1/31/2019

Maonyesho ya Mungu | "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu"


Maonyesho ya Mungu | "Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Mungu wa siku za mwisho hasa hutumia neno kumfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Hatumii ishara na maajabu kumdhulumu mwanadamu, ama kumshawishi mwanadamu; hii haiweki wazi nguvu za Mungu.

1/30/2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu”


Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Kumjua Mungu Ndiyo Njia ya Kumcha Mungu na Kuepuka Maovu”


Mwenyezi Mungu anasema, “‘Kumwogopa Mungu na kuepuka maovu’ na kumjua Mungu ni uhusiano usiogawanyishwa na uliounganishwa kwa nyuzi zisizohesabika, na uhusiano kati yao ni dhahiri. Iwapo mtu anataka kupata uwezo wa kuepuka maovu, lazima kwanza amche Mungu kwa kweli;

1/29/2019

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo|11. Kiini cha Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo|11. Kiini cha Ulipizaji Kisasi wa Mtu Binafsi


Zhou Li Mji wa Xintai, Mkoa wa Shandong

Wakati fulani kitambo, tulihitaji kuzichora wilaya katika eneo letu, na kwa msingi wa kanuni zetu kwa ajili ya uteuzi wa viongozi, kulikuwa na ndugu mmoja wa kiume aliyekuwa mtaradhia mzuri kiasi. Nilitayarisha kumpandisha cheo hadi kuwa kiongozi wa wilaya.

1/27/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 15

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 15


Kuonekana kwa Mungu tayari kumetokea katika makanisa yote. Roho ndiyo anayeongea, Yeye ni moto mkali, Yeye hubeba uadhama na Anahukumu; Yeye ni Mwana wa Adamu, liyevaa vazi lililofika kwa miguu, na kufungwa mshipi kwenye matiti na ukanda wa dhahabu. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu nyeupe, na macho Yake ni kama mwale wa moto; na miguu Yake iko kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti Yake kama sauti ya maji mengi. Ana nyota saba katika mkono Wake wa kuume, upanga wenye makali kuwili uko katika kinywa Chake na uso Wake ni kama jua liking'aa kwa nguvu zake!

1/26/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 14

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 14


Hapana muda wa kupoteza sasa. Roho Mtakatifu hutumia njia nyingi tofauti za kutuongoza katika maneno ya Mungu na kututayarisha na ukweli wote, kutakaswa, kuwa na undani wa kweli na ushirikiano na Mimi; huruhusiwi nafasi yoyote ya kuchagua. Kazi ya Roho Mtakatifu haina hisia na haijali wewe ni mtu wa aina gani. Mradi tu wewe uko tayari kutafuta na kufuata—si kutoa visingizio, si kubishana juu ya mafanikio yako mwenyewe na hasara lakini kutafuta na njaa na kiu ya haki, basi Nitakupa nuru. Bila kujali jinsi ulivyo mpumbavu na mjinga, Mimi sioni vitu kama hivyo.

1/25/2019

Wimbo wa Kuabudu 2019 | "Mungu Anashuka na Hukumu" | Christ of the Last Days Has Appeared


Nyimbo za Injili | "Mungu Anashuka na Hukumu" | Christ of the Last Days Has Appeared


Anapokuja chini katika taifa la joka kuu jekundu,
Mungu anageuka kuutazama ulimwengu na unaanza kutingika.
Je, kuna mahali popote ambapo hapatapata hukumu Yake?
Ama kuishi katika janga Analotoa?
Kila mahali Aendapo anamwaga mbegu ya janga,
lakini kupitia kwayo Anatoa wokovu na kuonyesha upendo Wake.
Mungu anatamani kuwafanya watu zaidi kumjua, kumwona na kumheshimu.
Hawajamwona kwa muda mrefu, lakini sasa Yeye ni wa kweli kabisa.

1/24/2019

"Wimbo wa Ushindi" (7) - Hukumu ya Mungu katika Siku za mwisho Huwafanya Washindi Kamili.


