7/30/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 98

Maneno ya Mungu | Sura ya 98

Mambo yote yatakuja juu ya kila mmoja wenu, na yatawawezesha kujua zaidi juu Yangu na kuwa na uhakika zaidi juu Yangu. Yatawawezesha kunijua, Mungu mmoja Mwenyewe, kunijua Mimi Mwenye uweza, kunijua Mimi Mungu Mwenyewe mwenye mwili. Baadaye, Nitatoka katika mwili, Nirudi Sayuni, Nirudi katika nchi nzuri ya Kanaani, ambayo ni makazi Yangu, ndiyo hatima Yangu, na ndio msingi ambao niliumba vitu vyote.

7/27/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 97

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 97
Nitafanya kila mtu aone matendo Yangu ya ajabu na kusikia maneno Yangu ya hekima. Ni lazima iwe kila mtu na ni lazima iwe juu ya kila suala. Hii ni amri Yangu ya utawala na ni ghadhabu Yangu. Nitahusisha kila mtu na kila jambo ili watu wote kutoka mwisho mmoja wa ulimwengu hadi mwingine wataona kwa macho yao wenyewe, la sivyo Sitaacha kamwe. Ghadhabu Yangu imemwagwa kikamilifu na hakuna hata chembe imezuiwa. Inaelekezwa kwa kila mtu mmoja ambaye anakubali jina hili (hivi karibuni itageuzwa juu ya mataifa yote ya dunia).

7/24/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 96

Maneno ya Mungu | Sura ya 96

Nitamwadibu kila mtu aliyezaliwa kutoka Kwangu ambaye bado hanijui ili kuonyesha ghadhabu Yangu yote, kuonyesha nguvu Zangu kuu, na kuonyesha hekima Yangu kamili. Ndani Yangu kila kitu ni chenye haki na bila shaka hakuna udhalimu, hakuna udanganyifu, na hakuna upotovu; yeyote ambaye ni mpotovu na mdanganyifu lazima awe ni mwana wa jahanamu—lazima amezaliwa huko kuzimu. 

7/21/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 95

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 95
Watu hufikiri kila kitu kuwa rahisi sana, wakati kwa kweli hali siyo hivyo. Ndani ya kila kitu kuna siri zilizofichwa, na vile vile hekima Yangu na mipango Yangu. Hakuna utondoti usioangaliwa, na yote yanapangwa na Mimi Mwenyewe. Hukumu ya siku kuu inawafikia wale wote wasionipenda kwa kweli (kumbuka, hukumu ya siku kuu inalenga kila mtu anayepokea jina hili) na kuwasababisha kulia na kusaga meno.

7/19/2019

Matamshi ya Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”



Matamshi ya Mungu | “Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Katika maisha yenu ya kila siku, mnaishi katika hali na mazingira yasiyo na ukweli ama fahamu nzuri. Hamna rasilimali ya uwepo na pia hamna msingi wa Kunijua au kujua ukweli. Imani yenu imejengwa tu juu ya ujasiri usio dhahiri au kwenye ibada za kidini na ujuzi kulingana na mafundisho ya kidini kabisa. Kila siku Ninatazama mienendo yenu na kuchunguza nia yenu na matunda yenu maovu.

7/16/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 94

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 94

Narudi Sayuni pamoja na wazaliwa Wangu wa kwanza—kweli mnaelewa maana ya kweli ya maneno haya? Nimewakumbusha tena na tena kwamba Mimi nataka mkue haraka ili mtawale na Mimi. Je, mnakumbuka? Vitu hivi vyote vinahusiana moja kwa moja na kupata mwili Kwangu. Kutoka Sayuni Nilikuja duniani katika nyama ili Nipate kupitia nyama kundi la watu ambao ni wa akili moja na Mimi, na kisha turudi Sayuni.

7/13/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 93

Sauti ya Mungu | Sura ya 93

Ukweli unatimizwa mbele ya macho ya mtu na mambo yote yametimizwa. Kazi Yangu inapata hatua, ikipanda juu kama roketi iliyofyatuliwa, ambayo hakuna mtu aliwahi kutarajia. Ni baada ya vitu kufanyika ndipo mtaelewa maana ya kweli ya maneno Yangu. Watoto wa joka kubwa jekundu si wa pekee na lazima wafanywe kushuhudia matendo Yangu ya ajabu kwa macho yao wenyewe. Usidhani kwamba Sitakutelekeza, sasa kwa kuwa una uhakika kunihusu baada ya kuona matendo Yangu—si rahisi hivyo!

