6/30/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 86

Sauti ya Mungu | Sura ya 86

Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia. 

6/29/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 85

Mimi huwatumia watu tofauti kufanikisha mapenzi Yangu. Laana Zangu hufanikishwa kwa wale Ninaowaadibu na baraka Zangu kufanikishwa kwa wale ambao Ninawapenda. Ambao sasa hukutana na baraka Zangu na ambao hupitia laana Zangu kwa neno Langu moja na tamko Langu. Unajua kuwa yeyote Ninayekuwa mzuri kwake sasa hakika atakutana na baraka Zangu wakati wote (kumaanisha kuwa wale wanaokuja kunijua polepole, wanaokuwa na uhakika kunihusu polepole, wale walio na mwanga mpya na ufunuo na walio na uwezo wa kwenda mwendo sawa na wa kazi Yangu).

6/28/2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Saba


Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Saba

Mwenyezi Mungu anasema, “Kuonekana kwa Bwana Yesu kulifanikisha kujali Kwake kwingi kwa minajili ya wafuasi Wake katika ubinadamu na akakupokeza kwa mwili Wake wa kiroho, au unaweza kusema uungu Wake. Kuonekana Kwake kuliwaruhusu watu kuwa na hali nyingine waliyopitia na hisia walizopitia zinazohusu kujali na utunzaji wa Mungu huku kukithibitisha kwa uthabiti kwamba Mungu Ndiye anayefungua enzi, anayeiendeleza enzi, na Yeye ndiye anayetamatisha enzi.

6/27/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 84

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 84
Kwa sababu ya ukosefu wao wa ujuzi kunihusu Mimi, mwanadamu amekatiza usimamizi Wangu na kudhoofisha mipango Yangu mara zisizo na idadi, lakini hawajawahi kuweza kuzuia hatua Zangu zinazoendelea mbele. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mungu wa hekima. Pamoja na Mimi kuna hekima isiyo na mipaka; pamoja na Mimi kuna siri isiyo na mipaka na isiyoweza kueleweka. Mwanadamu hajawahi kuweza kuielewa na kuifahamu kabisa tangu zamani za kale hadi milele. Je, hilo haliko hivyo?

6/26/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 83

Maneno ya Mungu | Sura ya 83

Hujui kwamba Mimi ni Mwenyezi Mungu; hujui kwamba mambo yote na vitu vyote viko chini ya udhibiti Wangu! Maana ya kila kitu huumbwa na kukamilishwa na Mimi ni ni? Baraka au misiba ya kila mtu hutegemea utimilifu Wangu, matendo Yangu. Mwanadamu anaweza kufanya nini? Mwanadamu anaweza kufanikisha nini kwa kufikiri? Katika enzi hii ya mwisho, katika enzi hii potovu, katika dunia hii ya giza ambayo Shetani ameipotosha sana, ni kina nani wachache ambao wako jinsi Nipendavyo?

6/25/2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 82

Matamshi ya Mungu | Sura ya 82

Wote wanaogopa wanaposikia neno Langu. Wote wamejawa na hofu. Mnaogopa nini? Sitawaua! Ni kwa sababu mnahisi hatia na mnaogopa kugunduliwa. Yale unayoyafanya nyuma Yangu ni ya upuuzi na yasiyo na maana kabisa. Hili limenifanya Nikuchukie sana hivi kwamba Ninatamani sana Ningekuwa nimewatupa wale ambao Sikuwa nimewajaalia wala kuwachagua katika shimo lisilokuwa na mwisho wavunjwe vipande vipande. Hata hivyo, Nina mpango Wangu, Nina malengo Yangu.

6/24/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 81

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Sauti ya Mungu | Sura ya 81

Oh, enzi hii mbaya na yenye uzinzi! Nitakumeza! Mlima Sayuni! Simama unisifu Mimi! Kwa kukamilika kwa mpango Wangu wa usimamizi, kwa kukamilika kwa kazi Yangu kuu, ni nani athubutuye kutoinuka na kufurahi! Ni nani athubutuye kutoinuka na kuruka kwa furaha bila kukoma! Atakutana na kifo chake mkononi Mwangu. Mimi hutekeleza haki kwa kila mtu, bila huruma hata kidogo au upendo wa fadhila, na bila kupendelea. Watu wote! Simameni ili kutoa sifa, Nipeni utukufu!

6/23/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI Utakatifu wa Mungu (III)” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema: “Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwa madhara na udhibiti wa Shetani.