"Wimbo wa Ushindi" (7) - Hukumu ya Mungu katika Siku za mwisho Huwafanya Washindi Kamili.


Ndugu wa Kanisa la Mwenyezi Mungu huvumilia shida kali na mateso kutoka kwa Chama Cha Kikomunisti cha China na ulimwengu wa dini. Kwa nini wanaendelea kukataa kujisalimisha, kuendelea kuhubiri injili na kumshuhudia Mungu? Je, Mwenyezi Mungu anawaongozaje kupitia hukumu na taabu ya Mungu ili kufikia utakaso na kuwa washindi? Tazama video hii!

Tazama Video: Filamu za Injili

1/23/2019

"Wimbo wa Ushindi" (6) - Njia Inayoongoza kwenye Utakaso na Wokovu


"Wimbo wa Ushindi" (6) - Njia Inayoongoza kwenye Utakaso na Wokovu


Je, kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho humtakasa na kumwokoa vipi mwanadamu? Je, kwa kweli tunapitiaje hukumu na kuadibiwa na Mungu ili tuweze kupata ukweli, uzima, na kustahili wokovu na kuingia katika ufalme wa mbinguni? Video hii itakuambia majibu, na kukuelekeza kwa njia ya kuingia ufalme wa mbinguni.

Tazama Video: Filamu za Injili

1/22/2019

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo|7. Roho Ya Majivuno Kabla ya Kuanguka

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo|7. Roho Ya Majivuno Kabla ya Kuanguka


Baixue Mji wa Shenyang

Kwa sababu ya mahitaji ya kazi, nilihamishiwa hadi sehemu nyingine ya kazi. Wakati huo, nilikuwa na shukurani sana kwa Mungu. Nilihisi kwamba nilikuwa ninapungukiwa sana, lakini kwa njia ya ukuzwaji mtakatifu na Mungu, nilipewa nafasi ya kutimiza wajibu wangu katika eneo la kazi la ajabu hivyo. Niliweka nadhiri kwa Mungu moyoni mwangu: Ningefanya lote ninaloweza kumlipa Mungu.

1/21/2019

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo|6. Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo|6. Huduma ya Aina Hii Kwa Hakika Ni Ya Kudharauliwa


Ding Ning Mji wa Heze, Mkoa wa Shandong

Katika siku chache zilizopita, kanisa limepanga mabadiliko katika kazi yangu. Nilipopokea wajibu huu mpya, niliwaza, "Ninahitaji kuchukua fursa hii ya mwisho kuita mkutano na ndugu zangu wa kiume na wa kike, niongee nao wazi juu ya mambo, na niwaache na picha nzuri." Kwa hiyo, nilikutana na mashemasi kadhaa, na kufikia mwisho wa wakati wetu pamoja, nikasema, "Nimeulizwa kuondoka hapa na kuenda kwa kazi tofauti. Natumaini mtamkubali kiongozi ambaye anakuja kuchukua nafasi yangu na kufanya kazi pamoja naye kwa moyo mmoja na wazo moja." Mara tu waliposikia nikisema maneno haya, baadhi ya dada waliokuwepo walipauka, na tabasamu zikawatoka nyusoni.

1/20/2019

"Wimbo wa Ushindi" (5) - Kwa nini Bwana Anarudi Kufanya Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho


"Wimbo wa Ushindi" (5) - Kwa nini Bwana Anarudi Kufanya Kazi ya Hukumu katika Siku za Mwisho


Watu wengi wanaamini kwamba tayari dhambi zetu zimesamehewa na kupata wokovu kwa sababu tulitangaza imani yetu kwa Bwana, basi kwa nini Bwana anakuja kutuchukua moja kwa moja hadi kwenye ufalme wa mbinguni? Kwa nini bado Anahitaji kuwahukumu na kuwatakasa? Je, hukumu ya Mungu kwa wanadamu katika siku za mwisho ni utakaso na wokovu, au ni shutuma na uharibifu wa wanadamu? Kipande hiki kitakufunulia siri hizo.