7/10/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 92

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 92
Kila mmoja anaweza kuuona uweza Wangu na hekima Yangu ndani ya maneno Ninayoyazungumza na mambo Ninayoyatenda. Popote Ninapokwenda, kazi Yangu iko pale. Hatua Zangu haziko nchini China pekee, bali muhimu zaidi, ziko katika mataifa yote ya dunia. Ya kwanza kulipokea jina hili, hata hivyo, ni mataifa saba tu ambayo yamezungumziwa hapo awali, kwani hizi ni hatua za kazi Yangu, na hivi karibuni mtaweza kufahamu kabisa kuihusu na mtaielewa kabisa.

7/07/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 91

Sauti ya Mungu | Sura ya 91

Roho Wangu huongea na kutamka sauti Yangu daima—wangapi kati yenu wanaweza kunijua Mimi? Kwa nini lazima Nipate mwili na kuja kati yenu? Hili ni fumbo kubwa. Ninyi mnanifikiria kuhusu Mimi na kunitamani sana siku nzima, na mnanisifu, kunifurahia na kunila na kuninywa kila siku, na ilhali leo bado hamnijui Mimi. Ninyi ni wajinga na vipofu kweli! Jinsi gani mnavyonijua kidogo! Ni wangapi kati yenu wanaweza kufikiria kuhusu mapenzi Yangu?

7/06/2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza



Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu  | “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” sehemu ya kwanza

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo.

7/05/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X  Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Tatu


3. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Watu Wanaomfuata Mungu


Mwenyezi Mungu anasema,"Baada ya hayo, hebu tuzungumzie mzunguko wa uhai na mauti wa wale wanaomfuata Mungu. Hili linawahusu, hivyo kuweni makini. Kwanza, fikiria kuhusu ni makundi gani ambamo watu wanaomfuata Mungu wanaweza kugawika. (Wateule wa Mungu na watendaji huduma.) Kuna mawili: wateule wa Mungu na watendaji huduma. Kwanza tutazungumza kuhusu wateule wa Mungu, ambao ni wachache.

7/04/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 90

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 90

Wote walio vipofu lazima waondoke kutoka Kwangu na wasiwepo kwa muda zaidi hata kidogo, kwani wale ambao Nataka ni wale ambao wanaweza kunijua, wanaoweza kuniona na wanaoweza kupata vitu vyote kutoka Kwangu. Na wanaoweza kweli kupata vitu vyote kutoka Kwangu ni nani? Hakika kuna wachache sana wa mtu wa aina hii na hakika watapata baraka Zangu. Nawapenda watu hawa na Nitawachukua mmoja baada ya mwingine kuwa wasaidizi Wangu wakuu, kuwa maonyesho Yangu, na Nitayafanya mataifa yote na watu wote wanisifu bila kukoma, wakishangilia bila kukoma kwa ajili yao wenyewe. 

7/03/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 89

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mungu | Sura ya 89
Sio rahisi kuwa sawa na makusudi Yangu kwa kila kitu unachofanya; sio jambo la kujilazimisha kudanganya, lakini inategemea ikiwa Nilikujalia na akili Yangu kabla ya kuumbwa kwa dunia, ambalo lilikuwa jukumu Langu. Hiki sio kitu watu wanachoweza kufanya. Nitampenda ninayempenda, na yeyote Ninayesema ni mzaliwa wa kwanza hakika ni mzaliwa wa kwanza, hii ni sawa kabisa. Unaweza kutaka kudanganya, lakini huku kutakuwa bure tu! Unadhani Sikutambui? Je, kuwa na tabia nzuri mbele Yangu inatosha?

7/02/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 88

Sauti ya Mungu | Sura ya 88

Watu hawawezi tu kuwaza kiasi ambacho mwendo Wangu umezidisha kasi: Ni ajabu ambayo imetokea isiyoeleweka kwa mwanadamu. Tangu uumbaji wa dunia, mwendo Wangu umeendelea na kazi Yangu haijawahi kusimama. Ulimwengu wote hubadilika siku kwa siku na watu pia wanabadilika mara kwa mara. Hizi zote ni kazi Zangu, mipango Yangu yote na hata zaidi, usimamizi Wangu—hakuna mtu anayejua au kuelewa hivi vitu.

7/01/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 87

Maneno ya Mungu | Sura ya 87

Lazima uharakishe hatua na ufanye kile Nataka kufanya. Hii ni kusudi Langu lenye hamu kwenu. Inawezekana kuwa kwa wakati huu bado hamjaelewa maana ya maneno Yangu? Inawezekana kuwa bado hamjui kusudi Langu? Nimezungumza wazi zaidi na zaidi, na kusema mengi zaidi, lakini, je, ninyi hamjajitahidi kujaribu kuelewa maana ya maneno Yangu? Shetani, usifikiri kwamba unaweza kuharibu mpango Wangu!