6/22/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 80

Maneno ya Mungu | Sura ya 80

Kila kitu kinahitaji mawasiliano halisi na Mimi ili kupata nuru na kuangazwa; aidha, ni kwa njia hii tu ndio roho inaweza kuwa na amani. La sivyo, haitakuwa na amani. Sasa ugonjwa mbaya zaidi kati yenu ni kutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida kutoka kwa uungu Wangu kamili; aidha, wengi wenu huweka mkazo kwa ubinadamu Wangu wa kawaida, kama kwamba kamwe hawajui kuwa Mimi nina uungu kamili pia. Hii inanikufuru Mimi! Je, mnajua? Ugonjwa wenu ni mbaya sana kiasi kwamba msipoharakisha kuurekebisha mtauawa kwa mikono Yangu.

6/21/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 79

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 79

Vipofu! Wajinga! Rundo la takataka lisilo na maana! Nyinyi hutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida na uungu Wangu! Je, hamfikiri kuwa hii ni dhambi dhidi Yangu? Na zaidi ni kuwa ni kitu ambacho ni vigumu kusamehe! Mungu wa vitendo anakuja miongoni mwenu leo lakini mwajua tu upande Wangu mmoja ambao ni ubinaamu Wangu wa kawaida, na hamjaona kabisa upande Wangu ambao ni wa kiungu kabisa. Je, unafikiri kuwa Sijui anayejaribu kunidanganya kisirisiri?

6/20/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 78

Umeme wa Mashariki,Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 78
Nimesema kabla ya kuwa kazi inafanywa na Mimi, sio na mwanadamu yeyote. Kwangu, kila kitu kimetulia na kufurahi, lakini na ninyi mambo ni tofauti sana na chochote mnachofanya ni kigumu sana. Kitu chochote Ninachokubali hakika kitatimizwa na Mimi, wakati mtu yeyote Ninayemkubali atakamilishwa na Mimi. Wanadamu—msiingilie katika kazi Yangu! Chote tu mnachohitaji kujishughulisha nacho ni kufuata uongozi Wangu, kufanya kile Ninachopenda, kukataa yote ambayo Ninayachukia, mjivute kutoka kwa dhambi, na mjitupe ndani ya kumbatio Langu lenye upendo.

6/19/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 77

Sauti ya Mungu | Sura ya 77

Kutokuwa na hakika ya maneno Yangu ni sawa na kushikilia mtazamo wa kukanusha kuelekea matendo Yangu. Yaani, maneno Yangu yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini hamyatilii maanani. Ninyi hamko makini! Maneno mengi yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini ninyi ni wenye mashaka, hamyajui sana. Ninyi ni vipofu! Hamwelewi madhumuni ya kila kitu ambacho Nimefanya. Je, maneno Ninayoyaeleza kupitia kwa Mwanangu si maneno Yangu?

6/18/2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Pili

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitu vyote haviwezi kutenganishwa na kanuni ya Mungu, na hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kujitenganisha kwenye kanuni Yake. Kupoteza kanuni Yake na kupoteza uangalizi wake kungekuwa na maana kwamba maisha ya watu, maisha ya watu katika mwili yangetoweka. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuanzisha mazingira kwa ajili ya binadamu kuendelea kuishi.

6/17/2019

Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”



Neno la Mungu | “Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu”

Mwenyezi Mungu anasema, “Vitendo vyote na matendo ya Shetani vinaonyeshwa kupitia kwa binadamu. Sasa vitendo vyote na matendo yote ya binadamu ni maonyesho ya Shetani na hivyo basi haviwezi kumwakilisha Mungu. Binadamu ni mfano halisi wa Shetani, na tabia ya mwanadamu haiwezi kuiwakilisha tabia ya Mungu. Baadhi ya wanadamu ni wenye tabia nzuri; Mungu anaweza kufanya baadhi ya kazi kupitia kwa tabia hiyo nayo kazi yao inatawaliwa na Roho Mtakatifu.

6/16/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 76

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 76

Matamshi Yangu yote ni maonyesho ya mapenzi Yangu. Ni nani anayeweza kuudhukuru mzigo Wangu? Nani anayeweza kuelewa nia Yangu? Je, mmefikiria kila moja ya maswali Niliyoibua kwenu? Uzembe ulioje! Unathubutu vipi kuvuruga mipango Yangu? Wewe u mshenzi kweli! Kazi kama hii ya pepo wabaya ikiendelea, Nitawatupa mautini mara moja katika shimo lisilo na mwisho! Kwa muda mrefu Nimeona waziwazi matendo mbalimbali ya pepo wabaya.

