo Biblia Inatiwa Msukumo na Mungu”


Dondoo ya Filamu ya Bwana Wangu Ni Nani – Yote kuhusu Mjadala wa “Iwapo Biblia Inatiwa Msukumo na Mungu


Kwa miaka elfu mbili, dunia ya kidini imetegemea kile alichosema Paulo kuhusu Biblia kutiwa msukumo na Mungu na daima iliamini kwamba “Biblia ni maneno ya Mungu,” na “Biblia inamwakilisha Bwana.” Je, mawazo haya ni sahihi? Video hii itafichua majibu kwako!
Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

3/20/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Tisa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Tisa

Siku hiyo ambayo vitu vyote vilifufuliwa, Nilikuja miongoni mwa wanadamu, na Nimeshinda naye kwa siku zilizokuwa za ajabu usiku na mchana. Ni katika hatua hii tu ndipo mwanadamu anaona wepesi Wangu wa kufikiwa, na vile uhusiano wake na Mimi unavyozidi kuwa mwingi, anaona baadhi ya kile Ninacho na Nilicho—na kwa sababu hii, anapata ufahamu kunihusu. Miongoni mwa watu wote, Ninainua kichwa Changu na kutazama, na wote wananiona. Hata hivyo, wakati maafa yanaikumba dunia, wanakuwa na wasiwasi mara moja, na sura Yangu inatoweka kutoka katika nyoyo zao; wakishikwa na hofu kutokana na kufika kwa maafa, hawasikii kusihi Kwangu.

3/19/2018

Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Jinsi ya Kufahamu Tabia Yenye Haki ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Watu wanaweza kupangwa kwa makundi, ambayo hubainishwa kwa roho zao. Watu wengine wana roho za binadamu, na wao huchaguliwa kwa njia iliyoamuliwa kabla. Ndani ya roho ya binadamu kuna sehemu iliyoamuliwa kabla. Watu wengine hawana roho; wao ni pepo ambao wamepenyeza.

3/18/2018

Juu ya Hatua za Kazi ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki,

Juu ya Hatua za Kazi ya Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Kutoka nje, inaonekana kwamba hatua za kazi ya Mungu katika kipindi hiki tayari zimemalizwa, na kwamba wanadamu tayari wamepitia hukumu, kuadibu, kuangamizwa, na usafishaji wa maneno Yake, na kwamba wamepitia hatua kama vile jaribio la watendaji huduma, kusafisha kwa nyakati za kuadibu, jaribio la kifo, jaribio la foili[b], na nyakati za[a]kumpenda Mungu. Ingawa watu wamepitia mateso makubwa katika kila hatua bado hawajaelewa mapenzi ya Mungu.

3/17/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Amri za Enzi Mpya

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Amri za Enzi Mpya

Mmeambiwa kuwa mjiandae kwa maneno ya Mungu, ya kuwa pasipo kujali kilichoandaliwa juu yenu, yote yamepangwa kwa mkono wa Mungu, na kwamba hakuna haja ya kuomba kwa bidii au kusali kwenu—haina maana.

3/16/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko La Ishirini Na Nane

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Nane

Nilipokuja kutoka Zayuni, vitu vyote vilikuwa vimenisubiri, na Niliporudi Zayuni, Nilisalimiwa na wanadamu wote. Nilipokuja na kwenda, hatua Zangu hazikuwahi zuiliwa na vitu vilivyokuwa na uadui Kwangu, na kwa hivyo kazi Yangu iliendelea kwa utaratibu. Leo, Ninapokuja miongoni mwa viumbe vyote, vitu vyote vinanisalimu kwa kimya, kwa uoga mkuu kuwa Nitaondoka tena na Niondoe usaidizi kwao.

3/15/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | "Wakati Wa Mabadiliko"(2) - Njia ya Pekee ya Kuinuliwa Kwenda Katika Ufalme wa Mbinguni


Kanisa la Mwenyezi Mungu | "Wakati Wa Mabadiliko"(2) - Njia ya Pekee ya Kuinuliwa Kwenda Katika Ufalme wa Mbinguni

Watu wengine huamini, kwa kuwa Mungu aliweza kuumba mbingu na dunia na vitu vyote kwa neno moja, kuweza kuwafufua wafu kwa neno moja, Mungu pia Ataweza kubadili taswira zetu mara moja, kutufanya watakatifu, kutuinua hewani kukutana na Bwana wakati Atakaporudi katika siku za mwisho. Je, kweli ni ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni? Je, kazi ya kurudi kwa Mungu katika siku za mwisho rahisi hivyo jinsi tunavyofikiri? Mungu husema, "Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo zaidi.

3/14/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu| "Wakati Wa Mabadiliko"(1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?


Kanisa la Mwenyezi Mungu |"Wakati Wa Mabadiliko"(1) - Wanawali Wenye Hekima Hunyakualiwaje?

Watu wengine huongozwa na maneno ya Paulo katika suala la kumngoja Bwana ili kuinuliwa kwenda katika ufalme wa mbinguni: "Kwa ghafla, kufumba na kufumbua, wakati wa tarumbeta ya mwisho: kwa maana tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa bila uovu, na tutabadilishwa" (1Kor 15:52). Wanaamini kwamba ingawa bado tunatenda dhambi siku zote bila kujinasua kutoka kwa pingu za asili ya dhambi, Bwana atazibadili taswira zetu mara moja na kutuleta katika ufalme wa mbinguni Atakapokuja. Pia kuna watu wanaoongozwa na neno la Mungu: "Si kila mtu aniitaye, Bwana, Bwana, ataingia katika ufalme wa mbinguni; lakini yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" (Mat 7:21). "… Kuweni watakatifu, maana mimi ni mtakatifu" (1Pe 1:16).

3/13/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi na Kuingia (6)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu|Kazi na Kuingia (6)


Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi.