Sikiliza zaidi: Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki, Msifuni Mwenyezi Mungu

1/19/2019

"Wimbo wa Ushindi" (4) - Ishara za kuja kwa Bwana Yesu kwa mara ya pili.


"Wimbo wa Ushindi" (4) - Ishara za kuja kwa Bwana Yesu kwa mara ya pili.


Wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, Alihubiri Injili ya Ufalme wa mbinguni popote kwa kiwango kikubwa, na ilivuma katika ulimwengu wote wa kidini na taifa la Kiyahudi. Siku ambayo Bwana Yesu anarudi kufanya kazi Yake, imewatikisa watu kutoka kwa kila farakano na kikundi, na kusababisha hisia fulani duniani kote. Je, umeona ishara za kuja kwa Bwana kwa mara ya pili? Je, umekaribisha kurudi Kwake?

1/18/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 13

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 13


Katika hali yenu ya sasa nyinyi hushika dhana ya "kibinafsi"zaidi kupindukia, na madakizo ya dini ni mazito kiasi. Mmeshindwa kutenda katika roho, hamuwezi kufahamu kazi ya Roho Mtakatifu, na mmekataa mwanga mpya. Huoni jua wakati wa mchana kwa sababu wewe ni kipofu. Huwaelewi watu, umeshindwa kuwaacha wazazi wako, umekosa utambuzi wa kiroho, huijui kazi ya Roho Mtakatifu, na huna wazo la jinsi ya kula na kunywa ya neno Langu[a]. Ni tatizo kuwa hujui jinsi ya kula na kunywa peke yako.

1/17/2019

"Wimbo wa Ushindi" (3) - Washindi wanakuwa aje?


Je, unajua historia ya uumbaji wa washindi 144,000 waliotabiriwa na Kitabu cha Ufunuo? Je, unaelewa umuhimu wa Mungu kuruhusu Chama Cha Kikomunisti cha China kutekeleza udhalimu wake wa hasira, ukandamizaji, na mateso ya watu waliochaguliwa na Mungu?

1/16/2019

"Wimbo wa Ushindi" (2) - Jinsi ya Kugundua Mafarisayo wa Kisasa

"Wimbo wa Ushindi" (2) - Jinsi ya Kugundua Mafarisayo wa Kisasa


Wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, mkuu wa ulimwengu wa dini alimshutumu na kumhukumu, na hatimaye wakaungana na serikali ya Kirumi kumsulubisha. Siku hizi mwenendo wa dhambi wa wale walio katika ulimwengu wa kidini ambao humpinga Mwenyezi Mungu ni sawa na maneno na matendo ya kutisha ya Wayahudi waliompinga Bwana Yesu wakati huo. Kwa nini hili liko hivi? Unajua sababu ya msingi ya kwa nini wanampinga Mungu? Je, unataka kuelewa kiini chao? Basi tazama video hii!

Tazama Video: Filamu za InjiliUmeme wa Mashariki Hutoka wapi?

1/15/2019

"Wimbo wa Ushindi" (1) - Je, Bwana Atatokeaje na Kufanya Kazi Yake Wakati Atakaporudi?

"Wimbo wa Ushindi" (1) - Je, Bwana Atatokeaje na Kufanya Kazi Yake Wakati Atakaporudi?


Ishara ya maafa makubwa wakati wa siku za mwisho- miezi minne ya damu imetokea na nyota za angani zimechukua kuonekana kwa ajabu; maafa makubwa yanakaribia, na wengi wa wale walio na imani katika Bwana wamepata hisia ya kurudi Kwake kwa pili au kwamba tayari Amewasili. Wakati wote wanasubiri kuja kwa mara ya pili kwa Bwana kwa hamu kubwa, labda tumefikiria juu ya maswali yafuatayo: Je, Bwana ataonekanaje kwa mwanadamu Atakaporudi katika siku za mwisho? Je, ni kazi gani ambayo Bwana atafanya wakati Atakapokuja tena? Je, unabii wa hukumu ya kiti kikuu cheupe cha enzi kutoka Kitabu cha Ufunuo utatimizwaje hasa? Video hii fupi itafunua majibu kwako!