6/15/2019

Matamshi ya Kristo | Sura ya 75

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Kristo | Sura ya 75
Yote yatatimizwa punde tu maneno Yangu yanapozungumzwa, bila kupotoka hata kidogo. Kuanzia sasa kwendelea, mafumbo yote yaliyofichwa hayatazuiwa au kufunikwa hata kidogo, na yatafichuliwa kwenu—wanangu wapendwa. Nitakufanya uone hata ishara na maajabu kubwa zaidi ndani Yangu, na kuona hata mafumbo makubwa zaidi. Mambo haya hakika yatawashangaza na kuwapa ufahamu bora zaidi wa Mimi, mwenyezi Mungu, na kuwaruhusu kufahamu hekima Yangu humo.

6/14/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 74

Sauti ya Mungu | Sura ya 74

Wamebarikiwa wale ambao wamelisoma neno Langu na kuamini kwamba litatimizwa—Sitakutendea vibaya, lakini Nitafanya yale unayoamini yatimizwe kwako. Hii ni baraka Yangu ikija juu yako. Neno Langu linapiga siri zilizofichwa ndani ya kila mtu. Kila mtu ana majeraha ya mauti, na Mimi ni tabibu mzuri ambaye anayaponya—njoo tu katika uwepo Wangu. Kwa nini Nilisema kuwa katika siku zijazo hakutakuwa tena na huzuni na hakutakuwa na machozi?

6/13/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 73

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 73

Maneno Yangu yanatimizwa mara tu yanaposemwa; hayabadiliki kamwe na ni sahihi kabisa. Kumbuka hili! Kila neno na kirai kutoka katika kinywa Changu lazima yafikiriwe kwa uangalifu. Kuwa makini zaidi, usije ukapitia upotezaji na kupokea hukumu Yangu, ghadhabu Yangu na moto Wangu pekee. Kazi Yangu sasa inasonga kwa haraka sana, lakini ni safi na ni ya kutaka uangalifu mkubwa hadi kwa kiasi fulani—karibu haionekani kwa jicho tupu na haiwezi kuguswa na mikono ya mwanadamu. Ni ya kutaka uangalifu mkubwa hasa.

6/12/2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IX Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (III)” Sehemu ya Tatu

Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu alipoumba vitu vyote, alitumia aina zote za mbinu na njia za kuziwekea uwiano, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya milima na maziwa, kuweka uwiano katika mazingira ya kuishi kwa ajili ya mimea na aina zote za wanyama, ndege, wadudu—lengo Lake lilikuwa ni kuruhusu aina zote za viumbe hai kuishi na kuongezeka ndani ya sheria ambazo alikuwa Amezianzisha.

6/11/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 72

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 72

Sharti unitegemee kuondoa upungufu ama udhaifu mara tu unapougundua. Usichelewe; vinginevyo kazi ya Roho Mtakatifu atakuwa mbali sana nawe, na utaanguka nyuma mbali sana. Kazi ambayo Nimekuaminia inaweza kutimizwa kwa kupitia tu kukaribia kwako mara kwa mara, kuomba, na kuwa na ushirika katika uwepo Wangu. Kama sivyo, hakuna matokeo yoyote yatakayofikiwa, na kila kitu kitakuwa bure. Kazi Yangu leo si kama ilivyokuwa awali. Kadiri ya maisha kwa watu Ninaowapenda si kama ilivyokuwa mbeleni.

6/10/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 71

Maneno ya Mungu | Sura ya 71

Mimi wote Nimejiweka dhahiri kwenu, lakini kwa nini mnashindwa kutafakari maneno Yangu kwa mioyo na nafsi zenu zote? Kwa nini mnachukua maneno Yangu kama takataka? Je,yote Ninayosema ni makosefu? Je, maneno Yangu yamekupiga katika sehemu ya uzima? Daima kuchelewesha, daima kusita, kwa nini mnafanya mambo hivi? Je, Mimi sijaongea wazi?

6/09/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 70

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu | Sura ya 70

Kwamba siri Yangu imefichuliwa na kuonyeshwa bayana, pasi kufichwa tena, ni kwa njia ya neema Yangu na huruma kabisa. Kwamba neno Langu linaonekana miongoni mwa wanadamu, pasi kufichwa tena, hata zaidi ni kwa neema na huruma Zangu. Ninawapenda wote wanaotumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu na kujitolea Kwangu. Ninawachukia wale wote waliozaliwa na Mimi ilhali ambao hawanijui, hata hunipinga Mimi.

6/08/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 69

 Sauti ya Mungu | Sura ya 69

Mapenzi Yangu yatokapo, yeyote anayethubutu kupinga na yeyote anayethubutu kuhukumu au kuwa na shaka, mara moja Nitamfukuza. Leo, yeyote ambaye hatendi kulingana na mapenzi Yangu, au yeyote anayeyafikiria mapenzi Yangu visivyo, ni lazima atupwe nje na kuondolewa kutoka kwa ufalme Wangu. Katika ufalme Wangu hakuna mtu mwingine—wote ni wana Wangu wa kiume, wale ambao Nawapenda na hunifikiria Mimi.