3/12/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (8)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (8)

Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, uwe umebadilishwa, hivyo kuokoa nafsi yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na Shetani; ni kwa sababu ya kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana.

3/11/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (4)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (4)


Ikiwa mwanadamu anaweza kuingia kabisa kulingana na kazi ya Roho Mtakatifu, maisha yake yatachipuka haraka kama mmea wa mwanzi baada ya mvua ya majira ya kuchipua. Kwa kuangalia kimo cha sasa wa watu wengi, hakuna mtu hata mmoja anayetilia mkazo umuhimu wa uzima. Badala yake, watu wanaweka umuhimu katika baadhi ya mambo ya juujuu yasiyokuwa na umuhimu. Au wanakimbia huku na kule na kufanya kazi bila malengo na ovyoovyo bila mwelekeo, hawajui waende njia gani na zaidi kwa ajili ya nani.

3/10/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (7)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (7)


Imemchukua mwanadamu mpaka siku hii kutambua kwamba kile mtu anachokosa si tu kuruzukiwa maisha ya kiroho na uzoefu wa kumjua Mungu, lakini, muhimu zaidi, mabadiliko katika tabia yake. Kutokana na ujinga kamili wa mwanadamu wa historia na utamaduni wa kale wa wanadamu, hana ujuzi wa kazi ya Mungu hata kidogo.

3/09/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Utendaji (2)

Katika nyakati zilizopita, watu walijifundisha wenyewe kuwa na Mungu na kuishi katikati ya roho kila wakati, ambao, ukilinganishwa na utendaji wa leo, ni mafundisho rahisi ya kiroho tu. Utendaji kama huu huja kabla ya kuingia kwa watu katika njia sahihi ya maisha, na ni mbinu ya juujuu zaidi na rahisi zaidi kati ya mbinu zote za utendaji. Ni utendaji wa hatua za mwanzoni kabisa za imani ya watu kwa Mungu. Ikiwa watu wataishi kila mara kwa utendaji huu, watakuwa na hisia nyingi sana, na hawataweza kuingia katika uzoefu ambao ni wa kina na wa kweli. Wataweza tu kuzifundisha roho zao, kuifanya mioyo yao iweze kusonga kwa kawaida karibu na Mungu, na kupata kila mara furaha nyingi mno katika kuwa na Mungu. Watakuwa wamejiwekea mipaka kwa ulimwengu mdogo wa kuwa na mshikamano na Mungu, wasiweze kuelewa kile kilicho katika vina vya ndani kabisa. Watu ambao huishi katika mipaka hii pekee hawana uwezo wa kupiga hatua yoyote kubwa. Wakati wowote, wanaweza kulia, "Aa! Bwana Yesu. Amina!" Wanapokula, wao hulia, "Ee Mungu! Nala na Wewe unakula...." Na ni hivi karibu kila siku. Huu ni utendaji wa nyakati zilizopita, ni utendaji wa kuishi ndani ya roho kila wakati. Huo sio utovu wa adabu? Leo, kama ni wakati wa kutafakari juu ya maneno ya Mungu, unapaswa kuyatafakari, kama ni wakati wa kutia ukweli katika vitendo unapaswa kuuweka katika vitendo, na wakati ni muda wa kutekeleza wajibu wako, unapaswa kuutekeleza. Kufanya utendaji hivyo ni huru kabisa, kunakufungua wewe. Sio kama vile wazee wa dini huomba na kusema neema. Bila shaka, hapo awali, hivi ndivyo watu walioamini katika Mungu walitakiwa kutenda—lakini kutenda kwa njia hii kila mara ni kuliko nyuma kimaendeleo kabisa. Utendaji wa wakati uliopita ni msingi wa utendaji wa leo. Ikiwa kungekuwa na njia kwa utendaji wa nyakati zilizopita, utendaji wa leo utakuwa rahisi zaidi. Kwa hiyo, leo, tunapozungumza juu ya "kumleta Mungu katika maisha halisi," ni hali gani ya utendaji inatajwa? "Maisha halisi" hasa yanahitaji watu wawe na ubinadamu wa kawaida; kile ambacho watu wanapaswa kuwa nacho ni kile ambacho Mungu anataka kutoka kwao leo. Kuyaleta maneno ya Mungu katika maisha halisi ndiyo maana halisi ya "kumleta Mungu katika maisha halisi." Leo, watu wanapaswa hasa kujiandaa wenyewe na yafuatayo: Kuhusu suala moja, lazima waendeleze uhodari wao, wafunzwe, waongeze msamiati wao, na kuendeleza ustadi wao wa kusoma; na katika lingine, lazima waishi maisha ya watu wa kawaida. Umerudi tu mbele ya Mungu kutoka ulimwenguni, na lazima kwanza uifunze roho yako, kuufunza moyo wako kuwa na amani mbele ya Mungu. Hili ndilo la msingi kabisa, na pia ni hatua ya kwanza katika kutimiza mabadiliko. Watu wengine ni wepesi kubadilika katika utendaji wao; wao hutafakari ukweli huku wakifua nguo zao, wakielewa ukweli wanaopaswa kuelewa na kanuni wanazopaswa kuweka katika vitendo kwa uhalisi. Katika suala moja, lazima uwe na maisha ya kawaida ya ubinadamu, na katika lingine lazima kuwe na kuingia katika ukweli. Huu ni utendaji bora zaidi kwa maisha halisi.