Tazama Video: Filamu za Injili,  Chanzo cha Mafanikio ya Umeme wa Mashariki

1/14/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 12

Matamshi ya Mwenyezi Mungu|Sura ya 12


Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako. Ilhali, katika hali rahisi, ungeboronga. Ni lazima uingie ndani kwa mtazamo chanya, uwe mwenye vitendo na si baridi.

1/12/2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 11

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 11


Je, Mimi ni Mungu wako? Je, Mimi ni Mfalme wako? Je, kweli umeniruhusu Mimi kutawala kama Mfalme ndani yako? Unapaswa kutafakari kujihusu kabisa. Je, hukuchunguza na kukataa mwanga mpya na hata kuthubutu kuacha kuufuata ulipokuwa ukija? Kwa sababu ya hii utastahimili hukumu na kuanguka hadi kifo chako, utahukumiwa na kutandikwa kiboko na kiboko cha chuma na hutahisi kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa haraka utapiga magoti katika ibada wakati huo ukilia kwa huzuni. Nimewaambia daima na daima Nimewaeleza na Nimewaambia kila kitu. Fikiria nyuma kulihusu, ni wakati upi Nimewahi kukosa kuwaambia kitu?

1/11/2019

Wimbo wa Kuabudu | "Ni kwa Kufanya Kazi Katika Mwili Pekee Ndiyo Mungu Anaweza Kumpata Binadamu"


Nyimbo za Injili | "Ni kwa Kufanya Kazi Katika Mwili Pekee Ndiyo Mungu Anaweza Kumpata Binadamu"


Kupitia neno la Mungu la utendaji,
unyonge wa mwanadamu na uasi yanahukumiwa na kufichuliwa.
Kisha wanadamu wanapokea wanachohitaji
Wanaona kuwa Mungu amekuja katika ulimwengu huu wa binadamu.
Kazi ya Mungu wa utendaji ina nia ya kumwokoa kila mmoja
kutoka kwa ushawishi wa Shetani,
kuwaokoa kutoka kwa uchafu na kwa tabia yao iliyopotoshwa na Shetani.

1/10/2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 10

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 10

Haupaswi kuwa na hofu ya hili na lile. Haidhuru wingi wa matatizo na hatari unazokabili, utabaki thabiti mbele Yangu; usizuiliwe na kitu chochote, ili mapenzi Yangu yaweze kufanyika. Huu utakuwa ni wajibu wako, vinginevyo utakabiliana na ghadhabu Yangu na mkono wangu uta..., na utavumilia mateso ya akili yasio na mwisho. Ni lazima uyavumilie yote, lazima uviachilie vitu vyote ulivyo navyo, na kufanya kila kitu unachoweza kunifuata Mimi, kulipa gharama zote kwa ajili Yangu.

1/09/2019

Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli

Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli


Mnapotaka kumpenda na kumjua Mungu leo, kwa upande mmoja ni lazima mstahimili mateso, usafishaji, na kwa ule upande mwingine, ni lazima mgharamike. Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu.

1/08/2019

Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God

Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God


Mungu huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni za kipekee,
haidhibitiwi na watu, matukio au vitu.
Na hakuna awezaye kubadili dhana au mawazo Yake,
au kumshawishi Ajaribu njia tofauti.
Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki!

Wimbo wa Kuabudu "Viumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu" | Manifestation of Power of God


Wimbo wa Kuabudu "Viumbe Wote Lazima Waje Chini ya Utawala wa Mungu" | Manifestation of Power of God


Mungu aliumba vitu vyote, na hivyo Yeye hufanya viumbe vyote
kuja chini ya amri Yake, na kutii utawala Wake.
Anaamuru vitu vyote, akividhibiti katika mikono Yake.