6/07/2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Nane



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” Sehemu ya Nane


 Mwenyezi Mungu anasema, “Ingawa Bwana Yesu alifufuliwa, moyo Wake na kazi Yake vyote havikuwa vimeondoka kwa wanadamu. Aliwaambia watu Alipoonekana ya kwamba haijalishi ni umbo gani Alilokuwemo ndani, Angeandamana na watu, kutembea na wao, na kuwa na wao siku zote na katika sehemu zote. Na nyakati zote na mahali popote, Angewatosheleza wanadamu na kuwachunga, kuwaruhusu kumgusa na kumwona Yeye, na kuhakikisha kwamba hawatawahi kuhisi tena kama wasio na msaada.

6/06/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 68

Maneno ya Mungu | Sura ya 68

Neno Langu linatekelezwa katika kila nchi, mahali, taifa na kikundi, na neno Langu linakamilishwa katika kila pembe wakati wowote. Maafa yanayotokea kila mahali si vita kati ya watu, wala si mapigano na silaha. Hakutakuwa na vita tena baadaye. Wote wako katika mfumbato Wangu. Wote watakabili hukumu Yangu na watadhoofika kati ya maafa. Acha wale wanaonipinga na wale wasioanza kushirikiana na Mimi wateseke uchungu wa maafa mbalimbali.

6/05/2019

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 67

Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Sura ya 67

Wana Wangu wanaonekana wazi, na wanaonekana mbele ya watu wote. Nitawaadhibu vikali wale wanaothubutu kuwakataa wao kwa wazi; hiyo ni hakika. Leo, wale wote wanaoweza kusimama na kuchunga kanisa wote sasa wamepata cheo cha wana wazaliwa wa kwanza na sasa wako pamoja katika utukufu Na Mimi—yale yote yaliyo Yangu ni yenu pia. Ninawakabidhi wale wanaonitii Mimi kwa dhati neema tele, ili uweze kuwa wenye nguvu, zaidi ya nguvu ya wanadamu wengine.

6/04/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 66

Sauti ya Mungu | Sura ya 66

Kazi Yangu imeendelea hadi hatua ya sasa na yote imefuata mipango ya busara ya mkono Wangu, na pia kuwa fanikio Langu kuu. Nani kati ya wanadamu anaweza kufanya kitu kama hiki? Na je, si wanaona ni afadhali waingilie kati usimamizi Wangu? Lakini lazima ujue kuwa hakuna namna yeyote anaweza kufanya kazi Yangu badala Yangu, sembuse kuizuia, kwani hakuna yeyote anayeweza kusema au kufanya vitu Nifanyavyo na kusema. 

6/03/2019

Sauti ya Mungu | Sura ya 65


Sauti ya Mungu | Sura ya 65
Maneno Yangu daima yanaendeleza barabara, yaani yanaonyesha udhaifu wenu wa jaala, vinginevyo bado mgekuwa mnakokota visigino vyenyu, bila wazo la muda gani ulioko sasa. Fahamu hili! Mimi Hutumia njia ya upendo ili kuwaokoa. Bila kujali jinsi nyinyi mlivyo, bila shaka Nitakamilisha mambo ambayo Nimekubali bila kufanya kosa lolote. Je, Ninaweza, Mwenyezi Mungu Mwenye haki, kufanya kosa? Je, hiyo siyo dhana ya mtu? Niambieni, kila kitu Mimi Hufanya na kusema si kwa ajili yenu?

6/02/2019



Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa “Maonyo Matatu”  | How to Be a Loyal Servant of God


Mwenyezi Mungu anasema, “Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi.

6/01/2019

Maneno ya Mungu | Sura ya 64

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Maneno ya Mungu  | Sura ya 64

Unapaswa kutoelewa neno Langu kwa njia ya upuuzi; unapaswa kuelewa maneno Yangu kwa kuangalia vipengele vyote na unapaswa kujaribu kuyaelewa zaidi na kuyafikiri sana kwa kurudia, sio tu kwa siku ama usiku mmoja. Hujui mahali ambapo mapenzi Yangu yapo ama ni katika kipengele kipi Nalipia gharama Yangu ya bidii za kazi; unawezaje kuyazingatia mapenzi Yangu? Ninyi watu wote mko hivi; hamna uwezo wa kuchunguza kwa utondoti, mkisisitiza tu sehemu ya juu na mkiwa tu na uwezo wa uigaji.