Zamani, watu walipitia magumu mengi sana, lakini mengine yalikuwa yasiohitajika kwa kweli, kwani mengine yalikuwa mambo ambayo hayakuhitajika kutendwa na mwanadamu. Wanapomleta Mungu katika maisha yao halisi, Mungu kimsingi anahitaji kwamba watu wamwabudu Mungu, wafuatilie ufahamu wa Mungu, na kutekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu katikati ya ubinadamu wa kawaida. Hawahitajiki kumwomba Mungu mara tu wanapoanza kufagia sakafu, wakihisi ni wadeni Wake wasipofanya hivyo. Utendaji wa leo sio hivyo; ni uliolegezwa na rahisi! Watu hawaambiwi watii mafundisho ya dini. Kila mmoja anapaswa kutenda kulingana na kimo chake mwenyewe: Ikiwa mume wako haamini, mchukulie kama mtu asiyemwamini Mungu, na ikiwa yeye huamini mchukulie kama muumini. Usisisitize kuhusu upendo na uvumilivu, bali kuhusu hekima. Watu wengine huenda kununua mboga, na wanapokuwa wakitembea wao hunong'ona: Ee Mungu! Ni mboga gani ambazo unanikubalia ninunue leo? Naomba usaidizi Wako. Je, nichague ninaponunua? Kisha wao hufikiria: Sitachagua; Mungu ananiambia kwamba nimtukuze Yeye, kwamba nilitukuze jina Lake katika mambo yote, na kwamba watu wote wawe na ushuhuda, kwa hiyo muuzaji akinipa kitu fulani cha kitambo na kilichokauka, bado nitampa Mungu shukrani—nitavumilia! Sisi tuaminio katika Mungu hatuchagui ni mboga gani za kununua. Unafikiri kwamba kufanya hivi ni kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na baada ya kutumia yuan[a] moja kununua mboga ya kitambo iliyo na kuvu, bado unaomba na kusema: Ee Mungu! Bado nitaila mboga hii iliyooza—maadamu Unikubali, nitaila. Je, utendaji kama huu sio wa kipumbavu? Je, huko sio kufuata mafundisho ya dini? Hapo awali, watu walizifundisha roho zao na waliishi ndani ya roho kila wakati, na hili lilihusiana na kazi iliyofanywa katika Enzi ya Neema. Uchaji Mungu, unyenyekevu, upendo, uvumilivu, kutoa shukrani kwa mambo yote—haya ndiyo yaliyotakiwa kutoka kwa kila muumini katika Enzi ya Neema. Wakati huo, watu walimwomba Mungu katika mambo yote; wangeomba waliponunua nguo, na walipofahamishwa juu ya mkutano, pia wangeomba na kusema: Ee Mungu! Je, Unanikubalia niende au la? Ikiwa unanikubalia kwenda, basi nitayarishie njia iliyonyooka, acha kila kitu kifanyike kwa urahisi. Na ikiwa hunikubalii kwenda, basi nifanye nianguke chini. Walipoomba, walimsihi Mungu. Baada ya kuomba walihisi wasio na utulivu, na hawakuenda. Pia kulikuwa na dada ambao, kwa vile waliogopa kupigwa na waume wao wasiomwamini Mungu wakati ambapo wangerudi, walihisi wasio na utulivu walipoomba—na kwa vile walihisi wasio na utulivu, hawakuenda kwa mkutano. Waliamini hayo yalikuwa mapenzi ya Mungu, ilhali kweli ni kwamba, iwapo wangeenda, hakuna chochote ambacho kingefanyika. Matokeo ni kwamba walikosa mkutano. Haya yote yalisababishwa na ujinga wa watu wenyewe. Watu wanaofanya utendaji kwa njia hii huishi kwa hisia zao wenyewe. Njia hii ya utendaji ina kosa na ni ya kipumbavu, haina udhahiri, na hisia na mawazo yao wenyewe kwa wingi sana. Ukiambiwa kuhusu mkutano, basi nenda, na usipoambiwa, basi usiende; unapoambiwa kuuhusu, hakuna haja ya kumwomba Mungu. Je, hili si rahisi? Ikiwa, leo, unahitaji kununua kipande fulani cha mavazi, basi nenda ukafanye hivyo. Usimwombe Mungu na kusema: Ee Mungu! Leo napaswa kununua kipande fulani cha mavazi, je, Unanikubalia niende au la? Ni aina gani ya mavazi ninayopaswa kununua? Je dada mmoja akija hapa nikiwa nimeenda? Kwa kuomba na kutafakari, unajiambia mwenyewe: "Sitaki kwenda leo, huenda dada fulani akaja hapa." Ilhali matokeo ni kwamba, kufikia jioni, hakuna aliyekuja hapo, na umekosa mengi. Hata katika Enzi ya Neema, njia hii ya utendaji ilikuwa na makosa na isiyo sahihi. Kwa hiyo, ikiwa watu watafanya utendaji kama katika nyakati zilizopita, hakutakuwa na mabadiliko katika maisha yao. Watakuwa tu watiifu, na hawatatilia maanani upambanuzi, na hawatafanya lolote ila kutii na kuvumilia pasipo kufikiria. Katika wakati huo, watu walisisitiza kuhusu kumtukuza Mungu—lakini Mungu hakupata utukufu wowote kutoka kwao, kwani hawakuwa wameishi kwa kudhihirisha lolote, na hawakuwa wamebadilika. Walijitiisha tu na kujiwekea mipaka wenyewe kulingana na dhana zao wenyewe, na hata miaka mingi ya utendaji haikuleta mabadiliko katika maisha yao; walijua tu kuvumilia, kuwa wanyenyekevu, kupenda, na kusamehe, na hawakupata nuru hata kidogo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Wangemjuaje Mungu?