1/06/2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 9

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 9


Nataka kukukumbusha kwamba huwezi kuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya neno Langu na kutokujali kwa aina yoyote hakukubaliki. Unapaswa kulisikiliza na kulitii na kutenda mambo kulingana na nia Zangu. Daima lazima uwe macho na kamwe usiwe na tabia ambayo ni ya kiburi na ya kujidai, na lazima kila wakati unitegemee Mimi ili kutupilia mbali tabia ya zamani ya asili ambayo hukaa ndani yako. Unapaswa daima kuwa na uwezo wa kudumisha hali ya kawaida mbele Yangu, na uwe na tabia thabiti Kuwaza kwako lazima kuwe kwa busara na wazi na hakupaswi kuyumbishwa au kudhibitiwa na mtu yeyote, tukio, au kitu.

1/05/2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 8

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 8


Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu.

1/04/2019

Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God


Wimbo wa Kuabudu | "Umuhumi wa Maombi" | How to Gain the Praise of God


Maombi ni njia moja ya mwanadamu kushirikiana na Mungu,
kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu.
Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kuangaziwa na kuwa mwenye nguvu-nia.
Watu kama hao wanaweza kufanywa kamili hivi karibuni.
Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo utakavyoguswa zaidi, kuangaziwa na kuwa mwenye nguvu-nia.
Watu kama hao wanaweza kufanywa kamili hivi karibuni.

1/03/2019

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (6) : Mwenyezi Mungu Hutoa Njia ya Uzima wa Milele kwa Binadamu


"Nimewahi Treni ya Mwisho" (6) : Mwenyezi Mungu Hutoa Njia ya Uzima wa Milele kwa Binadamu


Mwishoni mwa Enzi ya Sheria, Wayahudi walishikilia kwa ukaidi sheria yao na kukataa kukubali kazi ya Bwana Yesu, ambayo iliwafanya waanguke katika giza na kupoteza wokovu wa Mungu. Sasa katika zile siku za mwisho, dunia nzima ya kidini inalinda tu jina la Bwana Yesu na kukataa kumkubali Mwenyezi Mungu, na hivyo kuisababisha kuwa na ukiwa zaidi na zaidi na kuwa jangwa lilisoweza kuzaa matunda. Kwa nini hasa iko hivi?

1/02/2019

"Nimewahi Treni ya Mwisho" (5) : Matokeo Yanayofikiwa na Kazi ya Mungu Aliyepata Mwili


"Nimewahi Treni ya Mwisho" (5) : Matokeo Yanayofikiwa na Kazi ya Mungu Aliyepata Mwili


Bwana Yesu alitabiri kwamba katika zile siku za mwisho, ngano itatenganishwa na matawi, kondoo na mbuzi, na watumishi wema kutoka kwa watumishi waovu. Unajua jinsi unabii huu unatimizwa? Je, ungependa kujua njia ambayo Mungu anafanya kazi ya kutenganisha kila moja kwa aina yake katika zile siku za mwisho? Ikiwa unataka kupata ufahamu zaidi, tafadhali angalia video hii fupi!

 Tazama Video: Filamu za Injili

1/01/2019

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 7

Matamshi na Ushuhuda wa Kristo Mwanzoni | Sura ya 7


Kuinuka kwa mazingira pande zetu zote huharakisha kurudi nyuma kwetu katika roho. Usitende kwa moyo mgumu, usipuuze kwa vyovyote vile kama Roho Mtakatifu Ana wasiwasi, usijaribu kuwa mjanja na usiwe na ridhaa kupita kiasi na kuridhika kibinafsi au kuzingatia sana matatizo yako mwenyewe; kitu pekee cha kufanya ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Huwezi kuyaacha maneno ya Mungu nyuma au kuyapa kisogo; lazima uyaelewae kwa makini, rudia kuomba-kusoma kwako, na uelewe maisha ndani ya maneno hayo.