Watu wataingia tu kwa njia sahihi ya imani katika Mungu ikiwa watamleta Mungu ndani ya maisha yao halisi, na katika maisha yao ya kawaida ya ubinadamu. Leo, maneno ya Mungu yanawaongoza ninyi, na hakuna haja ya kutafuta na kupapasa kama nyakati zilizopita. Wakati ambapo unaweza kutenda kulingana na maneno haya, na unaweza kujichunguza na kujitathmini mwenyewe kulingana na hali ambazo Nimetaja, basi utaweza kubadilika. Haya siyo mafundisho ya dini, lakini kile ambacho Mungu anamtaka mwanadamu afanye. Leo, Nakwambia kiini cha jambo: Jishughulishe tu na kutenda kulingana na maneno Yangu. Matakwa Yangu kwako ni kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, na Nimekwambia hilo tayari; ikiwa unasisitiza kabisa kutenda kwa njia hii, utaweza kuufurahisha moyo wa Mungu. Siku hii ndio wakati wa kuishi katika maneno ya Mungu: Maneno ya Mungu yameeleza yote, yote yamefafanuliwa wazi, na maadamu unaishi kwa maneno ya Mungu, utaishi maisha yaliyo huru kabisa na yaliyokombolewa. Hapo awali, ulipomleta Mungu katika maisha yako halisi, ulipitia mafundisho ya dini na sherehe nyingi sana, ulimwomba Mungu hata katika mambo madogo sana, uliyaweka maneno dhahiri upande mmoja, kutoyasoma, na ukajitolea juhudi zako zote kwa kutafuta—na matokeo kwamba hakukuwa na athari. Chukua mfano wa, kile ulichovaa: Wakati ambapo uliomba, uliliweka jambo hili mikononi mwa Mungu, ukiomba kwamba Mungu achague kitu kinachofaa kwa wewe kuvaa. Mungu aliyasikia maneno haya na kusema: "Unaniomba Nijishughulishe Mimi na tondoti hafifu kama hizi? Ubinadamu wa kawaida na urazini Nilivyokuumbia vimeenda wapi? Wakati mwingine, mtu fulani atafanya makosa katika matendo yake, na ataamini kwamba amemkosea Mungu, naye huanza kufungwa. Hali za watu wengine ni nzuri sana, lakini wanapofanya kitu fulani kidogo kwa njia isiyo sahihi wao huamini kwamba Mungu anawaadibu. Kwa kweli, hii si kazi ya Mungu, lakini ya akili za watu wenyewe. Wakati mwingine, huwa hakuna kosa lolote na vile unavyopitia tukio, laini wengine husema kwamba unapitia tukio kwa njia isiyo sahihi, na hivyo unategwa—unakuwa mbaya, na mwenye giza ndani. Mara kwa mara, watu wakiwa baridi kwa njia hii, wao huamini kwamba wanaadibiwa na Mungu, lakini Mungu husema: "Sifanyi kazi ya kuadibu ndani yako, ungenilaumuje Mimi hivyo?" Watu ni wabaya sana. Wao pia ni wepesi kuhisi sana mara kwa mara na wao hulalamika kuhusu Mungu mara kwa mara. Mungu hakutaki wewe uteseke, ilhali wewe unajiacha uingie katika hali hiyo. Hakuna thamani katika kuteseka kwa aina hii. Kwa sababu watu hawajui kazi inayofanywa na Mungu, katika mambo mengi wao ni wajinga, na hawawezi kuona kwa dhahiri. Katika nyakati kama hizo, wao hunaswa katika mawazo yao wenyewe, wakiendelea kutegwa zaidi milele. Watu wengine husema kwamba vitu vyote na mambo yote yamo mikononi mwa Mungu—kwa hiyo Mungu hangejua watu wanapokuwa wabaya? bila shaka Mungu hujua. Wakati ambapo unategwa katika dhana za binadamu, Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi ndani yako. Wakati mwingi, watu wengine hutegwa katika hali mbaya, lakini Mimi bado huendelea na kazi Yangu. Kama wewe ni mbaya au mtendaji, Mimi sizuiliwi na wewe—lakini unapaswa kujua kwamba maneno mengi Ninenayo, na kiasi kikubwa sana cha kazi Nifanyayo, huja kwa wingi na haraka kulingana na hali ya watu. Wakati ambapo wewe ni mbaya, hili halizuii kazi ya Roho Mtakatifu. Katika nyakati za kuadibu na kifo, watu wote walitegwa ndani ya hali mbaya, lakini hili halikuizuia kazi Yangu; ulipokuwa mbaya, Roho Mtakatifu aliendelea kufanya kilichohitajika kufanywa ndani ya wengine. Unaweza kuendelea kusimama kwa mwezi mmoja, lakini Naendelea kufanya kazi—chochote ufanyacho katika siku za baadaye au sasa, hakiwezi kuizuia kazi ya Roho Mtakatifu. Hali nyingine mbaya hutokana na udhaifu wa binadamu; wakati ambapo watu hawawezi kweli kufanya jambo au kulielewa, wao huwa wabaya. Kwa mfano, katika nyakati za kuadibu, maneno ya Mungu yalizungumza kuhusu kumpenda Mungu kwa kiwango fulani wakati wa kuadibu—lakini wewe uliamini kwamba huwezi. Wakati wa hali hii watu walihisi hasa wenye huzuni na wakaomboleza, walisikitika kwamba miili yao ilikuwa imepotoshwa vikali na Shetani, na kwamba uhodari wao ulikuwa mbaya sana, walihisi kwamba ilisikitisha kuwa walizaliwa katika mazingira haya. Watu wengine walihisi kwamba wakati ulikuwa umepita sana wa kuamini katika Mungu na kumjua Mungu, na kwamba walikuwa hawastahili kufanywa wakamilifu. Hizi zote ni hali za kawaida.
Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za kutotii, ni mchafu ya kusikitisha, ni kitu kichafu. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi, kuna maonyesho mengi sana ya mwili, na kwa hiyo Mungu hudharau mwili kwa kiwango fulani. Watu wanapoacha uchafu, mambo potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini wakibaki bila kuweza kuachana na uchafu na upotovu, basi bado watamilikiwa na Shetani. Kula njama, udanganyifu, na uhalifu wa watu ni mambo ya Shetani; kwa kukuokoa wewe, Mungu hukutenganisha na mambo haya na kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa, na yote ni kwa sababu ya kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unaishi ukimilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na hutapokea urithi wa Mungu. Mara tu umetakaswa na kufanywa kamili, utakuwa mtakatifu, na utakuwa wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na wa kufurahisha kwa Mungu. Kazi inayofanywa na Mungu leo ni wokovu, na, zaidi ya hayo, ni hukumu, kuadibu, na laana. Ina hali nyingi. Je, maneno mengine ya Mungu sio hukumu na kuadibu tu, bali pia laana? Nazungumza ili kutimiza athari fulani, kuwafanya watu wajijue wenyewe, na sio kuwafisha watu; Moyo Wangu ni kwa ajili yenu. Kuzungumza ni mbinu mmojawapo ambayo Mimi hufanyia kazi, Natumia maneno kuonyesha tabia ya Mungu, na kukuruhusu wewe kuelewa mapenzi ya Mungu. Mwili wako waweze kufa, lakini una roho na nafsi. Kama watu wangekuwa na mwili tu, basi hakungekuwa na maana ya wao kuamini katika Mungu, wala hakungekuwa na maana kwa kazi hii yote ambayo Nimefanya. Leo, Nazungumza juu ya jambo moja na kisha lingine, wakati mmoja Ninachukia mno watu, na wakati mwingine Ninapenda kwa hali ya juu; Nafanya hili kuzibadilisha tabia zako, na kuzigeuza dhana zako.
Siku za mwisho zimefika, na nchi nyingi kutoka upande mmoja wa ulimwengu hadi mwingine ziko katika machafuko, kuna vurugu ya kisiasa, njaa, ndwele, mafuriko, na ukame unaonekana kila mahali, kuna maangamizi katika ulimwengu wa mwanadamu, na Mbingu imetuma msiba hapa chini. Hizi ni ishara za siku za mwisho. Lakini kwa watu, unaonekana kama ulimwengu wa uchangamfu na fahari, ambao unaendelea kuwa hivyo zaidi na zaidi. Watu wanapotazama ulimwengu, mioyo yao inavutiwa nao, na wengine hawawezi kujinasua kutoka kwa ulimwengu; idadi kubwa itadanganywa na wale wanaoshiriki katika hila na uchawi. Usipojitahidi ili kuendelea mbele, na huna maadili, utapeperushwa na wimbi hili lenye dhambi. China ni nchi iliyo nyuma sana kimaendeleo kuliko zote, ni nchi ambayo joka kuu jekundu limelala likiwa limejiviringisha, ina watu wengi zaidi wanaoabudu sanamu na kushiriki katika uchawi, hekalu nyingi zaidi, na ni mahali ambapo pepo wachafu huishi. Ulizaliwa ndani yake, unafurahia manufaa yake, na unapotoshwa na kuteswa nalo, lakini baada ya kupitia kujichungua unaachana nalo na unapatwa kabisa na Mungu. Huu ni utukufu wa Mungu, na kwa hiyo hatua hii ya kazi ina umuhimu mkubwa. Mungu amefanya kazi ya kiwango kikubwa hivi, amenena maneno mengi sana, na hatimaye Atawapata ninyi kabisa—hii ni sehemu moja ya kazi ya usimamizi wa Mungu, na ni "mateka ya ushindi" ya vita dhidi ya Shetani. Kadri watu hawa wanavyokuwa bora na kadri maisha ya kanisa yanavyokuwa thabiti, ndivyo joka kuu jekundu linavyotiishwa. Haya ni mambo ya ulimwengu wa kiroho, ni vita vya ulimwengu wa kiroho, na Mungu anapokuwa mshindi, Shetani ataaibishwa na kuanguka chini. Hatua hii ya kazi ya Mungu ina umuhimu wa ajabu. Kazi ya kiwango kikubwa hivyo huokoa kabisa kikundi hiki cha watu; unaponyoka kutoka kwa ushawishi wa Shetani, unaishi katika nchi takatifu, unaishi katika nuru ya Mungu, na hapo kuna uongozi na mwongozo wa nuru, na kisha kuna maana katika kuwa kwako hai. Mnachokula na kuvaa ni tofauti na wao; mnafurahia maneno ya Mungu, na kuishi maisha yenye maana—na wao hufurahia nini? Wao hufurahia tu urithi wa babu zao na "roho ya kitaifa." Hawana hata dalili ndogo kabisa ya ubinadamu! Mavazi, maneno, na matendo yenu vyote ni tofauti na vyao. Hatimaye, mtaacha kabisa uchafu, hamtategwa tena na ushawishi wa Shetani, na mtapata upaji wa Mungu wa kila siku. Mnapaswa kila mara kuwa waangalifu. Ingawa mnaishi mahali pachafu hamjawekwa mawaa na uchafu na mnaweza kuishi ubavuni mwa Mungu, mkipokea ulinzi Wake mkuu. Mmechaguliwa miongoni mwa wote walio katika nchi hii ya manjano. Je, ninyi sio watu waliobarikiwa zaidi? Kama kiumbe aliyeumbwa, unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu na uishi katika mwili mchafu, basi wewe siye mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kama binadamu, unapaswa kutumia rasilmali kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso. Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu, kama Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kinachotolewa na ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya Shetani, na kukanyagiwa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au njia ya kweli, basi ni nini maana ya maisha yako? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale wanaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?

Tanbihi:

a. Yuan: Fedha ya nchi ya China
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Soma Zaidi: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

3/08/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Tano

Mungu anapoweka mahitaji kwa wanadamu ambayo ni magumu kwao kueleza, na maneno Yake yanapogonga moja kwa moja katika moyo wa mwanadamu na watu wanatoa mioyo ya dhati ili Afurahie, basi Mungu huwapa watu nafasi ya kutafakari, kufanya uamuzi, na kutafuta njia ya kutenda. Kwa njia hii, wote ambao ni watu Wake kwa mara nyingine, ngumi zikiwa zimekunjwa kwa ujasiri, wanatoa hali zao zote kwa Mungu.

3/07/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Tamko la Ishirini na Saba


Mwenyezi Mungu alisema, Mienendo ya binadamu haijawahi kuugusa moyo Wangu kamwe, wala kuonekana Kwangu kama kitu cha thamani. Machoni mwa mwanadamu, Mimi humweka katika sheria kali kila wakati, na kila mara Nimemweka chini ya mamlaka kali. Ndani ya matendo yote ya mwanadamu, ni mambo machache sana anayonifanyia Mimi, na mara nyingi hapana kitendo chake kisimamacho imara machoni Pangu. Hatimaye, kila kitu kinachomhusu mwanadamu kimeporomoka polepole mbele Yangu, na ni katika nyakati kama hizi ndipo matendo Yangu hudhihirika, na kumfanya kila mmoja, katika upotovu wake, kunitambua Mimi. Hali ya mwanadamu haibadiliki kamwe. Kilicho ndani ya mioyo yao sio kulingana na mapenzi Yangu—sio Ninachohitaji. Jambo Ninalochukia zaidi ni ukaidi na uhalifu sugu wa mwanadamu na ukaidi sugu, lakini ni nguvu zipi ambazo huwachochea wanadamu waendelee kushindwa kunijua, kuwafanya wawe mbali nami kila mara, kuwafanya wasitende kulingana na mapenzi Yangu na kuwafanya wapinzani Wangu? Je, huu ndio uaminifu wao? Huu ndio upendo wao Kwangu? Mbona wasitubu dhambi zao na kuzaliwa mara ya pili? Mbona binadamu hupenda kuishi kwenye chemichemi badala ya kuishi mahali pasipo na matope? Inawezekana kuwa Mimi Nimewadhulumu? Inawezekana kuwa Mimi Nimewapotosha? Inawezekana kuwa Mimi nimewaelekeza kuzimu? Kila mtu anataka kuishi "kuzimu." Mwangaza unapotokea, macho yao hupofuka ghafla, kwa maana kila walichohifadhi machoni mwao kinatoka kuzimu. Lakini, binadamu hawana ufahamu wa mambo haya, kwa maana wanasherehekea tu "raha za motoni." Wao huweka mambo haya kama vitu vya thamani karibu nao kwa hofu nyingi kuwa Mimi Nitawapokonya, hivyo kuwaacha bila chanzo cha uhai. Wanadamu wananiogopa na ndio maana wao hukaa mbali na Mimi na kutokaa karibu Nami Ninapokuja duniani kwa maana "hawapendi kujiletea madhara," wakiwa na ombi la kuishi maisha ya amani katika jamii ili wawe na "maisha ya furaha duniani." Lakini Sitaruhusu mapenzi yao yafanyike, kwa maana lengo Langu haswa ni kuangamiza familia zao. Punde tu Nitakapofika, amani katika jamii zao itatoweka. Nitasambaratisha mataifa yote, na hata familia ya mwanadamu. Ni nani awezaye kuepuka mkono Wangu? Itawezekanaje kuwa wale wanaopokea baraka wataepuka kwa sababu ya kutonuia kwao? Itawezekanaje kamwe kuwa wale walioadibiwa watapata huruma Yangu kwa sababu ya wao kuwa na woga? Katika maneno Yangu yote, wanadamu wameona mapenzi Yangu na kuona matendo Yangu, lakini ni nani awezaye kujitoa katika minyororo ya mawazo yake mwenyewe? Ni nani anaweza kupata njia kutoka ndani au nje ya maneno Yangu?

Wanadamu waliutambua upendo Wangu, walinipa huduma itokayo moyoni, na walinitii kwa kweli na kunifanyia kila kitu katika uwepo Wangu. Lakini wanadamu leo hii hawajui kuifikia hali hii ya maisha, bali sasa wanaweza tu kulalamika katika nafsi zao kana kwamba ziliibiwa na mbwa mwitu wakali. Wanaweza tu kunitazama na macho yenye hamu, na kunililia wakitaka msaada. Lakini kutoka mwanzo hadi mwisho, hawawezi kujiondoa katika matatizo yanayowakumba. Ninakumbuka pale ambapo watu wa kale waliweka ahadi machoni Pangu, walikiri mpaka mwisho wa dunia mbele Zangu, kulipiza ukarimu Wangu kwa upendo. Walilia kwa uchungu mbele Yangu, na kilio chao kilikuwa cha kuvunja moyo na kigumu kuvumilia. Mara kwa mara, Niliwapa wanadamu msaada kwa sababu ya nia zao. Wanadamu wamekuja mbele Zangu mara nyingi kunitii, na mienendo yao ya kupendeza imekuwa ya kukumbukwa. Mara nyingi wanadamu wamekuja kunionyesha upendo kwa imani isiyotingisika, na hisia zao za kweli zimekuwa za kutamanika. Kwa mara nyingi, wamehatarisha maisha yao ili wanionyeshe upendo, wakanipenda Mimi hata zaidi ya wanavyojipenda wenyewe, na kwa vile Nimeona upendo huu ni wa kweli, Nimeukubali. Mara tena na tena wamejitoa kama sadaka mbele Yangu, bila kujali mauti kwa sababu Yangu, na Nimepangusa wasiwasi huo nyusoni mwao, na kwa uangalifu nimekadiria maumbile yao. Kuna nyakati zisizohesabika ambapo Nimewapenda kama mali Yangu ya thamani, na kuna wakati mwingine mwingi ambao Nimewachukia kama adui Zangu. Hivyo ndivyo Nilivyo—mwanadamu hawawezi kutambua kilicho fikirani Mwangu. Wanadamu wakiwa na huzuni, Mimi huja kuwafariji, na wakiwa wanyonge Mimi huja kuwasaidia katika mwendo. Wanapopotea njia, Mimi huwapa mwelekeo. Wanapolia, Mimi hufuta machozi yao. Hata hivyo, Nionapo huzuni, nani anaweza kunifariji kwa moyo wake? Ninapopatwa na hofu, ni nani hujali hisia Zangu? Ninapoona huzuni, ni nani aniondoleaye uchungu Ninaohisi? Ninapohitaji mtu karibu Nami, ni nani anayeshirikiana na Mimi? Inawezekana kuwa malengo yao ya kale Kwangu yamebadilika yasiweze kurudi tena? Ni kwa nini hakuna hata jambo moja kati ya haya wanalokumbuka? Inawezekanaje kuwa wanadamu wameyasahau yote haya? Je, si mambo haya yanatendeka kwa sababu mwanadamu amepotoshwa na adui zake?

Malaika wanapocheza muziki wakinisifu, hii inasisimua huruma kwa ajili ya binadamu. Ninajawa ghafla na huzuni moyoni Mwangu, na inakuwa vigumu kujiondoa katika hisia hii ya kuhuzunisha. Katika furaha na huzuni ya kutengana na kuunganika Kwangu na mwanadamu, siwezi kupata kubadilishana maoni. Kwa sababu tumetengana mbinguni na wanadamu ardhini, hatukutani mara kwa mara. Ni nani anayeweza kujitoa katika kuwaza mambo mazuri ya kale? Ni nani anayeweza kuzuia picha hizi za ukumbusho kumwonekania? Ni nani asingetumaini kuendelea kwa hisia hizi nzuri? Ni nani hawezi kutarajia kurudi Kwangu? Ni nani asingetamani sana kuunganishwa Kwangu na mwanadamu tena? Moyo Wangu una hofu nyingi, na nafsi ya binadamu imejawa na wasiwasi mwingi. Licha ya sisi kuwa katika nafsi moja, hatuwezi kuwa pamoja mara kwa mara, na hatuwezi kuonana mara kwa mara. Kwa sababu hii, maisha ya wanadamu wote yamepata pigo kuu na hayana nguzo za nguvu muhimu, kwa sababu wamekuwa na hamu kuu Kwangu. Ni kana kwamba wao ni viumbe waliorushwa kutoka mbinguni, wakiliita jina Langu kutoka duniani, wakiinua macho yao Kwangu kutoka ardhini—lakini wanawezaje kuepuka kutoka kwa midomo ya mbwa mwitu mlafi? Wanawezaje kujiokoa kutokana na tishio na majaribu yake? Ikawaje hawakuweza kujitoa wenyewe kwa utiifu kwenye njia ya mpango Wangu? Wanaponisihi kwa sauti, Ninageuza uso Wangu kutoka kwao, kwa maana Sitaki kushuhudia zaidi ya hayo; Lakini, itawezekanaje Nisisikie vilio vya watu hawa? Nitarekebisha udhalimu katika dunia ya mwanadamu. Nitafanya kazi Yangu kwa mikono Yangu mwenyewe ulimwenguni kote, Nikimkomesha Shetani asiwadhuru watu Wangu tena, Nikiwakomesha maadui wasifanye kile wapendacho tena. Nitakuwa Mfalme duniani na kukipeleka kiti Changu cha enzi huko, na kuwafanya maadui waanguke chini na kukiri makosa yao mbele Yangu. Katika hali Yangu ya huzuni na hasira, Nitashinda ulimwengu wote, bila kumwacha yeyote, na kuwashangaza adui wote. Nataka kuiacha dunia ikiwa kwenye maporomoko, ambamo adui wataishi milele, ili wasiweze kuwapotosha wanadamu tena. Mpango Wangu tayari umeamuliwa, na hakuna yeyote, haijalishi ni nani, atakayeweza kuubadilisha. Ninapoelea ulimwenguni Nikitamba, kila mwanadamu atakuwa na umbo jipya, na kila kitu kitapewa uhai tena. Mwandadmu hatalia tena, na hatanililia tena akitaka usaidizi. Hapo, moyo Wangu utajawa na furaha tele, na wanadamu Watanirudia kwa shangwe. Ulimwengu mzima, kutoka juu mpaka chini, utabubujikwa na nderemo …

    Leo hii, miongoni mwa mataifa ya ulimwengu, Ninaendeleza kazi Niliyokusudia kukamilisha. Ninamtembelea kila mmoja, Nikifanya kazi Yangu jinsi Nilivyopanga, na binadamu wote wanayagawanya mataifa mengine ya ulimwengu kulingana na mapenzi Yangu. Watu walio duniani wameweka mawazo yao katika hatima yao wenyewe, kwa maana siku yenyewe inakaribia na tarumbeta ya malaika imeshalia tayari. Hakutakuwa na kuchelewa tena, na kila kiumbe kitaanza kucheza kwa shangwe. Ni nani anayeweza kusongeza siku Yangu kwa uwezo wake? Inawezekana kiwe kiumbe cha duniani? Zinaweza kuwa nyota angani au malaika? Ninapotoa tamko la kuanza ukombozi wa wana wa Israeli, siku Yangu inawaelekea watu wote wa ulimwengu. Kila mwanadamu anahofia kurejea kwa taifa la Israeli. Litakaporejea, hiyo itakuwa siku Yangu ya utukufu, siku ambayo kila kitu kitabadilika na kuwa kipya. Hukumu ya haki itakapofika ulimwenguni, watu wote watakuwa na woga na hofu, kwa maana ulimwengu wa mwanadamu haufahamu haki. Wakati ambapo Jua la haki litaonekana, Mashariki itaangazwa, kisha litaangaza ulimwenguni kote, likimfikia kila mtu. Iwapo mwanadamu atatenda haki Yangu, ni kitu gani kitakuwa cha kuogopesha. Watu Wangu wote wanangoja siku ya kurudi Kwangu, wanatarajia kwa hamu siku Yangu. Wanangoja Mimi nilipize wanadamu wote na kuamua hatima ya wanadamu katika wajibu Wangu kama Jua la haki. Ufalme Wangu unaenea katika ulimwengu mzima, na kiti Changu cha enzi kimenyakua mioyo ya mamia ya milioni nyingi za watu. Kwa usaidizi wa malaika wa mbinguni, utimilifu Wangu mkuu utakamilika hivi karibuni. Halaiki zote za Wanangu na watu Wangu, wanangoja kwa hamu kurejea Kwangu, wakitarajia kuunganishwa Kwangu nao, tusije tukatengana tena. Itawezekanaje watu wote wa ufalme Wangu wasikimbie wakifurahiana kila mmoja kwa kuunganika pamoja na Mimi tena? Inawezekana huu uwe muungano usio na gharama? Mimi Ninaheshimiwa machoni pa kila mtu, Ninadhihirika katika maneno ya kila mtu. Nitakaporejea, Nitashinda nguvu zote za adui hata zaidi. Wakati umewadia! Nitaianza kazi Yangu, Nitatawala miongoni mwa wanadamu! Tazama, Ninarejea! Ninaondoka! Hili ndilo kila mmoja anatarajia, ndilo kila mmoja anatumainia. Nataka kila mmoja ashuhudie kufika kwa siku Yangu na aikaribishe siku Yangu kwa furaha tele!
Aprili 2,1992
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

3/06/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Zingatia Majaliwa ya Binadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Zingatia Majaliwa ya Binadamu


Zingatia Majaliwa ya Binadamu
Mungu awahimiza makabila yote, mataifa na nyanja zote:
Sikizeni sauti Yake, muione kazi Yake;
mzingatie hatima ya wanadamu;
mfanye Mungu Mtakatifu na Mheshimiwa, Mkuu na wa pekee wakuabudiwa,
ulimwengu wote, na wanadamu, waishi chini ya baraka Yake Mungu,
kama vizazi vya Ibrahimu, walivyoishi na ahadi ya Yehova,
kama viumbe vya Mungu, Adamu na Hawa, walivyoishi bustani Edeni.

3/05/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 26

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Sura ya 26

Ni nani ameshinda nyumbani Kwangu? Ni nani amesimama kwa ajili Yangu? Ni nani ameteseka kwa ajili Yangu? Ni nani ameweka ahadi yake mbele Zangu? Ni nani amenifuata hadi leo lakini hajakuwa wa kutojali? Mbona wanadamu wote wana ubaridi na hawana hisia? Mbona binadamu ameniacha? Mbona mwanadamu amechoka na Mimi? Mbona hakuna joto katika ulimwengu wa mwanadamu? Nikiwa Zayuni, Nimeonja joto lililo mbinguni, na Nikiwa Zayuni Nimefurahia baraka iliyoko mbinguni.

3/04/2018

"Ivunje Laana" (5) - Je, Wachungaji na Wazee wa Kanisa wa Ulimwengu wa Dini Wanateuliwa na Bwana Kweli?


"Ivunje Laana" (5) - Je, Wachungaji na Wazee wa Kanisa wa Ulimwengu wa Dini Wanateuliwa na Bwana Kweli?


Mungu mwenyewe hutoa ushuhuda kwa kila mtu Anayemteua na kumtumia. Angalau, wote hupokea uthibitisho wa kazi ya Roho Mtakatifu, huonyesha matunda ya kazi ya Roho Mtakatifu, na wanaweza kuwasaidia watu wa Mungu waliochaguliwa kupokea utoaji wa maisha na uchungaji wa kweli.

3/03/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Tatu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ufafanuzi wa Tamko la Tatu

Leo si tena Enzi ya Neema, wala enzi ya rehema, bali ni Enzi ya Ufalme ambamo watu wa Mungu wanafichuliwa, enzi ambayo kwayo Mungu hufanya mambo moja kwa moja kwa njia ya uungu. Hivyo, katika kifungu hiki cha maneno ya Mungu, Mungu huongoza wale wote ambao wanayakubali maneno Yake katika ulimwengu wa kiroho.

3/02/2018

Christian Testimony Video Swahili "Moyo Uliopotea Waja Nyumbani" Wokovu wa Ajabu wa Mungu


 Christian Testimony Video Swahili "Moyo Uliopotea Waja Nyumbani" Wokovu wa Ajabu wa Mungu


Tangu alipokuwa mdogo, Novo alimwamini Bwana Yesu, kama mama yake tu. Hata kama alisoma Biblia, kuomba, na kuhudhuria mahubiri mara kwa mara, mara nyingi hangeweza kujizuia bali kufuata mielekeo mibaya ya dunia, kutamani raha za mwili, na kudanganya na kusema uwongo…. Alikusudia mara nyingi kuyaacha maisha ya aina hiyo ya kuzunguka katika kutenda dhambi na kukiri, kukiri na kutenda dhambi. Hata hivyo, kila wakati hakufaulu.

3/01/2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Ishirini na Tano


Muda unapita, na kufumba na kufumbua leo imefika. Chini ya uongozi wa Roho Wangu, watu wote wanaishi katikati ya mwanga Wangu, na hakuna anayefikiria yaliyopita ama kuiwekea jana maanani. Nani hajawahi kuishi katika wakati wa sasa? Ni nani ambaye hajapata kupitia katika siku na miezi ya ajabu katika ufalme? Ni nani hajaishi chini ya jua? Ingawa ufalme umeshuka miongoni mwa mwanadamu, hakuna ambaye amepata kupitia ukunjufu wake; mwanadamu anautambua tu kutoka nje, bila kufahamu dutu lake.